JEURI NA KIBURI PIA HATMA YA DUNIA.
Bomu moja la Juu kabisa la Nyuklia toka kwa Mmarekani likitua Sehemu linaweza Kuua Watu 1,500,000 ( Milioni Moja na laki tano) kwa Mara Moja na kujeruhi wengine 3,700,000 (Milioni tatu na Laki saba)...hilo ni Bomu moja tu la hali ya juu ingawa Mataifa haya inawezekana kuna Secret Nuclear bombs wanaficha tena ambayo yanaweza Kuleta Maafa Makubwa zaidi ya hayo.
Inakadiriwa Kuwepo Silaha za NYUKLIA zaidi ya elfu 15 Duniani, na asilimia 90 ya Silaha hizo zinamilikiwa na Nchi Mbili United States Of America (U.S.A) na Russia kwa uwiano wa 6,800 (U.S.A) na 7000 (RUSSIA)..wakati Asilimia 10 inayobaki wanagawana wengine waliobaki ambao ni 300 (France)..215 (UK)..260 (China)..140 (Pakistan)...110 (India)...80 (Israel)..10 (North Korea)
Je ni kwa nini Marekani awe Inferior na kutaka kuanzisha Vita na North Korea ambao wana 10 tu na yeye ana 6800??...Turejee Historia
Pamoja na Marekani Kumiliki Vinu vya Nyuklia lakini Bado amekuwa Mwoga kuona Mataifa Mengine yanamiliki na kujaribu Silaha hizo... Marekani anaijua Vizuri athari ya Mabomu ya Nyuklia hasa baada ya kuyajaribu mnamo July mwaka 1945 Marekani alipoyadondosha katika Miji miwili ya Japan...Hiroshima na Nagasaki na kuleta Maafa Makubwa yasiyosahaulika!....Hiroshima Pekee walikufa watu wasiopungua 140,000 huku Nagasaki wakifa 74,000, na Maelfu ya wahanga(Survivors) waliobaki wakaendelea kuugua Saratani (Cancer) Wao na vizazi vyao..na wengine wanazaliwa na ulemavu mpaka leo...nani angepona iwapo Nyuzijoto juu ya Ardhi imefikia 4,000°C ??...umeona Hatari hii?
Baada ya Majaribio hayo ya Marekani ndipo Majaribio mengine kama hayo yakaendelea kufanywa na Soviet union miaka minne baadae kisha UK (1952), France (1960), na China (1964)....hali hii ya Mataifa Mfululizo ku-test Nyuklia ilileta Mjadala na kufikiwa Suluhisho Mwaka 1968 ambapo Mataifa hayo yakasaini Mkataba wa makubaliano - Nonproliferation Treaty (NPT) Mkataba unaotambua na kupewa Taarifa juu ya Mikakati na technology zote Mpya za Nyuklia kwa nchi zote wanachama!...Moja ya Nchi zilizosaini ilikuwepo Korea Kaskazini na Marekani, Kasoro India, Pakistani na Israel ambao walikataa kabisa.....Baadae Members wa NPT wakasaini Makubaliano Mengine ya kupiga Marufuku Majaribio ya Silaha za Nyuklia - Comprehensive Nuclear Test Ban Treaty (CTBT) mwaka 1996.
Kwa Mshangao wa wengi ilipofika January 2003 Korea Kasikazini kwa Bwana Panki wakatangaza rasmi kujitoa kwenye Mkataba wa NPT...hii ikawaweka huru kutokaguliwa na wala kupatikana kwa Taarifa zake kuhusu Nyuklia...na tangia hapo wamekuwa wakiendelea kujaribu Mabomu yao mpala leo hii ambayo wametamka Bayana kwamba Wataendelea kujaribu mabomu yao kila wiki...kila mwezi na kila Mwaka..hapa ndipo marekani anapagawa kabisa.
Korea Kaskazini wanasema kwamba Wana Kila aina ya Silaha kuweza kulinda Rasilimali zao na Watu wao na Wanajiandaa iwapo watachokozwa basi watapiga Japan, Korea kusini na Marekani kwa Pamoja.
USA imemuomba CHINA ajaribu kumuonya Korea Kaskazini lakini CHINA amekataa....inasemekana Nchi zingine zinazowekeza kwenye Nyuklia kisiri siri kinyume na Sheria za Mikataba ya Mataifa ni Syria, Libya na Iran.
Mwisho niseme tu kwamba Ubabe wa USA na RUSSIA pamoja na JEURI ya Mkorea Kaskazini vinaweza kuigeuza Dunia Chapati, Wao wababe wa Nyuklia wakati sisi Dunia ya Tatu na Magobole Mikononi....huu Mchuano sio sawa na mechi za Madrid na Barcelona, hii ni Vita na sio Entertainment, ....Tuombe yasitokee,.GOD have MERCY Upon US.
Taarifa hii kwa msaada wa mtandao