Elections 2010 Beatrice Shelukindo ambwaga Dr. Aisha Kigoda....

Smiles

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
1,231
107
Ni katika jimbo la Kilindi.

Shelukindo apata kura 12,040 dhidi ya kura 2,939 za Kigoda.
Hongera sana Beatrice Shelukindo.....kila la heri
 
Safi sana. Mama machachari sana huyu sio kama nyumba ndogo ya Seif Khatibu kazi kujikomboa tu.
 
Safi sana. Mama machachari sana huyu sio kama nyumba ndogo ya Seif Khatibu kazi kujikomboa tu.

Beatrice ni moto wa kuotea mbali! Kigoda alimfanyia rafu nyingi lakini akapambana kikamilifu. Kama Kigoda atarudi kwenye uongozi ni kwa sababu hiyo ya kuwa nanihii wa mananihii!
 
Ni katika jimbo la Kilindi.

Shelukindo apata kura 12,040 dhidi ya kura 2,939 za Kigoda.
Hongera sana Beatrice Shelukindo.....kila la heri

Hongera mwanangu ehh hongera nami nikuhongeree, hongera, naona furaha naona furaha tumbo langu limezaa limezaaa mtooto ehh hongera!! cherekoooooooo!!!

Nakupenda sana Beatrice! Huyo nunga yembe wa kisiasa alifuata nini huko Kilindi? Demokrasia imemuaibisha huyo. Hivi haoni kazi kubwa uliyofanya kule kilindi? Kulikuwa hakuna barabara (isolated), hakuna maendeleo yoyote yale utafikiri ni wilaya ya kule kwa watindiga!!! Beatrice sasa kaza buti endelea kufanya kazi na wale wanajimbo wa Kilindi na jimbo liendelee kupaa juu. Uwe mbunge wao wa kudumu kabisa. Wabunge wenye kuchapa kazi sioni ni sababu gani wapate upinzani majimboni mwao. Bwana Yesu asifiwe sanaaaaaaaa. Zile ndumba zimeshindwa na kulegea katika jina la Yesu. Shindwaaaaaaa!

Nilikuwa nasubiri matokea haya kama ambavyo ule usiku wa kuamkia ndoa yangu miaka ile ya kweusi!!! Mnajua maana yake kwa wale wa miaka ile!!! Tunda la hawa halionjwi hadi.......!!!

Kuna jamaa anaitwa Magawa Abdallah naye kapata kura ngapi? Alikuwa anamchafulia sana huyu dada yangu image yake...
 
Ila mzee kalala chali kule Bumbuli sasa ndio ulo msemo wa tutaishi pamoja kwa shida na raha n.k Mzee atakuwa anamsindikizi mamsap huko Idodomya ingawa safari hii atakosa jina la Mheshimiwa na Viyoyozi vya kwenye ukumbi wa Bunge,kwani ataishia kusikiliza hotuba kwenye spika pale nje ,hongera dada Beatrice
 
Nimekukubali betty...umenifundisha kutokukata tamaaa!
nakuaminia mpiganaji wangu...nenda nyota nenda mjengoni

mix with yours
 
Hongera sana Bethy kwa ushindi wa kishindo utaingia mjengoni kwa heshima pia ninaimani safari yako haitaishia hapo maana najua wewe ni mpambanaji wa kiukweli.
 
Hivi hawa William Shelukindo na Beatrice ni ndugu?
Mtu na mkewe. Angalau CCM sasa wameanza kuona umuhimu wa kupunguza hizi familia/ndugu kwenye siasa. Mzee Shelukindo kakosa, mama kapata. Aisha Kigoda kakosa, kaka yake, Abdallah Kigoda kapata. Mzee Malecela kakosa, mkewe, Anna Kilango kapata. Samwel Sitta kapata, mkewe Magreth atakosa kwa tuhuma za rushwa ingawa yeye alikuwa anakwenda "kumwona mgonjwa saa 7.30 usiku kwenye nyumba ya kulala wageni".
 
Ha ha haaaaaaa hii nimeipenda 'kumwona mgonjwa saa 7.30 usiku nyumba ya kulala wageni" Ngoja nikugongee senks! Lol
 
Mtu na mkewe. Angalau CCM sasa wameanza kuona umuhimu wa kupunguza hizi familia/ndugu kwenye siasa. Mzee Shelukindo kakosa, mama kapata. Aisha Kigoda kakosa, kaka yake, Abdallah Kigoda kapata. Mzee Malecela kakosa, mkewe, Anna Kilango kapata. Samwel Sitta kapata, mkewe Magreth atakosa kwa tuhuma za rushwa ingawa yeye alikuwa anakwenda "kumwona mgonjwa saa 7.30 usiku kwenye nyumba ya kulala wageni".

Mara hii wanaJF mmehamia CCM tena? mwanachadema akisimama mtampigia kura betty? ama kweli hili ndumilakuwili! du! tutaona mengi. Ila ile ishu ya mama sitta inautata kidogo, kama mlisoma kwenye magazeti, ni kuwa alipopigiwa simu kuna mgonjwa eti alienda kumwamsha katibu wa ccm. kulikoni akamwamshe katibu wa ccm, si bora angesema ndugu yake yeyote? Ile inaweza kuwa rushwa kweli, ila kama unamtetea basi una masilahi yako binafsi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom