Hichi ndicho alichokisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa na mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Nzega, HUSSEIN BASHE kuhusiana na kauli za Nape Nnauye leo asubuhi katika Power Breakfast..."Ukirudi katika Historia 2005 Nape Nnauye aliwahi kusema Jakaya akishinda atahama Nchi kwa kuwa alikuwa kambi ya Mzee MALECELA na baadae alihamia kambi ya mzee Mwandosya wakati wa tatu bora lakini hakuhama na akaja akateuliwa na Raisi JAKAYA MRISHO KIKWETE kuwa Mkuu wa Wilaya, na leo ni Katibu Mwenezi wa Chama, Vile Vile ni huyu huyu NAPE aliibuka na kusema jengo la makao makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ni ufisadi mtupu leo ndo yumo mule mule kwenye lile jengo anafanyia kazi na lile jengo linakipatia Chama fedha, na wale wanaokwenda Nyumbnani kwa Mhe. LOWASSA ni wale walioitikia wito wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya kuazaliwa kwa CCM kule Songea, .alisema tukimuona mtu ana uwezo na ana faa tumshawishi,.
Imefika time NAPE aondoke kwenye ukatibu uenezi aje hadharani afanye kampeni ya Mgombea wake kwa sababu anafahamika amesimamia maslahi ya nani yeye na kambi yake ni muda muafaka waje hadharani twende kwa wana CCM, twende kwa watanzania.
Watanzania na wana CCM wataamua mgombea wanaemtaka kuliko kutumia mwamvuli wa CCM na ukatibu uenezi kutisha wana CCM, Nape na Kundi lake hatutawaruhusu kutunga uongo, uongo ambao wa uamini wao, wautangaze wao na wautumie uongo huo kumuhukumuEDWARD LOWASSA. Imetosha ndani ya CCM kumfanya EDWARD LOWASSA punching Box, Mara nyingi wamemgeuza punching Box na amekuwa mvumilivu huu ni ujumbe kwa Nape na Kundi lake, kwani inajulikana.
NAPE hasimamii maslahi ya chama linapokuja suala la Uraisi bali ana simamia maslahi ya kundi lake kwani wamefanya trade off na Mgombea Mmoja wa Uraisi kuwa ataachiwa jimbo na anataka Ubunge na ili hoja yake ya Ubunge ifanikiwe lazima amsaidie huyo Mgombea kufanikisha malengo yake anayoyataka.
Tuna fahamau ndani ya CCM kuna aina nne ya wagombea wa uraisi
(1) Kuna ambao wana dhamira ya kuongoza nchi
(2) Kuna ambao wana tarajia kuupata Uraisi mezani hawa ndo wale wanataka demokrasia ifinywe ndani ya Chama
(3) kuna wale wanaowekeza kutafuta Uongozi wa baadae
(4) na kuna wale wanaitwa Wajasiriamali wa Uraisi wao wanatafuta umaarufu kwa kutengeneza majina ili wafanye biashara ya Uraisi kwa kukusanya fedha ndani na nje ya Nchi. NAPE akae pembeni ya ukatibu uenezi aachie uenezi watu wengine kwa sababu ni mjumbe wa Sekretarieti ya chama ana wajibu wa kuwa fair kutokuwa na mgombea.
Sasa aje afanye kampeni ya Mgombea wake hadharani aache kujificha kwenye kichaka cha ukatibu uenezi wa CCM. Inafahamika kaachiwa jimbo gani na anapelekwa na nani Jimboni kutembezwa na kunadiwa kuwa yeye ndo mrithi ni mda muafaka sasa apishe uenezi aje barabarani kumpigia kampeni Mgombea wake".