Basena atua, akataa wazembe Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Basena atua, akataa wazembe Simba

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Apr 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KOCHA mpya wa Simba Mosses Basena ametua nchini jana na leo anatarajia kusaini mkataba wa miezi sita na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa huku akitoa mapendekezo ya wachezaji anaowaitaji .

  Simba iliyokuwa ikinolewa na Patrick Phiri wa Zambia aliyemaliza mkataba wake, itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika. Basena pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Uganda, 'The Cranes'.

  Kocha huyo aliyewasili na ndege ya Shirika la Ndege la Uganda saa 10:45 jioni, baada ya ya kutua aliwaambia waandishi wa habari: "Nimekuja, naisikia Simba na nimekuja kuijenga Simba...mashabiki wasitarajie miujiza katika kipindi kifupi.

  "Nahitaji kupewa muda kuijenga Simba, nataka kuangalia wachezaji na zaidi napenda kuwa na wachezaji wanaojituma, wachezaji wanaotambua majukumu yao uwanjani na wanaoheshimu mashabiki.

  "Ili timi ifanye vizuri, lazima kuwe na ushirikiano wa viongozi, wachezaji na wanachama wa Simba...nafahamu nina jukumu kubwa la kuisuka Simba," alisema Basena ambaye alilakiwa na katibu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala.

  Basena aliyekuwa anainoa Kiyovu Sports ya Rwanda, alisema kwa sasa amekuja kutia saini mkataba wake pamoja na kuzungumza na viongozi na kusema yuko tayari kutoa ushirikiano katika suala zima la usajili.

  Akizungumzia Simba kupokwa ubingwa: "Simba wamepoteza ubingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, nawahesabu kama mabingwa pia kwani ubingwa wa jinsi hii si wa kutambia sana...," alisema.

  Awali Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage wiki iliyopita alimtangaza kocha huyo mpya kwa madai huku akisema walikuwa wamemalizana na Phiri lakini kama uongozi walimpa mkataba mwingine mpya wa miaka miwili lakini kocha huyo mpaka sasa hajaurudisha kwa hiyo ina maanisha hataki tena kurudi katika klabu hiyo.

  Alisema pia uongozi wao wameona waachane naye kwa kuwa amekuwa akiondoka kila mara timu yao inapokuwa inajiandaa kwa michezo mikubwa muhimu hali inayoonyesha wazi kuwa alikuwa hataki tena kuifundisha timu hiyo.

  Katibu Mkuu wa Simba, Mtawala alisema baada ya kusaini, kocha huyo atakuwa na kikao na kamati ya utendaji ya klabu hiyo pamoja na kamati ya ufundi kwa kuwa benchi lote la ufundi limevunjwa.

  Pia, alisema baada ya benchi la ufundi kuvunjwa rasmi katika kikao cha kamati ya utendaji kilichopita, wamempa kazi kocha huyo kutafuta msaidizi wake ambaye atasaidiana kuinoa timu hiyo.

  Katika hatua nyingine, sakata la mshambuliaji wa Simba Mbwana Samatta limezidi kuibua mapya baada ya Meneja na mlezi wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo kujitokeza na kusema kuwa mchezaji huyo ni mali halali ya Simba.

  Kisongo atakuwa mtu wa tatu kuthibitisha hili baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Baba mzazi wa mchezaji huyo Ally S,amatta kusema kuwa mchezaji huyo ni mali halali ya Simba.

  Mzozo huo umeibuka hivi karibuni baada ya timu ya TP Mazembe ya Congo kumnunua mchezaji huyo kwa dola 100,000 ambazo tayari klabu ya Simba wamekwisha kabidhiwa.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Kisongo alisema kuwa yeye kama mlezi na mshauri wa mchezaji huyo ameagizwa na mchezaji huyo kueleza masikitiko yake kutoka na marumbano yanayoendelea juu yake.
   
Loading...