Beginner | Noob & Pro: Fl Studio Music Production

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
700
Gwala kwa wana Jf, nawapa salamu wadau wa mziki.

Lengo la uzi huu ni kuwakutanisha wadau, wapenzi na waandaaji wa Muziki kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ambao wanatumia DAW-Digital Audio Workstation ya Fl Studio ambayo hapo awali ilikuwa ikifahamika kwa jina la Fruity Loops.

Hapa kutakuwa na sharing of ideas, critics ambazo ni constructive kwa kazi ambazo zitakuwa zikiwekwa na members mbalimbali.

Unaweza ku-share Tips za Muziki, Plugins (ambazo unatumia/ulitumia) ambazo unahisi zitawafaa watu watakaokuwa wakiomba msaada kwenye suala zima la Uandaaji wa Muziki.

Tunawakaribisha wataalamu wa Muziki wote ambao wao wanaufahamu mziki kiundani (hapa nawahusisha wale watu waliosoma Muziki kwa manota na wengine). Mimi si muandaaji wa Muziki niliyekamilika na nadhani hata jina la muandaaji wa Muziki hali-fit kwangu kwani huwa ninapiga tu Muziki basic kulingana na miondoko ya beat na Tempo inavyoenda.

Kiufupi naweza kujiita beat maker 😂😂😂😂.

Kwa vipindi mbalimbali nimetumia Fl Studio, na Fl Studio kwa mara ya kwanza niliitumia V12.0.0 na mpaka sasa nipo kwenye Fl Studio V20.7.2.

Napenda sana kutengeneza beats za Afrobeats na Afropop ingawa kwa muda sasa baada ya kuikacha Fl Studio nimekuwa nikijikuta nikitengeneza beats ambazo hata mimi nashindwa kuzi-categorise ila ndo hivyo huwa napenda nikiwa Free niguse japo kidogo.

Nita-share kazi yangu moja kwenye Reply ya kwanza.

SEE YOU THERE
 
Afrobeat| Tempo [100]
Hii beat ni RAW (Haina Mixing, Leveling wala Mastering yoyote) Nime-add soundgoodizer kuongeza volume ya beat lote.

🚨Tumia earphone au Headphone, kuna instruments nyingi ambazo waves zake zina HF (Frequency kubwa)
 
Attachments

  • fuhrer.mp3
    5.9 MB
Nimeanza safari ya kushangaza katika ulimwengu wa muziki. Kutokea kwenye Adobe Master Collection kwenda FL Studio kumenifungulia mlango wa kujionea kipaji changu cha kweli katika mziki. Kila wakati ninapogusa vyombo vya FL Studio, mawazo yanakataa kulala, na hata kula inakuwa jambo la pili. Ni kama vile nimepata wito wangu wa kweli.

Safari hii imejaa changamoto, lakini kila changamoto imenifundisha kitu kipya. Kutoka kutokuwa na uhakika na FL Studio mwanzoni hadi sasa, nimekuwa mtaalamu. Kupiga beat sio tu kazi kwangu bali ni sanaa inayonivutia. Ni furaha isiyo na kifani kubuni melody, na sasa, napojiendeleza, lengo langu ni kuunda melody kama wataalamu wa Afro beat.

Hakuna kitu kizuri kama kujua kwamba kuna mwelekeo na malengo. Kwa sasa, natamani kuchimba zaidi kwenye sanaa ya kutengeneza melody kama wataalamu. Najua itahitaji muda na juhudi, lakini niko tayari kuchukua hatua hizo. Kusikiliza kazi za wataalamu, kujifunza kutoka kwao, na kushirikiana na wenzangu kwenye tasnia kutanisaidia kufikia lengo langu.

Nina imani kubwa katika uwezo wangu, na ninafurahi kwa kila hatua ninayopiga. Studio ni ndoto yangu, na najua kwa kujituma zaidi, nitaweza kutengeneza hits zinazosikika kote. Mimi ni mwanzilishi wa ngoma zangu, na safari hii inakuwa bora kila siku. Nitaendelea kutafuta mafunzo na fursa zaidi, na nitajivunia kila mafanikio kidogo ninayoyapata.
 
Cha kukushauri mtz ukimuelekeza jambo kama hilo kwa kina unaweza kujitoduction peoples
 
Karibu uweke beats zako, nasubiri mchango wako
 
images.jpeg
 
Umeandika utadhani ume translate toka English kuja Kiswahili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom