Simulizi: Before I die

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,168
BEFORE I DIE

SEHEMU YA KWANZA


Ni Edson Benard pekee ambaye hakuungana na familia yao jioni hii ya katika mapokezi ya mdogo wake Innocent anayerejea nyumbani baada ya kuhitimu shahada ya kwanza ya uchumi na fedha katika chuo kikuu cha Columbia jijini New york Marekani.
Mzee Vincent Benard akiwa ameongozana na mkewe Bi Gloria Benard pamoja na binti yao Sarah walijawa na nyuso za furaha kwa kumpokea tena mtoto wao kipenzi Innocent ambaye ni mtoto wa tatu na wa mwisho kuzaliwa kati ya watoto watatu ambao bwana na bi Vincent Bernard walijaliwa kuwapata.Mtoto wa kwanza kuzaliwa alikuwa ni Edson ambaye kwa sasa ni mfanya kazi katika shirika moja lisilokuwa la kiserikali linaloshughulika na masuala ya elimu ya ukimwi kwa umma.Wa pili ni Sarah ambaye ni mwandishi wa habari katika televisheni ya Taifa na wa mwisho ni Innocent ambaye leo hii anarejea nyumbani akitokea Marekani baada ya kuhitimu shahada yake ya kwanza ya uchumi na fedha katika chuo kikuu cha Columbia.Familia hii ni moja ya familia ambazo tunaweza kusema kuwa ni familia bora zenye kujiweza kiuchumi.Mzee Vincent alimiliki kiwanda cha kutengeneza magodoro na kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa. vile vile alikuwa na hisa za kutosha katika viwanda kadhaa kikiwemo kiwanda cha sigara na saruji.
Ni vigumu kuelezea furaha waliyoipata baada ya Innocent kutokeza katika sehemu ya kusubiria wageni.Walimkumbatia kwa furaha na kumkaribisha tena nyumbani.Innocent au Inno kama walivyozoea kumwita hakukaukiwa tabasamu kama ilivyo kawaida yake.Ilikuwa ni furaha ilioje kuwasili tena nyumbani baada ya miaka kadhaa ya kuwa mbali na nyumbani.

“Karibu tena nyumbani mwanangu” Mzee Vincent akasema
“Ahsante baba nimeshakaribia.Mbona kaka Edson simuoni hapa? Nilifikiri mtakuwa naye.” Inno akasema
“Edson amepata safari ya dharura kwenda mikoani katika shughuli zao,ila alipenda sana kuungana nasi kuja kukupokea.” mama yake akasema
Saraha akamsaidia Inno kusukuma mabegi yake hadi katika gari lao halafu wote wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani.

“Ama kweli Marekani kuzuri.Inno umebadilika.Umependeza sana mdogo wangu” Sarah akasema huku akicheka kwa furaha.Innocent kijana asiyekaukiwa tabasamu akajibu.
“Na wewe Sarah bado hujaacha utani wako tu.”
“Siongei utani.Ni kweli kabisa umependeza sana mdogo wangu.Inaonekana hali ya huko imekukubali.Halafu mimi nikafikiri utakuja na wifi mzungu”
Wote mle ndani ya gari wakaangua kicheko kikubwa kwa utani ule wa Sara.
“Huyo mzungu nitampeleka wapi? Unafikiri mzee Vincent atakubali mwanae aoe mzungu na kuacha wasichana warembo wenye maadili ya kiafrika? Thubutu! “ Inno akaendeleza utani na kumfanya mzee Vincent acheke kwa nguvu.

“Ndiyo maana nakupenda mwanangu.Hapo umenena.Sioni sababu ya kuacha mamilioni ya mabinti warembo wa kiafrika wenye sifa na maadili ya kiafrika na kwenda kuoa mtu wa mbali ambaye hayuko tayari kufuata mila na desturi zetu.Hebu muangalieni mama yenu jinsi alivyo mzuri,ule uzuri asilia wa kiafrika.Ana umbo la mwanamke wa kiafrika.Sura pana yenye weusi wa kung’aa,macho makubwa yenye kurembua,miguu ambayo nyie vijana mnaiita ya bia” Kicheko kikubwa kikaanguka ndani ya gari.
“lakini baba hizi ni zama za utandawazi.Haijalishi ni mtu wa namna gani unahitaji kumuoa au kuolewa naye .Kitu cha msingi muwe mnapendana kwa dhati” Sarah akasema

“Sikatai mwanangu.Hayo unayosema ni ya kweli.Lakini pamoja na hayo ni lazima tuendelee kulinda mila na desturi zetu sisi kama waafrika.Iwapo utapata bwana wa kizungu ni wazi hautauthamini utamaduni wako tena.Malezi,makuzi ya wenzetu ni tofauti na sisi.Hebu angalia kwa sasa sijui wanashinikiza dunia nzima ihalalishe hivi vitendo vichafu visivyompendeza Mungu ambavyo ni kinyume na maadili yetu ya kiafrika.Siwakatazi na wala siwaingilii katika masuala yenu ya mahusiano lakini nisingependa mwanangu yeyote aoe au kuolewa na mtu wa mataifa ya kigeni na hasa huko Ulaya na marekani.Nitafurahi sana kama wanangu wote wataoa na kuolewa humu humu ndani ya nchi yao.”
Maongezi yalikuwa matamu na hatimaye wakajikuta wamewasili nyumbani.Giza tayari likwishatanda.Mabegi ya Innocent yakashushwa na kupelekwa ndani halafu kwa furaha kubwa Inno akakaribishwa ndani.
“Karibu nyumbani mwanangu” akasema mama yake.
“Nimeshakaribia mama.Hivi yule mbwa wangu Pura bado yupo? Inno akauliza
“Mbwa wako bado yuko tena anazidi kunawiri siku hizi.”
“Mama siwezi kuingia ndani hadi kwanza nikamsalimu Pura.Nimemnunulia sabuni nzuri ya kuogea.”
“ahahahahaaaa..mambo ya wazungu hayo yaani hadi mbwa unamnunulia sabuni ya kuogea! “ mama yake akasema huku akicheka.
“mama nampenda sana mbwa wangu ndiyo maana nikaona ni bora naye nimletee zawadi”
Innocent akaelekea katika banda la kufugia mbwa anakokaa mbwa wake ampendaye sana Pura.Japokuwa ilipita miaka takribani sita lakini mara moja Pura alimfahamu Inno akamchangamkia na kumrukia kwa furaha.Baada ya kuhakikisha mbwa wake yuko salama na mwenye afya njema akaufunga mlango na kurudi ndani.
“Shikamoo kaka” Innocent akasalimiwa na dada mmoja mwembamba mrefu wastani aliyejifunga kitambaa kichwani aliyekuwa amesimama hapo sebuleni akiwa na sinia la kubebea vinywaji alivyokuwa amewapelekea Bwana na Bi Benard.
“Maharaba dada yangu,habari za hapa? Innocent akajibu huku akitabasamu na kumuangalia yule dada ambaye hakumuacha pale nyumbani wakati anaondoka kuelekea Marekani kwa masomo.

“Habari za hapa nzuri,pole na safari”
“Nimeshapoa” Innocent akajibu huku akiunyoosha mkono ili asalimiane na yule dada.

“wewe Grace hebu haraka nenda kamuandalie Innocent maji ya kuoga halafu mwambie na sabrina muanze kuandaa meza haraka .” Ilikuwa ni sauti ya amri ya mama yake Inno
Binti yule akaondoka haraka baada ya kupokea amri ile.Innocent akamgeukia mama yake na kumtazama kwa mshangao.
“Innocent , wakati unaondoka hapa nyumbani kwenda masomoni hukuacha msichana wa kazi hapa ndani lakini kwa sasa kuna wasichana wawili tunaishi nao.Mmoja ni huyu Grace ambaye ametoka hapa sasa hivi ambaye ni binti tuliyemchukua atusaidie kazi za hapa nyumbani kama unavyojua baada ya Sarah kuanza kazi katika televisheni ya Taifa mama yako alizidiwa sana na kazi.Mwingine anaitwa Sabrina, yeye alikuwa ni mtoto wa Michael yule mfanyakazi wetu wa shambani ambaye nilikutaarifu katika simu kuwa alifariki dunia.Kwa kuwa niliishi naye vizuri sana yule bwana nikaona ni bora nimchukue binti yake wa pekee niishi naye hapa kwa sababu alihitaji uangalizi maalum kwani ni mlemavu wa ngozi yaani albino”Mzee Vincent akamfahamisha mwanae Inno.

“Ouh ! nafurahi kusikia hivyo baba.Unajua ni vizuri kuwa na familia kubwa .Familia inapokuwa na mchanganyiko mkubwa wa watu basi inakuwa na furaha zaidi.” Innocent akasema
Mrs Benard alikuwa amefura kwa hasira wakati mumewe akimfahamisha Innocent kuhusu wasichana wawili wanaoishi nao mle ndani.

“Nakwambia baba Eddy waondoe hawa wasichana humu mwangu,sitaki mwanangu akaribiane nao kabisa.Usipowatoa mimi nitawaondoa kwa nguvu” Akasema kwa hasira

“kwani mama kuna tatizo gani kuishi nao katika jumba hili kubwa? Innocent akauliza

“Baba yako ametuletea balaa humu ndani.Kaenda kamleta yule albino humu ndani.Hajui kama watu wale wana mikosi.halafu huyu mwingine ni muathirika wa ukimwi .Huoni kama nyumba yetu imeingiliwa? Mwanangu naomba ukae mbali nao kabisa hawa wasichana.”
Innocent akabaki mdomo wazi akishangaa

“mama ! kumbe hilo ndilo tatizo ? Mimi nilidhani labda ni tatizo kubwa lakini kama ni hilo tu basi hakuna tatizo lolote katika kuishi nao.Mzee Michael alikuwa ni kama ndugu yetu aliyekuwa akitulimia na kutulindia shamba letu kwa hiyo kukaa na binti yake hapa tena ambaye anahitaji uangalizi maalum ni jambo la busara sana.Tunahitaji kumuenzi yule mzee.Tunahitaji kumtunza mtoto wake bila ubaguzi wowote.Japokuwa ametoka katika familia ya kimasikini tofauti na sisi lakini hakuna sababu yoyote ya kumtenga.na hata huyu Grace ambaye unadai ameathirika na ugonjwa wa ukimwi,hatuna budi kumtunza na kumlea.Kuathirika na ugonjwa huu si sababu ya kunyanyapaliwa au kutengwa.Mama naomba tuwaonyeshe upendo wajisikie kama ni sehemu ya familia hii”
Innocent akasema na mara Grace akaingia mle sebuleni
“kaka maji ya kuoga tayari.”

“Ahsante Grace” Innocent akajibu huku akitabasamu na kumfanya mama yake anune.

“Nenda kaoge mwanangu tuje tujumuike pamoja kwa chakula cha usiku tufurahie kurejea kwako” mzee Vincent akasema
Innocent akaelekea chumbani kwake akabadili nguo na kwenda kuoga .Kisha oga akarudi tena sebuleni kujumuika na familia yake kwa chakula cha usiku.
“Mwanangu nimekuandalia sherehe kubwa ya kukukaribisha nyumbani jumamosi ijayo..”mzee Vincent akasema
“Nashukuru sana baba.Lakini sioni kama kuna umuhimu wa kufanya sherehe yoyote kwa ajili ya kurudi nyumbani na kutumia fedha nyingi wakati kuna maelfu ya watu wanazihitaji fedha hizo kwa ajili ya elimu ya watoto wao,wengine matibabu n.k.”
Huku akitabasamu Mzee Vincent akajibu
“mwanangu nalifahamu hilo.nafahamu una moyo wa kusaidia wengine toka ukiwa mdogo.lakini kuna kitu ninataka kukifanya siku hiyo ya jumamosi na ndiyo maana nikaamua kuandaa sherehe hiyo .”

“hakuna shida baba,nilikuwa najaribu tu kukumbusha kwamba tunapotumia fedha kwa mambo yasiyo ya lazima tukumbuke kuna watu masikini wanasumbuka usiku na mchana kutafuta fedha kama hizo kwa ajili ya mahitaji yao muhimu.Halafu mbona akina Grace siwaoni hapa?
Sarah na mama yake wakatazamana halafu Sarah akajibu

“Wana chakula chao jikoni”

“Ina maana wao hawajumuiki nasi hapa mezani? Innocent akauliza
“wao wanakula jikoni” mama yake akajibu
“No ! That’s not fair.Waiteni wajumuike nasi hapa,nao ni sehemu ya familia.” Innocent akasisitiza

“Waende wapi? Wao chakula chao kiko jikoni.Kwani kuna tatizo gani? Mama yake akasema kwa sauti yenye ukali kidogo ndani yake.
Innocent hakujibu kitu akachukua chakula katika sahani yake akainuka na kuelekea jikoni.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Mwanangu nimekuandalia sherehe kubwa ya kukukaribisha nyumbani jumamosi ijayo..”mzee Vincent akasema
“Nashukuru sana baba.Lakini sioni kama kuna umuhimu wa kufanya sherehe yoyote kwa ajili ya kurudi nyumbani na kutumia fedha nyingi wakati kuna maelfu ya watu wanazihitaji fedha hizo kwa ajili ya elimu ya watoto wao,wengine matibabu n.k.”
Huku akitabasamu Mzee Vincent akajibu
“mwanangu nalifahamu hilo.nafahamu una moyo wa kusaidia wengine toka ukiwa mdogo.lakini kuna kitu ninataka kukifanya siku hiyo ya jumamosi na ndiyo maana nikaamua kuandaa sherehe hiyo .”
“hakuna shida baba,nilikuwa najaribu tu kukumbusha kwamba tunapotumia fedha kwa mambo yasiyo ya lazima tukumbuke kuna watu masikini wanasumbuka usiku na mchana kutafuta fedha kama hizo kwa ajili ya mahitaji yao muhimu.Halafu mbona akina Grace siwaoni hapa?
Sarah na mama yake wakatazamana halafu Sarah akajibu
“Wana chakula chao jikoni”

“Ina maana wao hawajumuiki nasi hapa mezani? Innocent akauliza
“wao wanakula jikoni” mama yake akajibu
“No ! That’s not fair.Waiteni wajumuike nasi hapa,nao ni sehemu ya familia.” Innocent akasisitiza
“Waende wapi? Wao chakula chao kiko jikoni.Kwani kuna tatizo gani? Mama yake akasema kwa sauti yenye ukali kidogo ndani yake.
Innocent hakujibu kitu akachukua chakula katika sahani yake akainuka na kuelekea jikoni.


ENDELEA…………………………….


“jamani .mbona hamji kujumuika nasi kule mezani?” Innocent akawauliza grace na Grace waliokuwa wamekaa wakipata chakula jikoni.
“Sisi chakula chetu huwa kinabaki huku jikoni.Haturuhusiwi kukaa mezani na mama” Grace akajibu.
Innocent akatabasamu kama kawaida yake akamsogelea Sabrina na kumpa mkono.
“Naitwa Innocent.Sidhani kama unanikumbuka kwa sababu mara ya mwisho kukuona ulikuwa mdogo nadhani ulikuwa darasa la nne au la tano.Pole sana kwa msiba wa mzee .Mzee Michael nilikuwa namchukulia kama baba yangu na nilikuwa naelewana naye sana.” Innocent akasema na kumfanya Sabrina atokwe na machozi huku akimshangaa .Toka amekuja katika nyumba ile hakuna hata siku moja ambayo ameweza kuongea na mtu wa familia hii zaidi ya mzee Vincent kwa upole na heshima ya ajabu namna hii.Siku zote imekuwa ni kugombezwa na kufokewa.

“nyamaza kulia Sabrina.Ni kazi ya Mungu ambayo sisi wanadamu hatuna budi kuikubali.” Innocent akambembeleza.Sabrina hakuwa akilia kwa sababu ya kukumbushwa kifo cha baba yake bali kwa jinsi Innocent alivyomsalimia na kuongea naye kwa upole na ucheshi huku macho na sauti yake vikionyesha upendo wa hali ya juu.
Sabrina akafuta machozi na kumtazama Inno usoni.
“Ahsante sana kaka Innocent.Pole na safari”

“Nimekwisha poa.Nashukuru Mungu baada ya miaka sita sasa nimerudi nyumbani.Nadhani tutaendelea kuwa wote hapa kwa sababu sifikirii tena kwenda kusoma nje ya nchi labda hapo baadae sana.”

“kaka Innocent kuna kitu umekuja kuchukua huku jikoni? Grace akauliza baada ya kuona Inno hakuwa na dalili za kuondoka mle jikoni.
“hapana Grace nimekuja huku tule wote. mimi sijazoea kukaa mezani na kula bila maongezi .Kule mezani tunakula kimya kimya na hata mkiongea ni kuhusu maisha binafsi.Mimi nataka kula kwa uhuru halafu nahisi chakula cha huku ni kitamu kuliko hata cha kule mezani” Innocent akasema na kuwafanya Grace na grace waangue kicheko kinachosikika hadi sebuleni na kumfanya Mrs Benard kutoka haraka na kuja kuangalia.Alipoingia jikoni akakuta Innocent amekaa na akina Grace wakiongea na kucheka kwa furaha.Mara tu alipoingia maongezi na vicheko vikakoma.Mrs benard akaukunja uso na kusonya kwa hasira halafu akaondoka.
“Msijali sana,mama yangu ndivyo alivyo.Jitahidini kumzoea na kumvumilia” Innocent akasema na kuwafanya grace na Grace kutabasamu.
“I have to change things here.Ni lazima niwasaidie wasichana hawa masikini ili wawe na maisha mazuri na yenye furaha kama tulivyo sisi.Najua wana wakati mgumu sana kuishi na mama yangu.Ninamfahamu mama yangu vizuri.Hana roho nzuri.Nitafanya kila niwezalo kuwasaidia.
Baada ya kula chakula wakaendelea na maongezi yaliyotawaliwa na utani na vicheko.Laiti kama ungewakuta wakiongea ungedhani labda ni watu waliokaa pamoja zaidi ya miaka kumi kumbe ni leo tu wameonana.Wakati wakiendelea na maongezi yao jikoni ghafla Sarah akaingia.

“ Grace mnacheka huku wakati kule tumemaliza kula chakula.Hebu nenda kaondoe vyombo haraka .Na wewe Sabrina kwa nini usianze kuosha vyombo .Inuka mara moja uanze kazi.” Sarah akasema kwa ukali.

“Sawa dada Sarah” Grace akasema na kuondoka haraka kuelekea sebuleni kukusanya vyombo walivyolia chakula.
Baada ya Grace na Sabrina kuondoka mle jikoni Sarah akamuangalia Innocent kwa macho makali .

“Vipi kuna tatizo? Mbona unaniangalia hivyo? Innocent akauliza

“Yes lipo tatizo.Hebu acha uzungu uzungu wako uliotoka nao Marekani.Hawa wasichana huwa hawachangamani na sisi hata siku moja.Tena usijaribu kuwaozea”
Huku akicheka kichini chini Innocent akasema
“Sister mnavyofanya si vizuri.Hawa ni binadamu na isitoshe wana matatizo.Tunatakiwa tuishi nao kwa upendo mkubwa.Ikiwa tutaanza kuwanyanyapaa haitapendeza” Mara Grace akaingia mle jikoni akiwa na sinia la vyombo.Innocent akamshika mkono dada yake wakatoka.


* * * *



Mlio wa saa ya ukutani ndio ulimstua toka katika usingizi mzito.Akafunua shuka na kuangalia saa.Ilikuwa ni saa mbili za asubuhi.
“Leo nimelala usingizi ambao sijaulala kwa miaka kadhaa.Kweli nyumbani ni nyumbani.” Akawaza Innocent huku akijinyoosha nyoosha pale kitandani.
“Ngoja niendelee kulala kidogo mpaka saa tatu ndipo niamke. No ! I have to wash Pura” haraka haraka akainuka akavaa na kutoka nje.Kabla hajafunga mlango akasikia kelele za kufoka.Mama yake alikuwa akifoka maeneo ya jikoni.Taratibu akapiga hatua na kuelekea huko.
“Nimekwambia mwaka huu ni lazima utaondoka tu.Sitaki uiambukize familia yangu maradhi yako.Na kama baba Edson hataki kukuondoa humu ndani nitahama na kumuachia nyumba.Siwezi kuishi na mwathirika wa ukimwi ndani mwangu” mama yake Innocent alikuwa akimfokea Grace.Maneno yale yakamchoma sana Inno na hasa pale alipomuona Grace ameinama chini akilia na pembeni yake kukiwa na sahani ya udongo iliyovunjika.Huruma ikamwingia .
“Tena naomba usinililie hapa.Inuka sasa hivi ukaendelee na kazi.Na sahani yangu uliyoivunja utailipa” Mrs Benard akaendelea kufoka kwa nguvu.

“mama its enough” Innocent akaingilia kati.Mama yake akasimama na kumuangalia kwa macho makali.
“Mama kwa nini unawafanya hivi ? this isn’t right.Hawa ni wenzetu na ni lazima tuwapende na kuwaona ni sehemu ya familia yetu.” Innocent akasema huku akiinama na kuushika mkono wa Grace akamwinua
“Inuka Grace.” Akamshika mkono na kumpeleka chumbani kwake.
“Hebu pumzika kwanza humu chumbani kwako hadi baadae.halafu usilie sana utaumwa na kichwa.Mama yangu ndivyo alivyo.Unatakiwa uwe mvumilivu sana kuishi naye”

“kaka Innocent mimi nimevumilia lakini sasa naona nimeshindwa.Mama kila siku ananitukana kupita maelezo.Au kwa vile sina wazazi? Grace akasema kwa uchungu huku akilia.
“hapana usiseme hivyo Grace.Namfahamu mama yangu ni mkorofi sana.Nitaongea na baba ili tuone tutafanya nini kuwasaidia wewe na Sabrina”
“Kaka Innocent kwa mateso ninayoyapata katika hii nyumba ni bora niende nikateseke mtaani.Ninachoomba niombee nauli kwa baba ili niondoke hapa na kwenda kokote kule nikaishi.”
Grace akaendelea kulalamika huku uso wake umejaa machozi.Aliongea toka moyoni.Ni wazi alikuwa ameumia mno na maneno aliyoambiwa na Mrs benard.
“hapana usiseme hivyo Grace.Hautaenda sehemu yoyote ile,wewe utaishi katika nyumba hii miaka yote.Jihesabu ni mmoja kati ya wana familia hii.Naomba futa kabisa mawazo ya kuondoka katika nyumba hii.Kama walikuwa wakiwanyanyasa na kuwadharau ni wakati sipo.lakini kwa sasa hakuna mtu atakayethubutu kufanya hivyo tena nikiwa hapa nyumbani.Pumzika Grace tutaongea baadae”
Innocent akatoka mle chumbani kwa Grace na mara akakutana na mama yake akiwa amefura hasira.
“Naona sasa wamepata mwokozi wao” akasema Mrs Benard kwa dhihaka.
“Mama naomba niwe wazi.Mnavyowatendea hawa wasichana si vizuri.”
Mama yake hakujibu kitu akaondoka zake.Innocent akelekea katika banda anamolala mbwa wake Pura akamtoa na kumuogesha halafu akarudi ndani akaoga akapata chai na kuamua kwenda kupumzika bustanini..Akiwa pale bustanini mara Grace akatokea.

“Ouh Grace karibu”
“kaka Innocent samahani kwa kukusumbua.Nimekuja kukuuliza kama una nguo za kufua nikakufulie.”
Huku akitabasamu ,Inno akajibu.

“Grace nashukuru lakini nitazifua mwenyewe.Tafadhali pata muda wa kupumzika”
“Usijali kaka Innocent.Kama zipo nipe nikufulie kwani mama alisema tuchukue nguo zako tufue pia”
“Ina maana hata Sarah huwa mnafua nguo zake? Inno akauliza
“Ndiyo.Hata nguo za dada Sarah pia huwa tunafua.”
Innocent akakaa kimya halafu akasema.
“Grace nenda tu kapumzike.Nina nguo chache lakini nitazifua kesho mimi mwenyewe”
Grace akaondoka na kumwacha Innocent peke yake bustanini.
“Wasichana hawa wanatumikishwa namna hii kiasi kwamba hawana hata muda wa kupumzika na bado wanaendelea kunyanyaswa na kubaguliwa.I must stop this”



* * * *



Ni siku ya nne tangu Innocent arudi toka Marekani .Siku hii ya Jumamosi baba yake alikuwa amemuahidi kumfanyia sherehe ya kumkaribisha tena nyumbani.Ni sherehe iliyoandaliwa kwa siri japokuwa yeye Innocent alidokezwa kuwa itakuwa ni sherehe ndogo tu yenye kujumuisha watu wachache.
Saa kumi na mbili za jioni akiwa ndani ya suti nzuri nyeusi akaongozana na baba na mama yake pamoja na dada yake Sarah wakaingia garini na kuondoka kuelekea mahala inakofanyikia sherehe.
Lamona palace ni ukumbi mkubwa na wa kisasa kwa ajili ya semina hafla na sherehe mbali mbali.Ni katika ukumbi huu sherehe ya kumkaribisha nyumbani Innocent inafanyikia.Tayari wageni waalikwa wamekwisha wasili na waliokuwa wakisubiriwa ni Mr benard na familia yake.Mara tu walipoingia ukumbini ukumbi wote ukalipuka kwa makofi na vigere gere.Innocent akapatwa na mshangao mkubwa.Hakutegemea kama sherehe ya kukaribishwa kwake nyumbani ingekuwa kubwa namna ile.alitegemea sherehe ndogo yenye watu wachache lakini kwa umati alioukuta mle ukumbini akasimama na kushika mdomo wake kwa mshangao.Alihisi kuishiwa nguvu .Huku akitabasamu Mr Benard akamshika mkono na kumuongoza kuelekea meza kuu iliyoandaliwa maalum kwa ajili yao.
Sherehe ikafunguliwa na watu wakaanza kuburudika kwa vinywaji na ndipo Mr benard alipopewa nafasi ya kuongea.
“Ndugu zangu,wageni waalikwa,mabibi na mabwana.Nakosa neno kubwa la kuwashukuru kwa kuacha shughuli zenu leo hii na kuja kuungana na familia yangu katika sherehe hii ya kumkaribisha nyumbani kijana wetu Innocent aliyekuwa akisoma nchini Marekani.Ujio wenu jioni hii ya leo unaonesha ni jinsi gani mlivyotuthamini sisi kama familia.Tunasema Ahsanteni sana.Sina mambo mengi sana ya kusema kwani mengi yamekwisha semwa ila ningependa nitumie nafasi hii kutangaza jambo moja kwenu wote.”
Ukumbi wote ukakaa kimya kabisa kumsikiliza mzee huyu.
“Si kitu cha kuficha kuwa kwa sasa mimi na mke wangu umri umesogea sana na kwa maana hiyo tunahitaji muda mwingi zaidi wa kupumzika baada ya kazi ngumu tuliyokwisha ifanya kwa miaka mingi.Nimekuwa na majukumu ya kusimamia miradi na kampuni zote zilizoko chini ya familia yangu.Napenda nikiri kuwa hii ni kazi ngumu na bila usaidizi wa karibu basi hakuna ufanisi utakaopatikana.Ninachotaka kukisema hapa ni kwamba kutokana na kuzidiwa mno na majukumu na hivyo kukosa hata muda wa kupumzika,nimeonelea niyagawe majukumu ili walau nipate wasaa wa kupumua.Napenda sasa nitamke kuwa kampuni ya kutengeneza maji ya kunywa ya Benardo ambayo kwa siku za hivi karibuni ufanisi wake umeshuka sana kwa sasa itakuwa chini ya usimamizi wa kijana wangu Innocent benard.”
Ukumbi wote ukalipuka kwa kelele za kushangilia.
Hizi zilikuwa ni habari njema mno kwa wafanyakazi wote wa kampuni hii.Kampuni hii ilikuwa ikiyumba baada ya kukosa usimamizi thabiti.Kupata meneja mpya tena kijana msomi kama Innocent ilikuwa ni faraja kubwa sana kwa wafanyakazi waliokuwa wana wasiwasi na ajira zao iwapo ingetokea kampuni ile kufungwa.
Innocent akapatwa na mstuko mkubwa.Hakuwa ametegemea kama angeweza kupewa kampuni kubwa kama ile aisimamie.Alipomaliza masomo yake nchini Marekani angeweza kubaki na kufanya kazi huko lakini alitambua umuhimu wa kurudi nyumbani na kusimamia miradi ya familia.Aliinama na kushika kichwa kwa mshangao.Kwa jinsi watu walivyoshangilia walizidi kumchanganya akili kwani japokuwa hawamjui lakini walionekana kuwa na imani na matumaini makubwa kwake ndiyo maana walifurahi na kushangilia
Baada ya Mr benard kumaliza kuongea akamkaribisha Innocent aweze kuwasalimu wageni na kuongea machache.Ukumbi wote ukawa kimya kumsikiliza .Huku akitabasamu akaanza kwa kusema
“Ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana ,nakosa neno la kuweza kuelezea furaha yangu kwa makaribisho haya makubwa.Sikutegemea kama ningeweza kupata makaribisho makubwa kama haya.Kitu kimoja ninachoweza kukisema toka moyoni mwangu ni Ahsanteni sana kwa kuja katika sherehe hii.Kuna msemo usemao nyumbani ni nyumbani na mkataa kwako mtumwa.Ni kwa kuzingatia misemo hii ndiyo maana nikachagua kurudi na kuishi nyumbani Tanzania badala ya kuishi na kufanya kazi katika nchi za kigeni.Nimerudi nyumbani kusaidiana na watanzania wenzangu katika kuijenga nchi yetu,kuinua uchumi wetu.Nitatumia ujuzi na maarifa yote niliyoyapata katika kuhakikisha tunapiga hatua kimaendeleo. Japokuwa hapa si mahala pake kulisema hili lakini kwa wale ndugu zangu wa kampuni nitakayokuja kuisimamia,naomba niseme kuwa muwe na amani na ninaahidi kushirikiana nanyi kwa moyo mmoja kwa manufaa ya kampuni yetu,jamii na nchi yetu kwa ujumla.Mabibi na mabwana sina cha kuongezea zaidi ya kuwashukuru sana kwa kuja kwenu .Naomba tuendelee na sherehe hizi kwa amani na utulivu.Ahsanteni sana”
Makofi na vigele gele vikasikika katika kila kona ya ukumbi.Watu waimshangilia Innocent kwa maneno machache aliyoyatoa.Sherehe zikaendelea hadi usiku mwingi halafu watu wakatawanyika na kurudi majumbani kwao.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana ,nakosa neno la kuweza kuelezea furaha yangu kwa makaribisho haya makubwa.Sikutegemea kama ningeweza kupata makaribisho makubwa kama haya.Kitu kimoja ninachoweza kukisema toka moyoni mwangu ni Ahsanteni sana kwa kuja katika sherehe hii.Kuna msemo usemao nyumbani ni nyumbani na mkataa kwako mtumwa.Ni kwa kuzingatia misemo hii ndiyo maana nikachagua kurudi na kuishi nyumbani Tanzania badala ya kuishi na kufanya kazi katika nchi za kigeni.Nimerudi nyumbani kusaidiana na watanzania wenzangu katika kuijenga nchi yetu,kuinua uchumi wetu.Nitatumia ujuzi na maarifa yote niliyoyapata katika kuhakikisha tunapiga hatua kimaendeleo. Japokuwa hapa si mahala pake kulisema hili lakini kwa wale ndugu zangu wa kampuni nitakayokuja kuisimamia,naomba niseme kuwa muwe na amani na ninaahidi kushirikiana nanyi kwa moyo mmoja kwa manufaa ya kampuni yetu,jamii na nchi yetu kwa ujumla.Mabibi na mabwana sina cha kuongezea zaidi ya kuwashukuru sana kwa kuja kwenu .Naomba tuendelee na sherehe hizi kwa amani na utulivu.Ahsanteni sana”
Makofi na vigele gele vikasikika katika kila kona ya ukumbi.Watu waimshangilia Innocent kwa maneno machache aliyoyatoa.Sherehe zikaendelea hadi usiku mwingi halafu watu wakatawanyika na kurudi majumbani kwao.


ENDELEA…………………………………….


Ni jumapili siku iliyofuata baada ya kuhudhuria ibada ya misa Innocent akarejea nyumbani.Sebuleni akakutana na dada yake Sarah ambaye alikuwa na macho yaliyojaa uchovu.
“Pole sana” Innocent akamwambia Sarah huku akicheka

“Du! sherehe ya jana ilikuwa si mchezo.Hapa nahisi kizungu zungu kwa pombe nilizokunywa.” Saraha akasema
“jana ulikunywa sana pombe”

“Du! Jana nilikuwa na kampani yangu tulikunywa pombe kupita maelezo.Si unajua nafasi kama ile kupatikana huwa ni mara chache sana.Hapa nyumbani baba haruhusu mtu kuja amelewa.Nahitaji kunywa supu naomba uniitie hawa wasichana wakanitengenezee supu” Sarah akasema huku akikilaza kichwa chake sofani.
Innocent akamwangalia na kutabasamu.
“Sabrinaa…!! Sabrinaa..!! “
Saraha akaita kwa sauti kubwa.

“Beeee dada !! “ Sabrina akaitika toka nje,akaja mbio.
“Unafanya kazi gani? Sarah akauliza
“Ninafua dada” Sabrina akajibu kwa adabu

“acha kufua,nenda kwanza kaniandalie supu mara moja” Sarah akaamrisha
“Sawa dada” Sabrina akaitikia.
“No ! Sabrina nenda kaendelee na kazi zako.Nitamtengenezea hiyo supu mimi” Innocent akasema.Sabrina akamtazama Innocent kwa uoga.
“Nimekwambia nenda kaendelee na kazi uliyokuwa ukiifanya.Nitakwenda mimi kumtengenezea supu” Akasema tena Inno na Sabrina akaondoka
“Nashindwa kukuelewa Inno.Toka umekuja unawapa kiburi sana hawa wasichana.” Sarah akalalamika

“Si kweli kwamba ninawapa kiburi,bali siridhishwi kwa jinsi mnavyowatendea.Hawa nao ni binadamu kama sisi na tuna kila sababu ya kuwapenda na kuwaheshimu kama sehemu ya familia yetu.” Innocent akajibu
“Shauri lako kama hutaki kutusikia tunavyokwambia.Hawa ni wagonjwa kaa nao mbali kabisa.”
Innocent hakujibu kitu akaondoka na kuelekea jikoni kumuandalia dada yake supu.Supu ilipokuwa tayari akampelekea dada yake halafu akatoka nje Sabrina alikokuwa anafua.

“Sabrina, mtaarifu na Grace kuwa leo mmalize kazi zenu mapema tutatoka kwa matembezi baadae”
Sabrina akaacha kufua akamtazama Innocent kwa macho ya mshangao halafu akatabasamu na kusema.

“kaka Innocent ,nimefurahi sana kusikia unataka kutoka na sisi kwa sababu haijawahi kutokea hata siku moja tukaenda matembezi.Lakini naona utaenda na Grace kwa sababu leo ni zamu yangu kuwa jikoni na siku kama hii ya leo ambayo mama huwa anashinda nyumbani huwa anataka chakula kisichelewe Iwapo nitaondoka na kuchelewa kurudi nitasababisha ugomvi mkubwa na mama.”

“Sawa Sabrina kama ndiyo hivyo usijali tutakwenda siku nyingine,mtaarifu Grace ajiandae“
Saa tisa za alasiri Innocent akaazima gari la dada yake akamchukua mbwa wake Pura pamoja na Grace wakaingia garini na kuondoka kwenda kutembea.
“Umependeza sana Grace.Sikujua kama u mrembo namna hiyo”Innocent akasema na kumfanya Grace atabasamu na kusema

“Ahsante kaka Innocent.”

“Unafaa kabisa kuwa mrembo wa Taifa” Innocent akatania na kumfanya Grace acheke kwa nguvu.
“Sio utani Grace leo umependeza sana.”
“kaka Innocent unapenda sana utani.Mimi niwe mrembo wa Taifa? Grace akasema na kuendelea kucheka kwa nguvu

“Ndiyo unaweza ukawa mrembo wa Taifa.Una vigezo vyote vya kukufanya uwe mrembo wa juu .Una umbo zuri la uanamitindo,urefu unaotakiwa,tabasamu zuri la kiafrika tatizo ninaloliona mimi ni kwamba bado hujiamini”
“Si kwamba sijiamini kaka Innocent.mambo kama hayo tumeshayaacha kwa watu wenye uwezo wao mkubwa na elimu ya kutosha.Mtu kama mimi maisha yangu yameshakuwa hivi,sifikirii chochote katika maisha yaliyobakia”

“Kwani Grace una elimu gani?”
“Elimu yangu mimi ni darasa la saba.Kwa elimu yangu mimi siwezi kuwa kama hivyo unavyosema.”
Innocent akamtazama Grace ambaye kwa sasa alikuwa ameinama,macho yake yalionyesha majonzi makubwa.
“Grace nakuomba ukirudi nyumbani leo hebu kaa katika kioo na ujitazame jinsi ulivyo mrembo.Nina kuhakikishia kuwa unaweza ukafanya mambo makubwa hadi watu wakabaki wakishangaa” Innocent akajaribu kumpa moyo grace.
“kaka Innocent,mimi nimekwisha kata tamaa na maisha yangu.Sifikirii kufanya jambo lolote lile na ndio maana unaona pamoja na kwamba mama ni mkali lakini ninajitahidi kumvumilia kwa sababu sina tena tumaini lolote katika maisha haya.Sina mahala pa kwenda,sina wazazi na wala sina kipato ninachoweza kusema ninaweza kufanya hata biashara ya kukaanga samaki”
Kimya kikapita.Innocent akageuka na kumtazama mbwa wake Pura aliyemuweka sehemu ya nyuma ya gari ,akakanyaga mafuta na kuyapita magari mawili yaliyokuwa mbele yao halafu akamgeukia Grace.
“Grace kama hutajali unaweza kunielezea historia ya maisha yako japo kwa ufupi?”
Grace akainama akafuta machozi.
“Hapana sijasema ulie Grace.nyamaza kulia na unieleze historia ya maisha yako kama utakuwa tayari”Innocent akasisitiza

“kaka inocent,historia ya maisha yangu ni ndefu na yenye kusikitisha sana.”Grace akasema
“Naomba unieleze tafadhali” Innocent akasema
“Nilizaliwa mkoani Iringa katika kijiji cha Nyororo.Sikumjua mama yangu.Nilielezwa kwamba mama yangu alifariki nikiwa mtoto wa miezi mitatu hivyo ikamlazimu baba kuoa mwanamke mwingine wa kunilea..Nikiwa darasa la tatu baba yangu alipata ajali ya kugongwa na nyoka akiwa shambani,akafariki dunia .Toka hapo maisha yangu yalibadilika ghafla baada ya kubaki nikilelewa na mama wa kambo.Ni kipindi cha mateso makubwa niliyoyapata toka kwa mama wa kambo.Nilipata mateso makubwa ambayo nashindwa hata kuyaelezea.Nilivumilia yote hadi nilipomaliza darasa la saba.Sikuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.Nilibaki nikifanya kazi za nyumbani na vibarua vya kupalilia mashamba ya watu na hela yote mama akachukua.Sikuwa hata na nguo za kuvaa.Pamoja na hayo yote bado nilimpenda mama yangu na kumheshimu kwani ndiye mama pekee aliyenilea..
Siku moja alikuja mama mmoja ambaye alikuwa akitafuta mtumishi wa ndani.Mama akaniuza kwa shilingi laki tano.Japokuwa nilitoa machozi kwa kufanywa kama bidhaa lakini kwa upande mwingine nilishukuru Mungu kwani niliamini ule ungekuwa ni mwanzo wangu wa kuondokana na dhiki ile kubwa ya nyumbani kwetu.Nililetwa Dar es salaam na kuanza kufanya kazi za ndani kwa mama yule aliyenitoa Iringa.Baada ya wiki mbili mama yule akaniuza tena kwa mama mmoja wa kihindi.Nikawa nafanya kazi pale.Nilipata manyayaso makubwa sana katika familia ile.Baba mwenye ile nyumba alikuwa akija na kunilazimisha kufanya naye mapenzi kila siku kwa kigezo kwamba nikikataa atanifukuza kazi.Sikuwa na mwenyeji wala ndugu yeyote hapa dar hivyo ikanilazimu kukubali kufanya naye uchafu ule.Nilipoona sintaweza kuvumilia tena nikatoroka na kuingia mtaani.Sikuwa na mahala pa kula wala kulala.Nikiwa njiani usiku wa saa tatu nikakoswa kugongwa na gari.Mzee yule aliyetaka kunigonga alinitazama akagundua kuwa nilikuwa na matatizo.Baada ya kunihoji nikamuelezea historia nzima ya maisha yangu,akanionea huruma akanichukua hadi nyumbani kwake.Mzee huyu ni baba yako.Nilianza kuishi pale kwenu na kusaidia kazi za nyumbani.Siku moja mmoja kati ya walinzi wa baba alinibaka,nikamsemea kwa baba akamfukuza kazi.Nililia sana baada ya kusikia kuwa mlinzi yule alikuwa ameathirika na virusi vya ukimwi.Baadae nilianza kusumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara.Nilikuwa naumwa,nakohoa na kutapika Mama akasema nilikuwa nimeambukizwa ukimwi tayari.Toka wakati huo nimekata tama na maisha yangu ninasubiri siku ya kufa kwangu……………..” Grace akashindwa kuendelea akaanza kulia.

“Nyamaza kulia Grace.Tutaongea zaidi nikisha egesha gari” Innocent akasema huku akikata kona kuingia Salama beach resort..
Salama beach resort ni moja kati sehemu tulivu kandoni mwa bahari ya hindi .Pamoja na usalama na utulivu uliokuwapo mahala hapa,kilichowavutia watu zaidi ni kuwa na ufukwe mzuri na msafi.Mamia ya wakazi wa Dar es salaam walikuwa wakija hapa kila mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupumzika na kupata hewa safi.Siku hii ya jumapili idadi ya watu ilikuwa kubwa kama kawaida.
Innocent akapaki gari akafungua mlango akashuka halafu akazunguka akafungua mlango wa upande aliokaa Grace akashuka.Macho yake yalikuwa mekundu kwa machozi.Innocent akamwangalia bila kusema kitu halafu akazunguka gari na kumfungulia mbwa wake Pura akamshika mkanda akamshusha garini.

“Beba huu mfuko wa vinywaji tukakae katika jiwe lile kulee” Innocent akamwambia Grace
Wakaanza kutembea taratibu kuelekea katika moja ya jiwe ambalo Inno alichagua wakakae.Wakalifikia jiwe lile wakakaa na kuifurahia mandhari nzuri na upepo mwanana wa bahari.
“Sijawahi kufika sehemu kama hii.Toka nimefika hapa Dar es salaam nimekuwa nikiisikia bahari au kuiona kwenye runinga lakini sijawahi kuiona kwa macho.” Grace akasema na kumfanya Innocent atabasamu.
“Unajua kuogelea? Innocent akauliza.na kumfanya Grace acheke kwa nguvu
“kaka Innocent,kwetu Iringa hakuna bahari.Ningejua vipi kuogelea na isitoshe hata kama tungejaaliwa kuwa na bahari au ziwa nisingekuwa na huo muda wa kwenda kuogelea.Nilipokuwa nyumbani muda wote ilikuwa ni kazi tu.”
“Umenifurahisha sana Grace.Kujua kuogelea si lazima kuwe na bahari au ziwa.Unaweza ukajifunza hata katika mito ya msimu inayoletwa na mvua.Ningekufundisha kuogelea lakini kuanzia kesho nitaanza kazi kwa hiyo sintakuwa na muda wa kutosha.Ila siku nikipata nafasi nitawafundisha kuogelea wewe na Sabrina.”akasema Innocent
“kaka Innocent ina maana kuanzia kesho hautakuwa ukishinda nyumbani?
“Ndiyo Grace.Nitaanza kazi rasmi kesho kwa hiyo tutakuwa tukionana mida ya usiku tu.Nita wamiss sana wewe na Sabrina”
Grace hakujibu kitu akainua kopo lake la Juice ya maembe akanywa kidogo.Alipoliweka chini Innocent akasema.

“Grace ulinielezea historia yako nikasikia uchungu sana.Dunia hii ina watu mabaradhuli kupita maelezo.Pole sana kwa yote yaliyotokea.Hiyo ndiyo mikiki mikiki ya maisha ambayo sote ni lazima tuipitie.Unachotakiwa kufanya kwa sasa hebu jaribu kuyafuta yote yaliyotokea na ufungue ukurasa mpya wa maisha yako.Amini kwamba hiyo yote iliyotokea ni mitihani ya maisha ambayo inatusaidia kuufahamu vizuri ulimwengu huu .Vile vile mitihani hii inatufanya tuwe karibu na mwenyezi Mungu na kumtumaini yeye tu.Ni yeye pekee ambaye anaweza akayabadili maisha yetu na kuwa mapya.Ni yeye anayeweza akatusahaulisha yote yaliyopita na kutuweka juu ya mataifa.Kumbuka Daudi alikuwa mchunga Kondoo lakini kwa uweza wake Mungu akawa mfalme.Mpokee na kumuamini Yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako naye atakujaza uzima,atakupa amani ,atakuosha kwa damu yake na utakuwa mpya tena” Innocent akasema kwa hisia kali.Kila anapokumbuka mambo yaliyomtokea katika maisha yake Grace huwa anashindwa kujizuia kutokwa na machozi.
“kaka Innocent,sijui hata nisema nini lakini wewe ni mtu wa kwanza ambaye Mungu amekutuma uje unipe moyo wa kuendelea kupambana na mitihani ya ulimwengu huu.Toka umekuja ninajihisi kama mtu mpya.Umekuwa unanipa moyo kila siku na kunisihi nisikate tamaa.Kaka Innocent pamoja na kunifanya nijisikie amani na furaha moyoni lakini napenda nikiri kuwa kila nikifikiria juu ya hali yangu hii nakata tamaa kabisa.Kuwa muathirika wa ukimwi ninaona kama maisha yangu yote hayana thamani tena.” Machozi yakaendelea kumtoka.Innocent akamwamgalia kwa macho yake ya huruma na kusema
“Grace naomba nikuulize kitu kimoja.Katika maongezi yako yote sijasikia hata mara moja ukinitajia suala la hospitali.Je umekwisha kutana na wataalamu wa ushauri ukapatiwa ushauri nasaha na jinsi ya kuishi na virusi vya ukimwi? Ninavyofahamu mimi kuwa na virusi vya ukimwi si mwisho wa maisha yako au mwisho wa ndoto zako.Iwapo utafuata ushauri wa wataalamu unaweza ukaishi maisha marefu sana na ukatimiza ndoto zako zote maishani .”
“Kaka Iinocent kusema ukweli sijakwenda hospitali yoyote” Grace akasema kwa sauti ya chini
“Kwani siku ulipopima na ukakutwa umeathirika walikupa ushauri gani.Hawakukwambia kitu chochote? Innocent akadadisi
“Kusema ukweli kaka Innocent mimi sijakwenda hospitali yoyote kupima “
“Whaaat!!!….” Innocent akauliza kwa mshangao
“Unasema hujakwenda hospitali yoyote kupima ? Inno akauliza

“Ndiyo Kaka Innocent”
Jibu lile linamfanya Innocent avute pumzi ndefu.
“sasa umejuaje kama umeathirika ?

“baada ya kubakwa na yule mlinzi, kilipita kipindi cha kama mwaka mmoja na miezi mitatu hivi nikaanza kuumwa ,nikawa natapika na kuharisha.Nikaenda hospitali nikapewa dawa nikapona.Baada ya mwezi nikaanza kuumwa tena.Toka hapo homa za mara kwa mara zikawa hazikatiki,nikadhoofu na kukonda sana.Mama akaniambia tayari nilikuwa nimeshaathirika.Sikutaka hata kwenda hospitali kupima kwa sababu sikuona haja.Kama nilibakwa na mtu mwenye ukimwi basi ni wazi na mimi nitakuwa nina ukimwi


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEFORE I DIE


SEHEMU YA 4

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kaka inocent kusema ukweli sijakwenda hospitali yoyote” Grace akasema kwa sauti ya chini
“Kwani siku ulipopima na ukakutwa umeathirika walikupa ushauri gani.Hawakukwambia kitu chochote? Innocent akadadisi
“Kusema ukweli kaka Innocent mimi sijakwenda hospitali yoyote kupima “
“Whaaat!!!….” Innocent akauliza kwa mshangao
“Unasema hujakwenda hospitali yoyote kupima ? Inno akauliza

“Ndiyo Kaka Innocent”
Jibu lile linamfanya Innocent avute pumzi ndefu.
“sasa umejuaje kama umeathirika ?

“baada ya kubakwa na yule mlinzi, kilipita kipindi cha kama mwaka mmoja na miezi mitatu hivi nikaanza kuumwa ,nikawa natapika na kuharisha.Nikaenda hospitali nikapewa dawa nikapona.Baada ya mwezi nikaanza kuumwa tena.Toka hapo homa za mara kwa mara zikawa hazikatiki,nikadhoofu na kukonda sana.Mama akaniambia tayari nilikuwa nimeshaathirika.Sikutaka hata kwenda hospitali kupima kwa sababu sikuona haja.Kama nilibakwa na mtu mwenye ukimwi basi ni wazi na mimi nitakuwa nina ukimwi



ENDELEA………………………………..


Innocent akakaa kimya ,akamtazama mbwa wake Pura akamshika shika kichwa na kumfanya Pura achezeshe mkia halafu akamgeukia Grace.
"My dear Grace,naomba unisikilize kwa makini.Kwanza naomba futa machozi”
Grace akafuta machozi yaliyokuwa yakimchuruzika halafu Innocent akasema.
“Grace,nina kila sababu ya kukemea uzembe uliofanyika ambao umechangiwa na mama kwa kuamini kuwa kwa vile ulibakwa na mtu mwenye ukimwi basi tayari na wewe umekwisha athirika.Sikutegemea kama mama ambaye ni mwanamke msomi na mwenye ufahamu mpana kuhusu virusi vya ukimwi na maambukizi yake aamue kutunga kitu ambacho hana uhakika nacho.Naomba nikufahamishe kuwa si kweli kwamba kila unapotembea na mwathirika wa virusi vya ukimwi basi na wewe tayari unakuwa mwathirika.Kuna sababu mbali mbali zinachochangia kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kama utafanya mapenzi yasiyo salama na mtu aliyeathirika na virusi vya ukimwi, na kubwa zaidi ni iwapo kulikuwa na dalili zozote za mchubuko zilizosababisha damu ya mwathirika kupenya na kuingia mwilini mwako.Ninachokushauri kwa sasa ni kwenda hospitali kupima na kupata majibu yenye uhakika.Kwa sasa unaathirika kisaikolojia na kukufanya uendelee kuwa mgonjwa zaidi na mwenye kukata tamaa.Nakuomba dada yangu kesho uende hospitali ukapime na upate uhakika.Kama utakuwa umeathirika wapo wataalamu wa ushauri ,watakupa ushauri wenye kufaa ni jinsi gani unaweza ukaishi maisha yako ya kawaida ukiwa umeathirika.lakini yawezekana pia ukawa haujaathirika.Kama itakuwa hivyo tutaimba kwa furaha na kumtolea Mungu sadaka na utayaanza maisha mapya.Je uko tayari kwenda kupima na kuhakiki afya yako kesho?
Grace akakaa kimya kidogo akitafakari halafu akasema
“Nimekubali kaka Innocent.Nitakwenda kupima kesho na kuhakiki afya yangu.majibu yote yatakayotokea mimi nitayapokea kwa mikono miwili” akasema Grace.
“Nafurahi kusikia hivyo.Kesho baada ya kufika kazini nitamtuma dereva nitakayekuwa nimepewa aniendeshe ,aje akuchukue na kukupeleka hospitali yenye vipimo vya hali ya juu ili tupate uhakika wa afya yako.”




* * * *




Saa moja na nusu juu ya alama Innocent akawasili mahala pake pa kazi akiwa ameongozana na baba yake .Moja kwa moja bila kupoteza muda akapelekwa ofisini kwake na kukabidhiwa rasmi kampuni ile aiongoze.Mzee Ernest ngimanyu ambaye ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya umeneja akakabidhiwa amwelekeze Innocent kwa undani juu ya utendaji kazi wa kiwandani pale halafu mzee Benard akaondoka na kwenda kuendelea na majukumu mengine.
“Mzee Ngimanyu ninaomba kabla ya yote niongee na wafanyakazi japo kwa dakika chache.Naomba uwakusanye wote tafadhali.” Innocent akaomba
Wafanyakazi walikuwa na hamu kubwa ya kumsikia meneja wao mpya atawaambia kitu gani,hivyo kazi zikasimama kwa muda na wote wakakukusanyika tayari kwa kumsikiliza Innocent.

“Tayari wamekusanyika na wanakubiri mzee” Akasema mzee Ernest

“Mzee Ernest unapenda sana utani.Mimi na wewe nani mzee? Innocent akasema na wote wakaangua kicheko kikubwa halafu wakatoka na kuelekea katika bwalo la chakula ambalo huwa linatumiwa pia kwa mikutano.
Mara tu alipoingia ukumbini akiwa ameongozana na mzee Ernest makofi yakaanza kupigwa na kumfanya Inno atabasamu kwa mapokezi yale mazuri.
Bila kupoteza muda mzee Ernest akasimama akaongea machache na kumkaribisha meneja mpya aongee na wafanyakazi.
“Ndugu wafanyakazi,nina furaha kubwa kusimama mbele yenu muda huu na kuzungumza nanyi.Kwa wale msionifahamu ninaitwa Innocent Benard na nitakuwa meneja wenu mpya kuanzia sasa” Innocent akakatishwa na makofi ya kushangilia yaliyopigwa na wafanyakazi.
“Nashukuru sana kwa makaribisho yenu mazuri ,nimejiskia faraja sana.Kwa kuwa nitakuwa nanyi kwa kipindi kirefu tutazidi kuongea na kufahamiana zaidi lakini kwa asubuhi hii ningeomba niseme machache.Kwa mujibu wa maelezo ya awali niliyoyapata toka kwa kaimu meneja mzee Ernest ni kwamba kwa siku za hivi karibuni kampuni yetu imekuwa haifanyi vizuri.Mauzo yamepungua na hivyo kupunguza kasi ya uzalishaji.Hii ni changamoto yangu ya kwanza kuishughulikia.Si changamoto ya kwangu tu bali ni yetu sote sisi kama wafanyakazi.Japokuwa kampuni hii inamilikiwa na mzee Benard lakini wadau wakubwa ni nyinyi wafanyakazi.Kwa umoja wenu mnaweza mkaipandisha kampuni au mkaishusha na kuiua kabisa.Ndugu wafanyakazi nataka tuanze upya ili kwa pamoja tuweze kupambana na hii changamoto kubwa ya kushuka kwa uzalishaji na mauzo.Nataka kila mmoja mahala pake pa kazi aone kwamba yeye ni sehemu ya kampuni na hivyo jukumu zima la uzalishaji ni la kwake.Nataka sote kwa pamoja tuwe na ari mpya ya kufanya kazi kwa bidii ,maarifa na ushirikiano.Ni silaha hii tu ya ushirikiano ndiyo itakayotuweka juu katika soko hili la ushindani mkubwa.Kwa kuwa kampuni hii ni yetu sote nawaahidi iwapo tutafanya kazi kwa bidii na kuogeza uzalishaji na mauzo,mishara yetu itapanda na kuboresha zaidi hali za maisha yetu kwani wote hapa tunafanya kazi kwa ajili ya kuwa na maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto wetu wapate elimu bora.Yote haya yanawezekana kama tutajituma katika kazi .Naamini yote yanawezekana kama kila mmoja atatimiza wajibu wake.Mwisho kwa kumalizia napenda kuwataarifu kwamba ofisi yangu iko wazi kwa mtu yeyote mwenye shida au matatizo mbali mbali.Nitapokea vile vile ushauri toka kwa kila mtu anayetaka kunipa ushauri ni jinsi gani tutaweza kuipeleka mbele kampuni yetu..Mwisho kabisa nawahakikishia kwamba pamoja kwamba kampuni yetu inapitia kipindi kigumu kwa sasa lakini hakuna mfanyakazi hata moja atakayepoteza ajira yake.Ahsanteni sana kwa kuniskiliza.”
Makofi,vigelegele vikalipuka ukumbini baada ya Innocent kumaliza kuongea machache.Kila mfanyakazi alikuwa amejawa na uso wa furaha na tabasamu kwa maneno yale machache yenye kujaa matumaini.Vicheko na kupongezana vikaendelea.Hii ikawa ni nuru mpya ya matumaini kwa wafanyakazi na kampuni .



* * * *



Akiwa ametingwa na kazi ofisini,mara simu yake ikaita.Alikuwa ni dereva wake Juma ambaye alikuwa amemtuma ampeleke Grace hospitali kwa ajili ya vipimo.
“hallo Juma nipe habari” akasema Innocent
“Bosi habari si nzuri.Nimemleta Grace hospitali ,amepata vipimo na baada ya kupewa majibu ya vipimo vyake ameanguka na kupoteza fahamu.Hivi sasa ameingizwa katika chumba cha huduma ya kwanza na madaktari wanamuhudumia”
Innocent akabaki ameishikilia simu asijue afanye nini huku kijasho chembamba kikimtoka.

“Juma nakuja hapo sasa hivi” Akasema Innocent kwa sauti yenye kujaa uoga ndani yake.Haraka haraka akainuka, akachukua gari la kampuni na kuondoka kuelekea hospitali.
“Yuko wapi Grace? Innocent akamuuliza Juma dereva aliyempeleka Grace hospitali

“Bosi ,Grace amepelekwa katika chumba cha huduma ya kwanza ,anapatiwa matibabu.” Juma akasema.Huku ameshika kiuno chake Innocent akauliza
“Hebu nieleze Juma nini kimetokea”
“Bosi kilichotokea ni kwamba nilimleta hapa Grace kwa ajili ya vipimo kama ulivyokuwa umeniagiza.Tulikuwa tumekaa wote pale wakati akisubiri majibu.Majibu yalipokuwa tayari akaitwa chumbani ili apewe.Ghafla nikaona mtu akitolewa na machela akikimbizwa katika chumba cha huduma ya dharura.Nikauliza nikaambiwa kwamba alipoteza fahamu baada ya kupewa majibu”

“Kwa hiyo hukuyaona majibu hayo” Innocent akauliza
“hapana Bosi majibu yake sijayaona.” Juma akajibu na kumfanya Innocent ainame na kutafakari kwa kina
“Kitu gani kitakuwa kimempelekea Grace aanguke na kuzirai? Yawezekana akawa amekutwa ana virusi vya ukimwi na kumfanya astuke ? Inawezakana kabisa akawa kweli ana virusi vya ukimwi.Masikini Grace namuonea huruma sana.Nitajitahidi kadiri niwezavyo kumpa faraja ili asikate tamaa”
Wakati akiwaza hayo madaktari wakatoka katika chumba cha huduma ya dharura wakiwa na nyuso za tabasamu.Haraka haraka Innocent akajitambulisha kama kaka wa Grace halafu Daktari akamwita ofisini kwake.
“Ndugu Innocent,kwanza napenda kukupa pole sana kwa mstuko uliokupata.natumai umestuka sana baada ya kupata taarifa za kilichotokea kuhusu dada yako”

“Daktari nilikuwa kazini na dereva wangu akanipigia simu kuwa dada yangu amepoteza fahamu ghafla.Ikanibidi kuacha kazi na kukimbia hapa mara moja.Hebu nifahamishe dokta ni kitu gani kilitokea? “ Innocent akauliza.
“Kwa ufupi ni kwamba Dada yako alifika hapa hospitalini kupima afya yake.Akaonana na daktari mhusika akaeleza anataka kupima kila kitu yaani kuanzia sukari,shinikizo la damu,virusi vya ukimwi n.k.Madaktari walimshughulikia na mara tu majibu ya vipimo yalipokuwa tayari daktari akamwita ili kumpatia majibu yake.Nafikiri ni ule uoga aliokuwa nao ndio uliopelekea yeye apoteze fahamu.Matatizo kama haya ni ya kawaida hasa kwa watu wanaokuwa na wasi wasi na afya zao hususan wanaokuwa na wasi wasi labda wameambukizwa virusi vya ukimwi.Tulimchukua tukampatia huduma ya kwanza na kwa sasa tayari amekwisha rejewa na fahamu zake ila tumempumzisha kwa muda na kama hali yake ikiendelea vizuri basi tutamruhusu arudi nyumbani.”
Innocent akatoa kitambaa na kujifuta jasho halafu akauliza.

“Daktari kwani majibu yake yanaonesha ana tatizo gani?

“Ndugu Innocent,siku zote majibu ya mtu huwa ni siri yake .Huwa haturuhusiwi sisi kusema matokeo ya majibu ya mgonjwa wetu kwa watu wengine.Nadhani ingekuwa vyema kama ungesubiri kwa ridhaa yake yeye mwenyewe akueleze.”
Innocent akamtazama daktari kwa sekunde kadhaa halafu akauliza.
“Dokta ninaweza kuruhusiwa kumuona?
“Bila wasi wasi.Unaruhusiwa kumuona.Ngoja nikupeleke”
Daktari akamchukua Inno na kumpeleka katika chumba alimokuwa amelazwa Grace.
“Grace kaka yako amekuja kukuangalia” Akasema daktari huku akitabasamu.
Grace alipomuona Innocent akapata nguvu ya ghafla akasimama na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia.Innocent akazidi kushangaa.Daktari akafunga mlango na kutoka akawaacha Inno na Grace peke yao.

“kaka Innocent umekuja? Siamini kaka yangu.Walikwambia nimepoteza fahamu? Grace akasema huku akilia.
“Juma alinipigia simu na kuniambia kuwa ulipatwa na mstuko ukapoteza fahamu.Kulikuwa na tatizo gani?
Grace akakosa neno la kusema akakaa kitandani huku bado akilia.Innocent akakaa karibu yake akatoa kitambaa na kumfuta machozi.
“usilie Grace.hebu nieleze kuna tatizo gani?

“nashindwa hata niseme kitu gani kaka Innocent ” Grace akasema
“Kaza moyo.Nieleze.Niko hapa kukusaidia.Niambie tafadhali nini kimetokea? Majibu yanasemaje?
Grace akafungua mkoba wake na kutoa karatasi za majibu akampa Innocent.
“Soma mwenyewe,mimi sijui kiingereza.”
Innocent akaanza kuzipitia karatasi zile moja baada ya nyingine ghafla akajikuta akiachia tabasamu pana ,moyo ukaanza kumwenda mbio na machozi ya furaha yakimchuruzika.
“You are HIV negative…you are negative…ooh My God you are negative…” akasema Innocent


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 5

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Grace akakosa neno la kusema akakaa kitandani huku bado akilia.Innocent akakaa karibu yake akatoa kitambaa na kumfuta machozi.
“usilie Grace.hebu nieleze kuna tatizo gani?
“nashindwa hata niseme kitu gani kaka Innocent ” Grace akasema
“Kaza moyo.Nieleze.Niko hapa kukusaidia.Niambie tafadhali nini kimetokea? Majibu yanasemaje?
Grace akafungua mkoba wake na kutoa karatasi za majibu akampa Innocent.
“Soma mwenyewe,mimi sijui kiingereza.”
Innocent akaanza kuzipitia karatasi zile moja baada ya nyingine ghafla akajikuta akiachia tabasamu pana ,moyo ukaanza kumwenda mbio na machozi ya furaha yakimchuruzika.
“You are HIV negative…you are negative…ooh My God you are negative…” akasema Innocent



ENDELEA………………………………


Akamkumbatia Gace kwa nguvu huku naye machozi ya furaha yakimtoka.

“Grace huna ukimwi..huna ukimwi…Thank you God..thank you Jesus”
Innocent akasema kwa furaha huku amesimama na kumshukuru Mungu.
“Mungu baba wa mbinguni,ambaye kwako hakuna jambo lolote linaloshindikana,wewe unayeweza kutamka neno na kitu kikawa.Uliumba dunia na kila kilichomo ndani yake kwa kauli yako moja tu.Baba ninakushukuru sana kwa muujiza uliotuonyesha hapa leo.Umedhihirisha wewe ni mtukufu wewe ni mwenye enzi.Baba mwanao amekuwa akiteseka kwa muda mrefu akidhani ana maradhi haya ya ukimwi kumbe hana,baba ninashukuru kwa kutupa mwanga huu na kwa sasa baba wa majeshi ingia ndani yake na umfanye upya tena.Anapoenda kuyaanza maisha yake mapya baba mtume roho wako akae naye na kumuongoza katika njia zote njema na umbariki aweze kuwa na maisha mazuri yenye kukupendeza wewe peke yako bwana wa majeshi unayestahili kusifiwa na kuabudiwa,katika jina la Yesu ..Amen.
Baada ya maombi yale mafupi akatoa kitambaa akafuta machozi halafu akamwendea Grace aliyekuwa amekaa kitandani.
“Dada yangu ,bwana amekufungua na kukufanya mpya tena.Mwili wako ni safi na roho wake ataendelea kukuongoza.Hongera sana dada Grace.” Inno akasema huku akimpiga piga Grace mgongoni.

“kaka Innocent nadhani ni Mungu alikurudisha ili uweze kuyarejesha maisha yangu katika tumaini .Nimeteseka vya kutosha na nilikwisha kata tamaa ya kuendelea kuishi tena.Sijui hata nitakulipa kitu gani kaka Innocent kwa sababu wewe ndiye mtu wa kwanza kunipa ushauri wa kuja kuangalia afya yangu…” Grace akaendelea kulia.
“Nyamaza kulia Grace.hutakiwi kulia tena.Unatakiwa uyaanze maisha mapya ya furaha na amani.Leo umekuwa kiumbe mpya.”
Innocent akaenda kuonana na daktari na kumuuliza kama anaweza akaruhusiwa kuondoka na dada yake.Daktari akamruhusu,wakaingia garini na kuondoka.Wakiwa ndani ya gari Innocent akapiga simu nyumbani kwao iliyopokelewa na Sabrina.

“Hallo Sabrina nataka leo jioni uandae chakula safi.Chinja kuku andaa chakula kitamu kuna jambo kubwa na zuri la kusherehekea jioni ya leo kama famila.”
Mchana huo Innocent akawa akizunguka katika maduka mbali mbali yanayouza nguo na urembo,akawanunulia Grace na Sabrina nguo pamoja na kumpeleka Grace saluni ambako alipambwa ,akapambika,kiasi kwamba kama ulimuona asubuhi basi ungempotea katika muonekano huu mpya.

“wow ! I knew it you are so pretty.I knew it” Innocent akaongea kwa mshangao mara tu baada ya kumuona katika muonekano mpya.Grace hakusema kitu akabaki akitabasamu.
“Umependeza sana Grace.”

“ahsante kaka Innocent. “
saa kumi na mbili za jioni wakawasili nyumbani.Innocent akamfungulia mlango Grace akashuka.wa kwanza kumuona alikuwa ni Sabrina,akastuka sana.
“ouh Grace ni wewe kweli? Umebadilika ,umependeza sana.Sukujua kama ni wewe.”
Kabla Grace hajajibu kitu mama yake Innocent akatokea akiwa amefura kwa hasira.
“Na wewe umekuwa bosi siku hizi mpaka unarudi saa hizi? Unategemea kazi za nyumbani akufanyie nani? ….

“Mama nilikuwa nimekwe……….”
Kabla Grace hajamaliza kujibu Innocent akadakia.

“Alikuwa na mimi mama.Nilimpeleka hospitali na baadae nikampitishia saluni.Grace nendeni ndani”
mama yake akamwangalia Inno kwa hasira akasema
“Nakwambia unachokitafuta kwa huyo Malaya utakipata.Kila siku ninakuonya usiwe karibu na huyo chokoraa hutaki kusikia”
maneno yale yanamuudhi Innocent akajibu.
“mama tafadhali usimuite Grace Malaya.Huyu ni sawa na mwanao.Amekukosea kitu gani mama? Au anavyokaa hapa anakunyima kitu gani?

“Usinijibu hivyo Innocent.Naona huko Ulaya ulikotoka wamekufundisha vibaya sana.Wewe si wa kusimama na kuanza kujibizana na mimi.” Mama yake Inno akasema kwa hasira
“Sijibizani nawe mama yangu,ila ninajaribu kukuelewesha kuwa hawa Grace na Sabrina ni sehemu ya familia yetu…. Kabla hajamaliza kaka yake Edson anatokea.
“Wow brother” akasema Inno kisha wakakumbatiana kwa furaha.

“naona mzungu umerudi nyumbani” Edson akatania wote wakacheka.

“Vipi mbona nasikia makelele huku nje? Edson akauliza
“Huyu mdogo wako toka amekuja amekuwa akiwapa kiburi sana hawa wasichana.Toka Inno amerudi wasichana hawa wamekuwa na kiburi hawataki kunisikia hata kidogo.Muonye mdogo wako akae mbali na hawa wasichana” mama yake Inno akasema kwa ukali
“Inno mbona unamkorofisha mama namna hiyo? Edson akauliza

“Si hivyo brother ,tatizo ni kwamba hawa wasichana wanakaa humu,wanasaidia kazi za ndani lakini hakuna mtu yeyote anayewajali.Wamekuwa wakinyanyaswa na kubaguliwa kitu ambacho mimi, sikipendi”
Edson na Innocent wakaingia ndani na kumuacha mama yao pale nje amefura kwa hasira.
Saa mbili za usiku tayari meza ilikwisha andaliwa.Kila mmoja alikuwa akijiuliza nini ilikuwa sababu ya furaha ile ya Innocent. Innocent akaleta shampeni akaweka mezani halafu familia yote ikakusanyika mezani kwa ajili ya chakula cha usiku isipokuwa Grace na Sabrina ambao wao hulia chakula chao jikoni.kabla hawajaanza kula Innocent akasema
“jamani kabla hatujaanza kula chakula hiki,napenda niwafahamishe kwamba chakula hiki ni mahsusi kwa ajili ya kusherehekea mwanzo wa siku mpya na maisha mapya ya mmoja wa wanafamilia hii.”
Kila mmoja akamkazia macho Inno bila kuelewa alikuwa akimaanisha kitu gani.
Innocent akaenda jikoni na kuwaleta Grace na Sabrina akawakaribisha mezani.
“baba na mama,kaka Eddy na dada sarah,leo mmoja kati ya dada zetu hawa ameyaanza maisha mapya .Grace leo amepima afya na amekutwa hana maambukizi ya virusi vya ukimwi.Yuko mzima kabisa na ushahidi huu hapa”
Innocent akasema na kuweka mezani karatasi za majibu ya vipimo toka hospitali .Kila mmoja akapigwa na butwaa.
“Napenda tokea sasa mtambue kwamba Grace si muathirika wa virusi vya ukimwi na kwa maana hiyo basi anaanza maisha mapya na ningeomba watu wote humu ndani tumpe ushirikiano katika maisha mapya atakayoyaanza.Ni mapema bado kusema ni maisha ya namna gani atayaanza kwa sababu bado naangalia ni kitu gani cha kumsaidia ili aweze kuyaendesha maisha yake.”
Innocent akafungua shampeni wakashangilia na kumpongeza Grace isipokuwa mama yake Inno aliyekuwa amefura kwa hasira.



* * * *




Siku nne zimepita toka Grace alipopima afya yake na kujikuta hana maambukizi ya virusi vya ukimwi.Maisha yake yaliendelea kuwa ya furaha japokuwa bado alikuwa akikumbana na vikwazo vingi toka kwa mama yake Innocent.Kwa kufuata ushauri wa Innocent aliendelea kuwa mtulivu na mvumilivu wa manyanyaso yote aliyofanyiwa.
Ni siku ya alhamisi asubuhi na mapema,Innocent akijiandaa kupanda gari tayari kwa kuwahi ofisini,Grace akamfuata mbio.
“Kaka Innocent samahani kwa kukusumbua.Unajua toka umeanza kazi umekuwa haupatikani sana hapa nyumbani.Wiki yote hii nimekuwa nikitafuta nafasi ya kukuona na kukwambia kuwa nina maongezi na wewe pindi upatapo nafasi.Naomba kaka Innocent ukipata nafasi hata muda wa jioni uniambie nina maongezi na wewe ya muhimu” Grace akasema huku akitazama chini.Innocent akamshika bega na kumwambia.

“Usijali Grace.Kwa sasa nina kazi nyingi sana ofisini lakini nitajitahidi kutafuta muda ili tukae tuongee.Vipi lakini maisha yanakwendaje hapa nyumbani?
Huku akijitahidi kuuficha uso wake Grace akajibu

“Hapa nyumbani maisha ni kama kawaida.Nimeshayazoea”

“Sawa , Grace ngoja mimi niwahi ofisini halafu nikipata muda tutakaa tutaongea.”
“Ahsante kaka Innocent.Kazi njema”
Innocent akaingia katika gari lake na kuondoka kuelekea kazini.

“Nimeanza kuyaona mabadiliko kwa Grace.Kwa siku hizi chache toka apate majibu ya vipimo vyake amebadilika sana.Ninaiona nuru ya matumaini katika macho yake.Ninaona ni jinsi gani alivyo na shauku ya kuyaanza maisha yake mapya niliyomuahidi.Ni lazima nimsaidie binti yule ili aweze kutimiza ndoto zake maishani.” Innocent akawaza akiwa ndani ya gari kuelekea kazini.
Kwa siku chache toka Innocent alipokamata uongozi katika kampuni hii ya kutengeneza maji ya kunywa,hali ya kiutendaji imebadilika sana.Wafanyakazi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii wakiwa na matumaini makubwa ya kuboreshewa mishahara yao ahadi waliyopewa na na kiongozi wao mpya.Mabadiliko haya ya utendaji kazi miongoni mwa wafanyakazi yalimpa moyo sana Innocent na kumfanya aamini kuwa muda si mrefu uzalishaji utaongezeka na hivyo kuboresha zaidi hali za maisha ya wafanyakazi.
Asubuhi hii wafanyakazi wote walikwisha wahi katika sehemu zao za kazi na kazi iliendelea kufanyika.Innocent akasalimiana na baadhi ya wafanyakazi halafu akaingia ofisini kwake akaendelea na kazi zake.Akiwa ofisini kwake mara kwa mbali akasikia kama kuna mabishano katika ofisi ya katibu muhtasi wake,akaacha alichokuwa akikifanya akafungua mlango na kumkuta katibu wake akibishana na mama mtu mzima ambaye ni mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Kuna nini hapa Devotha? Innocent akauliza.

“Bosi kuna huyu mama hapa amekuja analazimisha kutaka kukuona nikamuuliza kama ana miadi na wewe akasema hana nikamuuliza ana shida gani akasema ni shida binafsi,basi ndiyo nikawa najaribu kumuelewesha utaratibu ulivyo wa kukuona lakini yeye bado hanielewi.” Devotha katibu muhtasi wa Innocent akasema.

“Basi mruhusu mama aingie ofisini.halafu Devotha usimzuie mfanyakazi yeyote kuja kuonana na mimi.Awe na shida yoyote ya kiofisi au binafsi.Kama nipo mruhusu kila mtu anione.Sawa?
“Sawa bosi” Devotha akasema huku akionyesha kuchukizwa na kitendo cha mama yule kubishana naye hadi akakutwa na bosi wake.

“Mama shikamoo.” Akasema Innocent huku akimuelekeza mama yule aketi kitini.

“Marahaba baba.habari za kazi”
“Habari za kazi nzuri mama yangu..Karibu sana sijui una tatizo gani?
“Baba mimi naitwa Mama Sophia.Ni mfanyakazi wa kampuni hii,sisi ndio tunaosafisha chupa za kuwekea maji.Mimi ni mjane na nina watoto wanne.Tatizo nililonalo baba yangu ni kwamba mwanangu wa kwanza ameshindwa kwenda shule kutokana na ukosefu wa fedha.Amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika shule ya bweni lakini mpaka sasa hivi ninavyokueleza ni kwamba hajafanikiwa kwenda shule kutokana na kukosekana kwa fedha ya kulipia huko shuleni.Nimekuja hapa kwako baba uone ni jinsi gani unaweza ukanisaidia ili mwanangu aweze kwenda shule kuendelea na masomo.Ikiwezekana naomba nikopeshwe fedha halafu nikatwe katika mshahara wa mwisho wa mwezi.Naomba unisaidie baba kwa sababu hapa nilipo niko mwenyewe sina msaada toka sehemu yoyote ile.Kazi hii niifanyayo hapa ndiyo kila kitu kwangu.”
Mama Sophia akajieleza kwa upole.Innocent akamsikiliza mama yule kwa makini na aliyoyasema yakamuingia moyoni,akamuonea huruma sana mama yule mjane.

“mama nimekusikia.Kwanza pole sana kwa matatizo na vile vile nikupe hongera kwa kuweza kumudu kulea na kuwasomesha watoto wako wote wanne wewe mwenyewe.Nakupongeza kwa sababu elimu ndiyo msingi bora wa maisha yao.Mama kwa kweli suala lako limenigusa sana.lakini pamoja na kuguswa huko mama yangu napenda nikufahamishe kuwa kwa sasa hali ya kampuni si nzuri kifedha kama nilivyowaeleza siku chache zilizopita.Nina imani kuwa kwa siku chache zijazo uzalishaji ukiongezeka basi tutakuwa sehemu nzuri kifedha.Pamoja na hayo mama yangu hebu niachie suala hili ili nione ni jinsi gani ninaweza kukusaidia.Naomba unipe siku ya leo nishughulike na suala lako.Hata kama nikikosa nitajitahidi kutafuta sehemu yoyote ile ili tufanikishe mwanao aende shule.Mama fedha hizo zitakuwa si mkopo bali nitakusaidia kama mama yangu .”Innocent akasema
“baba nashukuru sana kwa msaada wako.Sijui hata nikushukuruje lakini nakuombea kwa Mungu akubariki na kukuzidishia kwa moyo wako wa huruma.” Akasema mama Sophia huku akisimama na kuondoka.

“Kuna kila sababu ya kuboresha maisha ya wafanyakazi.Huyu mama amekuwa jasiri kuja kunieleza tatizo lake,lakini nina imani kuwa wapo wengine ambao hawana ujasiri wa kunieleza matatizo yao.Nitajitahidi kwa kila niwezavyo kuboresha mishahara na stahili zao nyingine ili maisha yao yaweze kuboreka.” Innocent akawaza. Halafu akaendelea na kazi .


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 6


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“mama nimekusikia.Kwanza pole sana kwa matatizo na vile vile nikupe hongera kwa kuweza kumudu kulea na kuwasomesha watoto wako wote wanne wewe mwenyewe.Nakupongeza kwa sababu elimu ndiyo msingi bora wa maisha yao.Mama kwa kweli suala lako limenigusa sana.lakini pamoja na kuguswa huko mama yangu napenda nikufahamishe kuwa kwa sasa hali ya kampuni si nzuri kifedha kama nilivyowaeleza siku chache zilizopita.Nina imani kuwa kwa siku chache zijazo uzalishaji ukiongezeka basi tutakuwa sehemu nzuri kifedha.Pamoja na hayo mama yangu hebu niachie suala hili ili nione ni jinsi gani ninaweza kukusaidia.Naomba unipe siku ya leo nishughulike na suala lako.Hata kama nikikosa nitajitahidi kutafuta sehemu yoyote ile ili tufanikishe mwanao aende shule.Mama fedha hizo zitakuwa si mkopo bali nitakusaidia kama mama yangu .”Innocent akasema
“baba nashukuru sana kwa msaada wako.Sijui hata nikushukuruje lakini nakuombea kwa Mungu akubariki na kukuzidishia kwa moyo wako wa huruma.” Akasema mama Sophia huku akisimama na kuondoka.

“Kuna kila sababu ya kuboresha maisha ya wafanyakazi.Huyu mama amekuwa jasiri kuja kunieleza tatizo lake,lakini nina imani kuwa wapo wengine ambao hawana ujasiri wa kunieleza matatizo yao.Nitajitahidi kwa kila niwezavyo kuboresha mishahara na stahili zao nyingine ili maisha yao yaweze kuboreka.” Innocent akawaza. Halafu akaendelea na kazi .


ENDELEA…………………………………..


Masaa mawili baadae akaja meneja mwajiri wa kampuni,na moja kwa moja akaingia ofisini kwa Innocent..

“Bosi kuna tatizo limetokea.”

“Tatizo gani tena Godson?
“Kuna fundi umeme mmoja anaitwa Joshua amekutwa amelewa chakari kiasi kwamba hawezi hata kufanya kazi .Kama kutatokea hitilafu yoyote ya kiufundi kwa sasa sielewi tutafanya nini.Hili ni kosa na si mara yake ya kwanza kufanya hivi.Nimekwisha muonya mara tatu sasa na kwa mujibu wa sheria za kazi ni kwamba kwa sasa kinachofuata ni kufukuzwa kazi.Kampuni haiwezi kuwavumilia watu wa namna hii ambao wanachangia kurudisha nyuma kampuni.Barua yake hii hapa imekwisha andaliwa nimekuletea utie saini yako.”
Innocent akainama akakuna kichwa akawaza na kuuliza.
“Huyu bwana amefanya kazi hapa kampuni kwa muda gani mpaka sasa?
“Huu ni mwaka wa kumi “
“Ana familia? Innocent akaulza tena

“Ndiyo.Ana familia ya mke na watoto watatu”
Innocent akakaa kimya halafu akasema
“Godson pamoja na kwamba amefanya kosa kisheria na adhabu yake ni kufukuzwa kazi hebu naomba tuiweke pembeni adhabu hii na tumpe tena nafasi nyingine.We cant afford to loose him now.We still need him.Naomba apelekwe dispensary akapumzishwe kule halafu akipata nafuu msimruhusu aondoke mpaka aonane na mimi”

“Sawa bosi.Wewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho lakini ukumbuke kuwa kuzidi kuwavumilia watu kama hawa tunazidi kulea uzembe hapa kazini”
“nakubaliana nawe Godson,lakini naomba tumpe tena nafasi ya mwisho.Kama atarudia tena kosa lake basi hatutakuwa na msaada tena.Jitahidi apumzike na asiondoke bila kuonana na mimi.” Innocent akasisitiza,Godson akaondoka lakini ni dhahiri alionyesha kutoridhishwa na maamuzi yale ya mkuu wake.
“Uongozi ni mgumu sana lakini kuna nyakati ambazo ni lazima utumie busara na ubinadamu katika maamuzi .Toka ndani ya moyo wangu siwezi kumfukuza kazi Joshua wakati ana familia inayomtegemea.Nitaongea naye halafu nione nini cha kufanya” Innocent akawaza akaendelea na kazi zake.





* * * *


Saa kumi na moja za jioni wakati wafanyakazi walioingia zamu ya asubuhi wamekwisha toka na kuwapisha wale wanaoingia zamu ya usiku,Joshua bado aliendelea kuwapo pale ofisini akimsubiri bosi wake amalize kazi zake kama alivyokuwa ameelekezwa.Alikuwa mwingi wa mawazo na alikuwa amejikunyata pembeni kama mgonjwa.Alifahamu kuwa ni lazima atafukuzwa kazi kutokana na kosa la kuwa mlevi kazini hivyo akawa akijipanga jinsi ya kuomba msamaha.
Saa kumi na mbili za jioni Innocent akatoka ofisini kwake tayari kuelekea nyumbani.Joshua aliyekuwa amekaa katika mti mkubwa wa maua alipomuona bosi wake akitoka akamkimbilia.
“Mzee samahani” Joshua akaita bada ya kumfikia Innocent
“Bila samahani” Innocent akageuka
“Mzee mimi naitwa Joshua nilipewa maagizo yako na afisa maslahi kwamba nisiondoke bali nikusubiri hadi ukimaliza kazi zako unahitaji kuonana na mimi.”

“Ouh nimekumbuka.Wewe ndiye Joshua?
“Ndiyo mimi mzee” Joshua akajibu huku ameibana mikono yake kwa nyuma.
“Ok bwana Joshua nataka unipeleke nikapaone nyumbani kwako”
Joshua akastuka ,akapatwa na baridi ya ghafla.
“Mzee nyumbani kwangu?
“Ndiyo nyumbani kwako.Nahitaji kujua mahala unapoishi” Innocent akasisitiza huku akipiga hatua kueleka liliko gari lake.Wakaingia garini na safari ya kuelekea kwa Joshua ikaanza.Njiani Joshua alikuwa ni mkimya na alionekana kuwa na mawazo mengi.hakufahamu nini dhamira ya mkuu wake wa kazi kutaka kwenda kupajua nyumbani kwake.Zaidi ya maelekezo ya njia Joshua aliyokuwa akimpa Innocent hawakuongea kitu kingine chochote.Innocent alitambua dhahiri uoga aliokuwa nao Joshua.
Hatimaye wakafika katika nyumba anayoishi Joshua.Wakashuka na kuelekea ndani
“karibu ndani bosi” Joshua akamkaribisha ndani Innocent kwa sauti ambayo ilikuwa ikitetema.
Innocent akakaribia ndani sebuleni kulikokuwa na kiza na kwa msaada wa tochi ya simu ya Joshua akaonyeshwa mahala pa kukaa.Lilikuwa ni kochi lisichokuwa na mito ya kukalia .Joshua akamwita mkewe alete taa ya chemli aliyokuwa akiitumia chumbani.Mkewe alipokuja sebuleni haraka haraka Joshua akamtambulisha kwa Innocent.

“Mama Deo leo nimekuja na mgeni.Huyu ndiye meneja wangu mpya pale kazini kwangu.” Baada ya utambulisho ule ambao ulimfanya mke wa Joshua abaki mdomo wazi Joshua akamgeukia Innocent
“Bosi huyu ndiye mke wangu,tuna watoto watatu ambao nadhani bado wanacheza huko nje.”
Innocent akasimama na kusalimiana na mke wa Joshua.
“ Nafurahi sana kukufahamu mama Deo” Innocent akasema.

“Sijui utakunywa kinywaji gani bosi? Joshua akauliza
“Nashukuru Joshua.Nitakunywa siku nyingine.Kwa vile nimekwisha pafahamu nyumbani nitakuwa nikipita hapa mara kwa mara.Mama Deo Nashukuru sana nimepafahamu nyumbani.Siku nyingine nikipata nafasi nitafika kuwasalimia.” I nnocent akasema huku akiinuka na kutoka.Joshua akamsindikiza hadi garini.
“Joshua nashukuru nimepafahamu kwako ila naomba kesho nikuone asubuhi ofisini kwangu.Kwa leo hebu chukua hizi uwanunulie watoto soda” Innocent akasema huku akiitoa pochi yake na kuhesabu noti nne za elfu kumi kumi akampatia Joshua ambaye aliona ni kama muujiza .Hakuwa ametegemea kupata kiasi kile cha fedha kwa usiku ule. Innocent akamuaga na kuondoa gari lake.
“Kwa kweli bado nina kazi kubwa ya kufanya ili kuboresha maisha ya wafanyakazi wangu.Mtu kama Joshua si kwamba anapenda kulewa lakini inambidi kutokana na maisha aliyonayo.Maisha yake yanaonekana magumu sana licha ya kwamba ana kazi inayomuingizia kipato.Ni lazima nimsaidie aondokane na maisha haya anayoyaishi.”



* * * *


Saa mbili na nusu Innocent akawasili nyumbani kwao.Akasalimiana na kila mmoja halafu akaenda bafuni kujimwagia maji.Baada ya kuoga akamwita Grace wakaelekea bustanini huku akiwa na mbwa wake Pura.

“Grace ulisema una jambo la kunieleza.”
“Kweli kaka Innocent nina jambo nilitaka nikueleze.”

“Jambo gani hilo Grace”

“Kaka Innocent baada ya kupima na kugundua hali yangu nimejikuta ninapata mwanga mpya wa kuyatengeza upya maisha yangu yaliyokwisha haribika.Kwa kuwa umri wangu bado ni mdogo na nina nguvu za kutosha sidhani kama litakuwa ni jambo la busara kuendelea kufanya kazi za ndani huku nikimtegemea mama kwa kila kitu.Kaka Innocent shida yangu kubwa ni kukuomba unitafutie japo kikazi chochote katika kampuni yako au hata kokote kule unakoweza kupata ili niweze kufanya na kujipatia kipato changu mimi mwenyewe.Kwa kuwa sina elimu ya kutosha kazi yoyote itakayopatikana mimi nitaifanya.Iwe ni kufagia,kudeki vyoo,usafi nakadhalika.Siwezi kuchagua kazi kaka Innocent naomba tafadhali unisaidie ili niweze kuyaendesha maisha yangu kwa kujtegemea” Grace akasema huku akitazama chini.Innocent akakaa kimya akatafakari.Akaziangalia nyota angani na baada ya muda aksema

“Grace wazo lako ni zuri sana.lakini ukumbuke kuwa nilikwisha kuahidi kukusaidia kuyajenga maisha yako upya wewe na sabrina.Sijaisahau ahadi yangu.Hata nikiwatafutia kazi ya kufanya kwa sasa itakuwa ni kazi ambayo haitakuwa na maslahi yoyote kutokana na elimu yenu ndogo.Kwa maana hiyo lengo langu ni kwanza kuwapeleka shule mkaendelee na masomo halafu baada ya kusoma ndipo niwatafutie kazi.Nataka muanze elimu ya sekondari haraka iwezekanavyo mara tu shule zitakapofunguliwa.kwa sasa niko katika mchakato wa kutafuta shule na pindi nitakapoipata shule nzuri itakayoniridhisha nitakutaarifuni.Tafadhali msiwe na papara na haya maisha.Bado hamjachelewa.Umri wenu una ruhusu kabisa kuyatengeneza upya maisha yenu.Naahidi kuwasaidia kwa kila hali ili muweze kufanikisha malengo yenuo na kuwa na maisha mazuri siku za usoni.”
Innocent akasema na kumfanya Grace atabasamu kwa furaha huku sura yake nzuri ikizungukwa na nuru ya matumaini ya maisha mapya.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 7

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Grace wazo lako ni zuri sana.lakini ukumbuke kuwa nilikwisha kuahidi kukusaidia kuyajenga maisha yako upya wewe na sabrina.Sijaisahau ahadi yangu.Hata nikiwatafutia kazi ya kufanya kwa sasa itakuwa ni kazi ambayo haitakuwa na maslahi yoyote kutokana na elimu yenu ndogo.Kwa maana hiyo lengo langu ni kwanza kuwapeleka shule mkaendelee na masomo halafu baada ya kusoma ndipo niwatafutie kazi.Nataka muanze elimu ya sekondari haraka iwezekanavyo mara tu shule zitakapofunguliwa.kwa sasa niko katika mchakato wa kutafuta shule na pindi nitakapoipata shule nzuri itakayoniridhisha nitakutaarifuni.Tafadhali msiwe na papara na haya maisha.Bado hamjachelewa.Umri wenu una ruhusu kabisa kuyatengeneza upya maisha yenu.Naahidi kuwasaidia kwa kila hali ili muweze kufanikisha malengo yenuo na kuwa na maisha mazuri siku za usoni.”
Innocent akasema na kumfanya Grace atabasamu kwa furaha huku sura yake nzuri ikizungukwa na nuru ya matumaini ya maisha mapya.


ENDELEA………………………………


Asubuhi na mapema siku iliyofuata,kabla hajaanza kazi Joshua akaenda katika ofisi ya bosi wake kama alivyokuwa ameelekezwa siku iliyotangulia.Usiku mzima alikesha akiwaza kitendo cha bosi wake kutaka kufahamu mahala anakoishi na zaidi ya yote akamuachia shilingi elfu arobaini pesa ambayo hakuwa ameota kama angeipata kwa usiku ule.Kilichomuumiza kichwa ni kwamba jana alikutwa amelewa kiasi cha kushindwa kufanya kazi na meneja mwajiri alikwisha kusudia kumfukuza kazi.Hakuwa na uhakika kama bosi wake angeweza kumsamehe kwa kosa hilo.Asubuhi hii alikuwa mnyonge sana akijua lolote linaweza kutokea.Aidha kufukuzwa kazi au kupewa karipio kali.
Saa moja na nusu juu ya alama Innocent akawasili na kuelekea moja kwa moja ofisini kwake.Katika sehemu wanayokaa wageni wanaosubiri kuonana naye alimkuta Joshua tayari amekwisha fika akimsubiri.Akamsalimu na kumkaribisha ndani.

“Ndiyo bwana Joshua habari za toka jana? Innocent akauliza huku akikoroga kikombe cha kahawa na kumpatia Joshua
“Habari za toka jana nzuri bosi.” Joshua akajibu kwa sauti iliyojaa uoga.

‘Mama na watoto hawajambo?
“Hawajambo bosi”
Innocent akaweka vitu vyake mezani sawa sawa halafu akamtazama Joshua kwa sekunde kadhaa.
“Joshua nimekuita asubuhi hii kuna mambo ambayo nataka tuyajadili mimi na wewe.Jana nililetewa barua ya kusaini kukufukuza kazi kwa kosa la kulewa kazini na kushindwa kufanya kazi.Kwa mujibu wa meneja maslahi, si mara ya kwanza kwa wewe kufanya kosa la namna hii.Wamekwisha kupa maonyo kadhaa lakini bado umeendelea na tabia hii ya ulevi kazini.Mimi nilikataa kusaini na nikamuomba meneja mwajiri anipe nafasi ya kukaa na kuongea na wewe ili nijue tatizo lako ni nini hadi unafikia hatua hii.Jana niliamua kwa makusudi kwenda kufahamu mahala unakoishi na jinsi gani unavyoyaendesha maisha yako.Kusema ukweli Joshua sijapendezwa na aina ya maisha unayoyaishi .Baada ya kujionea mimi mwenyewe maisha yako nimeguswa na niko hapa kwa ajili ya kukusaidia lakini kwa sharti moja tu kwamba unaniahidi utaachana kabisa na pombe.Joshua una watoto watatu kama ulivyonieleza na wote hao wanahitaji matunzo bora,elimu bora ambayo itawajengea msingi bora wa maisha yao.Watoto na familia yako wanahitaji kukaa katika nyumba nzuri na si ile unayoishi sasa.Yote haya yanaweza kufanyika iwapo utaachana na pombe.Kwa hiyo naomba uniahidi kama utaachana na pombe ili nione ni jinsi gani ya kuweza kukusaidia kwanza kupata nyumba bora na baadae kukuinua kiuchumi.”
Joshua alishindwa kujizuia kutokwa na machozi kwa kauli ile ya Inocent kwamba anahitaji kumsaidia.Akapiga magoti na kukiri kwamba toka siku ile ameachana kabisa na ulevi wa kupindukia.Innocent akamruhusu kwenda kuendelea na kazi na kuahidi kumsaidia muda si mrefu ili maisha yake yaweze kuboreka.


MIAKA MIWILI BAADAE


Miaka miwili sasa imekatika toka Innocent akabidhiwe kampuni hii ya kutengeneza maji ya kunywa.Kwa muda huu mfupi kampuni ilikuwa imerudia hali yake ya kawaida .Uzalishaji uliongezeka na hivyo kuifanya kampuni kuwa na fedha za kutosha na kama alivyowaahidi wafanyakazi Innocent hakuchelewa kuanza kuongeza mishahara ya watumishi wake.Pamoja na kuongeza mishahara yao aliweza kuwawezesha pia kwa usafiri wa kuja kazini na kurudi majumbani kwao kwa kununua mabasi ya kampuni maalum kwa ajili ya wafanyakazi tu.Vile vile ilianzishwa shule ya chekechea kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi Kingine alichokuwa akitazamia kukifanya ni kuanza zoezi la kutoa mikopo ya nyumba kwa wafanyakazi wake ambao hawakuwa bado na nyumba za kuishi.Hali za maisha ya wafanyakazi wa kiwanda hiki zilianza kuboreka na kila mmoja alijisikia furaha kufanya kazi hapa.Kila mfanyakazi alikuwa akijituma kwa namna alivyoweza.ili kuweza kuogeza uzalishaji.Hii ikampa faraja sana Innocent ambaye kwa muda huu mfupi alitokea kupendwa na wafanyakazi kupita kiasi.
Grace na Sabrina wote kwa pamoja walikwisha maliza masomo ya sekondari.Walisoma masomo ya sekondari katika ule mpango wa elimu ya sekondari kwa miaka miwili.Walikuwa na uhakika mkubwa wa kufaulu mitihani yao kwa sababu walikuwa na waalimu wazuri waliokuwa wakilipwa vizuri na Innocent ili kuhakikisha kwamba wasichana hawa wawili wanafaulu mitihani yao ya kidato cha nne.
Ilikuwa ni siku ya jumamosi ,siku ya mapumziko ya wiki .Siku hii innocent aliamua kuitumia kwa kulala nyumbani .hakutaka kwenda kazini au sehemu yoyote ile.Mchana wakati akipumzika dada yake Sarah akaja na kumweleza kwamba alikuwa akihitaji kwenda katika klabu ya usiku ili kupoteza mawazo baada ya kazi nyingi za wiki nzima.Alikuwa akitaka kuongozana na Innocent kwa sababu hakuruhusiwa kutoka yeye mwenyewe kwenda sehemu za starehe nyakati za usiku.Innocent hakutaka kumyima raha dada yake akakubali kuongozana naye kwa usiku huo kuelekea Club peninsula moja kati ya klabu mpya na inayolitikisa jiji la Dar.
Saa moja za jioni wakaanza safari ya kuelekea Klabu Peninsula.

“Inno kuna mahali tutapitia kwa ajili ya kuwachukua marafiki zangu wawili .Si unajua tunatakiwa tuwe na kampani ya kutosha.Tena nimekumbuka Lulu atakufaa kwa kampani ya usiku huu.” Sarah akasema huku akitabasamu
“Sarah kila siku umekuwa ukinipigia kelele kuhusu huyo rafikiyo Lulu.Ni msichana wa namna gani huyo? “ Innocent akauliza.

“Inno,Lulu ni msichana ambaye nina uhakika anaweza akakufaa.Ni msomi,ni mrembo na ni hivi majuzi ametoka Urusi alikokuwa akichukua shahada yake ya udaktari.Nilimuahidi kukukutanisha nawe lakini naona leo ndiyo siku muafaka” Sarah akasema na kumfanya Inno acheke kwa nguvu.
“Usinifurahishe sarah.Mwanamke wa ndoto zangu nitampata tu lakini si huyo Lulu wako unayempa sifa kama malaika.”
“Unasema hivyo kwa sababu bado hujaonana na Lulu.Nakuapia Inno ukimuona wewe mwenyewe utamkubali.Inakubidi kwa sasa utafute mchumba Innocent .wewe ni mtu mkubwa sasa hivi.”
“nakubaliana nawe Sarah,mchumba nitatafuta lakini si kwa kutafutiwa.Bado nina muda mzuri na wakutosha wa kutafuta mtu nimtakaye.”


* * * *



Saa tatu kasoro wakawasili klabu Peninsula.Ilikuwa ni sehemu yenye pilika pilika nyingi kwa usiku huu.Sarah ambaye ndiye aliyekuwa dereva akawasha endiketa ya kushoto kuashiria kwamba alikuwa akielekea hapo klabuni.Wakati gari yao imesimama wakisubiri gari mbili zilizokuwa mbele ziingie ndani ghafla Innocent akaona wasichana wanne wamesimama chini ya nguzo ya umeme.Mavazi yao yalionyesha wazi kwamba walikuwa ni wasichana wanaofanya biashara ya ukahaba.Katikati yao alikuwepo msichana mmoja mwenye umbo dogo ambaye kwa msaada wa mwanga wa taa Innocent aliweza kulisoma vyema umbo lake.Alikuwa ni binti mdogo kuliko wote waliokuwa wamesimama pale.Alikuwa amevaa sketi fupi sana iliyoacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi.Alikuwa ameegemea nguzo ya umeme huku akipuliza moshi wa sigara.Sijui kwa nini Innocent alikuwa akimuangalia msichana yule namna ile.
Wakati bado amekodoa macho kuwaangalia wasichana wale ,Sarah akakanyaga mafuta na gari yao ikaingia ndani .Bila kuchelewa wakakata tiketi na kuingia ukumbini.Innocent alikuwa mkimya sana na alionekana kutotulia ,kila mara alikuwa akiangalia saa yake.

“sarah naomba funguo za gari lako nakwenda kuwachukua rafiki zangu wawili nao waje ili tuwe na kampani ya kutosha kwa sababu naona hapa mwanaume niko peke yangu.” Innocent akasema na kuinuka akitoka nje ha kuwaacha Sarah na rafiki zake wakiangua kicheko kikubwa.
Baada ya kutoka nje ya ukumbi moja kwa moja inno akaelekea mahala alikokuwa amewaona wale akina dada.Kwa sasa walikuwa wamebakia wawili pale chini ya nguzo.Akapumua baada ya kumuona yule msichana mdogo bado yupo.Taratibu akarudi na kupanda gari ,akaliwasha na kutoka nje ya geti.Akashusha kioo cha mbele halafu akaita
“Psiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii…” wasichana kama sita hivi wakatimka na kulizingira gari lake.Kijasho kilikuwa kikimtoka kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuzingirwa na kundi la akina dada wanaouza miili yao.Aliogopa sana iwapo angeonekana na mtu yeyote anayemfahamu.Kwa haraka haraka akaangaza na kumuona yule binti aliyekuwa akimtaka bado ameegemea nguzo ya umeme .
“Namtaka yule binti pale kwenye nguzo ya umeme.”Innocent akawaambia wale akina dada..
“Ouh kumbe hana meno huyu anataka kifaranga chenye nyama laini….” Mmoja wao akasema huku akiondoka.

“Uncle achana na kale katoto kameshalewa bangi halafu hakajui chochote kale.Cheki huu mzigo unavyolipa” Akasema mmoja wao huku akijizungusha na kumuonyesha Inno sehemu zake za makalio.Innocent hakutaka kuendelea kukaa pale kwa muda mrefu akatoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kumpa mmoja wao.
“kamata hii,niitie yule binti mdogo pale chini ya nguzo.”
Mwanamke yule haraka haraka akaenda na kumleta binti yule,Innocent akafungua mlango akaingia na kuliondoa gari bila kuongea chochote.Innocent alikuwa akitokwa na jasho jingi.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusimama na kuzingirwa na kundi la akina dada wanaouza miili yao.Katika maisha yake hakuwahi kuota kama iko siku atakuja kufanya kitendo kama kile.

“Hivi ni mimi kweli ndiye nimefanya kitu hiki? Siamini bado kama nimeweza kufanya kitendo kama hiki.Nashukuru Mungu sijaonwa na mtu yeyote anayenifahamu .Ni kitendo cha aibu kubwa.Sielewi kimenitokea kitu gani mpaka nikaamua kufanya kitu cha ajabu namna hii.Lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya hii.Nisingeweza kumpata kirahisi binti huyu bila kujifanya ni mteja ninayehitaji huduma ya kimwili.Masikini binti mrembo kama huyu ni kwa nini aingie katika biashara ya kuuza mwili? Amekosa nini binti huyu mzuri hadi afikie hatua ya kuutoa sadaka mwili wake? Siwezi kuacha binti mrembo kama huyu apotee.I must do something.I must help her.” Innocent akawaza huku akimtazama binti yule aliyekuwa amekaa pembeni ambaye kwa sasa alikuwa akisinzia pale kitini.

“masikini anaonekana kama vile tayari amekwisha lewa.Inavyoonekana tayari atakuwa amefundishwa kutumia vilevi.Anatia huruma sana binti huyu.Hapana siwezi kukubali nitafanya lolote linalowezekana ili kumsaidia.Ni lazima nimtoe katika maisha haya anayoyaishi kwa gharama yoyote ile.” Innocent akawaza tena huku akimtazama binti yule mdogo mwenye uzuri wa asili uliofichika kutokana na aina ya maisha anayoyaishi.Haikuhitaji akili ya ziada kutambua kwamba binti yule alikuwa na uzuri wa kipekee kabisa lakini kutokana na maisha anayoyaishi uzuri wake tayari ulianza kufifia.

“Usiku huu nitaenda naye wapi? Nahitaji sehemu tulivu sana ambayo ninaweza kuwa na binti huyu kwa usiku huu .Ngoja niende naye 104 lodge.Ile ni moja kati ya sehemu tulivu sana.” Innocent akawaza huku akikanyaga pedeli ya mafuta na kulifanya gari liongeze mwendo.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEFORE I DIE


SEHEMU YA 8

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Amekosa nini binti huyu mzuri hadi afikie hatua ya kuutoa sadaka mwili wake? Siwezi kuacha binti mrembo kama huyu apotee.I must do something.I must help her.” Innocent akawaza huku akimtazama binti yule aliyekuwa amekaa pembeni ambaye kwa sasa alikuwa akisinzia pale kitini.

“masikini anaonekana kama vile tayari amekwisha lewa.Inavyoonekana tayari atakuwa amefundishwa kutumia vilevi.Anatia huruma sana binti huyu.Hapana siwezi kukubali nitafanya lolote linalowezekana ili kumsaidia.Ni lazima nimtoe katika maisha haya anayoyaishi kwa gharama yoyote ile.” Innocent akawaza tena huku akimtazama binti yule mdogo mwenye uzuri wa asili uliofichika kutokana na aina ya maisha anayoyaishi.Haikuhitaji akili ya ziada kutambua kwamba binti yule alikuwa na uzuri wa kipekee kabisa lakini kutokana na maisha anayoyaishi uzuri wake tayari ulianza kufifia.

“Usiku huu nitaenda naye wapi? Nahitaji sehemu tulivu sana ambayo ninaweza kuwa na binti huyu kwa usiku huu .Ngoja niende naye 104 lodge.Ile ni moja kati ya sehemu tulivu sana.” Innocent akawaza huku akikanyaga pedeli ya mafuta na kulifanya gari liongeze mwendo.


ENDELEA…………………………………..

Hatimaye wakafika 104 lodge moja kati ya hoteli kubwa za hadhi ya juu sana.Inno akamtikisa bega binti yule akastuka na kumtazama usoni.
“Du nimepitiwa na usingizi.Hapa tupo wapi? Akauliza binti yule ambaye sauti yake ilikuwa laini mno

“104 lodge” Innocent akajibu huku akimtazama.
Binti yule hakujibu kitu akafungua mlango wa gari na kushuka.Innocent naye akashuka halafu wakaongozana hadi hotelini ambako walipatiwa chumba ghorofa ya tatu.Muhudumu akaongozana nao hadi kilipo chumba chao akawafungulia mlango halafu akawaacha.Kilikuwa ni chumba kikubwa kinachomfanya binti yule astaajabie uzuri wake.Bila kupoteza muda akaenda kujitupa katika sofa kubwa lililokuwa mle chumbani
“Kaka unajua mimi nakufuata tu lakini bado hatujaelewana kama unanihitaji kwa usiku mzima au ni kwa masaa machache.Nyie watu wenye pesa zenu huwa hamkawii kubadilika baada ya kuridhishwa” Binti yule akasema
Innocent alikuwa amesimama akimkodolea macho binti yule ambaye alikuwa amekaa sofani huku kivazi alichovaa kikiwa kimepanda juu na kuifanya sehemu kubwa ya mapaja yake yanayong’aa kuwa wazi .Innocent alihisi kama damu yake ikichemka baada ya kuushuhudia mwili ule mwororo.
“nakuhitaji kwa usiku mzima.Unachaji kiasi gani kwa usiku mmoja? Innocent akauliza
“kwa usiku mmoja ni shilingi elfu kumi na tano tu” binti yule akasema

“Elfu kumi na tano?? Innocent akauliza kwa mshangao
“Yes elfu kumi na tano tu.Kwani vipi uncle,ni pesa nyingi sana ?Tunaweza kuongea kama unaona ni pesa nyingi lakini kwa muonekano wako unaonekana pesa si tatizo kwako.Nipatie hiyo elfu kumi na tano unitumie utakavyo usiku kucha” akasema Yule binti huku akirembua macho yake na kuzidi kuvutia

“Hapana elfu kumi na tano si pesa nyingi” Innocent akajibu huku akilivua shati lake na kubaki na fulana ya ndani .Alihisi joto.
“Uncle naomba kwanza uniagizie chakula.Nahisi njaa ya ajabu” Binti yule akasema huku amelishika tumbo lake.Innocent akamtazama kwa macho ya huruma.
Akaiendea simu na kuwapigia hotelini na kuomba aletewe vinywaji baridi na kuku wa kukaanga.Haikuchukua dakika tano chakula kikaletwa na kuwekwa mezani.Binti yule akala chakula kile kwa pupa huku Innocent akimtazama.
“Nashukuru uncle.Chakula kitamu sana” akasema binti yule baada ya kumaliza kula.Innocent akapiga simu hotelini na kuwaomba waje waondoe vyombo.
“Uncle naomba uniagizie Konyagi kubwa tafadhali” akasema binti yule na kumfanya Innocent amtazame kwa mshangao.
“Mbona unaniangalia hivyo uncle? Kweli nina hamu sana na konyagi.Iwapo nitapata mzinga mmoja ninaweza kukesha usiku kucha nikifanya mapenzi na wewe.Sikudanganyi uncle wewe niagizie konyagi halafu utakubaliana na shughuli yangu usiku wa leo.Kila siku utanitafuta.Wananiita B52 kutokana na mizungu yangu kitandani” Binti yule akasema kwa sauti kavu.Bado Innocent alikuwa akiendelea kumtazama usoni.
“Konyagi hapana.kwa umri wako hutakiwi kunywa konyagi” Innocent akasema
“We kaka vipi? Mimi nakunywa vitu vikali zaidi ya konyagi.We unashangaa mimi kunywa konyagi hahahahaaa.Usiangalie udogo wa reli uncle” Binti yule akasema
Innocent alikuwa amesimama ameshika kiuno akimtazama binti yule kwa mshangao.
“Ouh God please help me to save this girl.Her situation is totally complicated.Siamini kama binti mdogo kama huyu anaishi maisha ya namna hii.She looks totally lost.I need to change her life” Innocent akawaza.

“badala ya kunywa konyagi hebu jaribu kunywa juice kwa leo” Innocent akasema
“aagh ! we Uncle unachekesha sana yaani mimi ninywe juice? Hahahahaa uncle ni kama unanitukana vile.Mimi natumia vitu vikali,siwezi kutumia vinywaji vya watoto” Binti yule akasema na kumfanya Innocent azidi kuchoka.

“Du ! huu mziki niliokutana nao leo si mdogo.Nahisi ni kama nimenunua matatizo bila kujua.Lakini siwezi kukata tamaa.I need to do whatever I can to save her.” Akawaza Innocent.Binti yule alikuwa bado akimtazama kwa macho makali na kumfanya Innocent azidi kuushuhudia uzuri uliofichika ndani ya mboni za binti huyu.

“Uncle mbona uko mbali,sogea basi karibu tuanze mambo ili nipate na mie muda wa kupumzika.Naona kama unaniogopa vile.Hebu sogea hapa,mwenzio nataka mambo.Halafu kabla sijakupa mambo hebu nipatie changu kabisa ili asubuhi nikiamka mimi nashika hamsini zangu.” Akasema yule binti.

“Usijali kuhusu pesa.Unanionaje mimi? Unahisi ni kama nitakufanyia dhuluma? Hapana siko hivyo.” Inno akasema huku akimkaribia binti yule.

“Ningependa kulifahamu jina lako kwanza.Unaitwa nani? Innocent akauliza na kumfanya yule binti agune.
“mimi naitwa Innocent.wewe mwenzangu unaitwa nani? Innocent akauliza tena.Binti yule akamuangalia Innocent usoni halafu akasema

“naitwa Marina” akasema huku akibetua midomo yake
“Ouh Marina ! .Jina zuri sana.” Innocent akasema huku akiendelea kumtazama Marina na kuzishuhudia chuchu changa zilizokuwa zimechomoza katika kinguo chepesi alichokuwa amekivaa na kumfanya asisimkwe mwili.
“Marina wewe ni mwenyeji wa wapi? Innocent akauliza
“Uncle mbona unaniuliza maswali kama askari? Umetaka kujua jina langu nimeshakwambia sasa maswali mengi ya nini tena? Ulinichukua ili nije nikustareheshe au uje kuniuliza maswali? Marina akawa mkali
“Usiwe mkali Marina .Sijakuuliza kwa nia mbaya na wala mimi si askari.Si vibaya hata kama tutakuwa wote kwa usiku mmoja tukifahamiana.Huwezi jua pengine naweza nikawa mteja wako wa kudumu” Innocent akasema na kumfanya Marina atabasamu.

“Uncle hautajali kama nikivuta sigara humu ndani? Marina akauliza huku akifungua pochi yake na kutoa pakiti la sigara akalishika mkononi.

“Hakuna wasi wasi unaweza ukavuta” Innocent akasema
marina akachomoa sigara moja na kuanza kupiga mikupuo kadhaa na kutoa moshi mwingi uliosambaa mle chumbani.Innocent alikuwa akimtazama asiamini anachokiona.
‘uncle vipi mbona unanitazama namna hiyo? Halafu uncle naomba nikuulize swali moja”

“Uliza tu” Innocent akasema kwa sauti ya chini.Alikuwa amenyong’onyea kwa vituko vya Marina .
“Uncle wewe ni Padri au mchungaji ? “
“kwanini umeuliza hivyo? Inno akauliza huku akicheka kichini chini
Unaonekana tu. Hauonekani kama ni mtu aliyezoea kuchukua wanawake wanaojiuza.Unavyoonekana una wasi wasi sana.Ni mara yako ya kwanza kuchukua kahaba?”
Innocent akatabasamu na kucheka kidogo halafu akasema
“mimi si padre wala mchungaji kama unavyofikiri ,ila ni kweli kwamba sina mazoea ya kutoka na wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza.Kusema ukweli ni mara yangu ya kwanza na imekuwa ni kama muujiza Fulani kwa sababu sijielewi mpaka sasa hivi nimewezaje kufanya kitendo kama hiki.” Innocent akasema na kujishika kichwa.
“Sasa uncle kama ulikuwa huna mpango na mimi umenileta huku kufanya nini? Si ungeniacha basi pale kijiweni manake leo nilikuwa na mteja wangu wa kiarabu alikuwa aje kunichukua saa sita usiku halafu yeye analipa kwa dola.Kama huna mpango na mimi tufanye basi fasta fasta halafu nijikatae nikacheki mpango mwingine. “ Marina akasema huku akikivua kinguo chake cha juu na kubaki kifua wazi.Innocent anapatwa na mstuko wa ghafla kwa kuziona chuchu zile zilizosimama.
“Marina vaa nguo yako halafu tuongee.” Innocent akasema kwa msisitizo huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi.
“Uncle mbona unaniwekea usiku? Au wewe si mzima? Kama vipi niambie niende zangu” marina akalalama.

“Si hivyo marina .naomba vaa kwanza nguo yako halafu tutaongea.” Innocent akasema huku akiinuka na kuiendea simu.Akapiga simu mapokezi na kuomba waletewe mvinyo .
“mambo si hayo bwana.Muda wote nimekwambia uniagizie kinywaji unajivuuuuuuta kama nini” marina akasema huku akivaa ile nguo yake.
Innocent akarudi na kuketi karibu na marina akamwangalia kwa sekunde kadhaa.
“Unaogopa nini? Kama kondom ninazo.Ukitaka bila ya kondom itabidi tubadili bei ” Marina akasema

“ Hapana Marina sina maana hiyo na wala siogopi.” Innocent akasema
“ Sasa kama huogopi mbona unaniangalia kama vile ninataka kukutoa roho? Mimi ni wako nitumie utakavyo kwa usiku wa leo.”Marina akasema

“Marina naomba unisikilize vizuri”
“Ndiyo nakusikiliza” Marina akasema huku akikaa sawa
‘nimekuleta hapa si kwa ajili ya kukutumia na kukulipa.Mimi si mtu wa namna hiyo.Nilikuona katika lango la kuingilia pale klabuni ,nikajikuta nikistuka ghafla na kuguswa sana Nilijiuliza maswali mengi ni kwa nini uko pale na genge lile la akina dada wanaouza miili yao,nikakosa jibu .Nilitamani nishuke nikuondoe toka katika kundi lile lakini nikaamua niwatoroke wenzangu na kukuchukua kuja nawe hapa ili nipate walau fursa ya kuongea nawe.Kwa hiyo naomba ufahamu kwamba sina lengo la kuutumia mwili wako halafu nikulipe.Hata kama nikikulipa kiasi gani cha fedha ,hakitaweza kurudisha thamani ya utu wako.Kwa maana hiyo Marina naomba uwe huru na wazi kwangu,naomba tuongee kama marafiki.Lengo langu ni kukusaidia na pengine kukutoa kabisa katika biashara hii unayoifanya.”
Innocent alisema taratibu na kumfanya marina ainue uso wake na kumtazama usoni.Mara mlango ukagongwa,Inno akainuka na kwenda kufungua,alikuwa ni mtumishi wa hoteli aliyekuwa ameleta mvinyo.Inno akamimina katika glasi na kumpatia Marina ambaye aliupamba uso wake kwa tabasamu pana sana linalomfanya Innocent naye atabasamu

“Mtoto anaonekana anapenda sana ulevi huyu.” Innocent akawaza.
Marina akapiga mafunda kadhaa ya mvinyo ule halafu akakohoa kidogo na kusema
“Du ! huu mvinyo si mchezo.Kwani uncle ulikuwa unataka kunisaidia kivipi? Marina akauliza
“Ningependa kwanza kufahamu historia yako kwa ufupi tu,umetokea wapi,unaishi wapi,wazazi wako wako wapi, na mwisho ningependa kufahamu ni kwa nini uliingiia katika biashara hii ya ukahaba.”
Marina akainama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa ,akamimina mvinyo katika glasi ,akagugumia yote,akaongeza tena nusu yake akainywa yote.Akaiweka glasi chini halafu akainama.baada ya kama dakika moja hivi akainuka,akafungua pochi yake na kutoa kitambaa kidogo.uso wake ulikuwa umejaa machozi.Innocent akastuka.
“marina kulikoni mbona hivyo? Mbona unalia? Nimefanya vibaya kukuuliza?


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 9

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Innocent alisema taratibu na kumfanya marina ainue uso wake na kumtazama usoni.Mara mlango ukagongwa,Inno akainuka na kwenda kufungua,alikuwa ni mtumishi wa hoteli aliyekuwa ameleta mvinyo.Inno akamimina katika glasi na kumpatia Marina ambaye aliupamba uso wake kwa tabasamu pana sana linalomfanya Innocent naye atabasamu

“Mtoto anaonekana anapenda sana ulevi huyu.” Innocent akawaza.
Marina akapiga mafunda kadhaa ya mvinyo ule halafu akakohoa kidogo na kusema
“Du ! huu mvinyo si mchezo.Kwani uncle ulikuwa unataka kunisaidia kivipi? Marina akauliza
“Ningependa kwanza kufahamu historia yako kwa ufupi tu,umetokea wapi,unaishi wapi,wazazi wako wako wapi, na mwisho ningependa kufahamu ni kwa nini uliingiia katika biashara hii ya ukahaba.”
Marina akainama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa ,akamimina mvinyo katika glasi ,akagugumia yote,akaongeza tena nusu yake akainywa yote.Akaiweka glasi chini halafu akainama.baada ya kama dakika moja hivi akainuka,akafungua pochi yake na kutoa kitambaa kidogo.uso wake ulikuwa umejaa machozi.Innocent akastuka.

“marina kulikoni mbona hivyo? Mbona unalia? Nimefanya vibaya kukuuliza?



ENDELEA…………………………….


Huku akilia kichini chini Marina akasema

“Innocent kwa takribani miaka saba sasa sijawahi kukutana na mtu yeyote ambaye amewahi kuniuliza swali kama hili.Hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kuhoji ni kwa nini ninauza mwili wangu,hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kunionea huruma.Wewe ni mtu wa kwanza ambaye umeniuliza maswali ya namna hii.Wewe ni mtu wa kwanza ambaye umenirudishia tena historia mbaya ya maisha yangu ambayo tayari nilikwisha kuifuta kichwa mwangu.” Marina akasema huku akilia.

“Nyamaza kulia marina “ Innocent akamkaribia zaidi na kumbembeleza.
“Innocent ,ni mara ya kwanza leo nimekutana na mtu ambaye ameona thamani yangu na kukataa kuudhalilisha utu wangu kwa kuutumia mwili wangu na kunilipa fedha.Nimekuwa nikilala na wanaume wa kila aina,wengine ni viongozi serikalini lakini hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kunionea huruma hata kwa umri wangu huu mdogo badala yake wengine wamekuwa wakinibaka,wengine wananitumia kwa nguvu bila kunilipa chochote ,nimekutana na kila aina ya udhalilishaji wa dunia hii katika umri huu mdogo.Sijawahi thaminiwa hata siku moja.Ninaichukia dunia Innocent.Nimekwisha kata tamaa kabisa na maisha haya kiasi kwamba hata mimi mwenyewe sioni thamani ya utu wangu.” Marina akanyamaza na kuendelea kulia.Innocent akambembeleza hadi akanyamaza.Akamimina mvinyo katika glasi akapiga funda kubwa akaweka glasi chini akaufungua mkoba wake na kutoa sigara.akaiwasha na kupiga mikupuo kadhaa .Huku sigara yake ikiwa mkononi akamgeukia Innocent na kusema
“Innocent siku ya leo nahisi ni kama nimekutana na Malaika kwa sababu kwanza umenileta katika hoteli hii kubwa ya hadhi,umeninunulia chakula kizuri,mvinyo safi na zaidi ya yote umenionyesha thamani yangu mimi kama mwanamke na kama binadamu.” Marina akasema huku akipiga mkupuo mwingine wa sigara na kupuliza moshi mwingi

“Marina siku zote mimi nimekuwa nikiheshimu sana utu wa mtu na ndio maana niliguswa sana nilipokuona pale klabuni umekaa katika genge la wanawake wanaojiuza.Ninauthamini utu wako ndiyo sababu niko hapa na wewe sasa hivi ili kutaka kukufahamu vizuri na kuona ni jinsi gani ninaweza kukusaidia”
Marina akamtazama Innocent usoni,akapiga tena mkupuo mwingine wa sigara,akageukia pembeni na kuupuliza moshi .

“Innocent mimi kwa sasa kunisaidia itakuwa vigumu sana kwa sababu tayari nimekwisha haribika.Sasa hivi kazi hii imekwisha niingia kwenye damu na siwezi kuiacha tena.Tayari nimekwisha ingia katika matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya kama bangi.Wakati mwingine tunachanganya na unga wa kulevya.maisha yangu tayari yamekwisha haribika.Kwa umri huu mdogo nilionao nimeshapitia mambo mengi sana.Nimepitia maisha magumu ambayo nikikuhadithia unaweza ukatoa machozi.Innocent nimekwisha kata tamaa na maisha yangu haya.Hapa nilipo sielewi kama nimekwisha athirika na ukimwi au la kwa sababu kuna wanaume wengine hawataki kutumia kondomu kwa hiyo inanilazimu kufanya nao mapenzi bila kutumia kinga.”
Marina akainama chini na kuzama katika mawazo mengi.Innocent akamtazama kwa makini akamuonea huruma binti yule .Taratibu akainuka akaichukua simu yake na kumpigia dereva wake wa kazini na kumwambia achukue gari la kampuni na kuwafuata dada yake na rafiki zake klabuni alikowaacha kwani yeye hatarudi tena kule.Baada ya kuongea na Juma akampigia dada yake sarah
“Innocent uko wapi? Mbona umesema unarudi sasa hivi lakini muda unazidi kwenda huonekani? Au umemkimbia Lulu? “ Saraha akasema
“hapana si hivyo Saraha.Kuna mahala tumekwenda na rafiki zangu akina Abuu na nina wasi wasi tutachelewa kurudi.Kwa hiyo nimempigia simu Juma yule dereva wa kampuni aje awachukue na gari hapo klabuni.” Innocent akadanganya
“Haya Inno sisi tunaendelea tumeongezeka sasa tuko kama watu kumi na tano hivi.Leo ni mpaka asubuhi” Sarah akasema na kukata simu.Innocent akarejea pale sofani ambako bado marina alikuwa amejiinamia.
“Marina unaweza ukanieleza historia ya maisha yako? Innocent akauliza kwa sauti ya upole.
“Innocent historia ya maisha yangu hautapenda kamwe kuisikia.Haifurahishi na siku zote huwa sipendi kuongelea masuala yoyote yanaohusiana na historia ya maisha yangu kwa sababu huwa inaniumiza mno.”Marina akasema

“Jikaze Marina naomba unieleze japo kwa ufupi” Innocent akasisitiza
Marina akakaa kimya kidogo halafu akanywa mvinyo kidogo na kusema

“Innocent naona silewi kabisa.Unaweza ukaniruhusu nipulize jani kidogo?

“Jani gani? Innocent akauliza

“ah ! Innocent usijifanye hulifahamu jani bwana.Bangi” Marina akasema.Innocent akastuka,akafikiri kidogo halafu akasema

“Kuwa huru,we puliza tu” Innocent akajibu .Marina akatoa pakiti lililokuwa na bangi akaiweka mezani ,akachambua ,halafu akafunga katika karatasi moja nyeupe ,akainuka na kusogea pembeni,akaiwasha na kuvuta yote.alipomaliza akarudi sofani.
“sasa hapa najisikia kidogo afadhali” Marina akasema.Innocent akaendelea kumwangalia kwa mshangao.
“Innocent usishangae.Haya ndiyo maisha yangu.Bila kupata hii kitu maisha yangu hayaendi.Jani ndilo kila kitu kwangu,ndilo linanifanya niwe jasiri katika kukabiliana na maisha haya Hili ndilo linanifanya niwe kamanda.”Marina akasema.

“Marina hebu naomba unieleze historia ya maisha yako .”
Marina akamtazama Innocent ,macho yake yakiwa makavu halafu akasema
“kwa kuwa umeonyesha ni jinsi gani ulivyomstaarabu na mwenye utu ,nitakueleza bila kukuficha historia yangu yote hadi hapa nilipo japokuwa inaniumiza sana.” Marina akasema halafu akachukua glasi na kuumalizia mvinyo uliokuwa umebakia akatoa sigara na kuiwasha.
“Samahani kama ninakukera Innocent lakini siku zote nikiwa na mawazo mengi ni lazima nivute sigara “
“Usijali Marina jisikie huru” Innocent akajibu.
Marina aliivuta sigara ile kwa hisia kubwa akapuliza moshi mwingi juu huku Innocent akiendelea kumshangaa.Ilikuwa ni mara ya kwanza kushuhudia binti mdogo aliyekuwa amekubuhu katika ulevi namna ile.
“Historia yangu imeanza hivi” Akasema Marina huku akiishikilia sigara yake kwa mkono wa kulia.

“ Katika maisha yangu sikuwahi kumjua baba yangu mzazi.Kwa mujibu wa maelezo ya mama ni kwamba hata yeye hakumfahamu baba yangu ni nani. “ Marina akasema halafu akavuta tena sigara yake na kupuliza moshi juu ,akamtazama Innocent halafu akaendelea.

“kwa mujibu wa maelezo aliyonipa mama yangu,yeye alitokea mkoani Morogoro.Anadai kwamba huko alikotoka alikuwa yatima kwa hiyo baada ya taabu nyingi alizokuwa akipata kijijini kwao ,ikamlazimu kuja jijini dar es salaam kutafuta maisha.Alipofika hapa hakuwa na ndugu wala mtu yeyote aliyemfahamu.Alitafuta kazi sana bila mafanikio.baadae akapata kazi ya kuosha vyombo katika mgahawa wa mama mmoja maeneo ya Yombo.Kazi hiyo haikuwa na mshahara wa kutosha hivyo ikamlazimu kuacha kazi hiyo na kutafuta kazi nyingine.Alifanya kazi mali mbali kama kufua nguo za watu,kazi za ndani lakini bado hali ya maisha yake haikubadilika.Kwa kuwa alikuwa bado msichana mdogo na umbo lake lilikuwa la kupendeza akaamua kujiingiza katika biashara ya kuuza mwili baada ya kushawishiwa na rafiki zake.Alianza kuifanya biashara hiyo akiwa na umri wa miaka 18.Baada ya muda mfupi aliiona biashara hii kama ndiye mkombozi kwake kwa sababu iliweza kumsaidia kukidhi maisha yake na kumsaidia kimaisha.”
Marina akatulia tena akawasha sigara nyingine na kuvuta mikupuo kadhaa halafu,akaendelea na simulizi yake.

“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba kutokana na kuwa na wanaume wengi ambao hawakutaka kufanya mapenzi salama ,alikuwa akipata mimba nyingi na kutoa kwani hakuwa tayari kulea mtoto.Baada ya kuitoa mimba karibu saba akapata mimba nyingine na akajishauri sana katika kuitoa mimba ile na akaamua asiitoe ,akailea mimba ile na hatimaye akafanikiwa kuzaa mtoto ambaye ni mimi.Hata baada ya kunizaa mimi bado mama aliendelea na biashara ya ukahaba.Nikiwa darasa la tano mama akaanza kuumwa.hali yake ikazidi kuwa mbaya kadiri siku zilivyokuwa zikisonga.Maisha yetu yalibadilika kuanzia hapo kwa sababu maisha yetu kwa ujumla yalitegemaa biashara ile ya ukahaba aliyokuwa akiifanya mama.Mama akawa hawezi kutoka ndani na kwenda kufanya tena biashara ile na ndipo ilipobainika kwamba alikuwa ameathirika na virusi vya ukimwi.Hali ilikuwa mbaya ikanibidi kujiingiza katika biashara aliyokuwa akiifanya mama ya kuuza mwili kipindi hicho nikiwa mtoto mdogo wa miaka kumi na moja tu.Nilifanya biashara ile na kupata fedha za kumtibu mama na kuendesha maisha yetu.Wale waliokuwa wateja wa mama wakageuka na kuwa wateja wangu.Niliendelea na biashara ile na mwishowe ikanilazimu kuacha shule ili niweze kupata muda mzuri wa kufanya kazi ile.Nikakubuhu ukahaba katika umri mdogo.”
Marina akavuta tena sigara,akakaa kimya kidogo halafu akachukua chupa ile ya mvinyo akamimina mvinyo katika glasi akapiga funda kubwa halafu akaendelea.
“Siwezi kusahau uchungu nilioupata baada ya mama yangu kufariki dunia.Yeye ndiye aliyekuwa ndugu yangu pekee ninayemfahamu.Yeye ndiye alikuwa kila kitu kwangu.baada ya mama kufariki sikuwa na namna nyingine ya kufanya kwa sababu hakukuwa na mtu au ndugu wa kuweza kunisaidia katika maisha hali iliyonilazimu kuendeleza kazi hii ya ukahaba mpaka hivi leo.” Marina akasema halafu akainama na kuivuta sigara yake,akatazama juu na kupuliza moshi hewani.

“Haya ndiyo maisha yangu Innocent.” Marina akasema.Innocent akamtazama usoni akamuonea huruma sana.
“Pole sana Marina.”
“Ahsante Innocent “ Marina akasema na kuizima sigara yake iliyokuwa imemalizika.
“Hebu niambie ukweli Marina.Kazi hii inakuingizia kipato cha kutosha kuweza kukidhi mahitaji yako ya kila siku? Innocent akauliza
“Inategemea na siku.Kuna baadhi ya siku tunaingiza pesa ya kutosha na baadhi ya siku unamaliza hata usiku mzima huna mteja yeyote.Kiujumla maisha ni magumu na tunakumbana na matatizo mengi kama vile wateja wakorofi ambao wanakutumia na kugoma kukulipa fedha.” Marina akasema na kutazama juu.Innocent akamtazama usoni kwa huruma halafu akasema
“Marina historia ya maisha yako imenigusa sana .najua uliamua kuifanya kazi hii si kwa kuipenda bali ni kwa sababu hukuwa na njia nyingine ya kuweza kuishi.Toka moyoni mwangu nimeamua na niko tayari kukusaidia ili uweze kuondokana na maisha haya unayoyaishi.”
“Innocent katika maisha yangu yote sijawahi kutana na mtu yeyote ambaye ameonyesha kuguswa na matatizo yangu na kuamua kunisaidia.Nashukuru sana kwa hilo Innocent lakini sioni kama kuna haja ya kunisaidia na wala sioni sababu ya kunisaidia.maisha yangu yamekwishaharibika Maisha haya nimekwisha yazoea na sidhani kama kuna maisha mengine zaidi ya haya.” Marina akasema

“hapana Marina usiseme hivyo.Haya si maisha yako .Bado umri wako mdogo na una kila sababu ya kuishi maisha mazuri na yenye furaha.Unastahili maisha mazuri.” Innocent akasema
“hapana Innocent.Sihitaji maisha mazuri.Haya ndiyo maisha yangu.Sina baba,sina mama,sina ndugu yeyote sasa maisha mazuri niyatafute ya nini? Nimeridhika na maisha ninayoishi kwa sasa.”


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“Marina historia ya maisha yako imenigusa sana .najua uliamua kuifanya kazi hii si kwa kuipenda bali ni kwa sababu hukuwa na njia nyingine ya kuweza kuishi.Toka moyoni mwangu nimeamua na niko tayari kukusaidia ili uweze kuondokana na maisha haya unayoyaishi.”
“Innocent katika maisha yangu yote sijawahi kutana na mtu yeyote ambaye ameonyesha kuguswa na matatizo yangu na kuamua kunisaidia.Nashukuru sana kwa hilo Innocent lakini sioni kama kuna haja ya kunisaidia na wala sioni sababu ya kunisaidia.maisha yangu yamekwishaharibika Maisha haya nimekwisha yazoea na sidhani kama kuna maisha mengine zaidi ya haya.” Marina akasema

“hapana Marina usiseme hivyo.Haya si maisha yako .Bado umri wako mdogo na una kila sababu ya kuishi maisha mazuri na yenye furaha.Unastahili maisha mazuri.” Innocent akasema
“hapana Innocent.Sihitaji maisha mazuri.Haya ndiyo maisha yangu.Sina baba,sina mama,sina ndugu yeyote sasa maisha mazuri niyatafute ya nini? Nimeridhika na maisha ninayoishi kwa sasa.”



ENDELEA………………………………………



“Marina hebu nisikilize kwa makini.Ni kweli nina nia ya dhati ya kukuondoa katika maisha haya unayoyaishi .”
“Innocent nimekwisha kwambia unapoteza muda wako bure wa kutaka kunisaidia.Sielewi unataka kunisaidia vipi kwa sababu hapa nilipo sina hata elimu ya kutosha,sina ujuzi wowote wa biashara iwapo utataka kunipatia mtaji wa biashara Innocent tafadhali usipoteze muda wako mwingi katika jambo hili.”
“Marina nimekuelewa vizuri sana.Lakini pamoja na sababu ulizozieleza bado nina lengo la kukusaidia na kukutoa katika maisha haya unayoyaishi sasa hivi.Kuhusu elimu nitakusaidia ili uweze kupata elimu hadi chuo kikuu na kuhusu…….”
Kabla hajaendelea Marina akaanza kucheka.
“hahahahahaaaaa !! leo umenifurahisa sana Innocent.Yaani mimi Marina nikasome?

“Ndiyo Marina hilo linawezekana kabisa.Marina unahitaji kukubali mabadiliko.bado u msichana mdogo na ambaye hustahili kuishi maisha haya unayoyaishi.”
“Innocent kama unataka kunisaidia ,labda unipe fedha za kutosha”
“Fedha si tatizo Marina.Ninaweza kukupa mamilioni ya fedha lakini hayatakusaidia kitu chochote.Ninachokitaka ni mabadiliko ya kifikra,kimaisha na kiroho pia.Unatakiwa uishi maisha yenye kumpendeza Mungu siku zote na ni yeye ndiye atakayekunyooshea mkono wake na kukumiminia baraka zake nyingi na utakuwa na maisha ya amani na furaha tele daima.”
“hahahaaaa ! Leo nimekutana na mchungaji..Hahahaa” marina akacheka kwa nguvu.
“Kumbe hata ninyi wachungaji huwa mnafuata makahaba..hahahaa”
Innocent hakujibu kitu akaendelea kumtazama Marina aliyekuwa akicheka kicheko kikubwa.
“nadhani hatutaweza kuelewana.Tayari amekwisha lewa huyu.Ngoja nimsubiri mpaka asubuhi ulevi utakapokuwa umemtoka kichwani.Amenigusa sana mtoto huyu ,kamwe siwezi kuacha kumsaidia.Atake asitake ni lazima abadilike.Nitafanya kosa kubwa sana iwapo nitamuacha mtoto mzuri kama huyu aendelee kupotea.Mungu aliyenipa mimi uwezo ndiye aliyemnyima huyu binti hivyo ninapaswa kumsaidia kwa kila namna ninavyoweza.” Akawaza Innocent huku akimtazama Marina ambaye alikuwa ameanza kusinzia.Inno akamlaza vizuri pale sofani halafu akachukua shuka akamfunika vizuri yeye akapanda kitandani akajilaza.Ni usiku ambao Innocent alikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na jinsi atakavyomsaidia Marina.
Saa kumi na mbili za asubuhi Innocent akaamka.Kitu cha kwanza ilikuwa ni kumtazama Marina kama yupo kwa sababu alikwisha sikia sifa za makahaba kwamba huvizia usiku ambapo mteja wake amelala fofofo kisha hubeba kila kitu na kutokomea zake .Marina bado alikuwa amelala pale sofani.
Inno akainuka pale kitandani akanawa uso halafu akamwamsha Marina.

“Ouh kumbe kumekucha? Marina akasema kwa uchovu huku akiinuka na kujinyoosha.

“Amka nikupeleke nyumbani kwako” Innocent akasema
Marina akakaa pale sofani huku ameinama chini.baada ya dakika kama mbili hivi akainua kichwa na kuiona chupa ile ya mvinyo akaitikisa na kukuta bado mvinyo ulikuwepo akajimiminia katika glasi na kuunywa wote.

“Du ! Afadhali nimezimua manake nilikuwa nahisi kufa kufa.” Marina akasema huku Innocent akimtazama kwa mshangao.
“twende ukaniache mitaa ya kati” Akasema Marina
“nataka nifahamu mahala unapoishi” Innocent akasema
“Mimi naishi gheto na washkaji zangu.Mtu kama wewe hapakufai”
“Usijali Marina.Hata kama ungekuwa unaishi jalalani ningekufuata tu kujua mahala unapoishi” Innocent akasisitiza.
Wakatoka mle hotelini na kuingia garini na safari ikaanza ya kuelekea mahala anakoishi Marina.
“Simamisha gari hapa kwa sababu huko tunakoenda gari yako haiwezi kupita.” marina akamwambia Innocent ambaye alisimamisha gari wakashuka.Marina akamuita kijana mmoja aliyekuwa amesimama katika kibaraza kimoja.
“Juma hebu ilinde hii gari ya mshkaji naingia naye hapo maskani.Usijali jamaa atakutoa na kitu kidogo” Marina akasema huku akiwasha sigara.Innocent akatoa noti mbili za elfu kumi kumi na kumpatia yule jamaa aliyezipokea huku akishukuru.
Toka walipoacha gari walitembea kama mita mia mbili ,wakafika katika nyumba moja iliyochakaa,wakazunguka uani na kuingia katika chumba kimoja kilichokuwa na giza.
“Karibu Innocent.hapa ndio maskani kwetu” marina akasema huku akilifungua dirisha kwa ajili ya kupata mwanga na hewa. Innocent akapigwa na butwaa kwa mambo aliyoyaona mle ndani.Chumba kilinuka harufu mbaya ya uvundo iliyochanganyika na harufu ya moshi wa sigara,na bangi.Kondom zilizokuwa zimetumika zilitapakaa hovyo mle ndani.Juu ya mfuko wa nailoni kulionekana mabomba matatu ya sindano ambazo huwa wanazitumia katika kujidunga madawa ya kulevya.Mle ndani kulikuwa na kitanda kimoja ambacho juu yake walilala wasichana watano wengine wakiwa uchi.Innocent akahisi kama anataka kutapika.Akatoka nje akapiga chafya mfululizo ..

“Du ! siamini kama ndani ya chumba kile wanakaa binadamu. Chumba kidogo namna ile wanalala watu zaidi ya saba !!….” Wakati akiendelea na kuwaza alichokiona mle ndani akatoka mwanadada mmoja aliyevaa kaptura fupi na fulana ndogo .Mikononi alikuwa amejichora michoro na maandishi mengi.Macho yake yalikuwa mekundu na kwa jinsi alivyoonekana hakuwa mtu wa masihara.Moja kwa moja akamuelekea Innocent pale alipokuwa amesimama.

“kaka habari” Akasema dada yule mwenye sauti nzito kama ya mwanaume.
“Nzuri habari yako” Innocent akajibu
“Wewe ndiye umekuja na Marina? Akauliza kwa sauti ya ukali
“Yes ndiye mimi” Innocent akajibu.
“Mbona sasa uko nje? Si tabia nzuri hebu karibu ndani ukae.Au umeona hapalingani na hadhi yako?.Karibu ndani nina maongezi kidogo na wewe.Mimi ndiye mkubwa wa ghetto hili.” Akasema dada yule huku akigeuka na kurudi chumbani.Kwa kuwa alikuwa na lengo la dhati la kumsaidia Marina Innocent akakubali kurudi tena mle chumbani.Akafunua pazia na kuingia ndani.Kitu cha kwanza alichokutana nacho ni moshi wa bangi.Yule dada aliyesema kwamba yeye ndiye mkuu wa chumba kile alikuwa amegeukia ukutani akivuta bangi.Marina alikuwa amekaa chini pembeni ya kitanda akiwa anachambua bangi Innocent akapewa ndoo ya maji akalie kwa kuwa ndani mle hakukuwa na kiti wala kitu chochote cha kukalia.Kwa dakika zile chache alizokuwa amekaa mle ndani Innocent akahisi kama kizungu zungu kutokana na moshi wa bangi uliokuwa umejaa mle ndani na kusababisha kukosekana kwa hewa ya kutosha.
Akiwa bado anashangaa shangaa akastukia akishikwa mabega na yule dada mkubwa wa kile chumba.Kabla hajajua nini kinaendelea akajikuta akifunguliwa vifungo vya shati.Akasimama.
“Nini kinaendelea hapa? Innocent akauliza kwa mshangao

“Ina maana hujui kinachoendelea? Mwanaume yoyote akiingia humu ndani kitu cha kwanza ni lazima alale na mimi kwanza.Nashukuru Mungu Marina amekuleta kwa sababu usiku kucha wa jana sijapata mwanaume hata wa kulala naye bure.Leo utakata kiu yangu” Akasema dada yule mwenye sauti nzito na ambaye alionyesha kutokuwa na masihara.Macho yake yalikuwa mekundu na yaliashiria hakuwa akitania kwa kitendo kile.Kwa kasi na nguvu Innocent akamsukuma dada yule akaangukia ukutani na hivyo kumpa nafasi ya kuweza kuponyoka.Kabla hajatoka mlangoni akakutana na dada mwingine ambaye naye alikuwa akirudi kutoka katika mihangaiko yake.
“Ziada hebu mzuie huyo” Akasema yule dada aliyesukumwa na Innocent akimwambia yule mwenzake aliyesimama mlangoni amzuie Innocent.Ziada aliyekuwa amesimama mlangoni akamsukumia Innocent ndani na kujikuta akidakwa shati na dada yule aliyemuangusha chini.Ikaanza purukusahani kubwa kati ya wale akina dada na Innocent.Purukushani zile zikawavuta majirani ambao walimuokoa Innocent ambaye kwa wakati huo hakuwa na shati.Suruali yake ilikuwa imechanwa chanwa.Simu yake ilikuwa imechukuliwa halikadhalika pochi yake iliyokuwa na fedha.

“Nini kimetokea hapa? Mjumbe wa eneo lile ambaye alifika mara moja baada ya kuarifiwa kuhusu vurugu ile aliuliza.

“Mjumbe, huyu kaka amelala na mdogo wangu Marina na asubuhi hii amekataa kumlipa fedha na kutaka kukimbia,ndio maana tumeamua kumfundisha adabu ili asirudie tena kitendo kama hiki.” Akajibu mwanadada yule mkubwa wa ghetto.
“Eti Marina ni kweli hayo anayoyasema Mwanaidi? Mjumbe akauliza
Marina akakaa kimya huku akitazama chini.
“Marina hebu sema ukweli haraka “ Akaamrisha Mwanaidi ambaye alionekaa kuwa na amri kwa wasichana wote waliokuwa wakiishi katika chumba kile.
“Ni kweli mjumbe” Marina akasema huku akitazama chini.Innocent hakuyaamini masikio yake.Akabaki akiuma meno kwa hasira.Alikosa la kuongea.Hakutegemea kama Marina angeweza kumgeuka kiasi kile.
Mjumbe akamshika mkono Innocent na kuanza kuondoka naye eneo lile ambalo tayari lilianza kujaa watu.Innocent alihisi aibu ya aina yake.Katika maisha yake hakuwahi kuaibika kiasi kile.Alikuwa kifua wazi hakuwa na shati wala viatu.Suruali yake ailikuwa imechanwa chanwa.Kila mtu aliyekuwa akimuona alikuwa akimcheka.
“Huyooooo…kaumbuka leo”

“Sharobaro kaumbuliwa na changu doa !!!!…” Hizi zilikuwa ni kauli za kubeza zilizotolewa na watu walioshuhudia kitendo kile.Zilimuumiza mno Innocent .
“Kijana ninavyokuona wewe hufanani kabisa na mazingira haya.Kwa nini lakini umeamua kujidhalilisha namna hii kijana wangu?” Mjumbe akasema huku akimuongoza Innocent nyumbani kwake kwa madhumuni ya kumpatia shati la kuvaa na viatu.
“Mjumbe sijui hata nikueleze nini.Hapa nilipo siwezi hata kuongea.Katika maisha yangu sijawahi kukutwa na tukio kama hili la leo.Tukio hili limenifunza mambo mengi sana.Nashukuru mjumbe kwa kuniokoa kwa sababu mabaradhuli wale walikuwa wanifanyie kitu kibaya sana.” Innocent akasema
“Unatakiwa uwe makini sana unapojihusisha na akinadada kama wale.Si watu wazuri hata kidogo.Hata sisi hapa mtaani tuna mpango wa kuwaondoa kwa sababu imekuwa kero kubwa kwa watoto na wake zetu.Mipira ya kiume iliyotumika inaonekana imezagaa hovyo maeneo wanayoishi na watoto wetu wadogo wanaiokota na kuichezea kitu ambacho ni hatari kubwa.Sisi kama serikali ya mtaa tumefikia uamuzi wa kuwaondoa kabisa maeneo haya.Zoezi hili la kuwaondoa litaanza hivi karibuni” Akasema mjumbe.Innocent alikuwa amejiinamia chini akitafakari.
Mjumbe alimpatia shati suruali na viatu.Ingawa hazikumtosha Vyema lakini alishukuru kwa msaada ule uliomsitiri na aibu ile kubwa iliyompata.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Mjumbe sijui hata nikueleze nini.Hapa nilipo siwezi hata kuongea.Katika maisha yangu sijawahi kukutwa na tukio kama hili la leo.Tukio hili limenifunza mambo mengi sana.Nashukuru mjumbe kwa kuniokoa kwa sababu mabaradhuli wale walikuwa wanifanyie kitu kibaya sana.” Innocent akasema
“Unatakiwa uwe makini sana unapojihusisha na akinadada kama wale.Si watu wazuri hata kidogo.Hata sisi hapa mtaani tuna mpango wa kuwaondoa kwa sababu imekuwa kero kubwa kwa watoto na wake zetu.Mipira ya kiume iliyotumika inaonekana imezagaa hovyo maeneo wanayoishi na watoto wetu wadogo wanaiokota na kuichezea kitu ambacho ni hatari kubwa.Sisi kama serikali ya mtaa tumefikia uamuzi wa kuwaondoa kabisa maeneo haya.Zoezi hili la kuwaondoa litaanza hivi karibuni” Akasema mjumbe.Innocent alikuwa amejiinamia chini akitafakari.
Mjumbe alimpatia shati suruali na viatu.Ingawa hazikumtosha Vyema lakini alishukuru kwa msaada ule uliomsitiri na aibu ile kubwa iliyompata.



ENDELEA……………………………………..


“Mjumbe nashukuru sana mzee wangu kwa msaada wako huu mkubwa.Sijui ningepita mtaa upi leo.Hili ni fundisho kwangu.Sina cha kukupa mjumbe lakini naomba siku ya jumatatu ufike katika kampuni ya Benard & Sons company useme unahitaji kuonana na ndugu Innocent basi utaletwa moja kwa moja kwangu.Nahitaji kukupa ahsante kwa msaada wako mkubwa ulionisaidia..Tafadhali usikose mzee” Innocent akasema
“Nitafika bila kukosa .Siwezi kukosa kijana wangu..Halafu kabla hujaondoka mimi naitwa Bw.Mustapha kinyezi mwenzangu unaitwa nani?
“Mimi naitwa Innocent “ Innocent akasema huku akiinuka na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na mjumbe hadi mahala alipokuwa ameegesha gari lake .
“Mjumbe nashukuru tena kwa kila kitu.Nadhani tutaonana hiyo jumatatu” Innocent akasema huku akiufungua mlango wa gari.Katika mapambano yale na wale makahaba kitu kikubwa alichokuwa akikichunga ni funguo za gari .Bahati nzuri hazikuweza kupotea.
“Hili ni gari lako” akauliza mjumbe kwa mshangao
“ndiyo Mjumbe hili ni gari langu” Innocent akajibu na kuagana na mjumbe ,akaliondoa gari kwa kasi maeneo yale .


* * * *


Hakuna mtu aliyegundua kwamba Innocent alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtoka.Aliumia mno kwa kitendo alichofanyiwa.
“Siamini kama wema wangu leo umetaka kunitokea puani.Makahaba wale wameniabisha mno .Aibu niliyoipata ni kubwa mno.Nimetaka kubakwa hivi hivi.”
Akawaza Innocent.
Saa nne za asubuhi akawasili nyumbani kwao.Alikuwa amesawajika sana .Hakutaka kuongea na mtu yeyote moja kwa moja akaelekea katika chumba chake kujipumzisha.
“Bado siamini kama mtu ninayeheshimika kama mimi nimedhalilishwa na machangudoa.Wamenichukulia kila kitu nilichokuwa nacho.Kama si kwa jitihada za mjumbe wangefanikiwa kunibaka wale wanaharamu.I hate them so much.Halafu Marina naye alikuwa yuko radhi kuona nikiaibishwa .Hakuwa akijali chochote.Na hata alipoulizwa kama ni kweli nililala naye na kumdhulumu fedha zake alikubali kuwa ni kweli …Masikini pamoja na wema wangu wote na kuonyesha kila dalili za kutaka kumsaidia lakini bado hakuonyesha jitihada zozote za kuukubali msaada wangu.Aliipata bahati ambayo wenzake wanaitafuta usiku na mchana lakini yeye ameichezea na kuitupa mbali….Masikini mtoto mdogo kama yule anaangamia hivi hivi.Mtoto mzuri mwenye umbo safi na zuri anapotea hivi hivi jamii ikimuona…..Anyway sina namna nyingine ya kuweza kumsaidia.Kwa vile yeye mwenyewe ameonyesha hataki mabadiliko katika maisha yake na mimi sina budi kuachana naye.” Innocent akawaza akiwa kitandani kwake usingizi ukamchukua akalala.


* * * *



Jumatatu asubuhi Innocent akawasili ofisini kwake.Siku hii alionekana mkimya na mwenye mawazo mengi.Kilichokuwa kikimsumbua kichwa ni tukio lililomtokea siku iliyotangulia la kudhalilishwa na Marina pamoja na kundi lake la wasichana makahaba.Kitendo kile kilimuumiza sana kila alipokuwa akikumbuka.

“lengo langu lilikuwa zuri sana lakini sijui kwa nini msichana yule hakutaka kunielewa.Marina ameikosa bahati ambayo wenzake walio kama yeye wanaitafuta usiku na mchana.Ngoja niachane naye niendelee na kazi zangu japokuwa kila mara sura yake inanijia akilini na kunifanya nimkumbuke lakini sina namna nyingine ya kuweza kumsaidia.” Akawaza Innocent huku akiwa amekiegemeza kichwa chake katika kiti cha kuzunguka.Akiwa katika tafakari mara simu ya mezani ikalia akaiinua na kuiweka sikioni.
“Bosi kuna mtu mmoja anahitaji kukuona anasema ulimuahidi aje akuone leo hii ofisini.Anasema anaitwa Bw Mustapha.” Alisema katibu muhtasi wa Innocent.

“Ok mwambie apite ndani ” Innocent akasema na mara kumbu kumbu za tukio lililotokea jana zikarudi

“Mzee Mustapha habari yako? Innocent akasema baada ya Mzee Mustapha kuingia mle ofisini kwake.

“Ouh ! Mr Innocent habari yako? Akasema Mustapha katika hali ya mshangao kidogo.
“karibu kiti Mzee Mustapha.” Innocent akasema huku akitabasamu.
“Ahsante sana Innocent nimeshakaribia.” Akasema Mustapha
“habari za toka tulipoachana jana? Innocent akauliza
‘habari nzuri Bw Innocent.Pole sana na majukumu” mzee Mustapha akasema
‘Nashukuru sana mzee Mustapha.”
Mustapha alikuwa akitabasamu kana kwamba anatafuta kitu cha kuongea.
“Hongera sana Bw innocent,sikutambua toka mwanzo kama wewe ni mtu mkubwa namna hii katika kiwanda kikubwa kama hiki.” Mustapha akasema huku akitabasamu.

‘ Bw Mustapha mimi huwa sipendi kuonekana kwa watu kama meneja au mtu mwenye uwezo wa juu .Napenda kuishi maisha ya kwaida sawa na watu wengine wenye uwezo wa kawaida.”
Innocent akasema na kuifungua droo moja kati ya nne zilizoko katika meza yake akatoa bahasha nyeupe iliyokuwa imetuna

“Bw Mustapha nilikuahidi kukupa ahsante yangu kwa namna ulivyonisaidia jana asubuhi.kama si wewe ningeaibishwa sana na wale wanawake.Ahsante yangu ni hii hapa” Innocent akasema na kumkabidhi Mustapha ile bahasha.

“Bw Innocent nashukuru sana sana .U kijana muungwana sana.Napenda vile vile nikupe pole kwa tukio lile lililotokea.Lilikuwa ni tukio baya sana ambalo limekujengea picha mbaya .Mimi wale wasichana wanaishi eneo langu.Ninawafahamu vizuri sana na kama serikali ya mtaa tumepanga tuwaondoe eneo lile kutokana na athari wanazozisababisha kwa watoto wetu na wake zetu. wanaleta picha mbaya kwa vijana wetu wa shule ambao wanarubuniwa na kushawishika kufanya ngono isiyo salama na makahaba wale.Kwa ufupi ni kwamba tumechoshwa na wasichana wale na hivi nikwambiavyo tuko katika mkakati mkubwa wa kuwaondoa na zoezi hilo litafanyika muda wowote hivi karibuni.” Mustapha akasema huku akiiweka ile bahasha aliyopewa mfukoni
“Bw Mustapha mimi nakubaliana na wazo lako la kuwaondoa mahakaba wale toka katika mtaa wenu.Nilifanikiwa kuingia ndani mwao na kuangalia maisha wanayoyaishi kwa kweli si maisha ya kuishi binadamu na hasa wasichana kama wale.”Innocent akasema

“Kweli kabisa Innocent ,wasichana wale ambao wengi wao wana nguvu na uwezo wa kuweza kufanya kazi nyingine za kuwaingizia kipato halali,wanaishi kama wanyama ndani ya zizi.Maisha yao ni ajabu ajabu sana.Unajua mimi nilishangaa mno na nimejiuliza maswali mengi bila majibu kwamba iweje kijana mzuri ,mwenye heshima na uwezo wake ,kijana ambaye ana uwezo wa kumpata mwanamke yeyote amtakaye awafuate wale makahaba? Nimejiuliza sana bila kupata majibu”
Innocent akatabasamu na kusema
“Mzee Mustapha ukweli ni kwamba mimi sikuwa nimewafuata makahaba.Mimi ni kijana niliyelelewa katika maadili mazuri,familia yetu inauwezo mkubwa kiuchumi na hata kiwanda hiki ni mali ya familia.Katika maisha yangu sikuwahi kuota kama iko siku ningeweza kuwafuata wasichana kama wale.Kwa ufupi tu nikwamba mimi huwa ninaumia sana moyo ninapomuona binadamu mwingine akiteseka ama kuishi maisha ya shida hali mimi nina uwezo wa kutosha.Nimekuwa nikisaidia watu wengi tu ili waweze kuondokana na maisha wanayoyaishi .Siku ya jumamosi nikiwa na dada yangu na rafiki zetu kadhaa tulikwenda katika klabu moja ya burudani ili kustarehe kidogo baada ya shughuli za wiki nzima.Tukiwa pale nilimuona msichana ambaye baadae nilimtambua kama Marina akiwa kati kati ya kundi la makahaba.Kwa kweli niliumia sana na kujiuliza ni kitu gani kilipelekea msichana mdogo kama yule kuwapo usiku ule na makundi kama yale.Nilikuwa na nia ya dhati ya kumsaidia ,lakini kwanza nilitaka kumfahamu japo kwa undani kidogo ili nione ni jinsi gani nigeweza kumsaidia.Nilifanikiwa kuondoka naye kama mtu niliyekuwa nikitaka kulala naye kwa usiku.Nilikwenda naye hotelini lakini si kwa lengo la kufanya naye mapenzi kama yeye alivyokuwa akifikiri..Nilichokuwa nakitaka ilikuwa kumfahamu japo kwa ufupi na kujua sababu zilizopelekea yeye kujiingiza katika biashara ile .Alinieleza historia yake kwa ufupi ambayo kwa kweli inasikitisha sana.Nilimuonea huruma na kuamua kwa moyo wa dhati kabisa kumsaidia.Marina hakuwa tayari kwa msaaada niliokuwa nataka kumpatia ikiwa ni pamoja na kumpeleka shule na baadae kumtafutia kazi nzuri na kuyabadili maisha yake.Sikukata tamaa nikaamua kwenda naye hadi mahala anapoishi ili nione ni maisha ya namna gani anayaishi.Nilistuka sana na aina ya maisha wanayoishi wasichana wale baada ya kufika mahala anapoishi Marina.Nilishindwa kukaa katika chumba chao nikatoka nje.Pale nje nikafuatwa na mwanamke mmoja ambaye alionekana kama ndiye mkubwa wao akaniomba niingie ndani.Nilikubali nikaingia ndani na ndipo hapo purukushani ilioanza Walidai eti ni lazima nifanye mapenzi nao wote.Sikuwa tayari kwa upuuzi ule ndipo hapo vurugu ilipozuka hadi pale ulipotokea na kuniokoa toka mikononi mwa makahaba wale.Kibaya zaidi ni kwamba wakati nataka kufanyiwa mambo yale ya ajabu Marina alikuwa akiniangalia huku akivuta sigara yake akitabasamu.Inaonekana alikuwa amefurahi mimi kufanyiwa vile.Wema wangu,fadhila zangu vyote hakuviona kabisa.Nasikitika sana Mzee Mustapha kwa mambo waliyonifanyia,lakini mimi sikuwa nimekwenda pale kwa ajili ya kutafuta mapenzi,bali nilikuwa na lengo zuri la kutaka kumsaidia Marina.” akasema na kukaa kimya kwa muda huku akimtazama Mzee Mustapha.
“Pole sana Innocent kwa mkasa uliokupata.Sasa nimekuelewa vizuri.Nasikitika sana kwa binti mdogo kama yule kukataa msaada uliokuwa unataka kumpatia na akakubali wenzake watake kukufanyia kitendo kibaya.Lakini pamoja na yote yaliyotokea na baada ya kufahamu nini lilikuwa lengo lako ninaomba niongee mambo machache .” Mzee Mustapha akasema.

“hakuna shida mzee wangu unaweza kuendelea” akajibu huku akikaa makini kumsikiliza
“Ninamfahamu Marina toka amezaliwa.Ninamfahamu marehemu mama yake toka alipohamia katika mtaa wangu,ninayafahamu maisha aliyokuwa akiyaishi.Marina ni mmoja kati ya watoto waliopitia maisha magumu na ya shida mno baada ya mama yake kufariki dunia kwani alikuwa bado mdogo sana..Mara nyingi nimekuwa nikisononeka moyo ninapoyaona maisha anayoyaishi.Mimi mwenyewe si mtu mwenye uwezo mkubwa,laiti kama ningekuwa na uwezo wa kutosha ningeweza hata kuchukua jukumu la kumlea kipindi kile mama yake alipofariki dunia kwani ndicho kipindi Marina alipobadilika na kuamua kuacha shule na kujiingiza rasmi katika biashara ya ukahaba.Innocent ninaamini kwamba Mungu amekuleta ili uweze kumsaidia binti yuile na kuyabadili maisha yake.najua si kazi rahisi lakini kama kweli una nia ya dhati ya kumsaidia binti yule tafadhali usiache.Jitahidi kwa kila namna unavyoweza na umsaidie Marina.Najua kwa kitendo walichokufanyia rafiki zake hutakuwa na hamu tena hata ya kumuona Marina.Lakini nakusihi sana usije ukaachana na mpango wako wa kumsaidia Marina.Ni binti ambaye anahitaji msaada mkubwa kwanza wa kiushauri na baadae kimaisha.”
Maneno yale ya mzee Mustapha yakamuingia Innocent na kutokea upande wa pili wa sikio.Hakuwa na hamu tena ya kumuona Marina katika uso wake kutokana na namna walivyomtenda.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Ninamfahamu Marina toka amezaliwa.Ninamfahamu marehemu mama yake toka alipohamia katika mtaa wangu,ninayafahamu maisha aliyokuwa akiyaishi.Marina ni mmoja kati ya watoto waliopitia maisha magumu na ya shida mno baada ya mama yake kufariki dunia kwani alikuwa bado mdogo sana..Mara nyingi nimekuwa nikisononeka moyo ninapoyaona maisha anayoyaishi.Mimi mwenyewe si mtu mwenye uwezo mkubwa,laiti kama ningekuwa na uwezo wa kutosha ningeweza hata kuchukua jukumu la kumlea kipindi kile mama yake alipofariki dunia kwani ndicho kipindi Marina alipobadilika na kuamua kuacha shule na kujiingiza rasmi katika biashara ya ukahaba.Innocent ninaamini kwamba Mungu amekuleta ili uweze kumsaidia binti yuile na kuyabadili maisha yake.najua si kazi rahisi lakini kama kweli una nia ya dhati ya kumsaidia binti yule tafadhali usiache.Jitahidi kwa kila namna unavyoweza na umsaidie Marina.Najua kwa kitendo walichokufanyia rafiki zake hutakuwa na hamu tena hata ya kumuona Marina.Lakini nakusihi sana usije ukaachana na mpango wako wa kumsaidia Marina.Ni binti ambaye anahitaji msaada mkubwa kwanza wa kiushauri na baadae kimaisha.”
Maneno yale ya mzee Mustapha yakamuingia Innocent na kutokea upande wa pili wa sikio.Hakuwa na hamu tena ya kumuona Marina katika uso wake kutokana na namna walivyomtenda.



ENDELEA………………………………


“Mzee Mustapha nashukuru kwa ushauri wako,lakini sidhani kama nitathubutu tena kutaka kumsaidia Marina.Nilikuwa tayari kufanya jambo lolote lile ili kuweza kuyabadilisha maisha yake lakini hakuonesha kukubaliana nami na kukubali kubadilika badala yake akafurahi kuona wenzake wakinidhalilisha.Mzee Mustapha kila nikilikumbuka tukio lile ninapatwa na hasira na uchungu moyoni.Ni tukio la kwanza la aibu kuwahi kunitokea.Sidhani kama nitaweza tena kufikiria kumsaidia msichana yule asiye na shukrani.” akasema huku akiuma meno kwa hasira.

“Innocent nakubaliana nawe kwamba kitendo walichokufanyia si cha kibinadamu.Lakini naomba uelewe kitu kimoja kwamba wale wasichana kwa sasa wanatumia dawa za kulevya,bangi na kila aina ya ulevi.kwa maana hiyo naweza sema kwamba akili zao si nzuri na ndiyo maana wanaweza wakafanya kitendo chochote hata cha aibu bila kuona haya.Hebu jaribu kuivuta picha ya Marina akiwa ndani ya kile chumba wanachoishi,halafu vuta tena picha nyingine ya Marina akiwa ni binti mrembo,mzuri akiwa ndani ya gari lake anaendesha.nafikiri unapata picha mbili tofauti kabisa.Picha ya pili inawezekana kabisa lakini kuna vikwazo vingi hadi Marina akawa ni msichana wa kwenye picha ya pili.Ili Marina afikie hatua ya kuwa msichana wa picha ya pili ni lazima apate msaada mkubwa wa kumtoa hapa alipo sasa.Kumtoa Marina hapa alipo panahitaji watu wenye moyo mkubwa wa huruma na kujitolea.Nikiyatazama macho yako ninaona kabisa jinsi ulivyo na huruma na moyo wa kusaidia wengine.nakuomba tafadhali pamoja na mambo yote aliyokufanyia usiache kumsaidia binti yule.” Mzee Mustapha akasema na kumtazama Innocent machoni kwa sekunde kadhaa.Innocent akainama chini akafikiri halafu akavuta pumzi ndefu na kusema.

“mzee Mustapha nimekusikia na nimekubali tena kumsaidia Marina.lakini safari hii nataka nimsaidie kwa kushirikiana nawe.Tukiunganisha nguvu zetu sote tunaweza tukamsaidia .Nimeamua kumsaidia kwa sababu ya heshima na busara zako lakini nilikwisha futa kabisa mawazo ya kumsaidia. Tena” Innocent akasema huku akimtazama Mzee mustapha usoni.Huku akitabasamu mzee Mustapha akasema
“nashukuru sana Innocent kwa kukubali tena kumsaidia mtoto yule.Nakuahidi kuwa nitakuwa nawe bega kwa bega katika kutafuta njia ya kuweza kumsaidia binti yule.Nina imani kama tutaunganisha nguvu zetu sote tutaweza kabisa kumsaidia binti yule.”

“Nakubaliana nawe mzee Mustapha ,inatubidi tuunganishe nguvu katika kumsaidia Marina.Kama tumeamua hivyo ,naomba basi unipe ushauri tufanye kitu gani ili tuweze kumsaidia.? Innocent akauliza.Mzee Mustapha akawaza kidogo halafu akasema

“Mimi ni mwenyekiti wa eneo analoishi.Ananifahamu vizuri na ananiheshimu sana.Ananisikiliza kwa lolote nitakalowambia.Nikitoka hapa asubuhi hii ninakwenda kuonana naye pale mahala anapoishi.Najua ni lazima nitamkuta kwa sababu baada ya kazi wanazozifanya usiku ,mchana kutwa huwa wanautumia kwa kulala.Nitaongea naye na nina imani atanisikiliza.Nitamsikiliza yeye ana mawazo gani na anahitaji tumfanyie nini.Lolote nitakalolipata nitakupigia simu na kukutaarifu.” Mustapaha akasema
“Nashukuru mzee Mustapha kwa mawazo yako mazuri.Basi hakuna tatizo mzee wangu wewe fanya jitihada uonane naye,zungumza naye na usikie yeye ana mawazo gani na ni jinsi gani tunavyoweza kumsaidia.Lolote utakalolipata utanitaarifu kwa kupitia namba hizi hapa kwenye kadi hii” Innocent akasema huku akimpa mzee Mustapha kadi yenye namba zake za simu.
“Usijali Innocent.Nikitoka hapa ninaelekea moja kwa moja kwa Marina halafu nitakupigia simu.” Akasema mzee Mustapha huku akiinuka tayari kwa kuondoka.

“Bw Innocent ,pamoja na yote tuliyoongea lakini nina ombi moja ndugu yangu.” Akasema mzee Mustapha akiwa amekwisha inuka kitini.

“Sema tu mzee wangu” Innocent akasema
“Unajua hapa nilipo hata mimi sina kibarua chochote .Sina kazi yoyote ya kufanya kwa sasa.kwa kuwa wewe ndiye mkuu wa kiwanda hiki hauwezi ukanisaidia kunitafutia kibarua cha namna yoyote hapa ? Mzee Mustapha akasema.
Innocent akainamisha kichwa akafikiri kidogo halafu akasema

“Usijali mzee Mustapha.Naomba uniachie suala hilo kwa siku ya leo nilifanyie kazi halafu nitakupigia simu na kukutaarifu lini uje uanze kazi.usihofu kuhusu hilo.” Innocent akasema huku akimpa mkono na kumuaga mzee Mustapha ambaye alitoka mle ofisini akiwa na sura yenye tabasamu pana sana.



* * * *



Saa nne za asubuhi akiwa ofisini kwake simu yake ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake
“hallow” Innocent akaita baada ya kuipokea simu ile
“Hallow Innocent,mzee Mustapha anaongea”Ikajibu sauti ya upande wa pili

“Ouh Mzee Mustapha.habari za toka tulipoachana.?
“habari si nzuri sana Innocent”

“Kuna tatizo gani? Marina umeonana naye? Innocent akauliza

“Nilipotoka ofisini kwako nimekwenda moja kwa moja hadi anakoishi Marina kama tulivyokuwa tumepanga.Nimefika pale na kukuta kuna jambo limetokea.”
“Jambo gani tena limetokea mzee Mustapha? Innocent akauliza kwa shauku ya kutaka kufahamu
“Marina na wenzake watatu wamekamatwa na polisi asubuhi hii kwa madai ya wizi.Inasemekana kuna mtu walimuibia fedha na vitu vingine kama simu .Hivi sasa tunavyoongea Marina na wenzake wanashikiliwa kituoni na kwa jinsi ninavyofahamu kama akifikishwa mahakamani ni lazima atafungwa kwa sababu hana mtu yeyote wa kumuwekea dhamana.tafadhali Innocent tunatakiwa tumsaidie binti yule.Tunatakiwa tumsaidie haraka “ Mzee Mustapha akasema
Innocent akawaza kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Ok mzee Mustapha nakuja huko sasa hivi “
Dakika takribani tano zilipita huku Innocent akiwa bado amesimama ofisini kwake akitafakari.

“ Inanibidi nisahau yote yaliyopita na nimsaidie Marina.Hana ndugu wala mtu yeyote wa kumsaidia zaidi yangu.” Innocent akawaza huku akivuta pumzi ndefu
Saa tano na dakika ishirini Innocent akawasili maeneo anakoishi marina.Alikuwa anapakumbuka vyema.Akasimamisha gari mahala alipokuwa amesimamisha asubuhi ya siku ile alipokuja na Marina halafu akampigia simu mzee Mustapha ambaye hakuchukua muda akafika pale.
“Nipe habari mzee wangu nini kimetokea? Innocent akauliza

“Marina amekamatwa kwa kosa la wizi.Yeye na wenzake watatu wanasemekana kumuibia mtu jana usiku katika baa moja.Kwa mujibu wa maelezo ya wenzake ni kwamba Marina na wenzake wanasadikiwa kuiba fedha na vitu vingne kama simu na mpaka sasa hivi bado vifaa vyote havijajulikana thamani yake.” Mzee Mustapha akasema
“Twende kituoni tukapate taarifa zenye uhakika” Innocent akasema huku akimfungulia mlango mzee Mustapha akaingia garini halafu wakaelekea kituo cha polisi ambako Marina alikuwa akishikiliwa pamoja na wenzake watatu.

“namsikitikia sana binti yule kwa maisha anayoyaishi.: Innocent akasema
“hata mimi namuonea huruma mno .Mtoto mdogo kama yule kuanza kujiingiza katika makundi hatari katika umri mdogo kama ule .Laiti kama kungelikuwa na njia nyingine ya kuweza kumsaidia…” Mzee Mustapaha akasema
“Ngoja kwanza tufanye jitihada za kumtoa ndani halafu tuone ni jinsi gani tunaweza tukamsaidia.” Innocent akasema
baada ya kufika kituo cha polisi Innocent akajitambulisha kuwa ni ndugu na binti aitwaye Marina ambaye anashikiliwa kwa kosa la wizi.Askari aliyekuwa akishughulikia suala la akina Marina akamvuta Innocent pembeni na kumueleza kila kitu kuhusiana na Marina.
“kaka kesi ya ndugu yako si nzuri.Vifaa vilivyoibiwa thamani yake inakaribia shilingi millioni mbili.Tunamfahamu Marina.Si mara ya kwanza kufikishwa hapa kituoni.Amekuwa akiletwa hapa mara kwa mara.Tumekwisha mzoea.Mara nyingi tumekuwa tukijitahidi kumuonya aachane na tabia zake mbovu lakini mpaka sasa anaonekana amekwisha kuwa sugu.Nina hakika safari hii ni lazima afungwe gerezani.” Askari yule akamwambia Innocent wakiwa wamesimama faragha.
Innocent akainama chini akajaribu kutafakari nini cha kufanya.
“Afisa,Marina ni ndugu yangu.Nasikitika sana kwa maisha anayoyaishi lakini pamoja na mambo anayoyafanya siwezi kumuacha.Ni lazima nimsaidie.Afisa hebu niambie utanisaidiaje katika kesi hii ili ndugu yangu awe huru?

“Ndugu yangu sijui nikusaidiaje kutokana na ugumu wa kesi hii lakini kuna jambo moja ninaloweza kukushauri.” Askari akasema

“jambo gani hilo? Innocent akauliza
“Nenda ukaonane na mlalamikaji.Iwapo mtaonana mkaongea na mkakubaliana kwamba alipwe vitu vyake vilivyopotea basi kitakachofuata yeye atakuja hapa ,ataonana na mimi halafu tutafunga faili.Ni hilo tu ninaloweza kukusaidia kwa sasa.Jitahidi uonane na huyu jamaa mapema iwezekanavyo.”
Afisa yule wa polisi akampa Innocent namba za mtu anayelalamika kuibiwa vitu vyake na akina Marina.Innocent akashukuru na kumuaga afisa yule kwa ahadi ya kuonana naye baadae.
“mzee Mustapha kwa sasa inatubidi tukaonane na huyu bwana aitwaye Petro masawe ambaye ni malalamikaji katika kesi hii.Mimi niko tayari kumlipa vitu vyote vilivyopotea kama atakubali kufuta kesi ili Marina atoke .Ngoja nimpigie simu” Innocent akasema huku wakitembea kwa kasi kuelekea walipokuwa wamepaki gari.
“ hallo” Ikasema sauti ya upande wa pili wa simu aliyokuwa amepiga Inno.
“hallo habari yako ndugu? Inno akasema
“habari nzuri.naongea na nani?
“Ninaitwa Innocent.Samahani ndugu wewe ndiye bwana Petro steven masawe

“Ndiye mimi “
“Ok vizuri sana bwana petro.Mimi ni ndugu wa mmoja wa wale mabinti waliokuwa wamekuibia jana usiku ambao wanashililiwa na jeshi la polisi..”
“Ndiyo,unasemaje? Akauliza Petro
“Ndugu yangu nahitaji kuonana na wewe.Kuna mambo ninataka kuongea nawe.” Innocent akasema na kikapita kimya kidogo.Nadhani Petro alikuwa akifikiri.
“kwa sasa wewe uko wapi? Petro akauliza.
“Mimi niko hapa kituo cha polisi.”

“ kwa hiyo unataka tukutanie wapi? Petro akauliza

“Niambie uko wapi nikufuate sasa hivi”
Petro akamuelekeza Innocent katika baa yake naye kwa kasi akaongoza gari kuelekea kule.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 13

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ hallo” Ikasema sauti ya upande wa pili wa simu aliyokuwa amepiga Inno.

“hallo habari yako ndugu? Inno akasema
“habari nzuri.naongea na nani?

“Ninaitwa Innocent.Samahani ndugu wewe ndiye bwana Petro steven masawe?

“Ndiye mimi “
“Ok vizuri sana bwana petro.Mimi ni ndugu wa mmoja wa wale mabinti waliokuwa wamekuibia jana usiku ambao wanashililiwa na jeshi la polisi..”
“Ndiyo,unasemaje? Akauliza Petro
“Ndugu yangu nahitaji kuonana na wewe.Kuna mambo ninataka kuongea nawe.” Innocent akasema na kikapita kimya kidogo.Nadhani Petro alikuwa akifikiri.
“kwa sasa wewe uko wapi? Petro akauliza.
“Mimi niko hapa kituo cha polisi.”

“ kwa hiyo unataka tukutanie wapi? Petro akauliza
“Niambie uko wapi nikufuate sasa hivi”
Petro akamuelekeza Innocent katika baa yake naye kwa kasi akaongoza gari kuelekea kule.



ENDELEA……………………………..


“Kaka kwanza samahani sana kwa kukusumbua” Innocent akasema baada ya kufika katika baa aliyokuwa ameelekezwa na kuonana na Petro Masawe mlalamikaji katika kesi inayowakabili Marina na wenzake.

“Bila samahani ndugu yangu” Petro akajibu.
“Mimi naitwa Innocent na mzee wangu pale anaitwa mzee Mustapha.Nimepata taarifa kwamba marina na wenzake walifanya uhalifu hapa katika baa yako usiku wa kuamkia leo”

“Ndiyo kaka.Marina namfahamu sana Ni binti ambaye huwa anakuja hapa mara nyingi kutafuta riziki zake.Hata siku nyingine akikosa kabisa wateja huwa anakuja kwangu na kuniomba nimsaidie.Kama nina kitu basi huwa siachi kumsaidia.Jana majira ya saa saba za usiku akiwa na wenzake walifanikiwa kuvunja mlango wa chumba ambacho huwa ninalala na wakaiba fedha taslimu shilingi milioni moja na laki tatu,simu tatu zote zina thamani ya shilingi laki saba,vocha za simu zenye thamani ya laki nne na mzinga mkubwa wa pombe wenye thamani ya elfu thelathini.Wakati wakifanya uhalifu huo kuna baadhi ya watu waliwaona na wakanieleza.Kwa kusaidiana na polisi tulifanikiwa kuwakamata mahala wanakoishi na kuwakuta wakiwa na simu moja na mzinga wa pombe lakini vitu vingine bado havijapatikana.” Petro akasema huku akiwatazama akina Innocent.

“Pole sana Innocent kwa tukio hili baya.Sasa ndugu yangu pamoja na yote yaliyotokea nimekuja kwako ili tuweze kuongea kama wanaume.Marina ni ndugu yangu na sijisikii vizuri kuona akipelekwa gerezani.Ninakuomba mimi kama ndugu yako unikubalie nikulipe fedha zako zote zilizopotea kwa sharti moja tu la kwenda kufuta kesi ili ndugu yangu aweze kuwa huru.” Innocent akasema

“Kama mu tayari kunilipa fedha zangu zilizopotea pamoja na kafidia kadogo kwa ajili ya usumbufu na matengenezo ya mlango waliokuwa wameuharibu mimi sina tatizo.Nitafuta kesi mara moja na ndugu yako atakuwa huru.” Petro akasema huku akitabasamu.

“ Basi hakuna shida kaka.Sijui una nafasi ili tuweze kuongozana hadi benki nikukabidhi kiasi hicho cha fedha halafu tuongozane hadi kituoni kwa ajili ya kufunga faili?
“hakuna shaka,nisuburini dakika mbili nivae viatu” Petro akaondoka akiwa ni mwenye furaha sana na baada ya muda mfupi akarejea.
“tunaweza kuondoka.”
Wote wakaingia garini na safari ya kuelekea benki ikaanza.
“Ndugu yangu kwa nini unamuacha ndugu yako anajiingiza katika makundi hatari kama haya? Umri wake bado mdogo na hauendani kabisa na maisha anayoyaishi.” Petro akasema wakiwa ndani ya gari
“nakubaliana nawe Petro,maisha anayoyaishi Marina hayaendani kabisa na umri wake.Nitajitahidi baada ya suala hili kumalizika kutafuta namna ya kuweza kumsaidia.” Innocent akajibu kwa ufupi.
Shughuli ya benki ikakamilika na Petro akalipwa fedha zake zote alizokuwa akidai .Alifurahi sana.Toka benki safari ya kuelekea kituoni ikaanza.Kituoni mambo yalikwenda haraka haraka na baada ya kama saa moja hivi ya kuhangaika huku na kule hatimaye Marina na wenzake wakaachiwa huru.Baada ya kutolewa mahabusu akakutana na Innocent na mzee Mustapha waliokuwa wakimsubiri.Machozi yalikuwa yakimtoka.Marina alikuwa akitetemeka mwili wote.Alijaribu kuongea kitu lakini midomo ilikuwa ikimtetemeka.
“Marina unaumwa? Innocent akauliza huku amemshika mkono.
Hakujibu kitu alikuwa akitetemeka mwili mzima.

“Alosto hiyo..hajapata kitu tokea asubuhi” mmoja wa wasichana aliyekuwa amewekwa ndani na Marina akasema
Innocent alielewa walikuwa wakimaanisha nini.Akawachukua wote akawapakia ndani ya gari wakaondoka maeneo hayo ya kituoni.

“kaka tunashukuru sana kwa kutusaida.Kama si wewe tuliwa tunaenda kufungwa” Mmoja wa wasichana wale akasema huku machozi yakimchuruzika.Inno hakusema lolote akaendesha gari kwa kasi na moja kwa moja akaelekea katika hospitali binafsi ya mmoja wa marafiki zake iitwayo Yogini hospital.Marina ambaye hali yake ilikuwa ikiendelea kuwa mbaya akapokelewa na kupelekwa katika chumba cha vipimo ili kubaini anasumbuliwa na kitu gani.Wakati madaktari wakiendelea na shughuli zao Innocent,mzee Mustapha na wale wasichana wawili waliokuwa na Marina walikuwa wamekaa katika viti wakisubiri kuletewa taarifa.
“Kaka unajua mmekosea kumleta Marina hospitali.Ule si ugonjwa wa hospitali.Sisi tunalifahamu tatizo lake.Kuanzia asubuhi hajapata kitu.Alosto inamsumbua.” Akasema mmoja wa wale wasichana.
“Nimewasikia muda mrefu mizungumzia kuhusu alosto..mnataka tufanye nini? Innocent akauliza

“Inatakiwa atafutiwe kitu cha kumstua.Kumleta hapa hospitali mnamtesa bure.”
Innocent akawaangalia wale wasichana kwa macho makali halafu akauliza

“Hebu niwekeni wazi.Mnamaanisha nini mnaposema tumekosea kumleta hapa hospitali wakati mwenzenu anaumwa?

“kaka hatukufichi ,Marina amekuwa anatumia madawa ya kulevya.Leo kutwa nzima hajatumia na hicho ndicho kinachomtesa.Ilitakiwa tumpeleke mahala ili akapate kitu cha kumstua.Dakika kumi tu angekuwa ameshapona”
Inno akainama chini akafikiri halafu akasema

“No ! atatibiwa hapa hapa.Siwezi kukubali Marina aendelee tena na madawa ya kulevya.Huu ndio mwisho wake.Nitahakikisha anatibiwa na anapona kabisa na hata ninyi kama mnatumia madawa hayo nawaombeni muache mara moja.Ni hatari kubwa kwa afya zenu.”
Wasichana wale hawakujibu kitu wakabaki wakimtazama Innocent

“wasichana wazuri na warembo kama nyie ni kwa nini mmeamua kujihusisha na biashara ya ukahaba? Mzee Mustapha ambaye alikuwa kimya muda mrefu akauliza

“Mzee hali ngumu .Hatuna elimu,hatuna kazi za kufanya hatuna chochote ndiyo maana tumeamua kufanya kazi hii” mmoja wao aliyejulikana kama Aziza akasema
“Iwapo anatokea mtu wa kuwapatia msaada kama vile kazi za kufanya,au mtaji wa biashara mko tayari kuachana na biashara hii mnayoifanya? Mzee Mustapha akauliza.
Wasichana wale wakatazamana halafu wakajibu kwa pamoja.
“tuko tayari mzee.Sisi wenyewe hatufurahii kufanya biashara ya namna hii lakini ni hali ngumu ya maisha ndiyo inatulazimisha kujiingiza katika biashara kama hizi.”
“nafurahi kusikia mna nia ya dhati ya kutaka kubadilika.Huyu kaka mnamfahamu? Mzee Mustapha akauliza akimuonyeshea Innocent ambaye alikuwa amejitenga mbali nao akizunguka zunguka.

“Yule kaka mimi simfahamu bali nilimuona mara moja tu.Alikuja pale ghetto kwetu siku moja asubuhi akiwa na Marina na ukatokea ugomvi mkubwa kati yake na big sister.kwani yule kaka ni nani?

“Yule pale ni mtu mmoja mzito.Kama mna nia ya dhati ya kubadilika basi ongeeni naye na mumweleze ukweli .Ninaamini atawasaidia kwa sababu ni mtu mwenye roho nzuri sana.Hata Marina ni yeye ambaye amekuwa akitaka kumsaidia kumtoa katika biashara hii lakini mwenzenu amekuwa mgumu sana.” Mzee Mustapha akasema na wote wakageuka kumtazama Innocent aliyekuwa mbali nao akiongea na simu.
Baada ya kumaliza kuongea na simu Innocent akarudi kuungana na wenzake na mara muuguzi akajitokeza na kumuita akaonane na daktari mkuu bwana Ashraf Patel.
“Bwana Innocent tumemfanyia uchunguzi mgonjwa wako na hatujaona ugonjwa wowote.Tumemtundikia maji ambayo tumeweka dawa ili kumuongezea nguvu mwilini mwake.Hali yake inaendelea vizuri.Naomba msubiri baada ya drip ya mwisho kumalizika mtaondoka naye.” Dr Patel akasema
Kiza kilikwisha tanda wakati chupa ya mwisho aliyotundikiwa Marina ilipokwisha.baada ya kupewa dawa akaruhusiwa kuondoka.

“Pole sana marina.Unajisikiaje kwa sasa? Innocent akauliza akiwa ameongozana na Marina wakitoka ndani ya jengo la hospitali

“najisikia vizuri ila tumbo na miguu navisikia kama vinawaka moto” Marina akajibu kwa sauti ya upole .Alikuwa mpole sana siku ya leo tofauti na mara ya kwanza Innocent alipokutana naye.

“Umekula chochote toka asubuhi? Inno akauliza

“hapana sijala kitu toka jana saa mbili usiku.” Marina akajibu.
Wote wakaingia garini wakaondoka hapo hospitali.

“Akina dada nyie mnaelekea wapi? Innocent akauliza
“sisi tunaelekea Gheto kwetu.kwani Marina unampeleka wapi?

“Marina nitaondoka naye,nitakwenda kumtafutia chakula ale halafu nimtafutie sehemu nzuri ya kulala.Bado anaumnwa na hastahili kukaa ghetto.” Innocent akasema

“kaka Innocent na sisi tunaomba utuisaidie ili tuondokane na maisha haya ya ajabu namna hii” Aziza akasema na kumfanya Innocent atabasamu.
“Mna uhakika mna nia ya dhati ya kutaka kubadilika?

“kweli kaka Innocent.Tunataka kuachana na maisha haya.Tunaomba utusaidie”
“Ok kama kweli mko tayari kuachana na maisha haya mimi nitawasaidia.Mzee Mustapha atawaleta ofisini kwangu jumatatu ijayo saa mbili asubuhi” Innocent akasema
“Usijali nitawaleta” Mzee Mustapha ambaye amekuwa kimya muda mwingi akasema.Baada ya kumpeleka mzee Mustapha na wale wasichana wengine kwao Innocent akageuza gari kuanza safari ya kurudi akiwa na Marina ambaye alikuwa amelala katika kiti cha nyuma.

“Nadhani nyumbani kwetu ni mahali salama kwa Marina kukaa kwa sasa.Akiwa pale atapata huduma zote anazozitaka.Hali yake si nzuri sana .sintakubali tena arudi kuishi katika chumba kile alichokuwa akiishi.Nitahakikisha anaachana na zile tabia zake zote chafu.Nitahakikisha anasoma na hatumii tena pombe na dawa za kulevya.Kuanzia sasa Marina anaenda kuanza maisha mapya” Innocent akawaza.
Saa mbili na nusu za usiku akapaki gari nyumbani kwao.Akamshusha Marina ,akamshika mkono na kuanza kumuongoza kuelekea ndani.Miguu ya marina haikuwa na nguvu hali iliyomlazimu Inno auzungushe mkono wake mabegani kwake na kumsaidia kutembea.Ni muda wa chakula cha usiku.familia yote ilikuwa mezani,na mara Innocent akaingia akiwa na Marina.Wote mle sebuleni wakageuza shingo zao na kumuangalia kwa mshangao.Mama yake Innocent akaweka kijiko mezani na kumtazama Innocent kama vile ameona mzuka.

‘Innocent !!!..” mama yake akasema kwa sauti kubwa huku akiinuka kitini.

“huyu ni nani? Nini kimetokea ? Akauliza huku akimkaribia Marina na kumtazama machoni.
“Mama,huyu anaitwa Marina.Ni rafiki yangu na anaumwa.” Innocent akasema
“kwa hiyo hapa ni hospitali? Mama yake akauliza kwa dharau


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Nadhani nyumbani kwetu ni mahali salama kwa Marina kukaa kwa sasa.Akiwa pale atapata huduma zote anazozitaka.Hali yake si nzuri sana .sintakubali tena arudi kuishi katika chumba kile alichokuwa akiishi.Nitahakikisha anaachana na zile tabia zake zote chafu.Nitahakikisha anasoma na hatumii tena pombe na dawa za kulevya.Kuanzia sasa Marina anaenda kuanza maisha mapya” Innocent akawaza.
Saa mbili na nusu za usiku akapaki gari nyumbani kwao.Akamshusha Marina ,akamshika mkono na kuanza kumuongoza kuelekea ndani.Miguu ya marina haikuwa na nguvu hali iliyomlazimu Inno auzungushe mkono wake mabegani kwake na kumsaidia kutembea.Ni muda wa chakula cha usiku.familia yote ilikuwa mezani,na mara Innocent akaingia akiwa na Marina.Wote mle sebuleni wakageuza shingo zao na kumuangalia kwa mshangao.Mama yake Innocent akaweka kijiko mezani na kumtazama Innocent kama vile ameona mzuka.

‘Innocent !!!..” mama yake akasema kwa sauti kubwa huku akiinuka kitini.
“huyu ni nani? Nini kimetokea ? Akauliza huku akimkaribia Marina na kumtazama machoni.
“Mama,huyu anaitwa Marina.Ni rafiki yangu na anaumwa.” Innocent akasema
“kwa hiyo hapa ni hospitali? Mama yake akauliza kwa dharau


ENDELEA……………………………………….


“Hapana mama.Nimemleta akae hapa pamoja nasi ili aweze kupata huduma” Innocent akasema huku akimshika Marina na kumuongoza hadi katika chumba cha wageni.Grace alikuja kumsaidia kuandaa chumba na kisha wakamlaza Marina.
“Grace naomba kabla ya yote mtengenezee kwanza Marina uji laini anywe”
Haraka haraka Grace akatoka na kuelekea jikoni kuandaa uji kwa ajili ya marina.
“Innocent nakushukuru sana kwa kunisaidia.naomba unisamehe sana kwa yale yaliyotokea siku ile.Sikujua kama mtu niliyemfanyia ubaya ule leo hii angekuwa ndiye mwokozi wangu.Naomba unisamehe sana innocent.” Marina akasema kwa sauti ndogo huku akilia machozi

“Marina tafadhali usilie.Mwili wako bado hauna nguvu za kutosha.Ngoja kwanza upate nguvu halafu tutaongea.” Inno akasema
“Innocent ni lazima nilie kutokana na wema ambao umenifanyia.Bila wewe nilikuwa nakwenda gerezani.Umenipeleka hospitali,na sasa umenileta hapa ili niweze kupumzika.Sijawahi kukutana na mtu mwenye moyo wa huruma kama wako Innocent.Ninalia kwa sababu sistahili wema huu unaonifanyia” Marina akasema huku akiendelea kulia
“marina nilikuahidi toka siku ya kwanza nimekutana nawe kwamba lengo langu mimi ni kukusaidia.Leo hii narudia tena kusema kwamba nitakusaidia lakini naomba uniahidi kitu kimoja.nataka uniahidi kwamba kuanzia sasa utaachana kabisa na biashara ile uliyokuwa ukiifanya na vile vile utaachana kabisa na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya”
Huku akilia Marina akasema.
“Innocent ninataka kubadilika.Nilipokuwa kituo cha polisi nimefikiria sana kuhusu maisha yangu na nimeamua kwa dhati kabisa kubadilika.Nakuahidi kuanzia sasa sintajihusisha tena na kazi ile ya ukahaba.Kuanzia sasa sintatumia tena pombe ,sigara bangi wala madawa ya kulevya.Japokuwa kwa sasa ninaumia mno kwa kutokutumia kilevi chochote toka asubuhi lakini nitajitahidi kuvumilia mpaka nitashinda.” Marina akasema.Ni wazi maneno yale yalitoka ndani kabisa mwa moyo wake.Alikuwa akiongea kwa hisia kubwa hali iliyoonyesha kwamba alikuwa akiyajutia maisha yake aliyokuwa akiyaishi.Innocent akamuonea huruma sana.
“Marina nimefurahi sana kusikia hivyo.kama kweli umeamua kwa dhati kabisa kuachana na yale maisha yako ya nyuma mimi nitakusaidia kwa kila namna nitakavyoweza.Nitatumia kila gharama kuhakikisha kwamba unakuwa mtu mpya tena.”
Kwa mara ya kwanza Innocent akalishuhudia tabasamu zuri la binti yule baada ya maneno yale yenye faraja .Marina alikuwa akitabasamu japokuwa ilionyesha wazi kwamba alikuwa akisikia maumivu makali kupita kiasi.
“she is so pretty” Innocent akawaza huku akimuangalia marina usoni.mara Grace akaingia akiwa na chupa ya uji.
“Marina jitahidi unywe uji kwa sababu haujaweka kitu chochote tumboni tokea asubuhi.Jisikie nyumbani na uwe huru.Huyu ni dada yako anaitwa Grace,halafu kuna mwingine tena anaitwa Sabrina.Kesho nitakutambulisha kwa familia nzima.” Innocent akasema huku akitoka mle ndani na kumuacha Grace akimsaidia Marina kunywa uji.Moja kwa moja akaelekea sebuleni ambako akakutana na sura zilizokunjamana za familia yake.
“Innocent naona umefika wakati sasa ujenge nyumba yako na kuifanya kama kambi ya watu wenye matatizo.” Mama yake akasema baada ya Innocent kuingia sebuleni.

“kwani kuna nini mama?
“Huyu mtu uliyemleta hapa nyumbani.Umemleta kwa ruhusa ya nani? Baba yake akauliza.Innocent akakaa kimya akiwatazama
“nakuuliza Innocent huyu binti uliyekuja naye hapa ndani na moja kwa moja umempeleka katika chumba cha wageni na kumpatia malazi ,umemleta kwa ruhusa ya nani? Innocent bado hakujibu kitu.Alikabwa na fundo kubwa lililomfanya ashindwe kuongea

“Pamoja na kwamba tuna nyumba kubwa yenye vyumba vingi lakini hatuwezi kuchukua watu kiholela holela na kuwajaza hapa ndani.Hii ni nyumba yangu na mimi ndiye mwenye kuruhusu mtu kuishi hapa au la.Hakuna mwingine yeyote mwenye ruhusa hiyo.Kwanza binti mwenyewe amevaa kikahaba kahaba halafu unathubutu kumpitisha mbele ya wazazi wako.” Maneno yale ya baba yake yakamuumiza moyo sana .Akajitahidi kujizuia kusema neno lakini akashindwa.

“baba nafahamu nyumba hii ni yako na ni wewe ndiye mwenye uamuzi wa nani aishi hapa .Nalikubali hilo na ninaomba msamaha kwa kumleta binti yule bila ruhusa yako.Wazazi wangu naomba mfahamu kwamba nawaheshimu sana na haikuwa dhamira yangu kufanya hivi bila ridhaa yenu.Pamoja na hayo naomba mfahamu kwamba Marina ni mtoto yatima.Hapa mjini hana baba,mama wala ndugu yoyote.Hapa alipo ana matatizo makubwa ambayo hakuna mwingine yeyote wa kuweza kumsaidia zaidi yangu.Ukiacha matatizo aliyonayo bado ni mgonjwa sana na usiku huu nimemtoa hospitali.Kwa sababu sikuwa na sehemu nyingine ye kumpeleka ambako angeweza kupumzika niliamua kumleta hapa nyumbani,lakini .kama suala la yeye kukaa hapa litaonekana kuwa gumu basi ninaomba mnipe muda wa wiki mbili ili nijaribu kutafuta namna nyingine ya kuweza kumsaidia binti huyu.” Innocent akasema
“Kwa hiyo baada ya kuzunguka kote ukaona hapa ni kituo cha kulela watoto wasio na wazazi.Nakupa wiki moja huyu kahaba awe ameondoka humu ndani mwangu..” baba yake Inno akasema kwa ukali huku akiinuka na kuondoka pale sebuleni.Kwa unyonge Innocent akaondoka pale sebuleni na kuingia chumbani kwake.Kwa maneno makali aliyoambiwa na baba yake yakamfanya adondoshe chozi.Akasimama pembeni ya kabati la nguo akainama na kufikiri halafu akatoka na kurudi tena katika chumba cha marina.
“marina unajisikiaje kwa sasa?
“Kwa sasa naendelea vizuri.isipokuwa mwili ndio unawaka moto.nadhani ni kwa sababu ya yale madawa tunayotumia.hata hivyo nashukuru kwa sababu mimi ndiyo kwanza nimejifundisha kuyatumia kwa hiyo sikuwa bado mtumiaji mkubwa na ndio maana ninaimani nikiyavumilia mateso kwa muda mfupi nitashinda.”
“Sawa vumilia Marina ,kesho asubuhi nitaonana na daktari ili tuone namna tunavyoweza kukusaidia.Grace atakuletea chakula sasa hivi.Nakuomba ule halafu ulale.”
“nashukuru sana kaka Innocent”



* * * *


Asubuhi kabla ya kwenda kazini Innocent akaenda kumjulia hali Marina na kumkuta anaendelea vizuri japokuwa bado maumivu ya mwili yalikuwa yakiendelea.Saa tano akiwa ofisini kwake mara simu ikapigwa toka nyumbani kwao.Alikuwa ni Grace

“Grace habari za huko nyumbani?

“Habari za hapa nyumbani si nzuri sana”
“Kuna kitu gani kimetokea? Innocent akauliza huku akiwa na wasi wasi

“kaka Inocent leo asubuhi ulipoondoka Marina aliamka kwa ajili ya kwenda kuoga.Baada ya kuoga nikamtengenezea uji akanywa.Wakati akinywa mama akatokea na ghafla Marina akatapika kitendo kilichomuudhi mno mama ambaye alianza kumtukana na kumfukuza mle ndani.Hivi tunavyoongea Marina hajulikani yuko wapi.Nimeona nikufahamishe ili utafute namna ya kumsaidia .”
Innocent akapumua kwa nguvu na kuegemea kiti chake.akazama ghafla katika mawazo mazito.

“Marina amekwenda wapi? Yawezekana amerudi kule alikokuwa akiishi? Kwa nini mama amfukuze Marina nyumbani? Lakini sishangai kwa jambo kama hili kwa sababu toka jana familia nzima haikuonyesha kupendezwa na kitendo cha kumpeleka Marina pale nyumbani.Kwa mara ya kwanza hata baba alinitolea maneno makali mno.Ngoja kwanza nielekee nyumbani nijue nini kimetokea kule halafu nijue wapi pa kumtafutia Marina.Lazima nimpate” Innocent akawaza huku akiinuka na kuvaa koti lake,akatoka ofisini akaingia garini na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwao.

“maisha ya Marina yanaongezeka ugumu kila uchao.Jana kakamatwa kwa wizi,leo kafukuzwa nyumbani,nini itakuwa hatima yake? Binti yule anahitaji msaada mkubwa na hakuna mtu yeyote anayeonyesha kumjali.Kwa kuwa nimekwishajitoa kumsaidia sina budi kufanya kila linalowezekana ili kumuondoa binti yule katika maisha haya anayoyaishi sasa hivi.Kitu kikubwa ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumtafutia sehemu ya kuishi kwanza ndipo mambo mengine yafuate.Nilipenda sana aishi nyumbani kwetu kwa sababu pale angejiepusha na mambo mengi sana.Nikimpata leo hii nitarudi naye nyumbani na kujaribu kumshawishi tena mama ili akubali Marina aishi pale nyumbani wakati nikimtafutia sehemu nyingine ya kuishi” Aliwaza Innocent akiwa njiani kuelekea nyumbani.
Baada ya kuwasili nyumbani moja kwa moja akaelekea katika chumba alimokuwa amelala Marina,lakini hakuwepo mle chumbani.Alisimama na kuushika ukuta huku ameinamisha kichwa akifikiri,mara mlango unafunguliwa na Grace akaingia.Innocent akainua kichwa akamtazama halafu akasema

“Grace hebu nieleze ni kitu gani kimetokea mpaka Marina akaondoka?
“Kaka Innocent kilichotokea ni kwamba baada ya Marina kuamka alitengenezewa uji akanywa na mara tu baada ya kunywa alitapika sana mbele ya mama,kitendo kilichomuudhi na kuamua kumfukuza .”
“Alipoondoka hakuwaeleza alikuwa akieleka wapi? Innocent akauliza
“hapana kaka Innocent ,hakutuambia mahala alikokuwa akielekea.” Grace akajibu
“mama amekwenda wapi? Inno akauliza
“Alisema anakwenda kutengeneza nywele na atarejea muda si mrefu”.
Innocent akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akaingia katika gari lake akaondoka .
“Ni lazima marina apatikane leo.Amekwisha onyesha kila dalili za kutaka kubadilika.Nikimuacha atarudia maisha yake ya awali kwa sababu hana msaada wowote ule.Hana mtu yeyote wa kumsaidia zaidi yangu.Ngoja nikamuangalie kule anakoishi na wasichana wenzake.Litakuwa jambo la busara kama nikimtaarifu na mzee Mustapha kitu kilichotokea” Innocent akawaza huku akipunguza mwendo wa gari na kulisimamisha pembeni halafu akachukua simu yake na kumpigia mzee Mustapha


TUKUTANE SEHEMU IJAYO
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baada ya kuwasili nyumbani moja kwa moja akaelekea katika chumba alimokuwa amelala Marina,lakini hakuwepo mle chumbani.Alisimama na kuushika ukuta huku ameinamisha kichwa akifikiri,mara mlango unafunguliwa na Grace akaingia.Innocent akainua kichwa akamtazama halafu akasema

“Grace hebu nieleze ni kitu gani kimetokea mpaka Marina akaondoka?

“Kaka Innocent kilichotokea ni kwamba baada ya Marina kuamka alitengenezewa uji akanywa na mara tu baada ya kunywa alitapika sana mbele ya mama,kitendo kilichomuudhi na kuamua kumfukuza .”
“Alipoondoka hakuwaeleza alikuwa akieleka wapi? Innocent akauliza
“hapana kaka Innocent ,hakutuambia mahala alikokuwa akielekea.” Grace akajibu
“mama amekwenda wapi? Inno akauliza
“Alisema anakwenda kutengeneza nywele na atarejea muda si mrefu”.
Innocent akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akaingia katika gari lake akaondoka .
“Ni lazima marina apatikane leo.Amekwisha onyesha kila dalili za kutaka kubadilika.Nikimuacha atarudia maisha yake ya awali kwa sababu hana msaada wowote ule.Hana mtu yeyote wa kumsaidia zaidi yangu.Ngoja nikamuangalie kule anakoishi na wasichana wenzake.Litakuwa jambo la busara kama nikimtaarifu na mzee Mustapha kitu kilichotokea” Innocent akawaza huku akipunguza mwendo wa gari na kulisimamisha pembeni halafu akachukua simu yake na kumpigia mzee Mustapha


ENDELEA……………………………..

“Hallo mzee Mustapha shikamoo mzee wangu” Innocent akasema baada ya mzee Mustapha kupokea simu.

“Marahaba Innocent habari za toka jana?
“habari nzuri mzee ila kuna tatizo limetokea “
“Tatizo gani Innocent? Mzee Mustapha akauliza
“marina ametoweka nyumbani asubuhi ya leo na sijui yuko wapi.Kwa hivi sasa niko njiani nakuja ili tukamuangalie kule katika chumba chao”Inno akasema
“Nadhani atakuwa amerudi kule mahala wanakoishi.Maisha yale alikwisha yazoea hivyo itamchukua muda mrefu kuyazoea mazingira mapya.Nina imani atakuwa amerudi kule kwenye makazi yao” Mzee Mustapha akasema

“Ok mzee Mustapha nitafika hapo muda si mrefu ili tukamuangalie huko” Akasema Inno na kukata simu
Ilimchukua saa moja na dakika kadhaa kuwasili nyumbani kwa mzee Mustapha.Alitumia muda mrefu kutokana na foleni ndefu za magari katika jiji hili la Dar

“karibu sana Innocent” mzee Mustaha akamkaribisha Inno baada ya kuwasili pale kwake.
“ahsante sana mzee “ akasema Inno huku akishuka na kufunga milango ya gari halafu kwa pamoja wakaanza kuelekea katika makazi ya wasichana wale wanaofanya biashara ya kuuza miili ambako Marina naye huishi huko.

“Mzee Mustapha suala la Marina linaoneka kuwa gumu sana” Innocent akasema.Mzee Mustapha akamtazama halafu akasema

‘kama nilivyokwambia Innocent,Marina amekwisha yazoea maisha haya anayoyaishi kwa hiyo itamchukua muda kidogo kuubadili mfumo wa maisha yake na kuanza maisha mapya.Naomba usikate tamaa Innocent kwa sababu wewe ndiye mtu pekee ambaye uliyebaki wa kuweza kumsaidia.Kitu cha muhimu ninachokiona mimi ni kwamba ili kumsaida binti huyu ni lazima kwanza aondoke mahala hapa.Ni lazima aachane na magenge haya ya makahaba Kama akiendelea kukaa hapa tutakuwa tunatwanga maji katika kinu kwa sababu hataweza kuacha tabia zake.Akiwa hapa bado ataendelea kuvuta bangi,kutumia unga na biashara ya ngono.Ili tufanikiwe inatubidi tumuondoe hapa haraka” Mzee Mustapha akasema .Innocent hakusema kitu alikuwa akitembea huku ameinama chini akifikiri.

“Mzee Mustapha anayoyasema ni ya kweli kabisa.Kuna kila ulazima wa kumtoa Marina hapa.lakini ataishi wapi? Nilitegemea nyumbani kwetu kungekuwa ni sehemu nzuri na salama lakini nako mama anawasha moto hataki kumuona .Ngoja nikajaribu tena kwa mara nyingine kumshawishi mama akubali Marina akae pale nyumbani japo kwa siku kadhaa wakati nikiangalia uwezekano wa kumtafutia makazi ya kudumu.” Innocent akawaza wakati wakikata kona kuingia katika nyumba wanayoishi wasichana wanaofanya biashara ya ukahaba ambako anaishi pia Marina.Mzee Mustapaha ndiye aliyekuwa ametangulia mbele.Toka afanyiwe udhalilishaji na wasichana wakaao katika chumba hiki Innocent amekuwa muoga mno na kama si suala la Marina aliapa kutokurudi tena eneo hili.Mzee Mustapha akagonga mlango na ukafunguliwa na msichana mmoja mwenye macho mekundu aliyeonekana kana kwamba alikuwa ametoka kulala.
“Habari yako binti” mzee Msuatapha aksema

“Nzuri mzee Mustapha shikamoo” akasalimu binti yule
“Marahaba.namuulizia Marina .Yupo humu ndani?

“marina yupo.” Akasema yule binti huku akimuita Marina
Akiwa na sura iliyosawajika Marina akajitokeza pale mlangoni.Akatabasamu baada ya kuwaona mzee Mustapha na Innocent.

“karibuni ndani” akasema huku akijilazimisha kutabasamu
“ahsante Marina.Tulijua tutakukuta huku.Innocent amepigiwa simu akiwa kazini kwamba umetoroka nyumbani kwao.kwa nini umefanya hivyo Marina?.Mzee Mustapha akauliza
“Kweli Marina nimepigiwa simu na Grace akanitaarifu kwamba kulikuwa na kutokuelewana na mama kwa hiyo ukaamua kuondoka.Nimeamua kuacha kazi na kuja kukutafuta.” Innocent naye akaongezea.
Michirizi ya machozi ilionekana katika macho ya Marina na kwa kutumia viganja vya mikono yake akayafuta.
“Innocent najua wewe ni mtu mwema sana na una nia ya dhati ya kunisaidia.Si kwamba nilifanya makusudi kuondoka pale nyumbani lakini mama yako hakupenda nikae pale.Kuanzia asubuhi nimekuwa nikisikia akiongea maneno mengi sana ya kunikashifu.Nilivumilia kwa sababu nimekwisha zoea kashfa.Kilichonifanya niondoke ni baada ya kutapika uji niliopewa na Grace na mama yako akanitukana mno.Sikuona sababu ya mimi kutukanwa namna ile nikaamua kuondoka.” Marina akasema huku machozi yakiendelea kuchuruzika mashavuni mwake.
“Marina ,mama yangu ni mtu ambaye inahitaji moyo kuishi naye.Ninamfahamu vizuri mama yangu.Nafahamu kwamba hakupendezwa na suala la wewe kuwepo pale nyumbani lakini nilikwisha ongea naye pamoja na baba kwamba uwepo wako pale ni kwa muda mfupi wakati nikikuandalia sehemu nzuri ya kuishi.Wakati mchakato wakupata mahala utakapoweza kuishi kwa uhuru ukiendelea niliona ni vyema kama utakaa pale nyumbani ambako kuna huduma zote.Kwa hiyo Marina nimekuja kukuchukua tena ili ukaishi nyumbani kwetu wakati nakutafutia sehemu nzuri utakapoweza kuishi.” Innocent akasema huku akimsogelea marina aliyekuwa ameinama chini akitokwa na machozi
“Innocent siwezi tena kurudi kule kwenu.Mama yako anaweza hata kuniua kwa namna anavyonichukia.Mimi nitaendelea kuishi hapa hapa.japokuwa ni maisha ya shida lakini ninaishi kwa furaha na amani.” Marina akasema
“tafadhali marina ,nakuomba umsikilize Innocent anavyokwambia.Amini kile anachokueleza.Hapa unaposema unakaa kwa amani muda si mrefu serikali ya mtaa tutawahamisha wote,sasa utakwenda wapi? Nakuomba binti yangu kubali kufuatana na Innocent.Yeye ndiye anayejua nini amekiandaa kwa ajili yako” Mzee Mustapha akasema.Kauli ile inamfanya Marina kulegeza msimamo wake na akakubali kuondoka na Innocent.

“Oya brother mbona unamchukua mdogo wetu kienyeji enyeji ? ,tuachie basi hata msimbazi mmoja tupone asubuhi hii.”Alisema mwanamke mmoja mwenye sauti ya kukwaruza aliyekuwa amesimama mlangoni wakati Innocent na mzee Mustapha wakiondoka na Marina.Innocent akageuka akatabasamu ,akatoa pochi na kuchomoa noti moja ya shilingi elfu kumi akampa yule dada.

“brother wewe mzungu.Ila yule mzee mwanga tu.Kila siku anatuwangia kutaka kutuhamisha.Mwambie tutamfanyia kitu mbaya sisi,tumeshachoka na maisha haya” dada yule akalalama akimnyooshea kidole mzee Mustapha..
Innocent akaagana na mzee Mustapha halafu yeye na Marina wakaingia garini na kuondoka.

“marina naomba usiwe na wasi wasi na nyumbani kwetu.Pale ni sehemu salama na utakaa kwa muda tu wakati nikikutafutia sehemu nzuri ya kuishi” Innocent akasema
“Mimi sina tatizo Innocent..Mimi kamanda.Mimi naishi mazingira yoyote yale.Tatizo ni mama yako hataki kuniona nyumbani kwenu.” Marina aliongea huku akifumba macho kana kwamba anasikia maumivu makali.Innocent akamtazama halafu akauliza

“Unasikia maumivu makali?
“Nasikia maumivu makali hasa sehemu hizi” akasema huku akigusa sehemu alizokuwa akisikia maumivu.

“Toka lini umeanza kusikia maumivu hayo? Inno akauliza
“Muda mrefu sasa.Huu ni mwezi kama wa nane sasa.Maumivu haya huwa yanakuja na kupotea lakini kwa siku za hivi karibuni yamekuwa makali zaidi”

“Umeshawahi kwenda hospitali kupima na kuangalia nini kinakusumbua?
“ hapana sijakwenda.Nikisikia maumivu huwa natumia dawa maumivu yanapotea..”
“Umechoma sindano leo? Inno akauliza akimaanisha sindano ya dawa za kulevya
“Sijafikia bado kuchoma sindano.Dawa nimeanza kutumia hivi karibuni.Ninachotumia sana ni bangi na pombe.Unga ni mara chache sana.” Marina akasema

“ Ok.usijali Marina .Kwa sasa ninaelekea ofisini kwangu kuna kikao natakiwa kukiendesha.Nitakukabidhi kwa mtu akupeleke hospitali kwa ajili ya vipimo halafu jioni tutakwenda wote nyumbani”
Walifika ofisini ,Innocent akamkabidhi Marina kwa daktari wa kampuni ili ampeleke hospitali kucheki afya na yeye akaendelea na kazi zake.


* * * *



Saa kumi za jioni Dokta Peter Mbarali akarejea na Marina.Moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya meneja wake Innocent.
“Bosi nimempeleka Marina hospitali ,wamemfanyia uchunguzi na Marina amegundulika kuwa na matatizo ya figo.Kwa mujibu wa madaktari figo zake zote zinashindwa kufanya kazi sawasawa na madaktari wana wasi wasi kwamba kuna nafasi kubwa ya muda si mrefu figo hizo kushindwa kabisa kufanya kazi.Madaktari wameshauri uonane nao haraka iwezekanavyo ili kwa pamoja muangalie jinsi ya kuweza kumsaidia Marina.” Dr Peter akasema huku akimkabidhi Innocent bahasha lililokuwa na vyeti mbali mbali toka hospitali.Innocent akaviangalia vyeti vile akavuta pumzi ndefu.
“marina unajisikiaje kwa sasa? Inno akamuuliza marina aliyekuwa amekaa katika sofa la pembeni
“ najisikia afadhali si kama asubuhi.Nimepewa dawa zinanisaida sana”
Innocent akamuangalia marina usoni kwa dakika takribani mbili halafu akasema

“Dr Peter naomba umpumzishe Marina kule ofisini kwako,bado nina kazi muhimu nazimalizia.Hawa madaktari nitakwenda kuonana nao kesho” Dr Peter akamchukua Marina na kwenda kumpumzisha katika chumba cha kupumzishia wagonjwa kwa dharura pale kiwandani.

“My God why her? “ Innocent akasema taratibu baada ya Marina na Dr Peter kutoka mle ofisini mwake.

“kwa nini mzigo wa mambo yote haya umuelemee yeye peke yake? Lakini Leo nimegundua kitu ambacho sikuwa nimekigundua hapo awali.Marina ana uzuri wa asili uliojificha .Mtoto yule ni mzuri.Kuna kitu nimekiona katika macho yake ambacho kimenisisimua mwili wangu wote.Sielewi kama niko sahihi kwa hisia zangu lakini nahisi hisia zangu ziko sahihi.There is a connection between us.Kuna nguvu inayonivuta kuwa karibu na Marina.” Innocent akawaza halafu akainuka na kusimama huku mikono yake imeshikilia kiti
“No ! No No Innocent you are wrong.Marina isn’t the one”” Innocent akasema kwa sauti ndogo huku akizunguka zunguka mle ofisini.Akaenda na kusimama dirishani.

“ A woman of my deams must be simple,educated,full of love,…and…..” Innocent akawaza akahisi kama kichwa kikimuuma.
“marina is a simple girl,asiyekuwa na elimu but I can see something in her eyez..I can see passion..I can see love..Kama akibadilika anaweza akanifaa.” Mawazo ya innocent yakakatizwa na simu ya mezani iliyolia mle ofisini.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………………
 
Wakichungulia na huku ndio watakua ndio watachanganyikiwa wafate ipi waache ipi?
 
Mkuu kule nako ongeza basi kumbe bado hujachoka mpaka umeanzisha kitu kipya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom