BEHIND THE SCENE

thA goD

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
1,941
1,844
BEHIND THE SCENE.

Watu wanapenda kuangalia movie jinsi inavyoleta raha na msisimuko lakini hawajui behind the scene nguvu kubwa kiasi gani ilitumika kukamilisha hiyo scene inayosisimua kwenye movie. Watu wanafurahi kumuona Christian Ronaldo aki-perform vizuri uwanjani na kutupia magori, wanajisikia raha kweli lakini hawajui nyuma ya pazia amefanya vitu gani vilivyosababisha awe na uwezo unaotupa sisi raha kumtazama uwanjani. Watu walikuwa wanafurahia sana kila Folyd Myweather alipokuwa akimshinda adui wake kwa KO lakini hawajui gharama zilizolipwa na Myweather mpaka kufika hatua hiyo. Watu walikuwa wanafurahia sana jinsi Michael Jordan alivyokuwa analeta radha uwanjani lakini hawajui machozi aliyomwaga ili tu awape raha mashabiki wake uwanjani, hawajui kiasi cha usingizi alichojinyima ili tu mashabiki wake wafurahi. Michael Jackson watu walikuwa wanamfurahia sana kiasi kwamba wengine walikuwa wakimuona tu wanazia lakini walichokuwa hawakijui ni kuwa behind the scene ndo imesababisha awe hivyo.

Behind the scene ndiko kunakoandaa magwiji. Behind the scene ndiyo sehemu ambayo ukimkuta Christian Ronaldo au Jay Z au Diamond au Muigizaji yeyote UTAMUONEA HURUMA SANA. Behind the scene ndo sehemu imebeba machozi ya watu. Ndo sehemu watu hawalali ndo sehemu watu wanakubali maumivu makali. Ndo sehemu wanakuandalia kitu bora wewe. Ndo sehemu anapoandaliwa mtu atakayekupa raha wewe ukimuona uwanjani. Behind the scene ndo palipofanya watu wazimie kwa furaha baada ya kumuona Michael Jackson. Behind the scene ndipo mahali ambapo Mayweather anakubali maumivu ili mashabiki wake wafurahi na amshinde adui wake.

Kile kitu unachokifanya wakati wengine hawakuoni ndicho kitakufanya uonekane bora mbele za watu. Yale maumivu ya hiyari unayoyapata wakati wengine wamelala wanakula bata ndiyo yatawafanya hao wanakula bata wakushangilie na kukuona wewe mwamba.UKIONA MTU NI BORA KWENYE KITU FULANI BASI JUA KUWA KUNA KITU ANAFANYA BEHIND THE SCENE. KUNA KITU ANAFANYA WAKATI WENGINE HATUONI.

Ukiona mtu performance yake uwanjani ya dakika 90 imekuwa bora jua kuwa behind the scene ambako wewe haukuona alifanya mazoezi makali zaidi ya dakika hizo 90. Ukiona Diamond anafanya performance ya dakika 30 stejini basi jua kuwa behind the scene aliwekeza siku nyingi za kujiandaa na hizo dakika 30 za stejini. Ukiona Mtu amekuwa bora kwenye professional yake basi jua kuwa behind the scene ameumia sana, amewekeza muda wa kutosha na akili imeumia sana.GWIJI ANAANDALIWA BEHIND THE SCENE WAKATI WENGINE WOTE HAWAONI.

"Jijenge Sirini ukiwa pekeyako, Ili ukaushangaze ulimwengu hadharani". Kumbuka Mazoezi ni sirini, Performance ni Hadharani. UKIWA THE BEST SIRINI THEN UTAKUWA THE BEST HADHARANI!!

Ili uwashangaze na kuwafurahisha watu hadharani ni lazima ukubali kuumia sirini (behind the scene).

Behind the scene ndiko kunakotengeneza washindi. Behind the scene ndiko mafanikio yanakotengenezwa. Behind the scene ndipo Mahali panapotenganisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa.

Waafrika wengi tunatamani Sana Maisha ya wazungu, tunaona Kama wao wamebarikiwa mafanikio, tunatamani wanavyokuja kufanya utalii nchini kwetu. Lakini tusichokijua ni kuwa Behind the scene wanapambana sana na kufanya kazi kwa bidii ndiyo maana wamefanikiwa sana. VITU VIZURI VINATENGENEZWA BEHIND THE SCENE!!

Live Your Dream!!

God Bless My Tanzania
 
Uzi mzuri sana ila kinachosikitisha behind the scene ya huu uzi muandishi kakosa weledi kutokana na ukosefu wa breakfast na lunch.Alafu nikuulize swali hivi nyie watu mnaosemaga waafrika ninyi ni wadhungu au ni watu kutoka wapi.
 
Uzi mzuri sana ila kinachosikitisha behind the scene ya huu uzi muandishi kakosa weledi kutokana na ukosefu wa breakfast na lunch.Alafu nikuulize swali hivi nyie watu mnaosemaga waafrika ninyi ni wadhungu au ni watu kutoka wapi.
wanajiita walatini awoo
 
Wengi hutizama mafanikio bila kuangalia juudi alizotumia
 
Mbona alikiba huja mtaja hapo ila sema sipendi shobo ngoja ni bakiki behind the scene:yooooo
 
Back
Top Bottom