Bashe alivyoukwaa uenyekiti wa UVCCM kwa njia za panya

Kuna watu walishasema Hamis Kigwangalah anamwogopa Bashe kama ukoma, na kila comment anayoitoa Bashe au inayomhusu Kigwa lazima ajibu.
Kitu kimoja ambacho Mr Hamis Kigwa hujawahi kujibu kwa ufasaha ni ile tuhuma aliyoitoa Bashe juu ya wewe kuiba jina la mshindi std 7 kwenda Kigoma Secondary.
ninapita tu
 
Kule Igunga nilikaa na Bashe na Kigwangalal jirani pale Pick Hotel, walikuwa wakiongea vizuri huku wote wakitambiana...mwaka 2015 Nzega itawaka moto...japokuwa jimbo linaweza kugawanywa kutokana na Nzega kuwa Halmashauri ya Mji na kuwa na kata mpya

ninapita tu
 
Huyu jamaa si tunasikia ana kampuni yake na inafanya vizuri tu...
Wengine wanasema humu alifaidika na ufisadi wa stimulus package?


Kigwangala moto huo unakuja, 2015 anza kutafuta kijiwe cha kuvutia gepu la maisha nje ya siasa. Umecheza na moto, sasa unakuja kwa kasi ya kimbunga, Bashe huyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo! Supported by RA na EL, utauweza huo motooooooooooooooo! Anza kutafuta vijiwe 2015
 
Lowassa angefaa kuwa Rais kwa staili yake ya kuwakimbiza watendaji, lakini kwa jinsi alivyochafuka hawezi kufikia huko...
ataishia hapo hapo maana akiukwa urais lazima atalipiza visasi kwa Sitta, kwa JK, na wengine wote...itakuwa balaa

Hawatoweza kumuacha apenye hata iweje


EL ndo pekee anaweza kurekebisha makosa ya rafiki yake kwa miaka kumi. Wengine wote ni watu wa visasi tu. Tumpe nchi muone mambo. Kifupi hatutaki tena rais maskini maana nae hatatulia mpaka ajenge kwao.
 
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.

Hawa ndio wenye chama, fulana, sukari, kofia, kanga zinatoka kwao. Big-up Bashe
 
Sijui swala la urahia wa Hussein Bashe, lakini nilichotaka kusema kwamba I did get an opportunity ya kukaa na Bashe pamoja na Benno kwenye kikao. Huyu kijana Bashe ni balaa, hapo kichwani yuko vizuri sana. Kutokana na maongezi yaliyokuwa yanaendelea, mtu yeyote angechuja jinsi Benno kuwa mshabiki na mwenzake kuwa very strategical person. Nakubaliana na watu waliotangalia na kusema Benno amembebwa tu na hakuna cha maana anachoweza kuleta mezani.Bashe if he can stand alone he can do big things.
 
Sijui swala la urahia wa Hussein Bashe, lakini nilichotaka kusema kwamba I did get an opportunity ya kukaa na Bashe pamoja na Benno kwenye kikao. Huyu kijana Bashe ni balaa, hapo kichwani yuko vizuri sana. Kutokana na maongezi yaliyokuwa yanaendelea, mtu yeyote angechuja jinsi Benno kuwa mshabiki na mwenzake kuwa very strategical person. Nakubaliana na watu waliotangalia na kusema Benno amembebwa tu na hakuna cha maana anachoweza kuleta mezani.Bashe if he can stand alone he can do big things.

Wakati mwingine ukiwa na kichwa chenye seti tupu ni rahisi kudhani kila mtu ni kichwa.
 
Back
Top Bottom