Basi la Mwendokasi laharibika na kufunga barabara

Basi la Mwendokasi laharibika na kufunga barabara

Gari kuharibika ni kawaida.. Hakuna jipya hapo.. Tufanye kazi wakuu muda WA majungu hakuna
Ingekuwa Ni wewe umekadiria kuwahi Na mwendokasi halafu unakutana msongamano kwa sababu ya kupita njia ya kawaida ingekuwa hakuna jipya
 
Mradi una huduma mbpvu kabisa. wanatoa magari machache watu kibao. Kwanza hatujui yameingiza faida/hasara kiasi gani hadi sasa.
 
kwanini yaanze kuzima doubledouble?hiyo kwa maana nyingine itakuwa ni sabotage kwani katika hali ya kawaida sio rahisi,sio jambo la kushangaza mbona hata ndege zina pata failure kwenye runways na kusababisha congestation kama hizo.
 
Bwana nyumbatatu hi picha uliipiga ukiwa unakimbia au, lengo lako ni sisi kuona hilo li mwendo kasi lililoharibika, sasa hilo libarabara loooote ulo onyesha la nini?
 
Basi la mwendokasi limeharibika kituo cha shekilango Na kufunga njia yake hivyo kulazimisha mabasi mengine kupita barabara ya kawaida Na kuongeza kero . Inaonekana wameshindwa hata kuulivuta kulisogeza usawa wa kituo ili yapishane. Kama basi moja linaleta kero hivi sijui yakianza kuzima double double itakuwajeView attachment 535267 View attachment 535268 View attachment 535269 View attachment 535269
Niliwahi kumuuliza rafiki yangu Reggie polles wakati nafanya kibaruwa Dar,je likiharibika moja nje ya kituo itakuwaje?alinijibu lakini sikumbuki alinijibu nini,Bwana Reggie Polles njoo ujibu swali langu tena,najua kuna nafax kubwa umo humu!
Dzl
 
Nadhani mleta mada alikuwa anamaanisha usumbufu uliojitokeza kwa abiria kutokana na tatizo dogo km hilo
 
HATA BINADAMU HUUGUA GHAFLA, SASA CHA AJABU NI NINI GARI KUHARIBIKA?? TUJIELEKEZE KWENYE MASUALA YENYE TIJA
Kwa ufikiriaji wako hata hayo mambo yenye tija hayatakuwa Na tija!, hata ndege ya Medline Albright iliwahi kuharibika kwenye airport yetu lakini walichofanya Ni kubadili vibovu Na kufunga vipya papo hapo, hawakulala wala kusubiri spea kutoka marekani, hata mtu kuugua hakuna cha ajabu, ajabu huwa inakuja kwenye huduma anayopata.
 
Kama bado lipo njian chomoeni tair na vio muuze
Kama vile magar na boda zikipita njia ya m/kas wanavyofanya
In JPM voice
 
tulihoji kwa nn njia zake ni nyembamba sana haziruhusu kupishana??? wakajib kuwa wamejipanga
 
Nakumbuka hotuba ya Halima Mdee kuwa haya "makopo ya kichina" yamenunuliwa kwa mkopo wa NMB. Mkopaji ni Kisena/Simon Group, ila dhamana ni ardhi ya UDA ambayo inamilikiwa kwa 49% na serikali, lakini cha ajabu serikali haikuhusishwa kwenye huo mkopo. Inasikitisha kama ni kweli, na yameshaanza kubuma sijui kama deni limeshalipwa hata nusu.
Mdee yupo kolokoloni.
 
Inamaana iko siku daladala ikitokea ajali zitaingia DART.? au kunya kuku bata kaharisha ? Utasikia ingilieni uzuri mtokee migomogo..
 
tuta la katikati kwenye hizo njia liondolewe kama vile kuanzia ubungo maji kwenda kimara
 
Hicho n chombo cha moto muda wowote kinaweza loga ukiangalia zinatumika sana muda mwing barabaran
 
Nachoshangaa ni kitu kimoja.
Basi limeharibika njia ya kutokea Manzese kwenda Ubungo.

Lakini mabasi yaliyooneshwa hapo juu yanatokea Ubungo kwenda Manzese.
Ndio kusema kuwa Basi limeziba hadi upande wa pili wa njia ya kuelekea mjini???
 
Back
Top Bottom