Huu msemo alisingiziwa Jongwe ndio kauanzisha, sijui kama kuna ukweli wowote. Vyovyote vile huu msemo una ukweli kwa asilimia 99.99.
Kuna matukio kadhaa yamefanya niuamini huu msemo.
1.huku uswazi kuna kibanda cha mpesa, hapo kuna msichana mmoja mzuri sana lakini nasikitika kusema nilivyoongea nae nikajua huu msemo unamuhusu. Hakukawia baada ya miezi kadhaa vijana wa bodaboda washafanya yao!
2.kuna siku mchepuko wangu ukaniburuza hadi dukani kwa rafiki yake,pale tulikuta muuzaji ni binti mrembo sana, wakati tunaondoka mchepuko akaniambia umeona mtoto yule nikamwambia nimemuona ila I feel sorry for her, akaniuliza kwa nini nikamwambia watamuharibu. Sasa hivi ana mtoto baba kakimbia demu kachoka vibaya sana.
3.huyu ni mwingine kibanda cha mpesa, ni moja ya wasichana wazuri niliowahi kuwaona 2017! Nilipomfuatilia nilikuja kujua ana watoto watatu baba tofauti
4.sofia, huyu ni bartender 'kijiweni' kwangu. Mzuri balaa ila ndio kashazalishwa watu wanapokezana tu
Yaani hawa wanaoponzwa na uzuri wao wapo wengi sana. Dada zangu JF shukuruni Mungu kwa kuwapa Beauty With Brain.