Basi la Hood lapata ajali Mikumi likitokea Arusha kwenda Mbeya

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Imetokea ajali maeneo ya Mikumi. Basi la HOOD limepinduka saa tano usiku wa kuamkia leo likitoka Arusha kwenda Mbeya.

Aliyenipa taarifa alikuwepo kwenye gari na ameumia mguu ila yupo salama.

Mwenye taarifa zaidi atujuze maana jamaa simpati tena hewani..
 
Saa sita, ila kama saa tano imemkuta Mikumi angetumia busara kulala Morogoro...
Kuhusu kulala. Njiani Sio hood huyu jamaa safari ya Arusha mbeya amejimilikisha na nikipande kirefu Sana yupo zaidi YA miaka kumi sidhani kama kuna kampuni nyingine alishajaribu kunusa ihi root.... Huyu chalinze anapita saa kumi na mbil au saa moja jioni Ila kabla YA kuwepo torch alikuwa anapita saa sita au saba... Nissan diesel akikupita ndio kashakuacha.... Kupata ajali ni nadra Sana na nibahati mbaya poleni woteee
 
Hood biashara imemshinda.Mabasi yote namba A na yamezeeka sana.Pandeni New Force, Kimotco, Happy Nation, Kiazi Kitamu mk
New force via chalinze ametoa basi zake, ila hood anaikomalia iyo njia kwa sababu yuko peke yake, ila huwa nashangaa arusha to mbeya kuna arusha express via kondoa unafika saa 4uck na inaweza kuwahi Adi saa3uck Ila cha ajabu kuna watu wanakomaa na hood na wanafika Kesho.
 
Hiyo route haijafa tu? inakuwaje watu bado wanasafiri Arusha to mbeya kwa kuzunguka Chalinze?
Kwa nini wasipitie shortcut ya Dodoma, Iringa Mbeya ikiwa wanafika mapema kabisa?
Nini maana ya kujenga barabara sasa?
Watu wanaangalia biashara na SUMATRA hawawezi kumchagulia mtu njia.
 
Kuhusu kulala. Njiani Sio hood huyu jamaa safari ya Arusha mbeya amejimilikisha na nikipande kirefu Sana yupo zaidi YA miaka kumi sidhani kama kuna kampuni nyingine alishajaribu kunusa ihi root.... Huyu chalinze anapita saa kumi na mbil au saa moja jioni Ila kabla YA kuwepo torch alikuwa anapita saa sita au saba... Nissan diesel akikupita ndio kashakuacha.... Kupata ajali ni nadra Sana na nibahati mbaya poleni woteee
Nissan Diesel au Scania?
 
Back
Top Bottom