Bei ya dhahabu sasa yavuka $ 1,100 - Kikwete anakwenda jamaika kutafuta ....? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya dhahabu sasa yavuka $ 1,100 - Kikwete anakwenda jamaika kutafuta ....?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwafrika, Nov 12, 2009.

 1. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Gold keeps on surging, hits new high of $1,118  Source - yahoo kutoka AP

  http://news.yahoo.com/s/ap/20091111/ap_on_bi_ge/us_gold_prices

  Badala ya kutumia vyema rasilimali zilizopo (kama migodi mikubwa mitatu ya dhahabu nchini na mingine kibao midogo midogo), vasco da gama yeye anataka kwenda jamaica.
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  MwaAfrika:

  Tanzania haitakiwi kutumia migodi ya dhahabu au madini yoyote kama penacea ya matatizo yake.

  Wachumi wana kitu kinachoitwa economic cycles. Hivyo basi kuhusiana na bei ya dhahabu, watanzania ni lazima wachambue ni kitu gani kinachofanya dhahabu kupanda.

  Factor moja ya kupanda dhahabu ni kushuka kwa thamani ya dollar kiMarekani. Kuchuka huku kunawafanya watu wanao-invest katika masuala ya pesa au kuweka akiba kutumia gold.

  Hivyo basi kupanda kwa bei ya dhahabu ni kitu cha muda tu. Kwani dollar itakapoaanza kupanda basi kuna uwezekano mkubwa kwa dhahabu kushuka bei.

  Cha muhimu ni kuishauri serikali kutoanza miradi mikubwa mikubwa kwa kutegemea dhahabu. Kwani bei itakaposhuka, itashindwa kumalizia miradi hiyo.

  Wako

  ZaKenda
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Kwa kuwa sisi ni 3rd producer wa dhahabu kwa nini na sisi tusihodhi dhahabu kama walivyofanya Wamarekani? Mimi si mchumi kwa hiyo naomba tuisheni.
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kuhodhi dhahabu ni wazo zuri. Lakini je unafanya hivyo kwa sababu gani au kwa sababu waMarekani wanafanya hivyo?

  WaMarekani wanahodhi vitu vingi: vikiwemo vyakula, mafuta na vitu ambavyo ni muhimu kiusalama na kimaendeleo.

  Hivyo watu binafsi na serikali zinaweza kuhodhi dhahabu kwani katika kipindi hiki bei ya dhahabu iko juu watu au serikali ingeweza kufanya mengi na dhahabu kuliko na US dollar.

  Hivyo kwa kutumia economic cycles unaweza kuona kuwa bei ya dhahabu inapopanda basi thamani ya dollar inakuwa chini. Na thamani ya dollar inapopanda bei ya dhahabu inashuka. Na kwa kutumia mfano huu unaweza kuwa na mechanism ya kuhodhi dhahabu, lakini unatakiwa kuwa makini sana kuelewa mwanzo na mwisho wa mizunguko.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  By the way, kwani tunayo dhahabu sisi???? Ya kwetu kabla haijachimbwa ikichimbwa tuuu sio yetu ya wenyewe. Reserve yetu ya dhahabu nadhani tunainunua. Naomba mwongozo wenu wanazuoni waliobobea kwenye masuala ya uchumi.
   
 6. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Labda tu kwa kuongezea, bei ya soko "huria" siku zote hutegemea demand and supply, na kwa dhahabu ni hivyo hivyo. Mojawapo ya vitu vinavyo influence biashara sana sana demand ya dhahabu ni thamani ya sarafu mbalimbali hususani zile ambazo zinatumika na benki kuu pamoja na bodi za sarafu mbalimbali kuweka akiba za nchi zao.

  Unavyoongelea thamani ya dollar kuanguka ni sawa kabisa na hii ni moja tu ya currencies zenyewe ingawa ndio yenye uzito mkubwa. Lakini ukiangalia utaona pia ni volatility inayoonyeshwa na thamani ya sarafu nyingi ambayo inatoa msukumo mkubwa zaidi kwa benki kuu na wadau wa masoko kukimbilia dhahabu. Thamani ya Euro imeongezeka na it being more or less a basket currency has been relatively stable, but why has it not caught on as a reserve currency? Angalia hali mbaya ya uchumi kwa EU member states na uncertain future prospects zake. Besides EU wenyewe hawataki iongezeke thamani maana ina erode competitiveness katika external trade.

  Sababu nyingine kubwa ya kupanda kwa bei ya dhahabu ni kwamba katika masoko ya mitaji na bidhaa, bei ya natural tradeables kama mafuta pamoja na metals zingine kama Aluminium, Nickel etc. bado iko chini ya desired price na hivyo haziyield sufficient returns kwa wawekezaji. Hii inamaanisha ya kwamba wafanyabiashara wanalazimika kununua ile kitu ambayo bei inalipa.

  You are right unaposema kwamba its an economic cycle. Agents wanazidi kununua tu na pale wakapoona bei imepanda vya kutosha wataanza kuuza dhahabu zao na ndipo bei itakapokuwa depressed unless the gold cartels interfere with the supply side. Keep an eye out for the People's Bank of China.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Darasa zuri
   
 8. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jasusi!
  Kubadilisha au kuboresha mikataba mibovu ya madini ambapo Tanzania inapata what CCM ****** call mrahaba wa 3% ambacho hata kiasi wanachochimba hakuna anayekijua and the stupid Mkapa and Mramba walimteua Auditor akahakiki alipwe 1.9% and CCM boasts of having a stable and peaceful country na Vasco Da Gama anatamba kwamba he is the only person to meet Obama and Bush na huwa wanaongea nini? au ushoga!!!

  Kama kubadilisha kwa decree tuchukue 50% like they do it in Botwana ameshindwa anaendelea kuunda tume za kipuuzi kuchunguza what is just like day and night na kuendelea kuchezewa shere na akina Masha.Chenge, Rostam Aziz,Karamagi and many other CCM bastards who have high stakes kwenye madini actually we need a peoples revolution kwani kajeshi ketu kamewekwa mfukoni na Mafisadi
   
 9. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,718
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  mwafrika, ndiyo sababu akitwa vasco da gama...mzee wa kupiga misele bara na baharini
   
 10. K

  Koba JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Hope hii inafanya barric Gold more profitable and hope tunawavuna tax,royalty and fees in percentage,lakini hawa mafia sitashangaa wakisema wamepata hasara ili wasilipe kitu maana accounts wata spin mpaka incompetent serikali yetu itaona giza tuu,kama hotels tuu kama Holiday inn na Sheraton wanaweza kutuchezea game wasilipe tax miaka nenda rudi kwa kutumia loophole ndogo tuu unategemea nini kutoka kwa hawa mafia wenye cartels dunia nzima na wanaijua serikali yetu ilivyo corrupt and incompetent kuliko wanavyojijua wenyewe...hawa wakilipa kodi wamependa tuu
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa. Ninarudi kusoma nilichoandika na nikikuta nimeandika kuwa Tanzania inabidi inabidi kutumia madini kama penacea ya matatizo yake, nitajipeleka mwenyewe mirembe.

  Mkuu wangu Zakumi,

  Yaani badala ya kutumia mwanya huu ambapo circle imetupeleka juu na kupata pesa kama walivyofanya waarabu miaka miwili iliyopita wakati oil iko juu, sisi watanzania tuanze kukaa chini na kujiuliza nini kimepeleka dhahabu juu? Na tukishajua ni nini then what, tuandike vitabu au ndio tuanze kutake advantage ya hiyo bei?

  Hata kama kikiwa kitu cha muda, Tanzania na nchi zote zinazozalisha dhahabu zinaweza kufanya a big time killing. Kumbuka kuwa dhahabu imekuwa inachezea dola 1000 line for almost two years now.

  Hapa nakubaliana nawe mkuu, ndio maana hata mimi nimeongelea miradi iliyopo na sio mikubwa. Duniani nchi zote huwa zinachukua advantage ya bei au demand kwenye rasilimali zake.

  Wazalishaji mafuta hupata pesa nyingi mafuta yakienda juu, wazalishaji steel hupata mapesa kibao kukiwa na ujenzi wa nguvu unaoendana na matukio kama michezo nk.

  Tanzania yaweza pia kufaidika wakati huu ambapo bei iko juu. Wewe unaonaje?
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Maelezo mazuri sana mkuu,

  Lakini swali muhimu bado linabaki, Tanzania inafanya nini wakati huu bei ya dhahabu iko juu?
   
 13. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Indeed, kampuni ambazo zinafaidika ni zilizowekeza ambazo ni za Canada, Australia, South Africa nk yetu ni mrahaba wa 3%. Kwa kila wakia 1 yaani kwa kila $1,100 Tanzania inaambulia $33 tu, kampuni zinabaki na $1,067.00 kwa hiyo all that economics ya kuhodhi dhahabu hai-apply kwetu! Labda tununue kwa hizo kampuni ili kuhodhi kitu ambacho ni ni sawa na nchi nyingine zisozalisha dhahabu. Au Mwananchi na Mermeta zingeukuwa kweli za wazalendo sio mafisadi!! Dhahama hii yote ni mikataba ya Mkapa isiyo na tija kwetu!
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Koba,
  Barrick bado hawalipi taxes na royalty fee. Wanasema kuwa bado wanapata hasara na hawajamaliza kulipia gharama za vifaa vyao na leba. Labda baada ya miaka 25.
  Solution aliyopendekeza Mkreme ndiyo ambayo itatukwamua. Otherwisw tutabak watazamaji dhahabu ikiendelea kunufaisha wengine.
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jasusi,

  Hili la kulipia gharama zao za kuwekeza (ambazo ziko very inflated) ndilo linaimaliza nchi. Ni aibu kuwa nchi zingine zinaweza kujadiliana na wawekezaji kwenye hili lakini Tanzania kucheka cheka tu na matabasamu ndiyo tunauza kwa wawekezaji.
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hawa jamaa watakuwa wanatucheka sana, hakuna tofauti na enzi za mjerumani alipokuja na shanga na mablanket halafu babu zetu wakagawa dhahabu na almas pamoja na ardhi kwa mjerumani
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  labda anaenda kuosha 'macho'
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bei ya dhahabu siku za karibuni imkuwa inachezea dola 1200.
   
 19. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka si tuliaminishwa kwamba Meremeta ni sehemu ya jeshi unategemea kutakuwa na usalama wa kimaadili na ukereketwa wa jeshi kwa nchi? Naamini jibu litakuwa hapana, tuombe mungu.
   
 20. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kambarage alikuwa mchumi mzuri kwani hakuhurusu dhahabu yetu ichimbwe mpaka hapo watu wake watakapozinduka!! He was preseving our gold reserves!! Alipotoweka tu, mafisadi wakawaleta wezi wenzao na kuanza kupora reserves zetu na NDIO MAANA TUMEKUWA OMBAOMBA WAKATI NCHI IMEJAA KILA AINA YA RASILIMALI!!
   
Loading...