BASATA: Marufuku kusikiliza au kusambaza nyimbo zilizopigwa marufuku

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) limewaonya wote wanaotumia kazi zilizopigwa marufuku kuwa ni ukiukwaji wa sheria za nchi na wote wanaotumia kazi zilizopigwa Marufuku, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Wamedai bado kuna watu wanatumia kazi zilizopigwa marufuku ikiwemo clubs, Radio na Bodaboda.

Baraza limesisitiza kwa kutoa onyo na kuwakumbusha wote wanaotumia kazi hizo zilizopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria wanaweza kuingia mikononi mwa sheria.

Hayo yamesemwa leo wakati wakiufungia rasmi wimbo wa Nay wa Mitego uliosambaa mitandaoni, katibu mkuu wa baraza hilo amesema wanazuia wimbo huo kutumika kwa namna lolote lile kwa mujibu wa sheria.
basata.jpeg


=======

UPDATE II:

Siku moja baada ya Kukamatwa kwake, Rais Magufuli ameagizwa Ney wa Mitego aachiliwe na Nyimbo yake ipigwe katika vituo vyote vya Radio na TV. Kwa habari zaidi soma=>Rais Magufuli aamuru Ney wa Mitego aachiwe huru na wimbo wake upigwe vituo vyote redio na TV
 
BASATA ni kimbilio la wavivu kufanya kazi wao wanapiga soga siku nzima wakitegemea kuneemeka kupitia wasanii ndomana miaka nenda rudi hamna cha maana wanachokifanya
 
Kwa sheria gani inayokataza kupiga nyimbo private? Sheria inawatambua kama wasimamizi wa kazi za sanaa Tanzania
 
Basata watumie busara watuambie ni uchochezi gan uko Kwenye nyimbo, Kwan nyimbo imetaja ni viongoz wa nchi gan au rais gan, mahakaman Kesi hiyo wanashindwa waziwaz, poor Logic na waache F fallacy
 
Ni aibu kuona waliopewa kuongoza sanaa hawaijui sanaa na wajibu kwa jamii.
 
Back
Top Bottom