Barua ya wazi na pongezi kwa Mh Lukuvi

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,119
Kwanza nikupongeze kwa kurudishwa kwenye wizara ambayo umeitumikia katika serikali ya awamu ilyopita, binafsi sikuwa nafuatilia kwa karibu utendaji wako ila kitendo cha mh raisi kukuteua tena katika serikali yake kumenifanya niamini kama unaweza kwenda na kasi ya "hapa kazi tu" Tanzania bado tuna ardhi kubwa sana ambayo haijaendelezwa kiuhalisia ni mapori, nyumba za kupanga zimekuwa ni tatizo kwa sisi wafanyakazi wa kawaida kwani wamiliki wanataka kodi ya mwaka hii inavutia wizi makazini na mikopo, lengo ni kuweza kujikimu kwani kiuhalisia hela ambayo itatosha kodi kwa mwaka mzima ni ngumu kwa mishahara hii ya TGS.

Hapo ukiwachilia mbali zile nyumba tunazolipa kwa fedha za kigeni bado kuna hela ya dalali kiukweli ni mateso ikitokea unataka kuepuka adha ya nyumba za kupanga namaanisha kodi ya mwaka na madalali shida itakuja kwenye maeneo ya kununua kwani kasi ya upimaji wa maeneo hauendani kabisa na idadi ya watu inayo ongezeka kila kukicha, halmashauri zinapotangaza uuzaji wa maeneo huwa yananunuliwa yote na watu wachache kisha badae wanayauza kwa bei maradufu yaani nazungumzia ulanguzi wa maeneo, hii hushawishi watu kununua maenea ambayo hayajapimwa ambapo serikali inatafsiri kama uvamizi wa maeneo matokeo yake ni kubomolewa watu nyumba zao.

Ukiangalia kwa mtizamo wa kwangu utagundua kuna tatizo mahali kwani kiukweli maeneo yaliyopimwa nchi hayafiki hata asilimia hamsini adha ya kupima eneo ukianza kufuatilia utaratibu utalia ushauri wangu serikali kupitia wizara yako ingetoa bei elekezi kwa nyumba za kupanga yaani hili swalala.kulipa kodi ya mwaka miezi kumi miezi sita lisiwepo, mbona nyumba za nhc kodi inalipwa miezi mitatu tu? Na hizi nyumba kuzipata ni ndoto kwa mwananchi wakawaida? Hawa madalali wasiwepo sidhani kamakunamtu anawapenda wananyonya watu kuanzia wakulima wapangaji kila idara ushauri mwingine serikali ingeongeza kasi ya upimaji wa maeneo uendane na ongezeko la watu ama utaratibu wa upimaji maeneo uwe wa wazi na nafuu.

Natoka Kanda ya Ziwa pamoja tujenge Tanzania yetu
 
mwaka elfu mbili na kumi ni asilimia 12 ya nchi nzima ndiyo iliyokuwa imepimwa nimemuuliza huyu jamaa wa ujenzi anasema kwa mwaka huu hana uhakika ila bado haijafika asilimia 20 ya sehemu iliyopimwa
 
naona hili limeanza kufanyiwa kazi kama sikosei leo nimesikia mjadala kwenye east Africa radio kuhusu muswada wa kodi ya mwaka, juzi muheshimiwa Lukuvi alipiga marufuku uuzaji wa maeneo .....ila duh bomoa bomoa noma.sana
 
Back
Top Bottom