Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.
Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.