BASATA wana nguvukazi ya kutekeleza azimio/uamuzi wao?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
9,752
2,000
Nimesikia redioni na kusoma mitandaoni kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wameazimia na kuamua kuzipitia kazi zote za kisanaa za wanamuziki zikiwa kwenye sauti tupu (audio) au sauti na picha (video) kabla ya kuchezwa kwenye vyombo vya habari na burudani. Nimesikia na kusoma kuwa kila wimbo utakaotolewa na kila mwanamuziki utawasilishwa BASATA kwanza kwa ajili ya kupitiwa na kuridhiwa.

Kimsingi, naiona nia nzuri ya BASATA ya kuzuia nyimbo zisizo na maadili katika maneno na matendo ya nyimbo husika. Ni lazima kila wimbo usikiuke maadili ya kitanzania kwa kutumia lugha zisizo za staha na matendo ya kudhalilisha utu. Lakini, BASATA wana rasilimaliwatu ya kutosha kutekeleza hilo? Isije ikawa zoezi husika likafifisha sanaa kwa kuchelewesha kupitiwa na kuruhusiwa kwa nyimbo za wasanii.

Hatahivyo, kila msanii aanze kuwa mfano wa kuimba na kuonyesha nyimbo zenye heshima. Hakuna haja wala si ujanja kuimba wimbo wenye maneno ya matusi na unaodhalilisha utu wa awaye yeyote. Wanamuziki wa zamani walitamba na kusifika kwa nyimbo zao zenye lugha mwanana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom