Bei ya mahindi yaporomoka ghafla, wakulima wapigwa butwaa

Bei ya mahindi Kwa gunia la kilo 100 imeshuka ghafla Mikoa ya Nyanda za Juu kutoka wastani wa sh. 80,000 Hadi sh.65,000.

Serikali nayo imesitisha kununua mahindi Kwa Sababu imenunua Tani za kutosha na pesa imeisha.

Sababu zikizotajwa za bei kushuka ni kukosekana Kwa wanunuzi kutoka Nje.

Mahindi Yataendelea kushuka zaidi maana Kenya ambayo ndio mteja mkubwa wa Tanzania wamepata mazao mengi mwaka huu ambapo na huko kwao Rift Valley bei zimeporomoka pia.

Na bei zitazidi kushuka miaka ijayo Kwa sababu Wazungu wa Zimbabwe wamerejea na Zimbabwe iliwahi kuongoza Afrika Kuzalisha mahindi.
---

Wakulima wapigwa butwaa bei ya mahindi kushuka ghafla​

Songwe. Bei ya mahindi katika masoko mbalimbali katika Mkoa wa Songwe imeporomoka katika kipindi cha mwezi mmoja ikilinganisha na bei zilizokuwepo mwezi Juni na Julai mwaka huu.

Mmoja wa wakulima aliyehojiwa na Mwananchi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Sumbaluwela, Kata ya Ihanda wilayani Mbozi, Irine Nahaonga amesema amekuja kuuza kiasi kidogo cha mahindi ili aweze kutatua shida ndogo za nyumbani mwake, lakini amekuta bei imeshuka ghafla kutoka Sh85000 hadi 66,000 kwa gunia la kilo 100.

"Wanunuzi wenye stoo ambao wananunua mazao wametaka wanunue mahindi yangu kwa bei ya Sh66,000 badala ya Sh85,000 niliyokuwa nimeitarajia awali," amesema Nahaonga.

Aidha katika kipindi cha miezi Juni na Julai mwaka huu mahindi yalikuwa yakiuzwa kwa bei ya kati ya Sh80,000 na Sh84,000 kwa gunia lenye ujazo wa kilogramu 100.

Kutoka katika soko la mazao Mlowo wilayani Mbozi Tumaini Enson amesema katika kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu bei ya Mahindi ilishuka kufuatia wanunuzi kutofika hivyo kusababisha mahindi kurundikana.

"Kuanzia juzi walau bei imeanza kuongezeka kidogo kutoka Sh66,000 hadi Sh72,000 siku ya leo hivyo kuna nafuu kidogo,” amesema Tumaini.

Meneja wa Soko la kimataifa la mazao katika Halmashauri ya mji wa Tunduma, Edward Silwimba amesema katika soko hilo bei ya Mahindi kwa siku ya leo ni kati ya Sh72,000 na Sh78,000 kwa gunia lenye uzito wa kilogramu 100.

Kuhusu sababu za kushuka bei katika soko hilo kipindi hiki tofauti na miezi ya Juni na Julai, mwaka huu amesema hali hiyo inafuatia kukosekana kwa wanunuzi wanaoingia hata hivyo kwa sasa amesema wameanza kuja mmoja mmoja.

My Take
Njia pekee ya kuwa na uhakika wa soko la mahindi ni kukuza ufugaji wa Kisasa Ili mahindi yatumike kama chakula Cha mifugo badala ya kutumia kama chakula Cha binadamu pekee.
Hadi Michele

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1702618726573441195?t=7wgLCBMion30rJswkD4xlw&s=19
 
Wadau kwajinsi mnaovyoona Mahindi yatapanda Bei tena kwel?
 
Mbeya ni ndizi, kitimoto,viazi vya Mbeya, maharage, maziwa hapa lazima uwe bonge.
Ndo maana kina malafyale niangusage sambi zako wameshiba
Niangusage vijitu vidogo kama wandengereko wa Pwani.
Nimekaa nao Iringa.
Vanyambala akina Malafyale mbavu nene haswaa kasoro mwamba wa Malila tu.
 
My Take
Njia pekee ya kuwa na uhakika wa soko la mahindi ni kukuza ufugaji wa Kisasa Ili mahindi yatumike kama chakula Cha mifugo badala ya kutumia kama chakula Cha binadamu pekee.
Kwa lugha ya vijana wa sasa wanasema kizazi sana.
Point point. Japo kwa uzoefu wangu wa kufuga kuku, mazao yakishika bei, chakiula cha kuku nacho hushuka bei na mwishowe bei ya kuku huanguka . Multiplying effect.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom