Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
"Umadhubuti wa Chama chetu na hasa umadhubuti wa uongozi wako Dkt. Samia Suluhu Hassan katika vipindi ambavyo dunia imetikiswa, si Tanzania peke yake, tumepigwa na korona, kuna mabadiliko ya tabia nchi, kuna vita ambavyo vinatikisa uchumi wa dunia lakini pia kumezuka siasa za kujitambulisha kwa uzalendo uchwara wa kidini, wa kikabila, hata ubaguzi wa rangi - nchi yetu Tanzania imeendelea kusimama imara bila kuyumba hata pale ambapo dunia imetikishwa. Kwahiyo nawahakikishia chini ya Dkt. Samia akiwa Rais baada ya nyie kumchagua lakini akiwa Mwenyekiti wetu, nchi yetu itabaki imara. Na mimi nakupongeza. Dkt Bashiru Ali