BAVICHA yakanusha kuhusika na migomo UDSM na vyuo vikuu kwa ujumla....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
........M/kiti wa jumuiya ya vijana Taifa ya CDM John Heche amekanusha habari zilizotolewa na gazeti la UHURU kuwa CDM inahusika na migomo ya vyuo vikuu hapa Tanzania.

Ameihasa serikali iache kutibu matokeo badala yake itibu ugonjwa wenyewe ambao ni matatizo ya wanachuo wenyewe,na akaendelea kusema wanachofanya serikali ni kuipa promo ya bure kwa wananchi CDM kupitia PUBLICITY nadhani wale marketers wanaelewa maana ya PUBLICITY.

Source:Star TV
 
Na mimi nimesikia kutoka kwa rafiki yangu wa chuo kuwa kuna mkono wa chadema

huyo rafiki yako atakuwa hajui analolifanya ama nae ni mfanyakazi wa magamba? yeye anapesa za kujikimu? anafurahia wenzake kufukuzwa chuo? CDM wala haihusiki hapa ila watu ambao hawafikirii beyond the basket ndio wanafikiri tu CDM inahusika
 
Acheni siasa uchwara, someni na fuatilieni kwa umakini. Migomo UDSM imeanza rasmi mwaka 1971, CHADEMA kimezaliwa 1992. Matatizo yaliyopelekea migomo mwaka 1971 ni yale yale leo mwaka 2012. Njia ya utatuzi (propaganda - kuwachafua wanafunzi waonekani hawana maana kwenye jamii) ya mwaka 1971 ni ile ile ya mwaka 2012.

Waliounga mkono migomo na waliokuwa wakigoma UDSM mwaka 1971 wengi wao wako kwenye power kwenye serikali hii. Tafuteni suluhisho la matatizo vyuo vikuu. Bila hilo kufanyika hakutaisha migomo vyuoni.

Anayetaka kuelewa zaidi suala la migomo vyuoni asome kitabu kinaitwa

The Roots of Student Unrest in African Universities by Omari PB Mihyo.

Anayekitaka anaweza kudowload kwenye post yangu inazungumzia migomo hii iko kwenye jukwaa la elimu (Chanzo cha Migomo Vyuo Vikuu - Kitabu). Au anaweza kuni - PM email yake ili nimtumie.
 
Na mimi nimesikia kutoka kwa rafiki yangu wa chuo kuwa kuna mkono wa chadema

wapenzi wa vyama wapo kila kona. Wapenzi wa CCM wapo vyuoni hali kadhalika wapenzi wa CDM. Ukiona mwanachuo unakuambia kuna mkono wa CDM, huhitaji kujiuliza maswali kama ana kadi ya CCM au ni mtoto wa fisadi nchini, hana njaa, hajui shida maishani mwake.

Wenye njaa watakwambia wao ndio wahusika, kwani ni wao wanaoumia. inakuwaje waumie wanavyuo halafu CDM ilalamike? Hata kwa uelewa wa kawaida, hili halipo na haliwezekani.

Migomo vyuoni ni matokeo ya ubabe wa serikali, kuchelewesha pesa za watoto wa maskini.
 
wapenzi wa vyama wapo kila kona. Wapenzi wa CCM wapo vyuoni hali kadhalika wapenzi wa CDM. Ukiona mwanachuo unakuambia kuna mkono wa CDM, huhitaji kujiuliza maswali kama ana kadi ya CCM au ni mtoto wa fisadi nchini, hana njaa, hajui shida maishani mwake.

Wenye njaa watakwambia wao ndio wahusika, kwani ni wao wanaoumia. inakuwaje waumie wanavyuo halafu CDM ilalamike? Hata kwa uelewa wa kawaida, hili halipo na haliwezekani.

Migomo vyuoni ni matokeo ya ubabe wa serikali, kuchelewesha pesa za watoto wa maskini.

CCM wanaweweseka kila siku na CHADEMA. Pale UDSM kuna wana CCM na wanachama wa vyama vya upinzani wakiwemo wa CHADEMA. so CCM waache kuweweseka.
 
Ccm wakubali tu wameshaliwa vyuoni labda wajaribu shule za msingi kwani serikali wanayoiongoza imeboronga kila idara utoaji mikopo vyuoni na ajira ndo usiseme.
 
CCM wamepoteza mwelekeo, hawajui kuwa propaganda zao za kihuni zilikuwa zinafanya kazi zamani lakini sasa hivi wanapozidi kuisingizia chadema, wananchi wanagundua uongo wa ccm kabla hata chadema haijakanusha. kwahiyo wanaipaisha zaidi chadema kuliko kuiathiri.
 
Kama kweli vyombo vya habari vya ccm vinatoa propaganda kwamba chadema ina mkono kwenye migomo ya vyuo vikuu basi ccm ijue kuwa uhai wake kama chama cha siasa unaesabika. Hizi ni mbinu chakavu na hazina mashiko kwani matatizo ya vyuo vikuu yanajulikana na wanayajua ccm na serikali yake. Ebu wawatimizie matakwa yao kama kweli watagoma, ebu wafanye hata nusu tu ya kile wanachotakiwa kuwafanyia wanafunzi kama utasikia kuna mgomo wa wanafunzi. Je chadema pia ina mkono wake kwa madakitari wa muimbili.ccm inaonekana 2015 ni mbali sana na una dalili za kuanguka hata kabla ya hapo maana unatapatapa sasa. Maisha bora kwa kila mtanzania,na hakuna mtoto wa masikini atashindwa kusoma chuo kikuu. Timiza ahadi maana ahadi ni deni na mna deni kubwa kwa wanafunzi na watanzania kwa ujumla. Mlipochakachua uchaguzi mlifurahi sasa ni zamu ya kufurahia machungu ya kutowajibika na sera za kulindana. Tutaona mengi kabla amjaikabidhi nchi hapo 2015.
 
Back
Top Bottom