BBC Swahili weledi umepungua

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Wadau habarini za usiku,

Kama heading isemavyo, ni wazi hili shirika now days professionalism imepungua kwa kiasi kikubwa mnoo uandaaji wa habari usioeleweka.

Mfano Usiku huu nimetazama ripoti iliyosomwa na Lulu Odhiambo kuhusu kupungua maambukizi ya corona huko Kenya sasa katka display pale alipokaa Zuhura Yunus kunaonekana bendera ya taifa la Kenya na Tanzania (lakini hii taarifa inahusu Kenya kwanini bendera Tanzania?) To me it was wrong.

Secondly, katika taarifa hiyo wanasema kwamba eti kufuatia Kenya kuiorodhesha Tanzania katika nchi ambazo wasafiri toka nchi husika hawatakaa karantini ya lazima imepokelewa tofauti na wadau, then anaonekana mdau ambaye ni mmoja ya viongozi (CS) wa Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya. Sasa huyo CS anazungumzia ya kuwa kitendo icho ni kuimarisha mashirikiano na kustawisha biashara katika ukanda huu (if I qoute well). Nikabaki najiuliza sasa hao wadau wanaotoa maoni tofauti wako wapi mbona hawajahojiwa?

My Take:
Hiki chombo sasa kinafanya mambo shagalabaghala mnoo. Hiyo kama haitoshi, juzi kupitia idhaya ya Kiswahili matangazo ya jioni kupitia radio walizungumzia ripoti ya haki za binadamu na uhuru wa habari, na waka mhoji Mhe. Kabudi sasa kituko eti mtangazaji kamaliza mahojiano ana angua kicheko. Cha kimpasho. Huku ni kupoteza weledi katika kazi.
 
Masharti ya mamlaka za nchi zenye tv washirika kama tiizii yamewavuruga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom