Bei na ubora wa pikipiki

Statistics

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2013
Posts
3,762
Reaction score
8,016
Wakuu amani iwe nanyi,

Napenda kuwauliza watalamu wa pikipiki wanieleze toleo lipi litanifaa kwa matumizi ya kwendea kazini kila siku na inapobidi inatumika kama bodaboda.

Nataka kufahamu:
1.Aina yake na matumizi ya mafuta ie. Lita1 ni km ngapi.

2. Upatikanaji wa spea zake mkoani Mwanza na uvumilivu katika barabara za vumbi.

3. Bei ya chombo.

Kazi yangu ni mwalimu, naishi km 15 toka kituo cha kazi.


 
Nunua Boxer 150 au Sanlg ingawaje zipo feki nyingi mafuta lita 1 =35km.
Lita moja utakuwa unatumia kwenda na kurudi ambapo kwa wiki utakuwa unatumia Tsh 10,000 kwa mwezi 40,000 kwa ajili ya mafuta tu bado matengenezo madogo ikiwemo kubadilisha oil.
 
Nunua shanray chombo zimetulia sana hizi na bado hazijachakachuliwa.
 
Asanteni sana.

Nayafanyia kazi maoni yene.

Bei zake VP?
 
naomba kuuliza bei za pikipiki aina ya sanlg 125 na 150 kwa tanga mjini au dar kwa ambae anafahamu naomba anijuze
 
Ukitaka pikipiki imara ambayo hadi kitukuu chako aje kuitumia ni Honda Ace 125

Spear Dar zipo kibao ila cjajua mwanza kama zipo

Warranty ya Engine 2years

Bei ni 2.5mil mpaka 3.0

Lita 1 ya mafuta unaenda km 70

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mm nadhan boxer bm 150 ni nzuri kwako mkuu in terms of ubora wa pikipiki plus ulaji wa mafuta unaweza tembea more than 30km,,,,.......tatizo la boxer ukianza kumpa mtu afanyie boda ndio utapoteza ubora wake na gharama zake ni za juu upande wa utengenezaji ( spea)....ni hivyo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…