Bashe alivyoukwaa uenyekiti wa UVCCM kwa njia za panya

mudavadi

Member
Apr 19, 2011
53
14
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.
 
ndutu

Member
Mar 22, 2011
90
15
Kubenea alilisema hili siku nyingi mpaka akapigwa BAN. Malisa na Shigela wameidhalilisha UVCCM katika namna ambayo haijawahi kuonekana, na hii yote ni sababu ya tamaa na kukosa upeo. Halafu Malisa anadai kwamba eti kuna watu wanatumiwa na wawania urais 2015, kana kwamba yeye siyo kijana wa kazi wa mgombea urais.
 
banyimwa

Senior Member
Mar 1, 2011
116
23
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.

Kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?
 
Tiote

Senior Member
Mar 6, 2011
139
36
Kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?

If you rattle a snake you should be prepared to be beaten. Wamemchekea huyu dogo sasa ndiye anayetumika kukiyumbisha chama na hata serikali.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Jamaa ame-graduate kinoma. Alianza na kuwatafutia mabibi wakubwa zake na sasa ndiye anyetumika kama dynamite ya kukilipua chama na kwa vile yeye hana cha kupoteza hajali kama nchi hii itageuka kuwa haitawaliki kama kule Puntiland alikotoka.
 
Mpevu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,808
171
Haishangazi wala kustaajabisha kwa SIASA ZA TANZANIA & KUPAKANA MATOPE...kesho yake anageuka kuwa ni 'lulu'.
This is the Tanzania I know.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Sio mbaya wenye akili zao wanajua na kanuni ni ile ile USE AND ABUSE.Kama hao wanaowapa PESA wako Laboratory wanapumulia mashine sembuse makarani wao.Si ajabu kwa kuwa WHAT GOES AROUND COMES AROUND,walipata vyeo kwa majungu na naniniii sasa muda ukifika miti itaongea na nguvu itaisha .
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Kweli hii nchi haijawahi kuishiwa vituko.

Hawa uvccm si ndio walikuwa wakimshambulia FTS na ENL kwamba rais wa nchi hii 2015 hawezi kutoka kaskazini? Kwamba rais ajaye ni ,mwenyekiti wa ccm JK ndiye anamfahamu.

Sasa mara hii tena wameshahamia kambi ya kaskazini? Kweli njaa nyingine mbaya sana. Hatahivyo ni bora mara mia moja rais ajaye atoke kaskazini kuliko ukanda wa pwani. Ndugu zangu wa ukanda wa pwani mtanisamehe bure kwa hili.
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Siasa za hawa wahuni nzinajulikana sana..........acha waendelee kutoboana macho........two years down the line watakuwa vipofu tayari!!
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?

Rais alijisahau aliposema hayo! Akikumbuka atatwambia hile kauli yake imeishia wapi maana alitamka yeye mwenyewe kwa mdomo wake bila aibu.
 
Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,325
9,960
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na
girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.

Mkuu kwenye red hapo,i thought Benno was married,au?
 
Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
594
Bora Lowassa angekuwa president kuliko huyu m.kwere legelege. Hii post imekaa kimajungu majungu na kujihami kama Nape. Mtoa hoja hana data wala uthibitisho zaidi ya kudhania. Usiishi kwa kudhania kama mgambo wa jiji, weka data tujue hizo fedha zilichukuliwa bank gani na walikabidhiana lini, sio kukurupuka tu baada ya kuona gazeti la Bashe limewageuka magamba
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,282
37,502
Kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?

Wewe unamshangaa huyo Bashe, Mkapa ni raia wa Msumbiji lakini ameweza kuwa rais wa Tanzania kwa mika kumi. Nchi hii we acha tu, ndiyo maana Mzee Ruxa aliwahi kusema Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Bora Lowassa angekuwa president kuliko huyu m.kwere legelege. Hii post imekaa kimajungu majungu na kujihami kama Nape. Mtoa hoja hana data wala uthibitisho zaidi ya kudhania. Usiishi kwa kudhania kama mgambo wa jiji, weka data tujue hizo fedha zilichukuliwa bank gani na walikabidhiana lini, sio kukurupuka tu baada ya kuona gazeti la Bashe limewageuka magamba

Maswali ya kibwege hayo. Tuko mahakamani hapa? Kwani hizo wanazofanyia kampeni halali wamewahi kusema wamezitoa benki gani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom