hivi ni lazima vyama vya siasa viwe na umoja/mabaraza ya wanawake,vijana na wazee?mbona sijasikia umoja/baraza la vijana,wanawake au wazee la republican na democrat huko USA au labour na consevative huko UK?Kwanza siasa za huko hazina ofisi wala uongozi sijui wa mashina/msingi, matawi.kata wala wilaya.wenzetu wala hawana kadi za vyama wala hawachagui viongozi kwa kufuata vyama bali ilani za uchaguzi.ndiyo maana kuna wamarekani waliomchagua obama kwenye uchaguzi uliopita na huenda mwaka huu wasimpigie kura na wapo ambao hawakumpigia kura lakini mwaka huu wakaamua kumpigia.mimi sikubaliani na huu utaratibu wa kuwa na jumuia za vyama kwani zinachanganya watu sana.kwa mfano mwanamke anaweza kuwa mwanachama wa BAWACHA/UWT wakati huohuo mwanachama wa baraza la wazee/jumuia ya wazazi!vilevile vijana wa kiume na wa kike wenye umri kati ya miaka 35 na 40 hao utawaweka katika kundi gani?maana BAVICHA/UVCCM huko hawatakiwi na kwenye hayo mabaraza mengine pia hawana vigezo.