Bei ya Mashine za Kukoboa na Kusaga

Bei ya Mashine za Kukoboa na Kusaga

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,371
Reaction score
14,481
Habari za jioni wakuu?

Jamani naomba kujua bei za Mashine ya kukoboa na Kusaga zinazotumia Diesel, nitashukuru kama mtanisaidia.

Naomba kuwasilisha.
 
Bei kwa Injini ya 20 HP ni Ths. 950,000 zinapatikana kwa Wingi mtaa wa India duka la KILIMO BORA.
 
Mashine ya Kusaga ama kukoboa ina sehemu mbili. INJINI na KINU.

INJINI / MOTA zinapatikana kwa ukubwa tofauti yaan Horse Power mbalimbali. Eg. HP 12, 15, 20 na kuendelea. Injini nzuri kwa kupiga mzigo na Ulaji mzuri wa Mafuta ni HP 20 bei yake ni 950,000 aina ya Jiang Dong JD, ama DF ama AMEC zote za mchina. Usinunue Lister Peter.

Ukisha nunua Injini unanunua kinu cha Kusaga na kukoboa vinapatikana Sido ama kwa mafundi wa kuchomelea kwa bei ya 500,000-700,000 kutegemea na makubaliano.

Baada ya hapo utasimika mashine yako eneo ulilochagua.

Note
Injini moja inaweza kuvuta vinu viwili katika jengo lako kinachotakiwa ni kutafuta fundi mtaalamu. Ukiwa Dsm Injini zinapatikana Mtaa wa India duka la Jumla la Injini hizo linaitwa KILIMO BORA, AU AGRO METRO. Ukiwa Mwanza duka la Injini lipo Mtaa wa Rwagasore linaitwa SHYMOND.

Endapo utasimika mashine yako kwa usahihi kabisa Kila dumu la Lita ishirini la Diesel faida yake ni Tshs. 60,000 - 80,000 kulingana na bei ya Kusagiaa.

Karibu kwenye biashara isiyo na stress Mkuu.
 
Poa Mkuu nitafanya hivyo. Lkn kama unataka ufafanuzi uliza hapa kwa manufaa ya wengi.

Naomba ufafanuzi kwnye tofauti ya faida: kati ya anaye endesha mashine/Kinu kwakutumia DIESEL na anayetumia nishati ya UMEME.
 
Mimi nilikuwa nayo ya diesel naona kama inakula ghalama kubwa kuliko ya umeme. Ufafanuzi tafadhali
 
Mashine ya Umeme inalipa kuliko Mashine ya Mafuta.
Isipokuwa Mashine ya Umeme ni Aghali kuanzisha kuliko mashine ya Mafuta.
Mashine ya Umeme Utahitaji Mota, Kinu, Kulipia Tanesco Three Phase service, Kununua Cables, Kununua Starter, Maina Switch nk. Gharama zinaenda Mil 8-10. Lkn baada ya hapo utasahau usumbufu wowote. Lkn Mashine ya Mafuta kuisimika ni gharama kidogo kuanzia Mil 3-5 lkn Mziki wake sasa, mara Oil, mara, Filter, Mara Piston, Mara Water Pump thats why sehemu zenye Umeme huezi kukuta Mashine ya Mafuta
 
Gharama za Kuanzisha mashine ya Umeme.
Mota 20hp 1470 rpm Tshs 1 Mil, Kinu Lak 7, Starter ya MEM genuine Lak 4.5, Main Switch Lak 5, Control Lak 4, Tanesco Mil 2-3, Cables Lak 6 nk..
Note... Unaponunua Mota uwe makini usichukue Mota Hp kuuuubwa ukaishia kuifaidisha Tanesco, zingatia vipimo ili kuokoa matumiz ya Umeme yasiyo ya lazma ili upate faida zaidi.
Chekecheo la kinu chako pia ni mbinu ya kupata faida zaidi... Ni somo lefu Karibun kwa maswali zaidi.
 
Asante Mmteule! Utakuwa mzoefu kwenye hii bussines. changamoto zake zinaweza kuwa zipi nijipange kukabiliana nazo kabisa?
 
Gharama za Kuanzisha mashine ya Umeme.
Mota 20hp 1470 rpm Tshs 1 Mil, Kinu Lak 7, Starter ya MEM genuine Lak 4.5, Main Switch Lak 5, Control Lak 4, Tanesco Mil 2-3, Cables Lak 6 nk..
Note... Unaponunua Mota uwe makini usichukue Mota Hp kuuuubwa ukaishia kuifaidisha Tanesco, zingatia vipimo ili kuokoa matumiz ya Umeme yasiyo ya lazma ili upate faida zaidi.
Chekecheo la kinu chako pia ni mbinu ya kupata faida zaidi... Ni somo lefu Karibun kwa maswali zaidi.

I salute you mmteule
 
Heshima kwako.
 
Wadau kwa Uzoefu wangu wa Kufanya biashara nimegundua Kuwa Biashara ambayo ni non mobile yaan iliyotulia sehemu maalum au isiyohamishika ina changamoto chache mno ukilinganisha na ile ya kuhamahama. Kwa biashara ya Mashine changamoto kubwa ni VIPURI FEKI, MGAO WA UMEME na Ubabaishaji wa Wafanyakazi. Zingatia unaponunua Vifaa vya Mashine yako ununue VIFAA GENUINE INGAWA VITAKUA BEI AGHALI LKN UTAFAIDI ZAIDI. mf. Switch ya kuwasha Mashine FEKI INAUZWA LAK 2 Kkoo, Lkn ukienda kwa Dealer wa Vifaa vya MEM ya Uingereza vifaa ambavyo utapewa Grantii ya Miaka 20 hiyo Starter wanauza Lak 4.5
ukijiloga ukanunua starter feki ya lak 2 kwa mwaka itaungua zaidi ya Mara 6 au zaidi so wewe utakua daily ni kwenda kununua spea. Tujitahidi kutafuta vifaa imara. Wenzetu wanasema CHEAP IS EXPENSIVE
 
Mashine ya Kusaga ama kukoboa ina sehemu mbili. INJINI na KINU.
INJINI / MOTA zinapatikana kwa ukubwa tofauti yaan Horse Power mbalimbali. Eg. HP 12, 15, 20 na kuendelea. Injini nzuri kwa kupiga mzigo na Ulaji mzuri wa Mafuta ni HP 20 bei yake ni 950,000 aina ya Jiang Dong JD, ama DF ama AMEC zote za mchina. Usinunue Lister Peter.
Ukisha nunua Injini unanunua kinu cha Kusaga na kukoboa vinapatikana Sido ama kwa mafundi wa kuchomelea kwa bei ya 500,000-700,000 kutegemea na makubaliano.
Baada ya hapo utasimika mashine yako eneo ulilochagua. Note.... Injini moja inaweza kuvuta vinu viwili katika jengo lako kinachotakiwa ni kutafuta fundi mtaalamu. Ukiwa Dsm Injini zinapatikana Mtaa wa India duka la Jumla la Injini hizo linaitwa KILIMO BORA, AU AGRO METRO. Ukiwa Mwanza duka la Injini lipo Mtaa wa Rwagasore linaitwa SHYMOND.
Endapo utasimika mashine yako kwa usahihi kabisa Kila dumu la Lita ishirini la Diesel faida yake ni Tshs. 60,000 - 80,000 kulingana na bei ya Kusagiaa.
Karibu kwenye biashara isiyo na stress Mkuu.

Mkuu ubarikiwe sana!!!.
 
Gharama za Kuanzisha mashine ya Umeme.
Mota 20hp 1470 rpm Tshs 1 Mil, Kinu Lak 7, Starter ya MEM genuine Lak 4.5, Main Switch Lak 5, Control Lak 4, Tanesco Mil 2-3, Cables Lak 6 nk..
Note... Unaponunua Mota uwe makini usichukue Mota Hp kuuuubwa ukaishia kuifaidisha Tanesco, zingatia vipimo ili kuokoa matumiz ya Umeme yasiyo ya lazma ili upate faida zaidi.
Chekecheo la kinu chako pia ni mbinu ya kupata faida zaidi... Ni somo lefu Karibun kwa maswali zaidi.

Mkuu unazidi kunifungua ufahamu sana,hivi kubadilisha oil kwa Mashine za Mafuta ni kila baada ya muda gani??.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom