KILIVITE
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 1,302
- 556
Basi dogo maarufu kama Ihowanja kwetu linalomilikiwa na kada maarufu wa CCM wilayani Ulanga Mark Asenga ambaye pia ni diwani wa Mahenge limepata ajali katika barabara mbovu kuliko zote duniani maeneo ya Lwambanjuki karibu na kijiji cha Iragua na watu wanne kufa papo hapo na wengine wawili kufia njiani wakielekea hospitali,mmoja kati ya waliokufa ni mdogo wake Mark Asenga ambaye alikuwa msimamizi katika gari hilo.Pichani ni basi hilo kabla ya ajali.