Bashe abaini ufisadi wa Bilioni 10 Bodi ya Korosho

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Korosho nchini kuhakikisha shilingi bilioni 10 kutoka hazina zilizotolewa kwa ajili ya kununua mbolea na viwatilifu kwenye zao la korosho zinarudi hazina, baada ya bodi hiyo kuzitumia kinyume na maelekezo ya serikali.

Naibu Waziri Bashe aliyasema hayo katika ziara yake ya kukagua kontena zaidi ya 350 za mbolea na viatilifu yaliyopo katika bandari kavu tatu ikiwamo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Azam za jijini Dar es Salaam.

"Kuna kampuni inaitwa Bajuta imepewa bilioni 4.5 kati ya bilioni 10 na Bodi ya Korosho zilizotolewa na hazina kwenda kwa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), wakati Bodi ya korosho inafanya maamuzi hayo hayakuwa ni maamuzi ya serikali"- Alisema Bashe na kuongeza;

"Naagiza ufanyike ukaguzi maalum na ukaguzi wa uwezo kwa kampuni ya pembejeo na viwatilifu ya Bajuta, juu ya mnyororo wa usambazaji pamoja na usambazaji wa pembejeo katika sekta ya kilimo na ukaguzi huo usifanywe na Wizara ya kilimo Bali ufanywe na hazina ili viongozi wote waliobadilisha matumizi ya Sh. bilioni 10 zilizoelekezwa kwenda Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) wachukuliwe hatua mara moja."

Akifafanua alisema TFC ilipewa jukumu la kuagiza mbolea na dawa aina ya Salfa ili iweze kuuzwa kwa wakulima kwa bei nafuu, lakini ilipokea Sh. bilioni moja kati ya 10 iliyotolewa na Hazina na hivyo bodi hiyo kuwakwamisha kutimiza malengo ya serikali.

Alisema mwaka mmoja sasa TFC, bandari kavu hizo zinashikilia kontena zaidi ya 350 zenye mbolea na Salfa.

"Rais Dk. John Magufuli alipotoa fedha hizo kwenda TFC alikusudia wakulima wapate unafuu wa mbolea na viatilifu ili kuwaboreshea kilimo chao, nasisitiza kwamba Kampuni ya Bajuta irudishe Sh. bilioni 4.5 mali ya serikali," alisema Bashe.
 
Korosho Ina roho ya Korosho, Ukiisaliti lazima nayo ikusaliti

Kwanini Lugha hizo zinatoka Wiki hizi za mwanzo za kuanza mavuno ya Korosho?
 
Anatoa ushauri uchunguzi ufanyike, hapo hapo anatoa amri Bujuta warudishe 4.5 bilions.

Aende taratibu tujue anataka nini, uchunguzi ufanyike au anataka warudishe pesa hata kama walilipwa kihalali?!

Uwezo wa Bujuta wa kusambaza viatilifu ana ufahamu vipi kabla ya uchunguzi wa kitaalam kufanyika?!

Au ana personal interest za kufanya hivyo?!
 
Pamoja na kula pesa za michango ya NSSF ya wafanyakazi wa New Habari kwa zaidi ya miaka kumi, Leo hii unapata wapi ujasiri wa kukemea wengine? Siasa zetu ni miujiza tosha, Rais Magufuli ni kweli huoni Hussein Bashe kavunja sheria ya mifuko ya hifadhi pamoja na kuibia wafanyakazi zaidi ya 150 pesa zao za kila mwezi ama wao sio Watanzania wanyonge
 
Siku zote kiasili, Bashe ni jasiri, na ujasiri wake ni wa asili kama ilivyo kikawaida ya majasiri, Jasiri haachi asili.

Niliwahi kushauri hivi kumhusu Bashe

Hata mimi mwenyewe ni mwandishi jasiri sana tuu, naweza kumuuliza yeyote swali lolote bila kujali chochote, na mambo ninayopitia sasa nilipaswa kuachana na uandishi na kuchangia humu jf lakini..., hivyo mkisikia nimeunga mkono juhudi au nimejiunga mahali, nawaombeni msishangae wala msinishangae!.

Nakuomba msiuchanganye ujasiri wa Bashe na matatizo ya Media ikiwemo New Habari, jee unajua kuhusu michango ya wafanyakazi wa Uhuru Mzalendo?. Unajua hali ya media awamu hii?. Jee wajua kama sio Magufuli kuingilia kati, Channel Ten saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine.

Hali halisi ya media ni hii

P
 
Wewe ni jasiri gani wakati ulipigwa mkwara na Ndugaye ukarudi umeufyata na sasa umebakia kuwa mtu wa kusifia sifia tu?
Siku zote kiasili, Bashe ni jasiri, na ujasiri wake ni wa asili kama ilivyo kikawaida ya majasiri, Jasiri haachi asili.

Hata mimi ni mwandishi jasiri, mambo ninayopitia sasa nilipaswa kuachana na uandishi na kuchangia humu jf lakini...
P
 
Pamoja na kula pesa za michango ya NSSF ya wafanyakazi wa New Habari kwa zaidi ya miaka kumi, Leo hii unapata wapi ujasiri wa kukemea wengine? Siasa zetu ni miujiza tosha, Rais Magufuli ni kweli huoni Hussein Bashe kavunja sheria ya mifuko ya hifadhi pamoja na kuibia wafanyakazi zaidi ya 150 pesa zao za kila mwezi ama wao sio Watanzania wanyonge

Kama aliiba siyo kigezo cha kuvichua madudu katika wizara yake.

Nampongeza kama yupo sahihi na ushahidi anao.
 
Bashe kwa sasa hawezi kuguswa na yeyote na hata huyo Mungu wao hawezi kumgusa Bashe maana wanao tegemewa kuokoa jahazi la uchaguzi ndiyo wamemuweka hapo alipo

Pamoja na kula pesa za michango ya NSSF ya wafanyakazi wa New Habari kwa zaidi ya miaka kumi, Leo hii unapata wapi ujasiri wa kukemea wengine? Siasa zetu ni miujiza tosha, Rais Magufuli ni kweli huoni Hussein Bashe kavunja sheria ya mifuko ya hifadhi pamoja na kuibia wafanyakazi zaidi ya 150 pesa zao za kila mwezi ama wao sio Watanzania wanyonge
 
Siku zote kiasili, Bashe ni jasiri, na ujasiri wake ni wa asili kama ilivyo kikawaida ya majasiri, Jasiri haachi asili.

Hata mimi ni mwandishi jasiri, mambo ninayopitia sasa nilipaswa kuachana na uandishi na kuchangia humu jf lakini...
P
Mzee ujasiri endelea kupiga kelele CCM waache kuwabambikia kesi wapinzani wapunguze mrundikano wa kesi mahakamani.
 
Pamoja na kula pesa za michango ya NSSF ya wafanyakazi wa New Habari kwa zaidi ya miaka kumi, Leo hii unapata wapi ujasiri wa kukemea wengine? Siasa zetu ni miujiza tosha, Rais Magufuli ni kweli huoni Hussein Bashe kavunja sheria ya mifuko ya hifadhi pamoja na kuibia wafanyakazi zaidi ya 150 pesa zao za kila mwezi ama wao sio Watanzania wanyonge
Sijawahi kuona mwanaccm ambaye siyo mwizi.
 
Siku zote kiasili, Bashe ni jasiri, na ujasiri wake ni wa asili kama ilivyo kikawaida ya majasiri, Jasiri haachi asili.

Niliwahi kushauri hivi kumhusu Bashe

Hata mimi ni mwandishi jasiri, mambo ninayopitia sasa nilipaswa kuachana na uandishi na kuchangia humu jf lakini...

Nakuomba msiuchanganye ujasiri wa Bashe na matatizo ya Media ikiwemo New Habari, jee unajua kuhusu michango ya wafanyakazi wa Uhuru Mzalendo?. Unajua hali ya media awamu hii?. Jee wajua kama sio Magufuli kuingilia kati, Channel Ten saa hizi tungekuwa tunazungumza mengine.

Hali halisi ya media ni hii

P
potiiiiiiiiiiii....
 
Back
Top Bottom