Bei ya Pamba soko la dunia yaporomoka

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Kushuka kwa bei ya Pamba nyuzi katika Soko la dunia kumetajwa kuwa ndio chanzo cha makampuni ya ununuzi wa zao la Pamba mkoani Shinyanga kushindwa kununua kwa kuogopa kupata hasara.

Hayo yamebainishwa na Amiri Mwinyimkuu Meneja Shughuli wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) wakati akizungumza na waandishi wa Habari mjini Kahama kuhusiana na hatua walizichukua ili kukabiliana na tatizo hilo.

Amesema kwa sasa Kampuni za ununuzi wa zao hilo zimeshindwa kwenda sokoni kununua pamba kutokana na kushuka bei ya Pamba nyuzi katika soko la dunia hali ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufunguliwa kwa soko la Pamba.

Amefafanua kuwa bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia kwa sasa ni dola 1.39 ambayo ikibadilishwa kwa fedha za kitanzania ni shilingi 1,449 hivyo endapo watanunua pamba mbegu kwa shilingi 1,200 watapa hasara.

Ameongeza kuwa kampuni hizo zimeomba bei ya kununua kwa mkulima ishuke sokoni au serikali iwape kinga (guarantee) ya kuwafidia hasara itakayopatika baada ya kuuza pamba katika soko la dunia ambapo hadi sasa bado serikali haijatoa maekekezo yeyote.

Katika hatua nyingine Mwinyimkuu amesema wakulima katika wilaya ya kahama wamelima pamba ekari 40,869 na wanatarajia kuvuna kilo zaidi ya milioni 400.

Makampuni yaliyopatiwa leseni za kununua pamba hizo ni Kahama Cotton Campuny Limited (KCCL) Kahama Oil Mill, Afriacian na kampuni ya Fresho ambapo mpaka sasa kampuni mbili ndio zimeweza kununua zao hilo ambazo ni Fresho na Kahama Oil Mills.
 
Kilo moja ya pamba unaweza kutoa mashati 3-4 ambayo yanauzwa kwa $10-25 bei ya pamba ni chini dolla moja Kwa kilo moja ya pamba uku kwetu. Kwa nini wasianzishe viwanda vya Nguo, waboreshe mwatex, kilitex , sunguratex, mutex mambo yatakuwa mazuri
 
Je changamoto zilizo viua hivyo viwanda vya mwatex,kilitwx etc zimeshatuliwa?
 
Kilo moja ya pamba unaweza kutoa mashati 3-4 ambayo yanauzwa kwa $10-25 bei ya pamba ni chini dolla moja Kwa kilo moja ya pamba uku kwetu. Kwa nini wasianzishe viwanda vya Nguo, waboreshe mwatex, kilitex , sunguratex, mutex mambo yatakuwa mazuri
Hivi gharama za uzarishaji bidhaa hapa nchini unazijua?? Acha kabisa, ukiwasikiliza wana siasa utaamini kuwa hapa ni heaven!! Ila sasa ingia field utajuta!! Wewe anakuja waziri anakuta kuna tatizo labda la uchafuzi mazingira unalimwa bilioni 2 kama faini ilipwe ndani ya siku 7!!kodi, vibali bado umeme!! Mbona wengi wameshindwa
 
Katika hatua nyingine Mwinyimkuu amesema wakulima katika wilaya ya kahama wamelima pamba ekari 40,869 na wanatarajia kuvuna kilo zaidi ya milioni 400.

Hili andiko linapotosha sana, kama wakulima wamelima ekari 40,869 na matarajio ni kuvuna kilo milioni 400 ndio kusema ekari moja watavuna kilo 9,787.
Uzalishaji wa kiwango hicho haujawahi kufikiwa mahali popote duniani. Kiwango kikubwa cha mavuno ya pamba kupatikana Tanzania ni kilo milioni 370 mwaka 2005/06 (kama sikosei).
 
Kilo moja ya pamba unaweza kutoa mashati 3-4 ambayo yanauzwa kwa $10-25 bei ya pamba ni chini dolla moja Kwa kilo moja ya pamba uku kwetu. Kwa nini wasianzishe viwanda vya Nguo, waboreshe mwatex, kilitex , sunguratex, mutex mambo yatakuwa mazuri

Hii haina tofauti na ukulima wa matikiti maji kwenye makaratasi. Ukilima ekari moja utapata matikiti 3,000 ukipeleka Dar kila tikiti sh.2000 unapata milioni 6, ukitoa gharama milioni 1.5 faida milioni 4.5!!!

Sawa mashati 3-4 unauza Sh 23,000 - 57,500, swali inagharimu kiasi gani kupata kilo moja ya pamba nyuzi??
Na inagharimu kiasi gani kupata shati moja???
 
Hili andiko linapotosha sana, kama wakulima wamelima ekari 40,869 na matarajio ni kuvuna kilo milioni 400 ndio kusema ekari moja watavuna kilo 9,787.
Uzalishaji wa kiwango hicho haujawahi kufikiwa mahali popote duniani. Kiwango kikubwa cha mavuno ya pamba kupatikana Tanzania ni kilo milioni 370 mwaka 2005/06 (kama sikosei).
heka huwa inachezea kilo 600-700 kwa mia 9 pamechimbika
 
Wale wa korosho wameshalia hadi wamenyamaza acha kilio kihamie nyumbani
 
Mheshimiwa Rais usikubali kuchezewa na hawa mabeberu wanaojiita Soko la Dunia, pumbavu zao! Tuma JKT wakanunua pamba yote kwa bei mzuri kwa mkulima kisha waambie hao hao JKT waanze kuzalisha nguo za aina mbalimbali ambazo tutasafirisha na kupata fedha za kigeni!

Lazima mabeberu waanze kuvaa suruali na mashati yaliyotengenezwa na jeshi letu, kama ambavyo siku hizi wanavyofakamia korosho zilizobanguliwa na makamanda wetu!!
 
Back
Top Bottom