Batuli Kisaya Atikisa tena Arusha

Batuli Kisaya Atikisa tena Arusha

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Kundi LA Friends of Batuli linaloongozwa na Mwl.Batili Kisaya kwa Mara nyingine limetikisa jiji la Arusha baada ya kugawa kadi za bima ya Afya kwa watoto pamoja na kutoa msaada wa vyakula ,sabuni kwa wazee wasiojiweza.

Hatua hiyo imepongezwa na viongozi mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo iliyobamba katika ukumbi wa polisi mess Arusha na kudhuliwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo.

Hata hivyo baadhi ya wadau waliopewa fursa ya kuongea katika hafla hiyo akiwemo mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel(Monahan) ,wakurugenzi wa halmashauri , mbunge,Madiwani na wasomi mbalimbali waliwatupia lawama baadhi ya wanasiasa na wabunge wa viti maalumu kutotumia vipato vyao walivyojaliwa kuisaidia jamii yenye uhitaji.

Catherine Magige ni mbunge wa viti maalumu ccm katika jiji la Arusha ambaye amekuwa akitajwa kutokuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii .

Wadau kundi hilo. Pamoja na kipongeza jitihada za kuisaidia jamii wameitaka jamii kuiga mfano huo .
IMG-20190407-WA0006.jpeg
IMG-20190407-WA0014.jpeg
IMG-20190407-WA0016.jpeg
IMG-20190407-WA0012.jpeg
IMG-20190407-WA0007.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom