Bavicha waache utoto wa kupiga kelele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bavicha waache utoto wa kupiga kelele

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Seif al Islam, May 21, 2012.

 1. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  naushangaa sana uongozi wa bavicha chini ya bwana heche kwa kuendeleza kelele na majibizano yasiyo na msingi wala tija yoyote kwa cdm na wanachi kwa ujumla.sioni sababu ya wao kuibuka na kuanza kumjibu shibuda eti kisa tuu katangaza kuutaka urais kpitia cdm 2015.siioni mantiki ya vijana hawa kuacha kufanya kazi za maana za chama na kujiingiza kijinga kwenye mjadala wa shibuda.kwani ni mara ngapi watu wa aina ya shibuda wamejitokeza hadharani na kutoa matamko kama hayo na wakiulizwa wanajifanya kunakuliwa vibaya na waandishi wa habari?
  Wengine mara nyingi tuu hata juzi tuu hapa kiongozi mmoja wa cdm alisikika akidai kuwa atagombea urais 2015 kana kwamba chama hakina kanuni wala taratibu za wanachama kugombea nafasi mbalimbali.
  Naamini cha msingi na hata ambacho viongozi wa juu wanafanya sasa ni kujenga chama kimya kimya bila kujiingiza kwenye mtego wa kujibizana hovyo na watu hawa ambao kwa kujua au kutokujua wanatumiwa na ccm na hata mafisadi.
  Naamini wahuni hawa wachache watamezwa na matukio tuu.watapiga kelele sana hukom kwenye forums za ccm lakini mbele ya wanachama na wananchi kwa ujumla hawana lolote.
  My take.
  Kam,ati kuu ipige marufuku utoaji huu wa matamko yaiyo na mana kwasababu yanatumiwa na wanaokihujumu chama kukichafua.
   
 2. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaamini watakapokutana 24/05 busara itatumika na kuwakumbusha wajibu wa kila kiongozi wa Bavicha ili kuondoa migongano inayopandikizwa na mafisadi.
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Bavicha wanafanya kazi kubwa sana tusiwabeze niliona mchango wao mkubwa sana kwenye kampeni hasa za Arumeru na hata Igunga huku kupishana kauli ni jambo la kawaida kwenye siasa ila naamini viongozi wakuu Mbowe, Slaa, Zitto Arfi na wengine watawafunda zaidi ili waweze kujua zaidi njia muafaka za ku approach suala lolote lile unajua vijana hawa wa CDM damu zao zinachemka wanataka mabadiliko ya haraka na hatua za haraka haraka ndio maana unaweza kuona wakitoa kauli kali kidogo kama hizo ila watasahihishwa tu!!kwa wapenda mabadiliko tuwaunge mkono na kuwasaidia kimawazo sio kuwabeza na kuwadharau wana nia za dhati kuleta ukombozi!!
   
Loading...