BBC: Serikali ya umoja wa kitaifa siyo ya kidemokrasia

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Katika mahojiano na BBC Leo asubuhi, waziri mkuu wa Kenya amesema serikali ya umoja wa kitaifa siyo serikali iliyopatikana kidemokrasia. Amesema Ni serikali ya dharura inayotokana na kushindwa kwa demokrasia ya kweli na udanganyifu katika Uchaguzi. Kwamba Uchaguzi wa haki na huru ukifanyika ni lazima apatikane mshindi na msindwa kihalali. Siyo demokrasia vyama vyenye sera zinazopingana kuendesha serikali pamoja
 
Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Nimemsikia hoja yake, ni murua kabisa ingawa yeye chama chake kimo katika serikali ya namna hiyo. Alisema serikali hiyo ya pamoja ililazimishwa na watu wa nje kwa lengo moja tu -- kusimamisha kuuawana kulikokuwa kunaendelea wakati ule. Alisema mtindo huo siyo wa kuigwa kamwe ingawa aliongeza kuwa Mugabe aliuiga ili aendelee kubaki madarakani. Ni mtindo unaouua demokrasia humu Barani Afrika.
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Mi pia nakubaliana naye. Tatizo ni pale wanasiasa wa tz huiga haraka mambo yaliyofanywa na serkali za nje ambazo hunufaisha wanasiasa. Mfano kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo, na sasa kuweka serikali ya umoja wa kitaifa katika katiba. Sasa CUF iko ndani ya serikali ya ccm kutekeleza sera za ccm. Uchaguzi wa 2015 CUF itajinadi kwa lipi?
 
RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,376
2,000
Sijasikiliza BBC lakini jamaa ametoa ujumbe kwa nchi zote za Africa. Ni ujumbe ambao unatoa hali halisi barani afrika kuwa tukiendelea na huu upuuzi hatufiki popote. CUF wanasingizia wamekubali kwa maslahi ya wazanzibari, hiyo ni sawa na kukubali yaishe na kuona ulichokuwa unapigania kwa ajili ya wazanzibari hakikuwa na manufaa au hukuweza kufikisha ujumbe wako sawa sawa ili uungwe mkono.
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Walio madarakani wanavuruga uchaguzi na kuchakachua kura kwa makusudi na wakiona wananchi wamecharuka wanatoa peremende ya serikali ya mseto...at the end of the day wanaendelea kutawala na hakuna anayewajibishwa kwa kuvuruga uchaguzi! Huu ni mfumo hatari sana....
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,478
2,000
Izo serikali ni matokeo ya watu kutokukubali kushindwa na ni lazima zifikie ukomo period
Hatuwezi entartain watu wanaoleta mambo ya kifalme
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Izo serikali ni matokeo ya watu kutokukubali kushindwa na ni lazima zifikie ukomo period
Hatuwezi entartain watu wanaoleta mambo ya kifalme

Naam, hiyo ndiyo hasa ilikuwa ya Waziri Mkuu Raila kwama vyama tawala vikishindwa vikubali matokeo ili demkrasia ikue
 
mchillo

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
488
250
Sijasikiliza BBC lakini jamaa ametoa ujumbe kwa nchi zote za Africa. Ni ujumbe ambao unatoa hali halisi barani afrika kuwa tukiendelea na huu upuuzi hatufiki popote. CUF wanasingizia wamekubali kwa maslahi ya wazanzibari, hiyo ni sawa na kukubali yaishe na kuona ulichokuwa unapigania kwa ajili ya wazanzibari hakikuwa na manufaa au hukuweza kufikisha ujumbe wako sawa sawa ili uungwe mkono.
Binafsi sioni mantiki ya CUF kukubali serikali inayoitwa ya "Umoja wa kitaifa" ili "kukubali yaishe" maana sera zao zilikuwa tofauti kabisa na zile za CCM ambazo kwa haki kabisa CUF walikuwa wakizikosoa. Sasa nauliza mfano huu; kama polisi amembamba mwizi na akaanza kumfukuza hadi ikafika pahala polisi kugundua kuwa mwizi anayefukuzwa ana nguvu nyingi zaidi yake ni sahihi polisi huyo kuungana na mwizi huyo kwenda tekeleza uhalifu kwa vile "Ameshindikana"?
 
JohnShaaban

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
464
195
mchillo said:
... kama polisi amembamba mwizi na akaanza kumfukuza hadi ikafika pahala polisi kugundua kuwa mwizi anayefukuzwa ana nguvu nyingi zaidi yake ni sahihi polisi huyo kuungana na mwizi huyo kwenda tekeleza uhalifu kwa vile "Ameshindikana"?
Ni ishara tosha jinsi kizazi cha sasa kinavyojali maslahi binafsi, akina Nyerere, Kenyata, Lumumba, Nkruma wangeweza kukubaliana na Wakoloni na familia zao zikaneemeka. Lakini waligoma na kuhakikisha uhuru unapatikana. Leo hii tofauti ya Sera kati ya vyama ndio uhuru unaopiganiwa na vyama hivyo. Ni kinyaa na kichefuchefu kuona mpinzani anakubali kutekeleza sera alizokuwa anapinga, ni sawa na kusema amelainika hata kabla ya kupata uhuru wa kisera aliokuwa anaupigania. Tatizo ni ubinafsi wala si kujali maslahi ya nchi, maana Miafrika bila kuipa 'challenge' hakuna litakalofanyika.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
681
500
Katika mahojiano na BBC Leo asubuhi, waziri mkuu wa Kenya amesema serikali ya umoja wa kitaifa siyo serikali iliyopatikana kidemokrasia. Amesema Ni serikali ya dharura inayotokana na kushindwa kwa demokrasia ya kweli na udanganyifu katika Uchaguzi. Kwamba Uchaguzi wa haki na huru ukifanyika ni lazima apatikane mshindi na msindwa kihalali. Siyo demokrasia vyama vyenye sera zinazopingana kuendesha serikali pamoja
ViVA Raila, Kiongozi unayeweka kuuleza ukweli bila kigugumizi, hata kama unaishi katika hilo tatizo bado unaweza kukiri kuwa ni tatizo
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
14,825
2,000
Binafsi sioni mantiki ya CUF kukubali serikali inayoitwa ya "Umoja wa kitaifa" ili "kukubali yaishe" maana sera zao zilikuwa tofauti kabisa na zile za CCM ambazo kwa haki kabisa CUF walikuwa wakizikosoa. Sasa nauliza mfano huu; kama polisi amembamba mwizi na akaanza kumfukuza hadi ikafika pahala polisi kugundua kuwa mwizi anayefukuzwa ana nguvu nyingi zaidi yake ni sahihi polisi huyo kuungana na mwizi huyo kwenda tekeleza uhalifu kwa vile "Ameshindikana"?

Sijasikiliza BBC lakini jamaa ametoa ujumbe kwa nchi zote za Africa. Ni ujumbe ambao unatoa hali halisi barani afrika kuwa tukiendelea na huu upuuzi hatufiki popote. CUF wanasingizia wamekubali kwa maslahi ya wazanzibari, hiyo ni sawa na kukubali yaishe na kuona ulichokuwa unapigania kwa ajili ya wazanzibari hakikuwa na manufaa au hukuweza kufikisha ujumbe wako sawa sawa ili uungwe mkono.

Nimewasoma ila wakati tunapiga kelele matatizo ya ZANZIBAR ambayo yalishindikana no one dared to pose solutions! tulisema yatatuliwe yatatuliwe! CCM wana dola, huyo Raila anazungumza tu, Kibaki angekuwa katili wangeendelea kuaana , angewekewa vikwazo na bado anageendelea kushikiria madaraka, kwani Zimbabwe kukoje?

It was s solution, but good onee! ukisema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa is DEMOCRACY how can you solve a puzzle when 51% and 49% percent of votes as the case in Zanzibar? mnasema ni demkrasia asilimia 51 waongoze wale 49????

Akisema Raila then ni MSAHAFU? na nchi zinazofanya hivyo hakuna democrasia??
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,213
2,000
Mi pia nakubaliana naye. Tatizo ni pale wanasiasa wa tz huiga haraka mambo yaliyofanywa na serkali za nje ambazo hunufaisha wanasiasa. Mfano kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo, na sasa kuweka serikali ya umoja wa kitaifa katika katiba. Sasa CUF iko ndani ya serikali ya ccm kutekeleza sera za ccm. Uchaguzi wa 2015 CUF itajinadi kwa lipi?

tena uwashukuru wazenj kwa kuona mbali mapema. Unajua nini kingetokea kama seif angekataa matokeo? Kama katiba isingemtambua? Sio ccm wala cuf waliojiandaa kushindwa 2010 so bora walichagua hivyo kujiridhisha
 
mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
0
Yaani wewe rf inaonekana hujui demokrasia,ni lini cuf wamekaa na ccm kuwa ilani ya pamoja?then co lazima kila m2 awe ndani ya serkali mkirazimisha basi ni ubinafsi,51% ni haki yake kuongoza,tatizo badala ya kujenga taasisi tunajenga watu TUUNGANE KUJENGA MIFUMO,TUTAONDOKANA NA WATU KAMA MAALIM SEIF WABINAFSI
 
Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,712
1,225
Sijasikiliza BBC lakini jamaa ametoa ujumbe kwa nchi zote za Africa. Ni ujumbe ambao unatoa hali halisi barani afrika kuwa tukiendelea na huu upuuzi hatufiki popote. CUF wanasingizia wamekubali kwa maslahi ya wazanzibari, hiyo ni sawa na kukubali yaishe na kuona ulichokuwa unapigania kwa ajili ya wazanzibari hakikuwa na manufaa au hukuweza kufikisha ujumbe wako sawa sawa ili uungwe mkono.
Mbona unaumwa na jambo lisilokuhusu?????
 
Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,712
1,225
Mi pia nakubaliana naye. Tatizo ni pale wanasiasa wa tz huiga haraka mambo yaliyofanywa na serkali za nje ambazo hunufaisha wanasiasa. Mfano kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo, na sasa kuweka serikali ya umoja wa kitaifa katika katiba. Sasa CUF iko ndani ya serikali ya ccm kutekeleza sera za ccm. Uchaguzi wa 2015 CUF itajinadi kwa lipi?

Kwani pale panapokuwa na wagombea wengi kwenye chama kimoja wagombea hujinadi vipi????
 
Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,808
2,000
Katika mahojiano na BBC Leo asubuhi, waziri mkuu wa Kenya amesema serikali ya umoja wa kitaifa siyo serikali iliyopatikana kidemokrasia. Amesema Ni serikali ya dharura inayotokana na kushindwa kwa demokrasia ya kweli na udanganyifu katika Uchaguzi. Kwamba Uchaguzi wa haki na huru ukifanyika ni lazima apatikane mshindi na msindwa kihalali. Siyo demokrasia vyama vyenye sera zinazopingana kuendesha serikali pamoja

namsapoti Raila ila KWA UPANDE WA KENYA pamoja na NCHI NYINGINE ZINAZOPIGANA WAKATI na BAADA YA UCHAGUZI.Kwa hapo HOJA YAKE NI NZURI.

Lakini napinga hoja kuwa Serikali za umoja wa kitaifa ni lazima zitokane na mifumo ya kugoma kuachia madaraka au tamaa na mambo mengine kama hayo. (S.Afrika hawakuhitaji kugombana ila walijua wasipohusisha walioshindwa BAADAYE ingekuwa ndivyo sivyo..... Marekani ya Obama imehusisha viongozi wa republican)

Katika mfumo wa democrasia ya vyama vingi, utambue wazi waamuzi ni wananchi, so kama MSHINDI akashinda kwa 51% dhini ya 49% (tafakari hii namaanisha asilimia yoyote alizopata mshindwa ila angalia kwa hapo)ni wazi kabisa kuwa mshindwa nae anakubalika kwa asilimia kubwa na wananchi (wapiga kura). Hiyo inaweza kuwa ni kutokana na sera zake (mshindwa) au utendaji wake.

Kama ndivyo, na ukafikia maamuzi ya kuunda serikali ya chama kimoja katika mazingira kama hayo (hata kama wananchi wa nchi husika hawajafanya FUJO) ina maanisha muundo wa serikali husika UMEWAACHA PEMBENI asilimia kubwa (49% au vyovyote) nje ya kujihisisha na maamuzi juu ya nchi yao, wakati nao walikuwa wanayo matazamio yao kwa MGOMBEA SHINDWA na WANA HAKI YA kuchangia katika maendeleo ya Taifa lao.

Tukumbuke nchi inayotawaliwa hapo, ni yao wote....... WALIOSHINDI na WALIOSHINDWA.

ANGALIZO

Vyama tawala vingekuwa na mtazamo wa mbali, pindi wanaporuhusu siasa za vyama vingi, kabla ya uchaguzi wa kwanza, ili matokeo yanapotoka na wakichukua dola, WAVIHUSISHE NA VYAMA PINZANI.

Unaweza kuona hali halisi kwa South Africa, wao hawawezi kufanya fujo za msingi huo, kwa kuwa vyama vikubwa vya upinzani vimekuwa vikishirikishwa katika serikali, mabovu na mazuri YANAWAHUSU, ni rahisi hata chama TAWALA kuachia madaraka pindi kinaposhindwa, kwa kuwa HAKUNA CHA KUFICHA, maana wote wamekuwa wakiongoza serikali.

HITIMISHO.

Makosa yamefanywa na vyama tawala (Afrika) kwa kutoshirikisha upinzania katika kuunda serikali TOKEA mwanzo, NA SASA INAKUWA VIGUMU kukabidhi nchi, kwa kuhofia MATATIZO NA UOZO WALIOUFANYA KUIBULIWA na hata kushtakiwa baada ya kukabidhi nchi.

KWA TANZANIA.

1. CCM ilikuwa inaweza hata kumshirikisha Mrema kipindi kile, au hata kushirikisha upinzani, MAANA yote ambayo upinzania unakosoa CCM leo, CCM wangejibu kwa wananchi TULIKUWA WOTE katika kutawala , au hata wasingesema.

Na katika mfumo kama huu kampeni zinakuwa sio za kuzungumzia Mtu fulani au Makosa ya mtu fulani ILA MISINGI YA KULETA MAENDELEO KWA NCHI HUSIKA.

2.Kwa mtazamo halisi, baada ya UCHAGUZI huu wa 2010, CCM ingeweka pembenibaadhi ya vipengele vya katiba, na kuruhusu Rais achague hata mawaziri na watendaji wengine ambao wangeteuliwa na upinzania kuunda serikali hii ingesaidia KUPUNGUZA ADHABU AMBAZO WANAWEZA KUZIPATA PINDI WAKUPOTEZA DOLA... na hicho ndicho wanachokiogopa zaidi. Ila ingepunguza makali maana upinzani kwa miaka hiyo mitano wangekuwa wajua mengi ndani ya utawala.

ILA MSETO WA ZANZIBAR ni kiini macho
 
Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
0
Mi pia nakubaliana naye. Tatizo ni pale wanasiasa wa tz huiga haraka mambo yaliyofanywa na serkali za nje ambazo hunufaisha wanasiasa. Mfano kuanzishwa kwa mfuko wa jimbo, na sasa kuweka serikali ya umoja wa kitaifa katika katiba. Sasa CUF iko ndani ya serikali ya ccm kutekeleza sera za ccm. Uchaguzi wa 2015 CUF itajinadi kwa lipi?

Hili jambo linasikitisha, ni dhahiri viongozi wanaendekeza masilahi binafsi na si ya chama wala taifa!
 
Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,808
2,000
Kwani pale panapokuwa na wagombea wengi kwenye chama kimoja wagombea hujinadi vipi????

ELEWA HAPA
Wakiwa ndani ya CHAMA kimoja kama hoja yako invyosema.... wanajinadi KWA KIPI ATAKACHO KIFANYA YEYE, KWA KULINGANISHA NA MWENZIE PINDI AKIPATA RIDHAA

CUF kama CHAMA kinachohitaji ridhaa ya KUONGOZA TAIFA ZIMA.
WAkisema WATAFANYA (kuborehsa) HIKI kwa kulinganisha na KILE............ ni rahisi kwa mpiga kura kumuuliza "" mbona ulikuwepo kwa miaka mitani iliyopita HUJAFANYA???? wewe si kama wao tu""

KWA HIYO.
Kwa mtazamoa wangu , kampeni ni kipindi unachoweza kujinadi dhidi ya ALICHOFANYA/ATAKACHOFANYA mwenzio... LAKINI ni ngumu KAMA MTAKACHOFANYA/ULICHOFANYA mlikuwa pamoja.

tegemea kampeni (kwa CUf & CCM) za hivi.....

Maalim Seif Sharif:"yaani Dr. Shei ni noma, nampenda sana, anaongoza vizuri mno, nipe kura tutashirikiana nae"
Dr. Shein:" asalam aleykhum!!!, Leo Maalim Seif hatakuja kwenye kampeni... kwa hiyo nitasoma illani za chama chake nikimaliza nitasomma na za chama changu, ila niwaambie jamaa safi sana , tupeni ridhaa tuongoze nchi"

Hakutakuwa na kuthibitisha mapungufu ya mwenzako kwa HOFU HALI YA HEWA ITACHAFUKA, na kwa faida ya wazanzibar.

Kule ni kiini macho kaka
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Hili jambo linasikitisha, ni dhahiri viongozi wanaendekeza masilahi binafsi na si ya chama wala taifa!

Naam, kwa sababu hiyo, ni wachache sana Kama dr Slaa wanaweza kurisk kuacha ubunge halafu wanaibiwa kura za urais wanaamua kukaa kimya na kuendelea na maisha. Si unaona huko Ivory Coast jamaa wameapishwa wote wawili na wameunda serikali?
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,395
2,000
Nimewasoma ila wakati tunapiga kelele matatizo ya ZANZIBAR ambayo yalishindikana no one dared to pose solutions! tulisema yatatuliwe yatatuliwe! CCM wana dola, huyo Raila anazungumza tu, Kibaki angekuwa katili wangeendelea kuaana , angewekewa vikwazo na bado anageendelea kushikiria madaraka, kwani Zimbabwe kukoje?

It was s solution, but good onee! ukisema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa is DEMOCRACY how can you solve a puzzle when 51% and 49% percent of votes as the case in Zanzibar? mnasema ni demkrasia asilimia 51 waongoze wale 49????

Akisema Raila then ni MSAHAFU? na nchi zinazofanya hivyo hakuna democrasia??

kwa dunia ya sasa ukileta udicteta na kusababisha vifo ujue The Hague inakusubiri ukakae chumba karibu na Charles Taylor, huyo Kibaki hakika nakwambia akitoka tu madarakani mchakato wa kumpeleka the The Hague unaanza, hata Mugabe analijua hilo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom