Bei ya Mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya Mafuta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, May 6, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kufuati hali tete ya uchumi Ulaya na Marekani, bei ya mafuta leo imeshuka kwa karibu ya asilimia 10 katika soko la dunia na huenda ikashuka zaidi hivi karibuni. Kushuka huku kutakuwa na faida tu kama hali ile itaonekana kwenye pump zetu nyumbani na pia hali ya fedha yetu ikaimarika.
  Matarajio ya baadae ni kwamba; Kwa kuwa Marekani sasa hivi wanafanya quantitative easing yaani wanaongeza pesa kwenye mzunguko ili angalau uchumi usonge mbele, program hiyo inatarajiwa kuisha mwezi June kwahiyo huenda demand ya mafuta ikapungua na hivyo bei kuporomoka.
  Lakini angalizo kwa upande mwingine, licha ya bei kupungua pesa ya Marekani nchini kwetu hutumika ndio kama measure ya fedha yetu kwenda nyingine. Kwahiyo kama sera za fedha nchini kwetu zitakuwa zinafuatilia hali hii, ni lazima ifike wakati intervention itumike. Uchumi wetu si ule wa kuendeshwa ni demand na supply maana kuna factor nyingi zaidi ya hizo. Labda mfano mmoja; Baada ya kugundulika wizi wa fedha za EPA, tulitarajia mtikisiko mkubwa saana hasa kwa Bank ya CRDB ambayo ilikuwa implicated, lakini hilo halikuonekana. Kwahiyo, ni vyema taasisi husika ikautazama upya uchumi wa nchi yetu. Lakini wakati huo tufikirie, je hatuna njia zaidi za kupunguza mafuta kwa kufikiria vyanzo vipya vya energy? je hatuwezi kurekebisha barabara zetu ili huu uchumi unaosua uweze kuimarika?
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Kwa hapa mafuta yatapanda tatizo wenye dhamana hawawajibiki!!Leo maduka yanauza vitukwa $dollar!!utafikiri pesa yetu haitumiki na viongozi wapo wanashindwa kukemea!!natatizo hili serikali inajua ujinga huu lakini ipo kimya sihilo tu hata baadhi ya sekta za serikali niliwahi kukuta wanalipisha dollar nikashangaa!!!
   
 3. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mimi nashangaa taasisi za serikali kama NIMR kuomba ethical clearance kwa kiwango cha dola. Huo ni upuuzi.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapa kama vile kuna collusion kati ya authorities na wafanyabiashara, kwa mfano bei ya mafuta huko kwenye soko la dunia ikipanda the very same day or week EWURA wanatoa bei mpya elekezi na hapo hapo kwenye pump za mitaani wanapandisha bei bila ya consideration ya kwamba kuna old stock which was acquired using the previous lower prices. Lakini bei ikishuka kama leo hapa kwenye asilimia 10 ambako bei ime-slip to lower than US$100 kwa pipa utaona bei za juu zitabakia zile zile za kabla ya bei kushuka huko kwenye soko la dunia. Ina maana hakuna wa ku-oversee ethics za biashara au kutetea maslahi ya walaji, kama wapo basi kuna kitu sinister kati yao kinaendelea na wafanyabiashara. Pia kuna vitu vingi hapa kwetu abavyo unaweza kugundua uchumi wetu hauko sensitive kwa matukio ya sokoni au nchi kama hayoya EPA kwa benki ya CRDB aliyoeleza mtoa mada hapo juu, na mengine mengi tu!
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Hao viongozi ndio haohao wenye kumiliki hayo makampuni ya mafuta,
  halafu nimkuwa ni kifikiria kuhusu KODI inayopatikana kwenye MAFUTA, na hisi serekali inafanay makusudi kutoshusha bei ili IENDELEE KUPATA KODI KUBWA!
  wish hii KODI ingekuwa constant kama ni 500 basi ni hiyo hiyo kwa lita!
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Si NIMR peke yao wapo wengi tu wakiwemo Tanroads ambao adhabu ya kutokupima kwenye mizani (weigh bridge) yao ni USD 2,000. I'm told hata baadhi ya penalties za TRA ziko kwenye USD pia huu ulimbukeni sijuwi tumeutoa wapi. Then wasomi kama prof. Ndullu ukiwauliza kwanini USd inapanda kila siku against Tsh watakuambia vitu vya ajabu kabisa wakati mambo yako so obvious. Mahitaji ya USD nchini ni makubwa kuliko supply yake kwani hata vitu tulivyopswa kuvitoza kwa Tsh vinatozwa kwa USD.Upuuzi kama huu haukuwepo enzi za Mwalimu-we miss you so much Teacher.
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  sasa angalieni mafuta yatakavyozidi kupanda licha ya bei kushuka katika soko la dunia...


  hii nchi nadhani imelaaniwa, we need to do something
   
 8. markach

  markach Senior Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwalimu tutakukumbuka sana. Ukitaka kuamini nenda kwenye baadhi ya maduka pale posta,nenda Superdoll uone,wanauza vitu kwa dolla. Hii inamaanisha, leo utanunua kwa tshs bei fulani kesho tshs bei nyingine na huku kitu ni kile kile. Tanzanian tuwe macho na serikali hii na viongozi wake, kwani wao wananufaika na mfumo huu
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 631
  Trophy Points: 280
  Tanzania jamani Tanzania.
  Viongozi wetu wamekosa uamakini wa hali ya Juu!!

  1. Ni Tanzania Pekee Bei ya Soda imehalalishwa Tshs. 500. Lakini leo ukienda dukani Unauziwa Soda Tshs. 600.

  2. Ni Tanzania Pekee Bei ya Bia ni Tshs 1,500/= lakini Bar Karibu zote bia inauzwa 1,600/= (But I dont Drink :A S 114:)

  3. Ni Tanzania Pekee Ambapo huwezi pata huduma ya Kiserikali bila kitu Kidogo- Do I have to pay for a TIN.

  4.Ni Tanzania Pekee Umeme unapanda Bei Kisa Tanesco wameshindwa kumudu gharama ilhali wanapoteza mabilioni kwa watu Kucheza na Meter kupitia Wasoma meter wa Tanesco!!!

  5.Ni Tanzania pekee inaruhusu makaupuni ya simu kudanganya wateja wao. (babu yangu kule Monduli alipata meseji kuwa no. yake ya simu imechaguliwa atume jina lake kwenda a Certain No. anaweza shinda 3m Bila hili wale lile mzee akatuma jina zaidi ya mara kumi and all the airtime was gone) Naomba niulize ni wazee wangapi kule vijijini wanalizwa na hizi sms?

  6.Ni Tanzania pekee wageni wanachukua nafasi za juu katika NGOs, Huku wazawa wakipewa nafasi za chini na Mshara wa kiasi Cha Mboga.

  8.Ni Tanzania pekee Mbunge anafanya Biashara za mabilioni.

  9.Ni Tanzania Pekee mtoto wa Rais anaishi Kimjinimjini!

  10.Ni Tanzania pekee waziri anaasimamishwa utendaji wa kazi fulani katika Mkutano wa Hadhara.

  11.Ni Tanzania pekee Fisadi anaambiwa Rudisha mali ulizoiba la sivyo Ufunguliwe mashtaka.

  12.Ni Tanzania Pekee Bar iliyopo katikati ya makazi ya watu inapiga muziki(at full blasts) Usiku kucha.

  13.Kuna vibaka wana Gari moja Nyeusi saloon, wenye asili ya Kiarabu, Hawa vijana huwa wanavunja sana magari ya watu na kutoa, power windows, head reasts, Na redio, Mchana kweupeee, na hata kukwapua Laptops, wako sana masaki na Posta, Ila Ukiwakamata na kuwapeleka kituo cha polisi ni kama unajisumbua, They will never be detained! Wanajulikana sana pale oyester bay. Hii ipo Tanzania Tu!!

  I cant Exhaust the list!!!!
   
Loading...