BBC yazungumzia silaha za Korea ya Kaskazini

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
423
Korea Kaskazini inaaminika kumiliki silaha 1000 zaidi zenye uwezo tofautitofauti

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.

Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.

Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.

Marekani yatishia kuiadhibu Korea KaskaziniKombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaaTrump: tutaidhibiti Korea Kaskazini

Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.

Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.

Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.

Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani.

Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama KN-14.

Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.

Korea Kaskazini: Tutaishambulia Marekani kwa nyukliaKorea Kaskazini: Tutafanya majaribio kila wikiChina na Marekani waitisha suluhisho la amani Korea kaskazini

Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.

Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.

Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.

Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.

Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.

Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.

Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.

Korea Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza kombora la masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa kilomita 1000.

Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud ,lakini ni asilimia 50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.

Uchanganuzi wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu utafiti wa mikakati ,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga maeneo yote ya Korea Kusini na Japan.

Imeongezea kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa kombora hilo linaweza kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.

Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014 na 2016.

Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.

Makadirio yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa Israel ukitaja uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.

Duru nyengine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 4,000.

Kombora la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama Nodong B ama Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na Japan.

Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Guam.
Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine

Korea Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la masafa ya kadri, kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka kwa manuwari.

Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari 2017.

Pyongyang ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi kuliwasilisha na kurusha.

Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.

BBC wameripoti

Pamoja na ripoti hiyo ya BBC binafsi naona kwamba hii vita haina mashiko bado mazungumzo yanaweza kufanyika .

Badala ya kutumia mabilion ya fedha kuwekeza kwenye kuuana ni bora kuwekeza kwenye kuzalisha chakula na vitu vingine vya aina hiyo.

Madhara ya nyuklia yanajulikana hasa baada ya mashambulizi ya heroshima na Nagasaki ,hakuna anayeweza kubeza kwamba nyuklia si hatari.

Ukiachilia madhara ya uraniam yalivyo mabaya hamna jinsi ambavyo utazungumzia hiyo ambayo tayari imerutubishwa ni hatari mno.

Historia itaendelea kuhukumu iwapo vita hii itatokea hakuna jinsi ya kuzuia matumizi ya nyuklia hata kidogo wote wanazo za kutosha kufanya uharibifu mkubwa kwenye Dunia yetu

Ushabiki wowote hautusaidii badala yake unatufanya kuonekana jinsi tusivyofikiri kutokana na uharibifu utakaotokea .

Nawasilisha.
 
Tatizo la US ni kutengeneza masoko tu hapo na kuendeleza biashara zake. Ikimbukwe kwamba hiyo NK ni soko la silaha za Urrusi sasa ikichapwa tu na US kitskachofuata ni kubadili uongozi na mfumo .

Hapo tunawaletea silaha za US ili waje kuwa Wateja wetu. Hii ndio inamfanya Russia anakataa maana aliona yaliyotokea Iraq na Libya. Misimamo ya hao wawili ilikua madhubuti wakifikiri Russia ingeingia ila ikawa tofauti kilichotokea Russia ilipoteza masoko na ushawishi ndio maana inakataa hilo kutokea Siria na haitoruhusu pia kwa NK.
 
Changamoto kwa Marekani,Japan,South Korea na washirika wao bado HAWAJUI uimara wa Korea Kaskazini hasa KISILAHA.
 
NK wako vizuri kimsingi... marekani ni mvhokozi sana, yeye anajitia kuwa police wa dunia hii... Ilk wakati yeye mwnyw kafanya mabaya meng tu na yy ndo yuko nyuma ya vta vya wenuew zinazoendelea mashariki ya kati. All in all naombea hayo matatizo yao wayamalize kidiplomasia
 
Changamoto kwa Marekani,Japan,South Korea na washirika wao bado HAWAJUI uimara wa Korea Kaskazini hasa KISILAHA.
Hawa Jamaa wangeungana na ndugu yap wangekua na nguvu ya kutisha ila Us hawezi kuruhusu hilo kwani anavuna hela hiyo mitaa yote na amewekeza pale wanajeshi 30,000 sio kitu cha mchezo hicho hizo gharama zinalipika kibiashara ndio maana.
 
Hawa Jamaa wangeungana na ndugu yap wangekua na nguvu ya kutisha ila Us hawezi kuruhusu hilo kwani anavuna hela hiyo mitaa yote na amewekeza pale wanajeshi 30,000 sio kitu cha mchezo hicho hizo gharama zinalipika kibiashara ndio maana.
Ni huyo USA ndo alowagombanisha North na South Korea
 
NK wako vizuri kimsingi... marekani ni mvhokozi sana, yeye anajitia kuwa police wa dunia hii... Ilk wakati yeye mwnyw kafanya mabaya meng tu na yy ndo yuko nyuma ya vta vya wenuew zinazoendelea mashariki ya kati. All in all naombea hayo matatizo yao wayamalize kidiplomasia
Kwa kweli diplomasia ndio suala la msingi hapo ,hii vita ikipiganwa tutashuhudia kupotea kwa USA kama super power na kuibuka taifa lingine labda China maana uchumi wao uko vizuri ukilinganisha na wengine.

Sasa hapo tayari Russia ameshamshauri US itumike diplomasia ndio njia pekee kwenye hili hamna jinsi.

Ikumbukwe pia NK hana cha kupoteza atatumia silaha hovyo hovyo bila uangalifu italeta shida Kubwa.

Pia silaha za nuke si silaha nzuri sana kwa Dunia yetu maana majanga yake ni makubwa mno refer Heroshima na Nagasaki Japani.
 
Ninyi hamjuw kwanin wazungu wana msifia na kusema eti ni Hatar Hhhhhhh wanatafuta ushawishi wa Nchi nyingi Ili wamchape... Sababu Watasema atakuja kutuvamia siku moja... We fikiria BBC Wakisema NK hana silaha za maangamizi na hazifik 100 unazani NATO watakubal kumpiga wengi Watasema tutakuwa tumemwonea... BBC inatangaza Ili dunia ijuw kuwa Dogo anazo tena za masafa.... Hapo ushawishi Tayar na Dogo hana muda mwingi On the chair
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwa kweli diplomasia ndio suala la msingi hapo ,hii vita ikipiganwa tutashuhudia kupotea kwa USA kama super power na kuibuka taifa lingine labda China maana uchumi wao uko vizuri ukilinganisha na wengine.

Sasa hapo tayari Russia ameshamshauri US itumike diplomasia ndio njia pekee kwenye hili hamna jinsi.

Ikumbukwe pia NK hana cha kupoteza atatumia silaha hovyo hovyo bila uangalifu italeta shida Kubwa.

Pia silaha za nuke si silaha nzuri sana kwa Dunia yetu maana majanga yake ni makubwa mno refer Heroshima na Nagasaki Japani.
Hamna US $18Tr and china $11Tr economy
Predicted that kama US hataendelea kukuza uchumi na China akaendelea By 2050 China Atakuw superpower... Vice-versa ni ndoto kwA China
 
Back
Top Bottom