BAVICHA kufanya mkutano mkuu wa dharura Dodoma

Mh mm nisingeenda [emoji28][emoji28]
ImageUploadedByJamiiForums1468347063.993144.jpg
 
Nimewaelewa sana BAVICHA. Wamekamata vizuri siasa za Tanzania kwa wiki kadhaa sasa; Hakuna (Media, mitandao nk) anayezungumzia CCM & Mkutano wao bali BAVICHA.

You have really played well ... Keep it up. This is politics.
 
Watu wapo bize wanaandika proposal,na kubuni miradi ya maendeleo,nyie mpo mnaendeleza harakati zisizo na miguu wala mikono,mnaanzisha thread tu za kujipa moyo na BAVICHA yenu kushindana na dola,kama wanaume kweli nendeni Dodoma mtenguliwe miguu,mtembelee magongo ndo mke mpate akili ya Ku google neno "DEMOCRACY",.. Wengi wajanja wa maneno tu,waoga sana.Ujanja wenu ni humu JF tu.
 
Bavicha acheni uchokozi fanyeni kazi kwenye halmadhauri zenu. Mnaanza kupoteza umaarufu kwani kwa sasa serikali inaendelea kutatua kero zetu. Nanyi fanyeni hivyo kwa kubuni miradi ya kiuchumi tuwapongeze.
Kwani kuna ubaya gani wakifanya mkutano mkuu?
 
Yaani kipaumbele chenu ni kuzuia Mikutano ya Wapinzani,lakini yenu mnafanya bila shaka hapa ndio unapoona double Standard ya Jeshi la Polisi ,mmechemka sana weledi washaona mambo kwa jicho la tatu.
 
Bavicha acheni uchokozi fanyeni kazi kwenye halmadhauri zenu. Mnaanza kupoteza umaarufu kwani kwa sasa serikali inaendelea kutatua kero zetu. Nanyi fanyeni hivyo kwa kubuni miradi ya kiuchumi tuwapongeze.
Wata buni vipi hiyo miradi kama hawaruhusiwi kukutana? maana nimeskia kwa baadhi ya wilaya ni marufuku hata kutembea kikundi ca ukawa njiani
 
Wanao Uhuru wa kwenda popote ili mradi hawavunji sheria
 
Nchi yetu nadhani tunasahau maana ya mipango. Tunaongea sana juu ya michakato lakini ukitazama sana hakuna michakato na mikakati ya kweli. Ni nini kinaanza ni madawati ama madarasa? Kuna madawati ambayo yako nje kwani hakuna madarasa! Why should this happen?????????
 
Yaani kipaumbele chenu ni kuzuia Mikutano ya Wapinzani,lakini yenu mnafanya bila shaka hapa ndio unapoona double Standard ya Jeshi la Polisi ,mmechemka sana weledi washaona mambo kwa jicho la tatu.
Hapo sasa ndiyo patamu sanaaa...........

Jeshi la Polisi limesema lilichozuia ni mikutano ya hadhara na siyo mikutano ya ndani.........

Huo ulikuwa ni ufafanuzi wa kuhalalisha Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 23/07/2016 huko Dodoma.

Bavicha nao wamesema wanatarajia kufanya mkutano wao wa ndani wiki 2 zijazo huko huko Dodoma.

Sasa hapo ndipo Jeshi la Polisi litaingia kwenye majaribu makubwa........

Tamko la kuwa kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na maandamano ni la Polisi wenyewe....

Sasa itakuwa ni double standard ya hali ya juu iwapo Jeshi letu la Polisi litaruhusu kufanyika kwa mkutano wa ndani wa CCM na wakati huo huo kukataza mkutano wa ndani wa Bavicha!

Ndiyo maana naendelea kusisitiza kuwa hakuna kazi ambayo itakuwa ngumu katika serikali hii ya awamu ya 5, kama kazi ya Upolisi.......

Ugumu wake mkubwa unakuja kuwa kazi ya Upolisi ni ya kupokea amri toka kwa watawala, bila kutafakari kuwa amri hiyo ni halali au laa......

Katiba ya nchi yetu Ibara ya 3 inatamka wazi kuwa nchi hii itaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, kwa maana hiyo CCM na Chadema vyote ni vyama halali vilivyosajiliwa na Msajili wa vyama vya siasa ambavyo vyote vinatakiwa kufanya shughuli zake za kisiasa kwa kuzingatia sheria.

Kwa hiyo itakuwa ni maajabu ya karne iwapo Jeshi letu la Polisi litahalalisha mkutano wa CCM wa tarehe 23/7/2016 na wakati huo huo kuuharamisha mkutano wa Chadema wa Bavicha!!!

Let us wait and see, lakini so far niwapongeze sana Bavicha kwa strategies zenu za hali ya juu za kukabiliana na utendaji kazi wa double standard wa Jeshi letu la Polisi.

Hata hivyo kwa mwendo tunaokwenda Jeshi la Polisi kama linataka kujijengea heshima ndani ya jamii ya watanzania, linalazimika kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sheria za nchi na lijiepushe kabisa kufanya kazi zake kama 'kitengo' cha CCM.

Wakipuuza ushauri huu, basi wajue watakuwa wamedhamiria kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa..........
 
Kweli BAVICHWA ni vichwa ngumu..inamaana hamkumsikia Braza Mbowe au Yule Mzee Wa Mvi...Asiyesikii la wakuu wake..?
 
Maneno kuntu kutoka kwa kichwa chenye busara
 
Madawati yalitakiwa kununuliwa na change ya radar, wanaochangia sasa ni wajinga ndio waliwao.
Yangenunuliwa kwa hela ya rada hospitali wakakosa vitanda bado tungechangia. Ni nini kinakuuma watoto kusoma?
 
Back
Top Bottom