Wananchi wenye hasira wameteketeza kwa kuchoma moto basi la Mtei Express linalosafiri kati ya Singida - Arusha - Singida baada ya kugonga pikipiki na kuua watoto watatu hivi punde
Source: mpiga debe wa Mtei aliyeko stand kuu Arusha
Kwahiyo, mizigo yote, parcel zilizotumwa kwa ndg, jamaa na rafiki vyote ni majivu sasa! Wananchi wenye hasira bwana?!! balaa, ila unaweza kuta mwenye bodaboda (pikipiki ndiye aliyechemsha", poleni wote
Wadau nimepita hapa Singida nikitokea Arusha nimekutana na basi la Abiria mali ya kampuni ya Mtei. Chanzo ni kwamba gari hilo limemgonga bodaboda aliyekuwa amebeba watoto wawili waliofikwa na mauti.Hakika inasikitisha sana kwa upande wa wafiwa na kwa kuchomwa basi hili kwani mabegi na mali za abiria zilizokuwamo ndani ya gari vyote vimeteketezwa.