Bavicha: Kikwete toka hadharani uliombe taifa radhi

Bavicha: Kikwete toka hadharani uliombe taifa radhi

BAVICHA Taifa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
117
Reaction score
662
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


​
Wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba (BMK) wanaounda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA) walisusia vikao vya bunge hilo kwa sababu ya CCM kwa upande mmoja na serikali yake kwa upande mwingine kuendeleza vitendo vya kupanda chuki, ubaguzi wa waziwazi wa kikabila na dini, matusi pamoja na kuacha rasimu ya wananchi na kupenyeza rasimu ya CCM ndani ya bunge maalumu la Katiba.


Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) linapongeza kwa dhati hatua hii ya kuachana na Bunge ambalo kimsingi linaonekana kuwa hatari kwa umoja, mshikamano na amani ya Taifa letu.


Lugha za ubaguzi wa waziwazi wa kidini zilizotelewa na viongozi wa serikali na CCM ni sumu mbaya kwa taifa hili kwani kundi linalobaguliwa likikosa uvumilivu tutalishuhudia taifa letu likitumbikia kwenye machafuko kama yale yanayoendelea kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutibu donda kama hilo daima haiwezekani kama historia inavyotuasa.


Aidha kubagua watanzania kwa makabila yao ni kitendo haramu kichopaswa kukomeshwa mara moja kwani hii ni chemikali mbaya isiyo na kifani kwa umoja wa Taifa letu.

Hivyo ni mwendawazimu pekee angekubali kushiriki dhambi hii mbaya na isiyosameheka ya kulipasua taifa na kuhujumu maoni ya wananchi wanaotaka mabadiliko ya taifa lao kupitia Katiba mpya iliyokua ikiendelea ndani ya BMK.


BAVICHA inaamini kuwepo kwa hali ya namna hii inayojitokeza kwenye mchakato wa Katiba mpya kunatokana na udhaifu wa Rais Kikwete kama kiongozi wa nchi ambaye , kwa kuruhusu mawaziri wake na wbunge wa chama chake kufanya vitendo hivi, amekubali taifa limfie mikononi mwake.


Rais Kikwete kuasisi na kuzikubali lugha za vitisho dhidi ya wananchi wanaotaka mabadiliko kwenye muundo wa serikali ya Muungano kupitia yeye mwenyewe, mwaziri na viongozi mbalimbali wa serkali na chama chake kunadhihirisha jinsi asivyojali na alivyodhamiria kulipasua vipande vipande taifa hili.


Wakati BAVICHA tukiunga mkono na kupongeza juhudi za UKAWA za kuzunguka nchi nzima kuwaelimisha wananchi juu ya uchakachuzi na hujuma dhidi ya maoni yao zinavyofanywa na serikali na CCM, pia tunataka mambo ya fuatayo yafanyike;


1. Jakaya Mrisho Kikwete kama Rais aombe radhi taifa kwa lugha zake za vitisho alizozitoa wakati akizindua BMK kwani kauli yake haikua na tafsiri nyingine zaidi ya kuwa rasimu ya wananchi ikipita kama ilivyo basi ataliamuru Jeshi kuchukua mamlaka. Kauli kama hii haikupaswa kutoka kwenye kinywa cha mtu mwenye hadhi kama ya rais.

2. Jakaya Mrisho Kikwete kama Mwenyekiti wa CCM atoke sasa hadharani aliombe taifa msamaha kwa vitendo vichafu na viovu vinavyofanywa na wana CCM na mawaziri wake ndani na nje ya BMK. Sambamba na hilo, ili kurudisha imani na mshikamano ndani ya taifa letu, Kikwete akemee hadharani wabunge wa CCM na washirika wake kukoma mara moja tabia hii ambayo sio tu ni mbaya bali pia ni ya hatari kwa taifa letu.


3. Waziri Mkuu aliyemtuma waziri LUKUVI kwenda kuhubiri udini kwenye madhabau ya nyumba za Ibada na ndani ya BMK kwa niaba yake aombe radhi taifa kwa kitendeo hicho kwani kwa vyovyote vile haitarajiwi kiongozi wa serikali kupanda chuki za namna hii miongoni wa wananchi wa taifa letu.


4. Kwa kua mpaka sasa waziri Lukuvi, kwa kauli zake ameonekana kuwa kirusi cha hatari kwa umoja, mshikamano na amani ya taifa letu, ni vema na muhimu akafukuzwa kwenye nyadhifa zake zote.


5. Kwa kua tume aliyoiteua Rais Kikwete ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya iliundwa na watu waliokuwa na wanaoheshimika kwa utumishi wao ndani na nje ya taifa na ambao kwa uadilifu wao wamefanya kazi yao kama ilivyostahili hata kama haiipendezi serikali na CCM, waombwe radhi na Rais Kikwete mwenyewe hadhari kwa matusi waliotukanwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa CCM ndani nan je ya BMK. BAVICHA inaamini hata mtu angekua amepungukiwa na akili kiasi gani, matusi yaliyoelekezwa kwa wazee kama wakina Warioba, Butiku, Ahmed Salimu, Jaji Ramadhani, Prof Baregu na wengine hayavumiliki kwa kiwango chochote kile


Imetolewa leo tarehe 20.04.2014 Jijini Dar es salaam na;

John Heche
Mwenyekiti Taifa - BAVICHA
 
Good reasoning, Well articulated and well composed ...nitarejea punde...
 
wa kuomba radhi ni mgonjwa wa akili tundu lisu kwa kumtukana nyerere..bavicha ni misukule hawajielewi
 
pamoja sana kamanda kwakweli taifa lipo njiapanda kwa sasa.
 
dah, hilo la namba 1: sijui kwa nini lifanyike sasa wakati ni la muda mrefu sana
 
dah, hilo la namba 1: sijui kwa nini lifanyike sasa wakati ni la muda mrefu sana

Suala hilo halina muda mrefu. Hotuba aliyotoa Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa bunge ambayo wajumbe wanaotokana na CCM wameigeuza kuwa reference point badala ya Rasimu ya Katiba Mpya, ndiyo iliyoharibu mjadala wa Bunge Maalum la Katiba.

Huwezi kusema pia kuwa imepitwa na wakati ilhali majuzi umemsikia akirudia kauli zile zile, wakati wa mahojiano maalum na waandishi wa NMG.
 
Baraza la VIchaa Chadema(bavicha)


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Baraza la vijana wanaojitambua sio kama mavijana ya chama chakavu yanayopinga Rais kutotoka kaskazini kanakwamba imezuiwa hivyo kikatiba mlaaniwe sana maccm. Heko sana BAVICHA tamko sahihi na wakati mwafaka pamoja sana.

BACK TANGANYIKA
 
Heche na Munishi wanaongoza kwa ustadi sana wing hii ya vijana cdm.
 
Baraza la VIchaa Chadema(bavicha)


Sent from my iPhone using JamiiForums.
Hivi unadhani BAVICHA ni kama Umoja wa Vichaa wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)? Hivi unataka kumfananisha John Heche na Mtia kalikiti wenu Sadifa? Unataka kumfananisha Munishi na mlagongo wenu Mapunda?

GO BAVICHA
 
Hivi unadhani BAVICHA ni kama Umoja wa Vichaa wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)? Hivi unataka kumfananisha John Heche na Mtia kalikiti wenu Sadifa? Unataka kumfananisha Munishi na mlagongo wenu Mapunda?

GO BAVICHA

Kiboko, unapojaribu kumfanyia mwenzio ndivyo sivyo, naye hutafuta namna ya ku revenge. Hebu angalia sasa umejibiwa sawa sawa na kashfa zako. Mimi huwa najiuliza mbona matusi, kashfa, mipasho, na ubaguzi vinaonekana kutokea sana upande fulani? Halafu watu wazima na akili zao wanachekelea kana kwamba ni mambo mazuri. Hii haitupeleki kwenye mustakabali mzuri wa nchi yetu hata kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom