Bashe Umenifanya nilie, same study ifanyike kwenye upande wa Dawa (Pharmaceuticals)

Tunalia sana waTanzania wenzangu. Si maeneo hayo mnayoyasema, Afya, Kilimo pekee; bali kila sehemu utakayoitizama ina uozo.
Sasa kwa nini msijiulize tatizo lipo wapi hasa katika muundo wa serikali na katika sheria zetu.
Kama sheria zipo, hazitekelezwi, sasa kwa nini watu waogope kuiba.
Mtumishi kaiba eneo moja, suluhisho likawa ni kumhamishia eneo jingine, huku akiendelea kufaidi matunda ya wizi wake, kwa nini wote wasitamani kuwa sehmu itakayowawezesha kuiba?
Ndiyo maana siku hizi, hata uteuzi unapofanyika, watu wa karibu na mteuliwa wanashangilia, kwa sababu kapewa ulaji

Ukiniuliza mimi nitakwambia hivi: uozo umetapakaa toka huko juu kabisa kunakohimizwa bila aibu yoyote "watu wale kwa urefu wa kamba zao," hadi ngazi ya chini kabisa serikalini.

Kiongozi mkuu anapokuwa mtu anayevumilia uozo na kupindisha taratibu usitegemee kuwa patakuwepo na ufanisi katika kuzuia haya tunayo lalamikia.

Nenda China, au Vietnam uone wanafanya nini kukomesha ujinga unaovumiliwa hapa kwetu.
Hapa kwetu umesikia ni viongozi wangapi waliotuhumiwa na ubadhirifu wa mali ya umma wamepewa adhabu stahiki, bila ya kuoneana haya; kwa haki tupu.
Tukimpata kiongozi anayeweza kufanya hivyo utaona hali inabadilika.

Sahihi kabisa kabisa
Mtu anaiba then anatumbuliwa. Ukiiba ni kitanzi au kifungo cha maisha kisichokuwa na msamaha

Shida ni pale wiz unakuwa linked na state , mawaziri so hatawakurugenzi watafanya ivo
 
Yule Brigedia alipaswa kuwa Polisi. Nasikia alipiga sana pale hadi mama kuja kumchomoa. Lakini kuhusu bei za dawa pale ni tatizo. Nadhan pale ndio kuna majambazi zaidi ya kilimo. Na majambazi yanaanzia wizarani

Kama ikipigwa a simple audit kwenye manunuzi ya Dawa na bei wanazouzia wananchi ni billions of money

Wakati nipo Hospital tulikuwa hatutaki kabisa to channel our order pale . Imagine mkurugenzi wa hosp unaletewa order yenye tofauti ya 500M kati ya bohari kuu na mtaani

A simple audit inahitajika pale

Bashe awe waziri wa Afya
Bashe maneno mengi, action zero.Mpaka sasa ni 25% tu ya wakulima wamefikiwa na mbolea ya ruzuku nchi nzima!
Hiyo Wizara ya Afya apewe Makonda,yule mwehu haogopi mtu na ni mfuatiliaji mzuri!
 
I think Bashe is overrated. Bashe ni mpiga porojo tu. Ni mwaka wa ngapi huu akiwa sekta ya kilimo, tangu akiwa naibu na sasa waziri kamili, na amefanya nini?

Wakulima wa tumbaku mkoa wa Tabora mwaka Jana tu wamelia kama watoto. Kampuni iitwayo Mkwawa iliyoundwa kwa partnership ya wazawa akiwemo Bashe mwenyewe, Rostam na Ridhiwan, imenunua tumbaku kwa bei ya chini na kuwachelewashea malipo.

Kwa upande wa korosho, tangu awe waziri hakuna jipya. Bei mbovu na zinawanyonya wakulima. Bashe huyu huyu alianzisha mfumo wa stakabadhi gharani. Wakulima walioingia mkenge na kufuata mfumo huo hawajauza korosho mpk leo .

Wakulima wa mahindi nchi nzima wanalia na bei.

Sasa ubora wa Bashe upo ktk lipi?
Jamaa anapiga porojo tu, action zero.Wizara ya Afya apewe Makonda tuone kama huo uchafu hajafagilia mbali!
 
Umechanganya issue nyingi hadi umenipoteza ila ngoja turudi hapa ambapo ndio kuna msingi ili tuwe ukurasa mmoja..., amegundua kuna upigaji gani na unapigwa vipi na ni makosa ya nani ? (kama sio Serikali yake) na nini kifanyike au anakifanya

Issue ni kwamba wanaolima wengi ni peasants na hawana nguvu wala hawataipata bila kuungana wao kwa wao na ku-form cooperatives..., bila hao so called walanguzi hizo debe mbili au tatu anazovuna huyu peasant angeishia kuzila mwenyewe au kuliwa na panya....

Tupo karne ambayo kilimo kinaweza kufanywa na wachache na kulisha nchi nzima (efficiency imeongezeka na manpower need kupungua) sasa ni vipi Bashe anaweza kuwawezesha hawa wahusika ili kunufaika na hio efficiency... By the way bora sasa wanalimishwa hata wanapata ujira kidogo kuliko serikali yao iliyowasahau hata hicho kidogo cha kununua gongo na kaniki wasingekipata

Usipende sana kubisha bisha

Serikali isimamie wakulima na kuwapatia fursa, iwezeshe wakulima wadogo kuwa wakubwa

Hizo takataka ulizoongea zipo only Tanzania,hata uganda wametuzidi. Serikali ikiwezekana itoe hata financial assistance to support local farmers sambamba na kuwafungulia njia

Pia walanguzi wasajiliwe na walipe kodi , wawe na leseni za ulanguzi
 
Jamaa anapiga porojo tu, action zero.Wizara ya Afya apewe Makonda tuone kama huo uchafu hajafagilia mbali!

PCM wizara yoyote atafanya vema

Nashauri PCM apewe Wizara ya Afya akawaweke mwiko walanguzi wa dawa na maafisa wanaochezesha bei za dawa
 
I think Bashe is overrated. Bashe ni mpiga porojo tu. Ni mwaka wa ngapi huu akiwa sekta ya kilimo, tangu akiwa naibu na sasa waziri kamili, na amefanya nini?

Wakulima wa tumbaku mkoa wa Tabora mwaka Jana tu wamelia kama watoto. Kampuni iitwayo Mkwawa iliyoundwa kwa partnership ya wazawa akiwemo Bashe mwenyewe, Rostam na Ridhiwan, imenunua tumbaku kwa bei ya chini na kuwachelewashea malipo.

Kwa upande wa korosho, tangu awe waziri hakuna jipya. Bei mbovu na zinawanyonya wakulima. Bashe huyu huyu alianzisha mfumo wa stakabadhi gharani. Wakulima walioingia mkenge na kufuata mfumo huo hawajauza korosho mpk leo .

Wakulima wa mahindi nchi nzima wanalia na bei.

Sasa ubora wa Bashe upo ktk lipi?

Tupe hoja zaid tukusikilize, unakitu
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Bashe maneno mengi, action zero.Mpaka sasa ni 25% tu ya wakulima wamefikiwa na mbolea ya ruzuku nchi nzima!
Hiyo Wizara ya Afya apewe Makonda,yule mwehu haogopi mtu na ni mfuatiliaji mzuri!

Ninaafika,PCM wizara ya Afya ataiweza yule ngosha na wamamchukia maana kuna majambazi pale
 
Angalia kodi ya mafuta,PM ameacha kufuatilia lts ngapi za mafuta zimeingizwa nchini na kiasi gani cha kodi ya barabara kimekusanywa.na kwanini baadhi ya majimbo barabara haziendi wakati masheli ya mafuta yapo?

Kwanini PM kaacha kufuatilia ?
 
Usipende sana kubisha bisha
Kubisha nini na wewe umejibu nini ?
Serikali isimamie wakulima na kuwapatia fursa, iwezeshe wakulima wadogo kuwa wakubwa
Na nani anawakilisha serikali katika hii sekta na kama hayo hayafanyiki kosa la nani ? Na fursa zinapatikana vipi kama tu wameshindwa kuhakikisha masoko ya kile wanacholima
Hizo takataka ulizoongea zipo only Tanzania,hata uganda wametuzidi. Serikali ikiwezekana itoe hata financial assistance to support local farmers sambamba na kuwafungulia njia
Local assistance ya nini pesa / Ruzuku au ? (Kumbuka hizo ni kodi za huyu huyu mkulima anakatwa ili zitoke kama ruzuku...,

Hata tu kuhakikisha wauze wanapoweza kupata pesa zaidi bado kuna ngonjera mara wauze nje mara wasiuze basi tu ni siasa siasani....
Pia walanguzi wasajiliwe na walipe kodi , wawe na leseni za ulanguzi
Walipe Kodi ili Serikali ndio ichukue hio Kodi mnunuzi wa mwisho bei ipande ? Kama hao walanguzi wanatoa pesa ndogo kwanini hio serikali badala ya kutoa ruzuku isinunue hayo mazao kwa hio so called bei nzuri na kuyapeleka huko kwenye bei nzuri zaidi (utaona ni win win situation)....
 
Kubisha nini na wewe umejibu nini ?

Na nani anawakilisha serikali katika hii sekta na kama hayo hayafanyiki kosa la nani ? Na fursa zinapatikana vipi kama tu wameshindwa kuhakikisha masoko ya kile wanacholima

Local assistance ya nini pesa / Ruzuku au ? (Kumbuka hizo ni kodi za huyu huyu mkulima anakatwa ili zitoke kama ruzuku...,

Hata tu kuhakikisha wauze wanapoweza kupata pesa zaidi bado kuna ngonjera mara wauze nje mara wasiuze basi tu ni siasa siasani....

Walipe Kodi ili Serikali ndio ichukue hio Kodi mnunuzi wa mwisho bei ipande ? Kama hao walanguzi wanatoa pesa ndogo kwanini hio serikali badala ya kutoa ruzuku isinunue hayo mazao kwa hio so called bei nzuri na kuyapeleka huko kwenye bei nzuri zaidi (utaona ni win win situation)....

Una kitu na utafika mbali.Mimi sio mtaalam sana wa kilimo. Mimi ni daktari wa kuua na kufufua (an anesthesiologist).

Kwahiyo Bashe kafanya politics za kuingiza pesa mkono wa kushoto na kuchukua mkuno wa kulia

Dah hilo Taifa bwana, halina maisha
 
Shida ni pale wiz unakuwa linked na state , mawaziri so hatawakurugenzi watafanya ivo
Mawaziri na wakurugenzi na wengine wote wenye nafasi za kukupua mali ya umma wanafanya hivyo kwa kujuwa walio juu yao wanakwapua zaidi ya wao.

Nijisahihishe kidogo mwenyewe katika bandiko lililopita. Rais wa nchi katika mfumo kama wetu anayo nafasi ya kupunguza au hata kuzuia kama ni kiongozi aliyedhamiria hivyo bila kujali kumuudhi nani ndani ya chama chake.
Lakini ukitaka kukomesha ujinga huu wa viongozi kuwa mafisadi, ni kwa chama kuwa na msimamo wa kutovumilia ufisadi.
China, siyo Xi pekee anayehakikisha hali hiyo haishamiri nchini humo. Ni mfumo wa chama chao cha Kikomunisti. Hata majizi yaliyomo humo yanaogopa yataanzia wapi kulegeza nati.
Badala yake, kwetu sisi na CCM yetu, chama ndicho kinahimiza watu waibe. Chaguzi zao zote ni rushwa tupu, tena nje nje. Watu kama hao wataanzia wapi kukomesha wizi.
 
Back
Top Bottom