Behind the curtain: September 11

BEHIND THE CURTAIN: SEPTEMBER 11


SEHEMU YA SABA



Siku moja kabla ya Tukio: September 10


(Katika sehemu ya mwisho ya mfululizo wa makala hizi nitaeleza kilichokuwa kinaendelea kwenye "US Intelligence Community" siku moja kabla ya 9/11 lakini kwenye Sehemu hii ya Sita nitaongelea kidogo tu upande wa Atta na wenzake)

Baada ya kuwa mipango yote imekamilika na wamepeana maelekezo kuhusu nini cha kufanya hatimaye ukafika muda wa kupeana jukumu LA mwisho. Nani awe kwenye ndege ipi? Kumbuka kwamba wote waliandaliwa kuwa tayari kwa ajili ya kuhusika kwenye target yeyote atakayopewa, lakini kama ambavyo Osama kupitia KSM alivyoagiza kwamba wengine wote wasijue details kamili mpaka siku ya mwisho.

Sasa, mkakati ulikuwa kwamba wahusika wote wagawanywe kwenye vikundi vinne vyenye watu watano kila kimoja.
Lakini kutokana na Mohammed al-Qahatani kuzuiliwa asiingie Marekani pale uwanja wa ndege hii ikasababisha wawe wahusika 19 tu na kupelekea kikundi kimoja kiwe na watu wanne tu. Hii ilikuja kuwa na athari kama tutakavyoona hapo baadae.

Atta kama kiongozi wa wenzake wote akawagawa wenzake, na kila kikundi alikipa jina kutokana na "code name” ya target waliyokuwa wameipa kjpindi cha mikakati.

Aliwagawanya kama ifuatavyo;

1. Code name: Faculty of Town Planning

"Kitivo" hiki kilikuwa na Mohamed Atta, Abdulaziz al-Omari, Wail al-Shehri, Waleed al-Shehri, Satam al-Suqam.

Rubani na kiongozi wa hiki kitivo alikuwa ni Mohamed Atta.

Target yao ilikuwa ni World Trade Center (North Tower)


2. Code name: Faculty of Town Planning II

"Kitivo" hiki kiliundwa na Marwan al-Shehi, Fayez Banihammad, Mohand al-Shehri, Hamza al-Ghamdi, Ahmed al-Ghamdi.

Rubani na kiongozi wa hiki kitivo alikuwa ni Marwan al-Shehi.

Target yao ilikuwa ni World Trade Center (South Tower)


3. Code name: Faculty of Fine Arts

"Kitivo" hiki kiliundwa na Hani Hanjour, Khalid al-Mihdhar, Majed Moqed, Nawaf al-Hamzi, na Salem al-Hamzi.

Rubani na kiongozi wa hiki kitivo alikuwa ni Hani Hanjour.

Target yak ilikuwa ni The Pentagon

4. Code name: Faculty of Law.

"Kitivo" hiki kiliundwa na Ziad Jarrah, Ahmed al-Haznawi, Ahmed al-Nami na Saeed al-Ghamdi.

(Hiki ndio 'kitivo' ambacho kilikuwa nanupingufu wa mtu mmoja)

Rubani na kiongozi wa kitivo hiki alikuwa ni Ziad Jarrah.

Target yao ilikuwa ni The Whitehouse.



HATIMAYE: SIKU YA 9/11

Kwa wiki nzima ilikuwa inahofiwa kwamba kungeliweza kutokea kimbunga katika pwani ya Kaskazini Mashariki mwa Marekani.
Picha za Satellite zilikuwa zinaonyesha Kujikusanya kwa kimbunga Erin (Hurricane Erin) katika pwani ya New York.
Hii ilipelekea kutolewa kwa tahadhari kwamba kama hali itaendelea hivo hii ikasababisha kusitishwa kwa usafiri wa anga katika maeneo mengi ya masharili mwa Marekani.

Lakini kwa bahati nzuri (ambayo ilikuja kuwa mbaya) kulipokucha siku hii ya Jumanne, September 11 hali ilibadilika sana. Japokuwa Hurricane Erin alikuwa imejikusanya mpaka kufika umbali wa mita 500 kutoka pwani ya New York lakini riponi za kitaamu za utabiri wa hali ya hewa zilithibitisha kuwa kimbunga hicho hakitapiga. Hivyo basi ratiba za usafiri wa anga zikaruhusiwa kama kawaida.


Uzuri huu wa hali ya hewa haukuthibishwa na ripoti za kitaalamu pekee bali pia hata hali ya hewa yenyewe ilishihirisha kuwa mambo yako "shwari" kabisa.

Jiji LA New York siku hii ilikuwa na kiwango cha kati tu, na muonekano wa hali ya hewa angani ilipendeza mno.
Anga kilikuwa blue iliyokolea haswaa (crystalline blue) na hakukuwa na wingu hata tone.
Hali hii upendwa sana na marubani ambao wenyewe huita "severe clear" inayowezesha kufanya uone mbali mpaka kupita upeo wacho (infinite visibility).

Hivyo basi watu waliendelea kufurahia uzuri wa siku hii na kuelekea maofisini kuendelea na shughuli zao.

Kama sehemu nyingine ambavyo shughuli kilikuwa zinaendelea pia ndivyo ilivyokuwa katika moja ya sehemu muhimu zaidi jijini New York, mitaa ya Lower Manhattan ambako kuna maghorofa saba ya kipekee yanaykunda "World Trade Center Complex."

Majengo haya yaliyokaa juu ya eneo lilichukua takribani zaidi ya mita za mraba milioni moja, ambayo yalizinduliwa rasmi mwaka 1973 ikiwa ni ndoto ya David Rockerfeller mjukuu wa mfanyabiasha nguli katika historia ya dunia, Bw. John D. Rockefeller.
David alikuwa amemshirikisha ndugu yake Gavana wa New York kipindi hicho ambaye alikuwa ni mtoto wa Rockefeller na wakafanikiwa kushawishi malaka ya Bandari ya New York (New York Ports Authority) na kwa kushirikiana kwa pamoja wakajenga majengo haya adhimu na ya kipekee ili kuwezesha biashara za kimataifa.

Majengo haya ambayo yalikuwa moja ya "lulu" za taifa la Marekani, katika siku hii yanakadiriwa kuwa yalikuwa na wafanyakazi wapatao 50,000 na pia kama ilivyo siku zote walikuwa wanategemea kupata zaidi ya wageni 200,000 kwa siku hiyo kupita hapo nankuondoka kwa ajili ya kupata huduma mbali mbali.


Pia kwa upande mwingine, kwenye Kaunti ya Arlington, mjini Virginia katika ofisi za Wizara ya Ulinzi ya Marekani (US Department of Defense) shughuli na michakato ya kulilinda taifa la Marekani zilikuwa zinaendelea.

Ofisi hizi za wizara ambazo zipo kwenye jengo la kihistoria la "Pentagon" lililobuniwa kijeshi, kwenye mwezi huu September lilikuwa linaadhimisha miaka 60 tangu lijengwe mwaka 1941.

Jengo la linahesabika moja kati ya majengo makubwa zaidi ya kiofisi ulimwenguni, likiwa limekaa juu ya eneo lenye ukubwa wa takribani mita za mraba 600,000 na likiwa na wafanyakazi wa kijeshi 23,000 na wasaidizi wengine wa kiraia 3,000 ambapo jengo lenyewe linasimama likiwa na ghorofa tano kwenda angani na ghorofa mbili kwenda chini ardhini.

Nako pia shughuli zilikuwa zinaendelea kama kawaida.


Wakati watu wakiendelea na shughuli zao za kila siku na wakifurahia hali nzuri ya hewa ya asubuhi hii, Mohamed Atta na "vitivo" vyake nao walikuwa kwenye viwanja vya ndege mbali mbali wakifanga safari kama abiria wengine.

Kitivo kilichoongozwa na Marwan kilikuwa Logan International Airport, huku kitivo kilichoongozwa na Hani Njour likiwa maeneo ya Dulles, mjini Virginia kwenye uwanja wa ndege was Washington Dulles International Airport.
Kitivo ambacho alikiongoza Ziad Jarrah zilikuwa jimboni New Jersey kwenye uwanja wa ndege was Newark International Airport.

Mohamed Atta mwenye na kitengo chake japokuwa walilenga wakaiteke ndege kwenye uwanja wa ndege wa Logan International Airport, lakini safari yao waliianzia katika wa Portland International Airport.


Soma sehemu ya 8 post inayofuata..
 
BEHIND THE CURTAIN: SEPTEMBER 11


SEHEMU YA NANE


"..usimbugudhi mnyama wakati wa kumchinja, noa kisu chako vyema.."



Sehumu hii ya Saba itakuwa ni mwisho wa upande huu wa kwanza namba tukio lilivyopangwa na kutekelezwa.. Kuanzia kesho tutaanza kuangalia upande wa pili wa masuala yenye utata kuhusu tukil hili (ndio hii nimeita "behind the curtain")

Tuendelee..

Saa 5:40 AM alfajiri, Mohamed Atta na 'kitivo' chake walipanda ndege ya Colgan Air (US Airways Express) flight BE-1900 na kuelekea Boston kwenye uwanja wa ndege wa Logan International Airport.

Walifika Boston majira ya saa 6:45 AM asubuhi.
Akiwa hapo uwanjani alipokea simu kutoka kwa Marwan al-Shehhi, inaaminika kuwa al-Shehhi alikuwa anaconfirm kuwa upande wao nao mchakato ulikuwa unaenda vizuri.

Kama ilivyo kawaida ya uzembe unaotokea kwenye viwanja vya ndege, begi moja la Atta lilisahaulika kupandishwa kwenye ndege.

Siku kadhaa baadae FBI walipokuja kuligundua walikuta vitu kadhaa ndani, ikiwemo vijarida vya namna ya kutumia silaha, vijarida vya namna ya kuendesha ndege, lakini kitu 'interesting' zaidi walikuwa karatasi kadhaa zilizoandikwa kwa mkono na Atta mwenyewe.

Karatasi hizi zimeandikwa kiarabu kwahiyo nimejaribu kutafsiri kwa kiswahili kadiri vile nilivyoweza.

Karatasi ya kwanza imeandikwa;

" weka kiapo cha kifo na huisha upya maazimio yako”

Karatasi ya pili iliandikwa;

"Hakiki silaha yako kabla ya kuondoka. Noa kisu chako sawia na usimbugudhi mnyama wakati wa kumchinja"

Haijajulikana kama maneno haya alikuwa anaandika ili kujipa moyo au yalikuwa ni maelekezo kutoka kwa mtu mwingine katika njia ya fumbo.

Atta akapanda ndege ya American Airlines, Flight 11 na akakaa daraja la Biashara (Business Class) siti namna 8D.

Saa 7:59 ndege ikaruka kuelekea New York.

Dakika kumi na tano baadae ndege ikapoteza mawasiliano na waongozaji ardhini, na inaaminika ni hapa ambapo Atta na wenzake waliiteka na kuwadhibiti wahudumu na abiria.

Dakika kadhaa baadae Air Traffic Control walijaribu kuwasiliana na Flight 11, badala ya kuongea na rubani, wakakutana na sauti ya kiarabu ya Mohamed Atta.


(SIKILIZA HAPA CHINI SAUTI YA MOHAMED ATTA)
\



Wakati huo huo,

Katika uwanja wa ndege wa huo huo wa Logan International Airport "kitivo" kingine kinachoongozwa na Marwan al-Shehhi kiliwasili.

Al-Shehhi na wenzake waliwasili tofauti tofauti kuanzia saa 07:23 AM hadi 07:28 AM.

Baada ya kupanda ndege Fayez alikaa daraja la kwanza siti namna 2A, Al-Shehri nao alikaa daraja la kwanza siti namba 2B.
Marwan mwenyewe alikaa Business Class siti namba 6C pamoja na Ahmed al-Ghamdi aliyekaa siti namba 9D.
Hamza al-Ghadi pia alikaa Business Class siti namba 9C.

Ndege iliruka saa 8:14 AM.

Mpaka kufikia saa 8:37 AM ndege nilikuwa inaruka umbali wa futi 31,000 kutoka ardhini na wakapokea tahadhari kutoka ardhini kwenye kituo cha uongozaji ndege kwamba wajaribu kuwa makini kwasababu kuna ndege nyingine inayopita njia hiyo wamepoteza mawasiliano nao (flight 11 iliyotekwa na Atta na kitivo chake).

Dakika tano baadae yaani saa 8:42 AM Fayez pamoja na al-Shehri wakaingia kwa nguvu kwenye chumba cha marubani.
Papo hapo Ahmed na Hamza wakawakusanya wahudumu na abiria wote nyuma kabisa ya ndege.
Marwana Al-Shehhi akachukua "usukani" kama rubani.

Tofauti na ndege iliyotekwa na Atta pamoja na wenzake ndege hii flight 175 Al-Shehhi hakuzima 'transponder' ya ndege kwahiyo huku chini ardhini walikuwa wanaiona muelekeo wake katika njia.

Kama dakika tano baada ya kuiteka ndege ikaanza kubadili njia na hata waongozaji wa ndege ardhini walipojaribu kuwasiliana nao kwanini wanatoka kwenye njia, hawakupata jibu lolote (mpaka hapa hawakujua kuwa ndege imeshatekwa).

Katika njia mpya ambayo flight 175 iliingia pia nilikuwa na ndege ya kampuni ya Delta Airlines, flight 2315 nayo inapita njia hiyo hiyo.

Ndipo hapa muongozaji wa ndege akamuamuru rubani wa ndege ya Delta a-dive kwenda chini ili kuepuka kuogongana uso kwa uso na flight 175.
Ndege hizi zilikosana kwa mita 90 pekee kugongana.

Baadae tena kidogo flight 175 ikabakia kidogo kugongana na ndege ya shirika la Mid West Express, flight 7 iliyokuwa inatokea Milwaukee kuelekea New York.

Mapaka kufikia hapa huku chini ardhini wakang'amua hii ndege nayo imetekwa.




Upande mwingine katika eneo la Dulles, mjini Virginia napo Hani Hanjour na kitivo chake nao walikuwa kwenye mchakato.

Saa 07:15 AM Khalid al-Mihdhar na Majed Moqed waliwasili kwenye uwanja wa Washington Dulles International Airport.

Saa 7: 29 waliwasili ndugu Nawaf al-Hazmi na Salem al-Hazmi.

Hani Hanjour mwenyewe waliwasili saa 7:35 AM.

Baada ya kupanda ndege (American Airlines, flight 77), Hani alikaa daraja la kwanza mbele kabisa siti namba 1A.

Ndugu wawili Nawaf na Salem walikaa siti namba 5E na 5F kila mmoja.

Majed alikaa siti namba 12A na Khalid alikaa siti namba 12B.

Inakadiriwa kuwa mnamo majira ya saa 8:51 AM takribano kama nusu saa Baada ya ndege kuruka ndipo Hani na wenzake wakawadhibiti abiria na Marubani na kuiteka ndege.

Dakika Tatu baadae, yaani saa 8:54 AM ndege ikaanza kutoka kwenye njia yake badala ya kufuata njia kuelekea Los Angels, ikageza kwenda Washington.

Dakika mbili baadae, saa 8:56 AM 'transponder' ya ndege ikazimwa na Hani Hanjour akaiweka ndege kwenye "Auto Pilot" kuelekea Washington.



Huko New Jersey nako Ziad Jarrah na kitivo chake hawakuwa nyuma, nao walikuwa wanenda sawa kabisa na ratiba ya mchakato.

Kitivo kilianza kuwasili mnamo majira ya saa 7:03 AM na wa kwanza kuwasili alikuwa ni Ghamdi.

Saa 07:24 AM aliwasili al-Nami. Na dakika moja baadae aliwasili Haznawi.

Ziad Jarrah mwenyewe aliwasili saa 07:39 na kabla ya kupanda ndege akampigia simu mchuma wake yule aliye Hamburg Ujerumani (Aysel Sengun).
Katika maongezi yao kila Baada ya sentensi Jarrah alikuwa anarudia tena na tena maneno "I love you, everything will be OK"!!

Wakapanda ndege na ndege ya shirika la United Airlines, flight 93 na iliruka saa 08:42 AM.
Muda huu ulikuwa ni takribani dakika nne kabla ndege ya Atta kufikia target yake ya North Tower, na ni muda huu huu ambapo huko angani flight 175 ulikuwa inatekwa na al-Shehhi na kitivo chake.


Kutokana na mfululizo wa Waongoza ndege ardhini kupoteza mawasiliano na ndege kadhaa zilizopo angani, hivyo basi muongoza ndege (dispatcher) wa shirika la United Airlines, Bw. Ed Ballinger akaanza kuwasiliana na marubani wa ndege zote za shirika lao waliopo angani.
Kutokana na kusimamia ndege nyingi mlimchukua muda mrefu kuwasiliana na marubani wengine mpaka kuwafikia marubani wa flight 93.
Baada kupata mawasiliano saa 9:23 AM nao akawapa tahadhari kwamba wasiruhusu mtu yeyote asiyehusika kuingia kwenye " cockpit".

Saa 9:26 AM rubani Jason Dahl alijubu kwa kutumia ujumbe mfupi kwamba kila kitu kipo "OK"!!

Rekodi zinaonyesha kuwa saa 9:27 AM sekunde ya 25 walipokea simu ya kawaida (routine) kutoka waongozaji ndege ardhini (Air Traffic Control).

Lakini ghafla dakika moja baadae, yaani saa 9:28 AM sekunde ya 17 rubani msaidizi Bw. LeRoy Homer alipiga simu ya kuomba msaada wa dharura (Mayday) akiwa amepanika na sauti imejaa hofu kubwa.

Ziad Jarrah na kitivo chake, tayari walikuwa wameidhibiti ndege.

(SIKILIZA HAPA CHINI SAUTI YA RUBANI LeRoy Homer AKIOMBA MSAADA WA DHARURA (MAYDAY))



Itaendelea Ijumaa…..
 
SEHEMU YA SABA, POST # 692

SEHEMU YA NANE, POST 693


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein
 
Nimejaribu nipandishe sauti ya Atta na Rubani kama nilivyofanya huko whatsapp ila naona inagoma.. so naomba niweke ‘transcript’..



Hii ulikuwa ni saa 8:33 AM sekunde ya 24

Mohammed Atta Anasikika akisema;

"..we have some planes. Just stay quite and you will be OK. We are returning to the airport..... Nobody move, everything will be OK! If you try make any move you will endanger yourself and the airplane. Just stay quite."

"...nobody move please. We are going back to the airport. Don't try to make any stupid moves.."



Rubani LeRoy Homer anasikia akipiga kelele;

"Mayday, Mayday, Mayday!! Get out of here.. May day, mayday! Get out of here Mayday!!"

Alafu anakuwa kimya kwa sekunde tano na kisha kurudia tena Kuita "Mayday"!

Mwishoni muhudumu wa uongozaji ndege kutoka Cleveland Air traffic Control anamuuliza " somebody call Cleveland??" lakini hapati majibu yoyote na simu hiyo ya dharura inakatwa.
 
Nimejaribu nipandishe sauti ya Atta na Rubani kama nilivyofanya huko whatsapp ila naona inagoma.. so naomba niweke ‘transcript’..



Hii ulikuwa ni saa 8:33 AM sekunde ya 24

Mohammed Atta Anasikika akisema;

"..we have some planes. Just stay quite and you will be OK. We are returning to the airport..... Nobody move, everything will be OK! If you try make any move you will endanger yourself and the airplane. Just stay quite."

"...nobody move please. We are going back to the airport. Don't try to make any stupid moves.."



Rubani LeRoy Homer anasikia akipiga kelele;

"Mayday, Mayday, Mayday!! Get out of here.. May day, mayday! Get out of here Mayday!!"

Alafu anakuwa kimya kwa sekunde tano na kisha kurudia tena Kuita "Mayday"!

Mwishoni muhudumu wa uongozaji ndege kutoka Cleveland Air traffic Control anamuuliza " somebody call Cleveland??" lakini hapati majibu yoyote na simu hiyo ya dharura inakatwa.
Duuh balaaaaa
 
Back
Top Bottom