DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi na Mbunge mstaafu Dkt. Bashiru Ali Kakurwa amewatoa hofu Vijana na Watanzania kwa ujumla, akiwaeleza kuwa Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi madhubuti na hodari aliyeyashinda majaribu mengi, akisisitiza kuwa anao uwezo mkubwa wa kudhibiti rapsha rapsha za sasa na kile alichokiita "Vijimaneno" vya kupanga.
Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 08, 2025 Mwanza Mjini kwenye Viwanja vya Nyamagana wakati wa muendelezo wa Kampeni za Dkt. Samia, akisema anasikia maneno na wasiwasi kutoka kwa Vijana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania.
"Kama nchi yetu imebaki nchi moja, Chama chetu kimeendelea kuwa kimoja, usalama na amani umetamalaki tena katika kipindi kigumu sana cha mabadiliko ya serikali ya ghafla, tumevuka. Hizi rapsharapsha hizi ambazo zinapangwa na hivi vineno vineno ambavyo vinapangwa, ni rahisi kuvidhibiti.
"Simaanishi kwamba tupuuze majaribio ya kutikisa amani ya nchi yetu hata kidogo, simaanishi kwamba tupuuze jaribio la kutikiza misingi ya amani ya nchi yetu. Ninachotaka kusema huyu kiongozi ni hazina ya uzoefu wa uongozi katika Vipindi vigumu sana." Amesisitiza Dkt. Bashiru.
Bashiru pia amekiri kuwa hana wasiwasi kwasababu Watanzania waliomuunga Mkono kipindi kile ndiyo hao hao na hawajabadilika sawa na wale waliomuombea dua na kutangaza kazi nzuri aliyoifanya, akihoji walipo Watanzania wa kuvunja amani ya nchi.