Baada ya azimio la Bavicha la kuzuia mkutano mkuu wa Ccm kutikisa nchi kiasi cha kulifanya jeshi la polisi 'kuandamana' mji mzima wa Dodoma wakiwa na magari ya washa washa na siraha nzito nzito. Na baada ya zuio la mwenyekiti wa chama taifa kwa azimio hilo, badala yake Bavicha watafanya mkutano mkuu wa dharula ndani ya wiki mbili toka hivi sasa mkoani Dodoma.
Mkutano huo mkuu maalum utajadili ukandamizwaji wa demokrasia unaoendelea nchini ikiwa ni pamoja na kukamatwa, kupigwa, kudhalilishwa na kufunguliwa kwa kesi kwa viongozi wakuu wa baraza hilo. Utakumbukwa pia mkutano wa baraza kuu la wanawake (Bawacha) chini ya Halima Mdee ulifanyika Dodoma pia.
Kinachosubiriwa ni viongozi wakuu wa baraza hilo kurudi Dar es Salaam ili kutoa taarifa rasmi ya kusudio hilo kwa katibu mkuu ambaye hatarajiwi kukataa ombi lao