Bei ya sembe hatarini kupaa

Bei ya sembe hatarini kupaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki na Wazalishaji sembe na dona (Uwawase), Oscar Munisi alisema jana kuwa kupanda kwa bei ya mahindi kumetokana na kuadimika kwa nafaka hiyo nchini, hususani inayotoka Dodoma na Ruvuma, mikoa ambayo alisema imekumbwa na ukame. “Bei ya kununulia mahindi imepanda mara mbili ya awali. Tunaiomba Serikali itusaidie tupate mahindi, hali ikizidi kuwa kama hivi sasa atakayeumia ni mwananchi wa kawaida,” alisema Munisi.

Munisi alisema umoja huo ndiyo unaosambaza unga kwa asilimia kubwa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na Zanzibar hivyo kuiomba Serikali iingilie kati kuimarisha hali ya upatikanaji wa mahindi ili kusitokee mfumuko wa bei. Alisema sababu zinazosababisha uhaba wa mahindi mwaka huu ni Serikali kuchelewa kuzuia bidhaa hiyo kusafirishwa nje kwa kuwa mahindi yalikuwa yameshasafirishwa. Pia alisema migogoro baina ya wakulima na wafugaji ulisababisha mimea kukatwa au kuliwa na mifugo.

Munisi alisema tatizo hilo lilijitokeza pia mwaka jana ila hali haikuwa kama ya mwaka huu baada ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoa mahindi na kuwauzia kwa bei ya Sh480 mpaka 500 kwa kilo.

Msimamizi wa Kampuni ya Msouth Extra Power Sembe, Evod Sanga alisema wameanza kuuza kiroba mara mbili ya bei ya awali ili kupata faida ya shughuli wanazofanya kuzalisha sembe.

“Tangu kuanza kwa hili tatizo, hata bei zetu tumepandisha. Kwa sasa, awali bei ya kiroba cha kilo tano ilikuwa Sh3,000 lakini sasa tunauza Sh6,000, cha kilo kumi kilikuwa kinauzwa Sh7,000 sasa Sh11,000 pia cha kilo 25 tulikuwa tunauza Sh17,000, lakini sasa ni Sh26,000 na cha kilo 50 ilikuwa Sh30,000 sasa imefikia Sh 53,000 na bado hatupati faida,” alisema Sanga.

Mshauri wa masuala ya fedha kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Revelian Ngaiza alisema wafanyabiashara na wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani msimu mpya utaanza Februari mwakani hivyo upatikanaji wa mahindi utakuwa wa kawaida. “Mikoa ambayo wanaegemea kupata mahindi ni ile inayotegemea msimu mmoja kwa mwaka tofauti na Kanda ya Ziwa wanaotegemea misimu miwili. Pia hali hiyo inachangiwa na mahitaji na usambazaji wa mahindi maana watu ni wengi na hiki si kipindi cha mavuno,” alisema Ngaiza

Ngaiza aliongeza kuwa endapo hali itazidi kuwa mbaya, Serikali itaingilia kwa kuuza kwa wafanyabiashara mahindi yanayohifadhiwa na NFRA ili kukabiliana na hali hiyo.
 
Huyo Bw. Ngaiza ajue pia kuna tishio la ukame.
Waandishi wanapaswa kuiambia ukweli serikali juu ya balaa la njaa wakati ufaao.
Wasiogope! Hata kama kuna mwenzao kule Kagera alipigwa mkwara mzito kwa kusema ukweli.
 
Iongezeke tu kadri namba zinavyosomeka,
Umeme tushaambiwa utapanda,
Mafuta ndio hivyo yanapanda,
Maji pia yapo njiani
 
Bei ikiongezeka ndio nafuu kwa Mkulima.Kwani huoni Korosho nazo zimepanda bei.
 
Tatizo siyo ukame tu ,watu hawalimi mahindi kutokana na kuwa hakuna soko wakulima wakilima mengi soko hakuna wasipolima soko lipo.
Mfano mwaka huu watalima mengi kwa sababu wanafikiri na mwakani soko litakuwepo ikifika mwakani kwa sababu yatakuwa mengi bei itapungua sana na mkulima kupata hasara hivyo mwaka 2018 hawatalima mengi na mahindi yata adimika tena.
 
