BASATA imeshindwa kazi, ifutwe

BASATA imeshindwa kazi, ifutwe

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,981
Reaction score
4,174
Baraza la sanaa nchini(BASATA) ndicho chombo pekee kilichoundwa kwq minajili ya kusimamia maadili ya nchi kupitia sanaa na watu wote wanaojuhusisha moja kwa moja na tasnia hiyo burudani nchini, lakini chombo hichi kinaonekana kimeshindwa kwenda na wakati hasa kipindi hiki cha kushamiri kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kupashana habari na matukio za wasanii nchini.

Lazima tukubaliane kwamba, ndani ya miaka mitatu minne ya hivi karibuni matumizi ya mitandao yameongezeka kwa kasi, hivyo hii inaweza kuwa changamoto mpya kwa BASATA katika kuhakikisha misingi ya kuanzishwa kwake inaheshimiwa na vile vile kuhakikisha kwamba, sekta ya sanaa haiwi chombo cha kuharibu vijana ambao ndio mashabiki wakubwa wa muziki na sinema.

BASATA iliwahi kumfungia kufanya shughuli za muziki mwanamuziki shilole kwa madai ya kukiuka maadili ya jamii, pia waliupiga marufuku wimbo wa chura wa msanii snura ingawa walichelewa, hivi sasa wimbo huo haupigwi redioni na luningani lakini unaonekana youtube!(huu ni uzembe wa kuchelewa kuchukua hatua mapema).

BASATA inapiga marufuku uvunjifu wa maadili kwenye radio na televisheni lakini hapo hapo linaacha kuwachunga wasanii kwenye mitandao, matokeo yake wanakaa uchi na kutukanana na wengine kujiuza kabisa ingawa sio kwa uwazi..

Ukitazama hawa wanaoitwa wasanii hasa wa kike wamekuwa kama wacheza filamu za ngono, hawana adabu, maadili wala staha kwenye jamii! Kwa kuwa mambo hayo tunayaona na yameachwa tuyaone, basi ni vema BASATA ikafutwa tu, na gharama zinazotumiwa kuendesha chombo hicho zikatumiwa kushughulikia matatizo mengine ya nchi. Hakuna faida ya kuwa na chombo kisicho na faida.

Kama BASATA ipo tayari kujirekebisha, basi haina budi kufumuliwa na kusukwa upya na vile vile kuhakikisha kwamba BASATA inasajiri vikundi, jumuiya au mtu yeyote atakayetaka kufanya sanaa, vile vile kuzihakiki filamu na nyimbo zote ili kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria za maadili ya nchi.

Nimeshindwa kuweka screenshot ya baadhi ya wasanii wanavyotia aibu mitandaoni utadhani sekta ya burudani imekuwa ngono. Wasanii hawa ndio wamekuwa kama kioo cha jamii ya vijana wa kitanzania, watoto wanawaona, kuwasikiliza na kuwasoma mitandaoni, sijui tunajenga taifa la namna gani.
 
Kumbe ulikuwa hujui!! Kwa Tanzania ya sasa ili uonekane wewe ni msanii ni lazima yale maovu yanayopigwa vita yawe ni sehemu ya maisha yako mf wanaume kuvaa hereni moja, usuke nywele, uvae mlegezo, uimbe matusi, uharibu lugha, na wanawake kujiuza, kuvaa nusu uchi, kufanya ngono na watu maarufu nk.
 
Kumbe ulikuwa hujui!! Kwa Tanzania ya sasa ili uonekane wewe ni msanii ni lazima yale maovu yanayopigwa vita yawe ni sehemu ya maisha yako mf wanaume kuvaa hereni moja, usuke nywele, uvae mlegezo, uimbe matusi, uharibu lugha, na wanawake kujiuza, kuvaa nusu uchi, kufanya ngono na watu maarufu nk.
Ni bora tu BASATA ikafutwa isichezee kodi zetu. Wapo kama hawapo vile.
 
Back
Top Bottom