Basi la sumry mbeya arusha na harufu ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Basi la sumry mbeya arusha na harufu ya ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASHADA, Sep 17, 2012.

 1. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana jamvi, hivi majuzi nilisafiri na basi la Sumry lililokuwa linatoka Arusha kuja Mbeya. Tulipoondoka Morogoro, alipanda mtu mmoja aliyevaa nguo za Jeshi (bila shaka ni mwanajeshi yule),tulipofika usawa wa lile bwawa upande wa kushoto ukielekea Iringa (Sijui jina lake), na kabla ya kufikia walipo traffic, mara basi likasimama. Kuangalia upande wa kushoto wa barabara, tukaona gari dogo limepaki pembeni, watu watatu wako mle ndani, milango yote minne imefunguliwa. Walipoona basi limefika wale jamaa kwenye gari dogo walishuka kijeshi kijeshi fasta, wakafungua buti, wakatoa mabox fulani wakayaingiza kwenye buti la sumry kwa style ya haraka sana. Wakati wanamalizia kupakia yale maboksi, yule mwanajeshi aliyekuwa kwenye basi akashuka na kuingia kwenye gari dogo na kuondoka na hilo gari dogo, na basi likaendelea na safari.

  Abiria tukaanza kushikwa na mshangao na kujiulizamaswali kibao. Mtu aliyekaa karibu na mimi akaniambia hii ni mara ya tatu anasafiri na hili basi na kuona wakifanya huu mchezo. Kuna kila dalili kuwa kuna magendo au mzigo haramu unasafirishwa, kwani waweza kujiuliza, kwa nini wasioakie stend? Kwa nini wakapakie maporini? Kwa nini yule mwanajeshi kapandia Morogoro na kushukia tuu pale mbele? Kumbe siyo msafiri? Na ana uhusiano gani na wale waliokuwa wametangulia na gari dogo?

  Bila shaka kuna harufu ya ufisadi na utakuwa unafanywa na vigogo serikalini.
   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo Bongo. Watu wanatafuta fedha kwa njia haramu. Inawezekana suala hilo hata mmliki wa Summry halifahamu. Unachoweza kufanya ni kuwatonya vijana wa Said Mwema ingawa kwa jinsi nchi yetu ilivyo unaweza ukawa umewapatia ulaji nao.
   
 3. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uwezekano ni mkubwa kwamba walikuwa wanapakia aidha bangi au mchanga wenye dhahabu maana pale mindu kuna wakati watu walikuwa wanachimba dhahabu wakapigwa stop.
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kweli. Nami nakumbuka kuna wakati wananchi walijaa eneo hilo wakichimba dhahabu kabla ya kufukuzwa.
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Si nasikia ni Mh Sana.
   
 6. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,321
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Imekuwa ni nchi ya kuishi kwa ujanjaujanja, nchi ya kitu kidogo inayoongozwa na mtu wa dhaifu wa kijiweni. Kwa hisani ya sources mbalimbali Eg. Jenerali Ulimwengu na Mnyika.
   
Loading...