Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,374
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake dhidi ya vita ya maneno inayoendelea kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Taarifa iliyotolewa leo jioni Jumatatu Desemba 3, 2018 na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole inaeleza kuwa kauli ya Bashiru kumtaka Membe ambaye ni mwanachama wa chama hicho kufika ofisini kwake ni ya kawaida ndani ya CCM.

“CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Bashiru kwa Membe,” inaeleza taarifa hiyo.

“Ni kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.”

Chama hicho kimetoa rai kwa Watanzania kuwa wito huo ulikuwa ni wa kawaida hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea katika mitandao ya kijamii ina hila mbaya kwa CCM.

Katika taarifa hiyo Polepole amesema CCM inawataka Watanzania kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo katika kipindi hiki ambacho Rais John Magufuli anaendelea kuongoza nchi katika mageuzi ya uchumi na maendeleo.

Chama hicho pia kimeeleza ushindi wake ilioupata katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye Kata 47 Tanzania Bara uliofanyika Desemba 2, 2018.

Amesema CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi chama hicho kimeshinda kwa kishindo.

Desemba 17 na 18, 2018 jijini Dar es Salaam chama hicho kitakuwa na kikao cha kawaida cha uongozi wa Taifa.

Amefafanua kuwa Desemba 17, kitakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huku Desemba 18, kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Chanzo: Mwananchi
 
Sasa mzushi. mchonganishi, mfitini na msambaza uvumi ni nani kama sio Katibu Mkuu wa CCM ambae ndie alitangaza kutaka kumhoji Membe kwa tuhuma zilizotolewa na mwendawazimu mmoja??!!

Sasa mzushi, mchonganishi, mfini na msambaza uvumi ni nani kama sio Katibu Mkuu wa CCM ambae baadae akabadili kauli yake na kudai anamwita Membe ili kuchota busara za kiongozi huyo huyo kindakindaki wa CCM?

Sasa mzushi, mchonganishi, mfitini na msambaza uvumi ni nani kama sio wewe Polepole ambae, baada ya kuona tangu Bashiru achukue ukatibu mkuu hivi sasa huongelewi tena, leo hii unaibuka na kumchonganisha katibu mkuu wako kwamba kumbe aliyowahi kuongea hapo kabla ni uongo mtupu na kwamba katibu mkuu wako ni mropokaji tu??!!!!
 
Mbona kasi ya wito imeisha Ghafla. Maana mwanzo Bashiru alisema na kuuliza kwani nyie hamumsikii Membe.. leo imekuwa ni aje kwa hiari na ni kubadilishana uzoefu na sio kuthibitisha tuhuma???
Mara nyingi huwa nikangalia Bashiru akiongea huwa namuoa kama ni mtu wa kupayuka, kuropoka na kupaniki haraka
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa msimamo wake dhidi ya vita ya maneno inayoendelea kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Taarifa iliyotolewa leo jioni Jumatatu Desemba 3, 2018 na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole inaeleza kuwa kauli ya Bashiru kumtaka Membe ambaye ni mwanachama wa chama hicho kufika ofisini kwake ni ya kawaida ndani ya CCM.

“CCM inapenda kuwafahamisha kuwa imefuatilia kwa ukaribu mjadala unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wito alioutoa Bashiru kwa Membe,” inaeleza taarifa hiyo.

“Ni kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Katibu Mkuu kukutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.”

Chama hicho kimetoa rai kwa Watanzania kuwa wito huo ulikuwa ni wa kawaida hivyo uzushi, uchonganishi, fitina na uvumi mwingine wowote unaoendelea katika mitandao ya kijamii ina hila mbaya kwa CCM.

Katika taarifa hiyo Polepole amesema CCM inawataka Watanzania kuendelea kuwa na umoja, mshikamano na upendo katika kipindi hiki ambacho Rais John Magufuli anaendelea kuongoza nchi katika mageuzi ya uchumi na maendeleo.

Chama hicho pia kimeeleza ushindi wake ilioupata katika uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye Kata 47 Tanzania Bara uliofanyika Desemba 2, 2018.

Amesema CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi chama hicho kimeshinda kwa kishindo.

Desemba 17 na 18, 2018 jijini Dar es Salaam chama hicho kitakuwa na kikao cha kawaida cha uongozi wa Taifa.

Amefafanua kuwa Desemba 17, kitakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huku Desemba 18, kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa.

Chanzo: Mwananchi
Polepole yuleyule aliyekuwa anamfundisha CAG na watanzania hisabati?!
 
Huyu chakubanga bora angeuchuna tu, KM amemuita Membe kwa njia isiyo sahihi na pia amemtwika tuhuma nzito za kumhujumu Mh.Rais halafu anasema ni jambo la kawaida, yaani KM na huyu chaku wote ndiyo wale wale aliosema Zitto.
 
Back
Top Bottom