Dar es Salaam. Bei ya unga wa sembe huenda ikapanda kutoka Sh1,200 hadi Sh2,000 kwa kilo kwenye maduka ya rejareja baada ya bei ya mahindi kupanda mara mbili ya bei ya awali.

Kwa sasa mahindi yanauzwa Sh760 kwa kilo kutoka Sh350 za awali.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki na Wazalishaji sembe na dona (Uwawase), Oscar Munisi alisema jana kuwa kupanda kwa bei ya mahindi kumetokana na kuadimika kwa nafaka hiyo nchini, hususani inayotoka Dodoma na Ruvuma, mikoa ambayo alisema imekumbwa na ukame. “Bei ya kununulia mahindi imepanda mara mbili ya awali. Tunaiomba Serikali itusaidie tupate mahindi, hali ikizidi kuwa kama hivi sasa atakayeumia ni mwananchi wa kawaida,” alisema Munisi.

Munisi alisema umoja huo ndiyo unaosambaza unga kwa asilimia kubwa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Tanga na Zanzibar hivyo kuiomba Serikali iingilie kati kuimarisha hali ya upatikanaji wa mahindi ili kusitokee mfumuko wa bei. Alisema sababu zinazosababisha uhaba wa mahindi mwaka huu ni Serikali kuchelewa kuzuia bidhaa hiyo kusafirishwa nje kwa kuwa mahindi yalikuwa yameshasafirishwa. Pia alisema migogoro baina ya wakulima na wafugaji ulisababisha mimea kukatwa au kuliwa na mifugo.

Munisi alisema tatizo hilo lilijitokeza pia mwaka jana ila hali haikuwa kama ya mwaka huu baada ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kutoa mahindi na kuwauzia kwa bei ya Sh480 mpaka 500 kwa kilo.

Msimamizi wa Kampuni ya Msouth Extra Power Sembe, Evod Sanga alisema wameanza kuuza kiroba mara mbili ya bei ya awali ili kupata faida ya shughuli wanazofanya kuzalisha sembe.

“Tangu kuanza kwa hili tatizo, hata bei zetu tumepandisha. Kwa sasa, awali bei ya kiroba cha kilo tano ilikuwa Sh3,000 lakini sasa tunauza Sh6,000, cha kilo kumi kilikuwa kinauzwa Sh7,000 sasa Sh11,000 pia cha kilo 25 tulikuwa tunauza Sh17,000, lakini sasa ni Sh26,000 na cha kilo 50 ilikuwa Sh30,000 sasa imefikia Sh 53,000 na bado hatupati faida,” alisema Sanga.

Mshauri wa masuala ya fedha kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Revelian Ngaiza alisema wafanyabiashara na wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani msimu mpya utaanza Februari mwakani hivyo upatikanaji wa mahindi utakuwa wa kawaida. “Mikoa ambayo wanaegemea kupata mahindi ni ile inayotegemea msimu mmoja kwa mwaka tofauti na Kanda ya Ziwa wanaotegemea misimu miwili. Pia hali hiyo inachangiwa na mahitaji na usambazaji wa mahindi maana watu ni wengi na hiki si kipindi cha mavuno,” alisema Ngaiza

Ngaiza aliongeza kuwa endapo hali itazidi kuwa mbaya, Serikali itaingilia kwa kuuza kwa wafanyabiashara mahindi yanayohifadhiwa na NFRA ili kukabiliana na hali hiyo.
 
acha ipae tutengeneze hela,maana huko mjini si ndo hela zilipo,pia itasaidia kuwafanya mrudi kijijini kulima.
 
leti zemu ridi namba ee, CCM fronti tu frontiii!!
 
Kuna wakati katika kipindi cha Kikwete mambo yalikuwa hivihivi, Kikwete akaamuru yasambazwe masokoni mahindi ya hifadhi ya taifa ya chakula masokoni bei ushuke, na KWELI.

Tunatumai na Mheshimiwa Rais Magufuli atafanya vivyo hivyo.

Tutakukumbuka sana Kikwete kwa hifadhi ya Taifa ya chakula, kitu ambacho kilikuwa hakuna kabla ya utawala wako.
 
Back
Top Bottom