Katika mahojiano na BBC Leo asubuhi, waziri mkuu wa Kenya amesema serikali ya umoja wa kitaifa siyo serikali iliyopatikana kidemokrasia. Amesema Ni serikali ya dharura inayotokana na kushindwa kwa demokrasia ya kweli na udanganyifu katika Uchaguzi. Kwamba Uchaguzi wa haki na huru ukifanyika ni lazima apatikane mshindi na msindwa kihalali. Siyo demokrasia vyama vyenye sera zinazopingana kuendesha serikali pamoja
namsapoti Raila ila KWA UPANDE WA KENYA pamoja na NCHI NYINGINE ZINAZOPIGANA WAKATI na BAADA YA UCHAGUZI.Kwa hapo HOJA YAKE NI NZURI.
Lakini napinga hoja kuwa Serikali za umoja wa kitaifa ni lazima zitokane na mifumo ya kugoma kuachia madaraka au tamaa na mambo mengine kama hayo. (S.Afrika hawakuhitaji kugombana ila walijua wasipohusisha walioshindwa BAADAYE ingekuwa ndivyo sivyo..... Marekani ya Obama imehusisha viongozi wa republican)
Katika mfumo wa democrasia ya vyama vingi, utambue wazi waamuzi ni wananchi, so kama MSHINDI akashinda kwa 51% dhini ya 49% (tafakari hii namaanisha asilimia yoyote alizopata mshindwa ila angalia kwa hapo)ni wazi kabisa kuwa mshindwa nae anakubalika kwa asilimia kubwa na wananchi (wapiga kura). Hiyo inaweza kuwa ni kutokana na sera zake (mshindwa) au utendaji wake.
Kama ndivyo, na ukafikia maamuzi ya kuunda serikali ya chama kimoja katika mazingira kama hayo (hata kama wananchi wa nchi husika hawajafanya FUJO) ina maanisha muundo wa serikali husika UMEWAACHA PEMBENI asilimia kubwa (49% au vyovyote) nje ya kujihisisha na maamuzi juu ya nchi yao, wakati nao walikuwa wanayo matazamio yao kwa MGOMBEA SHINDWA na WANA HAKI YA kuchangia katika maendeleo ya Taifa lao.
Tukumbuke nchi inayotawaliwa hapo, ni yao wote....... WALIOSHINDI na WALIOSHINDWA.
ANGALIZO
Vyama tawala vingekuwa na mtazamo wa mbali, pindi wanaporuhusu siasa za vyama vingi, kabla ya uchaguzi wa kwanza, ili matokeo yanapotoka na wakichukua dola, WAVIHUSISHE NA VYAMA PINZANI.
Unaweza kuona hali halisi kwa South Africa, wao hawawezi kufanya fujo za msingi huo, kwa kuwa vyama vikubwa vya upinzani vimekuwa vikishirikishwa katika serikali, mabovu na mazuri YANAWAHUSU, ni rahisi hata chama TAWALA kuachia madaraka pindi kinaposhindwa, kwa kuwa HAKUNA CHA KUFICHA, maana wote wamekuwa wakiongoza serikali.
HITIMISHO.
Makosa yamefanywa na vyama tawala (Afrika) kwa kutoshirikisha upinzania katika kuunda serikali TOKEA mwanzo, NA SASA INAKUWA VIGUMU kukabidhi nchi, kwa kuhofia MATATIZO NA UOZO WALIOUFANYA KUIBULIWA na hata kushtakiwa baada ya kukabidhi nchi.
KWA TANZANIA.
1. CCM ilikuwa inaweza hata kumshirikisha Mrema kipindi kile, au hata kushirikisha upinzani, MAANA yote ambayo upinzania unakosoa CCM leo, CCM wangejibu kwa wananchi TULIKUWA WOTE katika kutawala , au hata wasingesema.
Na katika mfumo kama huu kampeni zinakuwa sio za kuzungumzia Mtu fulani au Makosa ya mtu fulani ILA MISINGI YA KULETA MAENDELEO KWA NCHI HUSIKA.
2.Kwa mtazamo halisi, baada ya UCHAGUZI huu wa 2010, CCM ingeweka pembenibaadhi ya vipengele vya katiba, na kuruhusu Rais achague hata mawaziri na watendaji wengine ambao wangeteuliwa na upinzania kuunda serikali hii ingesaidia KUPUNGUZA ADHABU AMBAZO WANAWEZA KUZIPATA PINDI WAKUPOTEZA DOLA... na hicho ndicho wanachokiogopa zaidi. Ila ingepunguza makali maana upinzani kwa miaka hiyo mitano wangekuwa wajua mengi ndani ya utawala.
ILA MSETO WA ZANZIBAR ni kiini macho