Basi la Champion laua watu wanane Dodoma

EMT

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Messages
14,483
Points
2,000

EMT

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2010
14,483 2,000
BASI la Champion lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Dar es Salaam, limepata ajali mbaya jana na kusababisha vifo vya watu wanane papo hapo, abiria wengine 53 wamejeruhiwa vibaya, 21 kati ya hao hali zao mbaya. Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Stephen Zelothe alisema, ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi wa basi hilo. Dereva wa basi hilo alijaribu kukimbia baada ya ajali lakini alikamatwa.

Kamanda Zelothe alisema, basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi muda wa saa 8:30 mchana, likapasuka matairi ya mbele katika eneo la Nala kilometa 13 kutoka Dodoma mjini na likapinduka mara mbili. Kwa mujibu wa Zelothe, majeruhi 21 ambao hali zao ni mbaya na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, wengine walipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Baadhi majerihi ambao majina yao yalipatikana ni Ashura Kitala, Mohamed Issa, Veneranda Resalilo, Rashid Mkoma, Abdallah Jurababu na John Macha. Wengine ni Wilson Kilule, Raj Sigha, Masumbuko Mariori, Augustino Moshi, Suzana Mwita, Alex Pamilo, Rose Richard, Flaviana Hemed, Hugen Issa na Magessa Bwire. Pia wapo Amos Tarimo, Joshua Abdallah, Elizabeth Petro, Rebecca Daniel na Issa Hussein.

Habari Leo
 

Forum statistics

Threads 1,356,562
Members 518,911
Posts 33,133,185
Top