BBT yaanza kukwama. Tulisema hapa kuwa BBT ni shimo la kuzikia fedha za Kodi zetu

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,581
50,475
Vijana wa BBT waliojikita ktk ufugaji wa ng'ombe wameanza kulia kwa kukosa soko la ng'ombe wao.

Hata bibi yangu anayefuga ng'ombe zake kule Katavi kilio chake ni hicho hicho?

Serikali ilipaswa kujikita ktk kutafua changamoto za wakulima na wafugaji nchini na siyo kujiingiza kwenye miradi ya mazingaombwe kama BBT.


Source: ITV habari.
 
Viwanda ndiyo jawabu sahihi.

Kutegemea soko la mpaka upewe mashariti ya kukubali ushoga ndiyo wanunue kwa bei nzuri ni ujinga
Mtu anakwambia Ufuge ng' ombe wa kisasa ambaye mathalani atakugharimu laki saba kumtunza kuanzia anazaliwa hadi anakomaa kuuzwa.

Ukienda sokoni unakuta ng' ombe anauzwa laki saba hiyo hiyo.

Vilimo vya makaratasi viko namna hii.
 
Kilimo na ufugaji ni kazi zinazohitaji bidii na uvumilivu, na zaidi pale ambapo mhusila Hana mtaji mkubwa wa kuajiri wasaidizi wa kutosha na wataalamu.
Vijana wengi siku hizi siyo wavumilivu, maisha ni ya ushindani, utandawazi unatamanisha na hivyo wengi wa BBT watapata changamoto hizo.
 
Una hamu project za serikali kukwamua watu wake zifeli,unapata faida gani!?..ng'ombe hakosi soko,labda ng'ombe wao wamenona Sana Bei kubwa
Miradi mingi ya serikali inakwama kwa sababu wanao ileta hiyo miradi wanakuwa na nia ya kiupigaji zaidi kuliko kuwainua wananchi kiuchumi.

Mf; kulikuwa na mradi wa kuwagawia wananchi wa vijijini mitungi ya gesi
Hivi unafikiri kipi bora kati ya kupunguza gharama za kujaza gesi au kuwagawia wananchi mitungi ya gesi bure ambayo baada ya gesi kwisha hawataweza kuijaza tena

Miradi kama Mkukuta, Mkurabita, tasaf, BBT, hiyo miradi imejaa upigaji mwingi.
 
Una hamu project za serikali kukwamua watu wake zifeli,unapata faida gani!?..ng'ombe hakosi soko,labda ng'ombe wao wamenona Sana Bei kubwa
Projects za serikali za kukusanya wapiga picha, ma DJ, wacheza sarakasi na madalali wa nguo kwenda kuwapa "training" ili walime?

Kwamba Bashe haamini vyuo vya kilimo kama SUA na LITA vyote mpaka akakusanye wavaa pensi Dar awapeleke kwenye vituo mikoani? Bashe haamini vyuo vinavyosimamiwa na wizara ya elimu na ya kwake ya kilimo anaamini vijana aliookoteleza.

Yani siku wizara ya elimu ianzishe shule za sayansi mpya ianze kutafuta madalali wa vyumba ikawafundishe ufundi kisha ndio wawe walimu wakati wizara hiyohiyo inatoa graduates kibao wenye utaalamu huo.

Na wewe ukakaa ukisubiria matokeo chanya.
 
Serikali inayosubiri Rais atoe hela mfukoni kwake ndo hii inatufikisha hapa.

Tusubiri rais atoe hela za kununulia hao ng'ombe
 
Afadhali umedhihirisha utupu wa fuvu lako,kwa hiyo ulitaka fursa hizo za kilimo wapewe watu waliosoma vyuo vya kilimo na ufundi tu!?..unajua malengo ya BBT au walau tatizo la ajira tz!?..lipo kwa wasomi tu!?..watu wenye elimu ya chuo ni wangapi tz!?
 
RITA


LITA


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anakwambia Ufuge ng' ombe wa kisasa ambaye mathalani atakugharimu laki saba kumtunza kuanzia anazaliwa hadi anakomaa kuuzwa.

Ukienda sokoni unakuta ng' ombe anauzwa laki saba hiyo hiyo.


Vilimo vya makaratasi viko namna hii.
Unaenda sokoni unakuta wateja wanataka kumnunua kwa laki 5 huyo ng'ombe aliyekugharimu laki 7 kumfuga . Nchi hii aliyeturoga naye karogwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…