Baruakwa motyo wa binadamu

mzurisana

Senior Member
Joined
Jun 23, 2011
Messages
133
Points
0

mzurisana

Senior Member
Joined Jun 23, 2011
133 0
JAMAA FULANI
BOX
NI HUKU HUKU KITAA

26th 08 2011.
KITAA.

MWILI WA BINADAMU.
MOYO .
Mpendwa,
YAH:KUINGILIA MAJUKUMU AMBAYO HAYA KUHUSU.
Tafadhali rejea kichwa cha barua hapo juu,Mimi ni binadamu niitwae jamaa flani mkazi wa Tanzania,kwa muda mrefu nimekua nikitafuta njia sahihi ya kukufikishia barua hii lakini sijajua hadi leo hii sijui nitumie FeDex,DHL, CDS au UPS au labda shirika la posta,pia niliwaza niimeze mdomoni labda itakufikia lakini nimegundua itafika kwako ikiwa imeloa mate na hautopata ujumbe vizuri…..

Ila dhumuni la barua hii ni kutaka kukwambia kuwa tangu nilipozaliwa wewe uliwekwa kwenye mwili wangu kwa lengo moja tu la kusukuma damu mwilini kwa kutumia Left and Right ventrical pamoja na left and right Atrium,LAKINI “MOYO” mbona leo hii umejiongezea majukumu yasiyokuhusu?
“MOYO” umeacha kusukuma damu na sasa umejiingiza kwenye suala la mapenzi kwanini? “MOYO” hata wahenga walishasema mshika mawili siku zote moja humponyoka ,sasa kwanini wewe unashika mawili?
Nakumbuka “MOYO” ni wewe ulimuua rafiki yangu baada ya kumfumania mkewe, ni wewe “MOYO” uka-Panic na kusukuma damu yake kwa nguvu hatimae akapatwa presha akaanguka chini na kufa,kwanini ulimtendea ukatili kiasi kile!!.
Nimeamua kukuandikia barua hii sababu siku hizi naona na kwangu “MOYO” umeanza kujihusisha na mapenzi kwani imefikia hatua “MOYO” umekua unauma sababu ya mapenzi nna wasi wasi na mimi utakuja kuniua.
“MOYO” kwanini usitulie kama wenzako ini na Figo na ukafanya kilichokuleta mwilini kwangu,mbona una tamaa hivyo lakini?
Nakuomba suala la mapenzi plz “MOYO” liache kwa ubongo wenyewe ndio utajua umpe nani jukumu hilo na wewe uendelee na kazi yako ya kusukuma damu tu mwilini maana hyo ndio Proffesional yako.
Nadhani ombi langu utalifanyia kazi………

Wako mtiifu..
Jamaa flani
 

Forum statistics

Threads 1,358,206
Members 519,262
Posts 33,162,479
Top