BBC Wachemsha

BBC Wachemsha

MpigfilimbiwaHamelin

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2014
Posts
652
Reaction score
169
Nimefurahi kusikia BBC wakiripoti uongo!
Kwa kawaida ukisikiliza radio za Tanzania hukosi kupata vituko kwa watangazaji kuvurunda kwa umbumbumbu au hata kutangaza mambo yasiyo halisi.
Leo asubuhi BBC katika matangazo yao ya Amka na BBC walitangaza kuwa mabaki yameonekana ya ndege inayodhaniwa ni ya Malaysia iliyopotea miezi sita iliyopita. Nilisubiri wasahihishe na kuomba radhi lakini walirudia kutamka hivyo hivyo mara tatu; na hadi kipindi cha amka na BBC kinamalizika hawakurekebisha.
Ukweli ni kuwa ndege hiyo ilipotea tangu mwaka jana mwezi Machi na siyo miezi 6 iliyopita.
Naona tatizo ni kizazi hiki vijana hawako makini na yanayotokea duniani.
 
Zamani nilijua hawa jamaa wako makini sana, lakini habari zao za siku hizi zina walakini hata story wanazipost kwenye mtandao wao ni vitu vya ajabu kabis.
 
Sasa kinachofurahisha nini hapo?? Hutakiwi kufurahi kwa yeyote anayekosea hata watangazaji wetu wa ndani hawapaswi kukoseakosea.
 
Hukupaswa kufurahia makosa, kila mtu anakosea kiufundi ama kiutendaji
 
Nimefurahi kusikia BBC wakiripoti uongo!
Kwa kawaida ukisikiliza radio za Tanzania hukosi kupata vituko kwa watangazaji kuvurunda kwa umbumbumbu au hata kutangaza mambo yasiyo halisi.
Leo asubuhi BBC katika matangazo yao ya Amka na BBC walitangaza kuwa mabaki yameonekana ya ndege inayodhaniwa ni ya Malaysia iliyopotea miezi sita iliyopita. Nilisubiri wasahihishe na kuomba radhi lakini walirudia kutamka hivyo hivyo mara tatu; na hadi kipindi cha amka na BBC kinamalizika hawakurekebisha.
Ukweli ni kuwa ndege hiyo ilipotea tangu mwaka jana mwezi Machi na siyo miezi 6 iliyopita.
Naona tatizo ni kizazi hiki vijana hawako makini na yanayotokea duniani.

Unatabia za "mswahili"
 
Ni kwel kabisa unachosema mkuu...... Zimepita kama wiki mbili kwenye dira ya jion wakawa wanatangaza Habari za michezo....... Kilichonishangaza walikuwa wanatoa habar za mwaka jana za uefa champions League huku wanatoa na matokeo yake na kueleza mechi zitakazochezwa kesho yake wakitaja mechi za robo fainali. Hawakundua Hilo mpaka kipindi kinaisha..... Ila nilichokuja kugundua ni kwamba jamaa siku hiz hawako serious kabisa.
 
Si kwamba hawafahamu siku tukio lile la ndege lilipotokea, ila ni maiosa ya bahati mbaya tu ambayo kibinadamu mtu yoyote anaweza kuyafanya. Ila kuna vitu vyao vingine vya kijinga sana huwa wanapost kwenye mitandao huwezi kudhania kama ni wao
 
Mimi mwenyewe nilishtuka sana kusikia hiyo ndege ilipotea miezi sita iliyopita wakati si kweli.... LAKINI MWANADAMU KAUMBWA NA MAKOSA.... WAO SI MALAIKA....
 
teh teh ....... ....... ahsante mleta mada! napenda kuona extraordinaries do ordinaries and vice versa!
 
Sasa kinachofurahisha nini hapo?? Hutakiwi kufurahi kwa yeyote anayekosea hata watangazaji wetu wa ndani hawapaswi kukoseakosea.

Ni kawaida ya mtu mnyonge kufurahi mtu mwingine akikosea. Inferiority Complexion
 
BBC Swahili walipoamua kuifanya ya "kiswahili" ndio walipoteza mwelekeo.

Tatizo lao wamekusanya wajiitao waandishi kutoka Tanzania. Hawajiandai na hawasomi. Ni vyema waandishi wa Tanzania baada ya hivyo vidigrii na vidiploma vyao, waendelee kujisomea, wapende kusoma na sikudai "wamesoma". Mwandishi mzuri ni yule "anayesoma" siyo "aliyesoma!"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom