BASATA kufungia wasanii hawa wa dansi 100 si halali

BASATA kufungia wasanii hawa wa dansi 100 si halali

The Wolf

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
9,468
Reaction score
20,877
Makundi mawili ambayo yalifuzu kushiriki hatua ya robo fainali katika shindano la Dance100% 2016 yameondolewa kushiriki katika shindano hilo kutokana na utovu wa nidhamu na kukiuka kanuni za shindano hilo.

Kundi la Best Boys Kaka zao ambalo limeondolewa ushiriki wa Dance100%
Makundi yaliyotolewa ni Best Boys pamoja na P.O.D ambayo yote yalitakiwa shiriki robo fainali ya Jumamosi tarehe 13 Agost, 2016 viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam
Akizungumza wakati washiriki hao walipoitwa kusaini mikataba ya kushiriki shindano hilo mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bwana Kurwijira N. Maregesi amesema katika mashindano yoyote duniani nidhamu ni kitu muhimu sana ambacho kinaweza kumfanya mshindanaji kufika mbali katika kufanikiwa kwenye maisha na shindano.
‘’Hatuwezi kuwaita kuja kushiriki shughuli yenu na ninyi mnakuja baada ya masaa mawili baada ya tukio kuanza, tena makundi mengine yametuma mwakilishi mmoja, huu ni utovu wa nidhamu na BASATA kama msimamizi wa sanaa Tanzania hatuwezi kuvumilia jambo hili ni lazima tuoneshe mfano kwa kuwasimamisha ili wakati mwingine iwe fundisho kwa makundi mengine’’ Amesema Bwn. Maregesi.

Aidha Bwan Maregesi ameongeza kuwa lengo la makundi hayo kuitwa ni kuweza kusaini mikataba ambapo mtu mmoja hawezi kusaini mkataba wa kundi zima hivyo makundi ambayo wametuma mtu mmoja watalazimika kupisha shindano na kuacha wenye nia kuendelea.
Kwa upande wake mmoja wa Jaji wa shindano hilo Super Nyamwela amewataka washiriki wote kuheshimu muda hasa katika kipindi hiki ambacho makundi hayo yanakutana na majaji kwa ajili ya kuweza kufundishwa namna ya kutawala jukwaa, kuchagua nyimbo, pamoja na kwenda na muda.
Makundi ambayo yatashiriki Dance100% Jumamosi katika mchuano wa robo fainali Jumamosi Agusti 13, 2016 ni pamoja na B.B.K Crew Boys , Mazebe Powder , D.D.I Crew, The Quest Crew, The Hero's Crew , Clevers Boys, Mafia Crew ,T.W.C Crew , Makorokocho Crew ,Ikulu Vegas Crew ,Wazawa Crew ,J Combat Crew.

Source:Eatv

Hoja yangu
1. Hivi hawa BASATA wapo kwa ajili ya kufungia wasanii, kufuta na kutoa onyo tuu kwa wasanii wetu?kwanini hatusikii hata siku moja waki promote na kutetea maslahi mapana ya wasanii?

2. Maamuzi yanaonekana ni kukomoana, na hawa vijana Best boys na P.O.B walikwishafuzu kuingia katika mashindano haya je BASATA haioni kuwanyima fursa hiyo kwanza itasababisha vijana hawa kukosa haki yao halali ya kushiriki na kujishindia zawadi na hata kusababisha mashabiki wao kukosa burudani?

3. Je BASATA ndio waandaji wa haya mashindano?
 
kwahyo wao kuchelewa na kuleta mwakilish mmoja wa kundi ni sawa kwako?
 
Best boys watoto wa kigamboni, poleni sana wana, wapeni hi wazee wa mikinda, midizini, sombepa kwa mopela, ashoor , kwa msomali, west zone kwa Jepa, magenge ya juu, raha leo .

Poleni sana wana. Nmepamiss home
 
Hahahah! Mambo mengi basata wako nyuma ya mda, nani wa kuwawajibisha.

Onyo la mdomo lingefaa zaidi,kuliko la kuwafungia limekaa kama kuwakomoa hivi.
 
Hilo la kutuma mtu mmoja kusaini mkataba sioni kama ni tatizo.Wao kama kundi wamemchagua mtu mmoja awawakilishe inamaaana wanamwamini.
 
Basata wame -overreact kuchelewa sio sawa ila adhabu ni kubwa sana isiyokuwa na ulazima.
Na mimi nashangaa yani kuchelewa tuu ndo kuondolewa kushiriki...Mimi nilidhani utovu huo wa nidhamu labda walipigana au kusabanisha fujo..
 
Back
Top Bottom