Barua ya wazi wa Mhe. Rais JPM ili ku-suppliment ongezeko la Tax collection Tanzania

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Mhe. Rais JPM, tunakupongeza kwa juhudi zako kubwa za kujenga mifumo mbalimbali ili kukuza uchumi wa Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Wewe umejipambanua kuhimiza ujenzi wa viwanda kama moja ya nyenzo (tools) kufikia uchumi wa kati.

Inaeleweka kabisa, kwa lugha rahisi yenye tafsiri rahisi ambayo iko applicable kuwa Watanzania tukiwa na uwezo wa kumudu kulipia kulipia huduma za afya, maji, makazi bora, umeme, gharama za simu kama muda wa maongezi au data kwa ajili ya internet. Wengine wakijenga uwezo wanaweza kununua gari hata kama ni IST inayokula mafuta machache na mhusika atalazimika kununua mafuta ikiwa ni diesel au petrol.

Moja ya eneo ambalo litasaidia makusanyo ya kodi ni kujenga mifumo imara ya watu kufanya biashara ya bidhaa na huduma ili kuongeza mzunguko wa fedha. Kama baadhi ya biashara zinafunga, watu wanapunguzwa kazi kwa sababu ya makadirio makubwa ya kodi yanayofanywa na TRA, sawia na jana ulivyosema, hakuna mshindi katika hilo. Biashara zikifungwa, fursa ya kukusanya kodi tokana na mauzo ya bidhaa au hudumua kutoka katika hiyo biashara huwa inapotea.

Taarifa kutoka vyanzo kadhaa vinaonesha baadhi taasisi binafsi za biashara zimeanguka na hivyo imepelekea kupunguza wafanyakazi. Baadhi ya mabenki, vyombo vya habari, tasisi za bima zimepunguza wafanyakazi kwa kuwa “turnover” ya biashara imepungua na kuwafanya wamiliki wa biashara kutomudu gharama ya kujiendesha ikiwemo mishahara ya wafanyakazi. Wiki jana Joseph Kusaga mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group wakati akisheherekea miaka 19 ya Clouds FM, aliweka wazi kupungua kwa mapato ya kampuni yao kutokana na kupungua kwa matangazo ya biashara ambayo walikuwa wakipata kutoka kwa partners wao wa biashara.

Nijenge dhana rahisi yenye hesabu rahisi ambayo wengi tunaweza kuielewa. Kwa sasa tuna Watanzania zaidi ya milioni 23 wanatumia/wanamiliki simu za mkononi. Mzunguko wa fedha ukiwa mzuri na Watanzania hawa milioni 23 kili mmoja akatumia sh. 10,000 kwa waki kununua vocha kwa ajili ya internet na muda wa maongezi, TRA itavuna kodi kwa wastani wa zaidi bilioni 150 kutoka kwa watumiaji wa simu tu. Inawezekana kati ya hao Watanzania milioni 23 takribani milioni 21 hawajasajiliwa kama walipa kodi na hawana TIN ila kuna namna TRA itapata makato ya kodi moja kwa moja kupitia “purchasing power” ya hawa wahusika.

Achilia mbali baadhi ya biashara ikipunguza wafanyakazi say 200; moja kwa moja kodi za hao wahusika zinapungua na mtiririko wa fedha ambazo wahusika walitakiwa ku-spend itapungua au kusimama kwa muda wakati wanaji-position kufanya shughuli zingine. Ni Watanzania hawa hawa ambao wananunua bidhaa na huduma madukani. Na kama walikuwa wemekopa bank au kwingineko, kuachishwa kazi kunapelekea kushindwa kurejesha mikopo, makusanyo ya kodi yanapungua, mifuko ya hifadhi ya jamii nayo inapunguza kupokea michango ambayo kila mwezi ilikuwa inachangwa na muajiri na mfanyakazi.

Nini kifanyike. Kama kuna ulazima, serikali inaweza kuzi-bail out bishara halali ambazo zikiporomoka zinakuwa na athari kubwa ikiwepo kupotea/kupungua kwa tax base. Mwaka 2009, Rais Barack Obama aliamua kui-bail out GM Motors kwa lengo la kuokoa ajira za Wamarekani na kodi ya mauzo ya magari na vipuri ambayo Serikali ingekosa kama GM Motors ingefirisika na kufungwa. Leo hii, GM Motors inaendelea na biashara.

Jambo jingine, kama kuna uwezekano, iko haja BOT kutoa guanrantee kwenye Miradi mikubwa yenye kuleta tija kwenye kujenga uchumi wa Tanzania.

BOT wanaweza leverage kwenye “Project Investment Financing” ili Watanzania wenye uwezo wa kuanzisha viwanda wa bidhaa ambazo ni consumables kwa soko la ndani wafanya hivyo.

Nimewahi kutoa mfano hapa mara kwa mara kuwa, kuna Mtanzania ana mradi wa uwekezaji kwenye sekta ya kuchakata na kusindika mazao ya kilimo kwa soko la ndani na soko la nje ikiwemo AGOA. Mhusika amepata “consultants na Contractors” to make the project happen toka Holland na Israel. Holland kuna bank iko tarayi kutoa mkopo kwa uwekezaji huu. Wanachohitaji na “collateral” au Bank Guarantee au Government guarantee. Kwa serikali kutoa guarantee, ndani ya miezi 6-9 uwekezaji unaingia kwenye uzalishaji kwa kuchakata mazoa husika. Uwekezaji huu unatoa ajira ambapo wafnyakazi watakatwa kodi, wataingia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na bima ya afya.

Kuna Daktari wa Kitanzania ana investment project ya kuunda vifaa tiba ambavyo hakuna kiwanda kabisa kusini mwa jangwa la sahara. Kiwanda chake kinaweza kuajiri moja kwa moja watu 20 na kimahesabu, soko la ndani tu, kupitia MSD kuna uwezekano wa kuuza zaidi ya asilimia 75 kuhudumia Watanzania. Kama kiwanda hicho kikiwepo, Watanzania wataajiriwa, mwisho wa mwaka kitalipa corporate tax, na tutapunguza foreign cash outflows kununua vifaa tiba ambavyo mpaka sasa zaidi ya 90% tunaangiza nje ya Tanzania hasa India.

Kwa dhana ya hao Watanzania wawili ninaowafamu mie, bila shaka wako wengi. Uwekezaji kama huu ukiwa facilitated na kujiendesha utarejesha fedha za mkopo na kuna potential ya kupanuka.

Wakati mmoja Rais ulitabainisha kuwa Bank ya Maendeleo ya kilimo ina fedha zaidi ya bilioni 600 na hapakuwa na mkopo uliotolewa ndani ya miezi 9. Kwa kuwa kumekuwa na fedha kwa mikopo ya kuendeleza/kupanua sekta ya kilimo na na kuna Watanzania wame-tender investment project kupata funds yet hawajakopeshwa, something is very wrong kwa wakoeshaji au mashartu ya namna ya ku-access mikopo havitekelezeki. Wewe mwenyewe umeshuhudia jinsi TRA walivyo compliacate suala la vitambulisho vya wamachinga ambavyo ulikusudia kila mmoja alipie sh. 10,000 tu na sasa umekuja na initiative yako ambapo vitambulisho vya wamachinga 670,000 vikichukuliwa vyote itapatikana sh. Bil 13.4.

Mhe. Rais, akina Sergey Brin muasisi wa Google au Mark Zuckerberg muasisi wa Facebook vijana ambao ni mabilionea wakubwa kwa sasa, kwa namna ya masharti yaliyopoTanzania kwa viable start-up business, bila shaka hata wao wasingefua dafu kwenye kufungua biashara zao ambazo leo wanakuwa sehemu ya kujenga uchumi wa Marekani. Nataka kuamini hata Tanzania tuna brains, mazingira ni key

Mhe. Rais, wewe unapotaka kufanya jambo kwa mamlaka uliyonayo mambo yanakwenda. Ulitoa agizo la TRA kutengeneza vitambulisho wa machinga kw ash. 10,000 walisuasua. Wewe kwa initiative, you have made that happen. Umeingia madarakani nchi haina ndege kwa ajili ya biashara ya usafriri, you have made that happen.

Kama kuna namna ambayo unaweza kutengeneza back door channel kwa Watanzania ambao wana miradi mizuri yenye tija kukuza uchumi na wanakwamishwa/wanacheleweshwa, basi iwepo njia mbadala wakikutafuta uweze kuingilia kati ili mambo yatokee.

Inajulikana kuna baadhi ya watu huko serikalini ambao either hawako connected na vision yako au wapo wapo tu, achilia mbali wale wanaokuhujumu kama yule aliekuwa RPC ambae mmemgundua na mkamtumbua.

Mhe. Rais, kuna watu katika maeneo ya huduma katika taasisi za serikali ambao wanatakiwa ku-facilitate michakato wana ukosefu wa ubunifu na kujituma unapelekea matokeo yawe kiduchu sana.

Mr. President, I see you have a challenge to create, communicate and measure to attract, engage and retain talentend Tanzanian youngsters in business and investment who have not been given given chances to be amongst actors and being part of building Industrialized economy. They day you tap in such people’s potential who believes in what you believe; they’ll work and supplement your economic development vision with blood, sweat and tears to make it happen.

Mr. President, consider leveraging at least to go through their investment project which can make a significant difference.

Niliwahi kuandika hapa, kuna wakati Farao wa Misri alilazimika kumsikiza “mfungwa” aliekuwa gerezani kwa tuhuma za kutaka kumbaka mke wa bosi wake. Bila kujali tuhuma, alipopata nafasi ya kusikizwa alimpa Farao jibu la ukezaji mkubwa wa akiba ya chakula wakati ambapo chakula kilikuwa kingi na wakati wa ukame ulipofika, Farao, watu wake na nchi jirani wakawa wamepona kutoka katika njaa.

Sir, sometimes in future make initiative of getting in-touch with people outside the circles which you normally meet. You will be amazed on strategic investment project which can be implemented in Tanzania which inturn will expand the tax base.

Mhe Rais JPM, tukishirikiana kuongeza/kukuza juhudi za mzunguko wa fedha, kodi itakuja very automatic through spending in purchase of goods and services.


Asalam Aleykum
 
Back
Top Bottom